24 February 2011

Prince Charles akutana na Cheryl

LONDON, Uingereza

MRITHI wa Ufalme wa Uingereza, Prince Charles juzi alikutana na nyota wa muziki wa pop, Cheryl Cole kwa ajili ya kujadiliana jinsi ya kuendeleza
mfuko wa kusaidia vijana.

Cheryl ambaye ni mwimbaji wa wimbo wa Girls Aloud, alianziasha mfuko uuitwao 'Cheryl Cole Foundation'  Aprili, mwaka jana kwa lengo la kusaidia vijana katika mji wake uliopo Newcastle.

Fedha zinacochangishwa katika mfuko wa Cheryl, sehemu yake zitatolewa kwa mfuko wa Prince kwa ajili ya eneo la Kaskazini-Mashariki.

Jaji wa X Factor, Cheryl mwenye umri wa miaka 27, ambaye alikutana na Charles mwenye umri wa miaka 62, Clarence House London alisema: "Vijana wanaweza kwenda nje ya reli kama hawatapata uangalizi na kusaidiwa.

"Ninataka mfuko wangu kuwasaidia kujitambua umuhimu wao na kufanya maisha yao kuwa katika mstari."

No comments:

Post a Comment