09 February 2011

Wabunge wa CHADEMA watoka tena bungeni

*Ni kupinga bunge kubadili kanuni kuwabana

Na Kulwa Mzee, Dodoma

KIONGOZI wa Upinzani bungeni, Bw. Freeman Mbowe jana aliwaongoza na wabunge wa chama hicho kutoka nje ya bunge kupinga
kubadilishwa kwa kanuni iliyokuwa inakitambua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilichofikisha asilimia 12.5 ya wabunge kama Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Wabunge hao waliamua kutoka bungeni mara baada ya mchango wa Bw. Mbowe kuhusu mjadala wa kubadili kanuni hiyo, ambayo mtoa hoja, Naibu Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai, alisema ni Azimio la kutafsiri kanuni maneno 'Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni'.

Katika mchango wake Bw. Mbowe alisema wamba hawatendewi
haki, watakuwa wanafiki kama watashiriki katika utaratibu wa mwisho wa suala hilo.

Bw. Mbowe alilazimika kuwa mchangiaji wa mwisho baada ya Mbunge wa ubungo, Bw. John Mnyika kuomba mwongozo wa spika, kwa kuwa mjadala ulikuwa unaelekea kumalizika bila Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani kupewa nafasi, na hivyo kuomba mjadala uahirishwe, lakini Spika Anna Makinda aliamua kumpa nafasi.

Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA, alisema hawawezi kuingizwa katika ndoa wasiyoiridhia kwa kuwa wananchi walioamua kutoa ridhaa kwa CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani ndio hao waliamua kila chama kipate kura zilizopatikana katika uchaguzi mkuu.

"Hatuna ugomvi na chama chochote, tunatofautiana kwa misimamo, tuheshimu kanuni lakini kanuni ikiua msingi wa haki ni batili," alisema.

Alisema kila chama kina haki, katika hilo hawakutendewa haki hivyo watakuwa wanafiki kama watashiriki katika utaratibu wa mwisho wa kubariki hilo. Baada ya kauli hiyo, wabunge wote wa chama hicho waliinuka na kutoka ndani ya ukumbi.

Akizungumzia hilo Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda alisema katika hilo CHADEMA wamepitiwa, hawana uhalali wowote na kuongeza kwamba siasa ni kuvumiliana na kuwa wakweli.

"Kutoka nje hiyo si tabia ya kibunge, wanatakiwa kuonesha wanaweza kutawala na kuongoza baadaye," alisema na kuhoji kwamba hali itakuwaje ambapo kila panapokuwa na hoja ya kubishania wanatoka nje kwani hiyo ndiyo kazi waliyotumwa na wananchi?

Baada ya CHADEMA kutoka nje, Bunge lilipitisha hoja kwa sauti za ndiyoooo, kutoka kwa wabunge wa vyama vingine, hivyo Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni itaundwa na wabunge wote wa vyama vya upinzani.

Mapema akichangua hoja hiyo, Mbunge wa Kawe, Bi. Halima Mdee (CHADEMA) aliwashtukia baadhi ya wabunge wa upinzani akisema sasa wamegeuka kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) B, baada ya muafaka wa Zanzibar kuonekana kuingizwa kinyemela kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mjadala huo ulihusu hoja ilizowasilishwa na Mbunge wa Kigoma Kusini, Bw. David Kafula (NCCR-Mageuzi) na Mbunge wa Wawi, Bw. Ahmad Rashid (CUF) waliotaka neno 'Kambi Rasmi ya Upinzani' lifutwe kwenye Kanuni za Bunge za mwaka 2007 na wabunge wote wa upinzani waunde kambi ya upinzani badala ya chama chenye viti vingi bungeni.

Kutokana na hoja hiyo, bunge liliwasilisha azimio la kutaka 'kutafsiri' kanuni hiyo na kufanya maneno 'Kambi Rasmi ya Upinzani yamaanishe wabunge wa vyama vyote, ambao si wa chama tawala.

Kulingana na kanuni hizo, kambi Rasmi ilikuwa imaanisha wabunge wa chama ambacho kimefikisha asilimia 12.5 ya wabunmge wote, ambacho kwa bunge hili ni CHADEMA, bila kukilazimisha kuwajumuisha wapinzani wengine.

Bi. Mdee alisema kwa mara ya kwanza wapinzani wanapigiwa makofi na wabunge wa CCM wakati wakiunga mkono hoja hiyo, hali aliyosema inaonesha wabunge wanajivisha viremba vya wawakilishi kama wapinzani, leo wanageuka CCM B.

Alisema anachoona ni muafaka Zanzibar unataka kuletwa bungeni kinyumenyume kuzimisha nguvu ya CHADEMA kwani haiwezekani kuwaongoza watu wanaotofautiana kisera, lakini kwa kuwa wako wengi wanaopigia kura azimio la mabadiliko hayo litapita, ukweli utabaki pale ple.

"Tunajua wenyeviti wa kamati kazi yao ni kupata ajenda za bunge, upepo huu wa ushirikiano na CCM tutakuta ajenda zinazoletwa ni zile za mtawala anazotaka," alisema.

Akichangia mabadiliko hayo, Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), Bw. John Cheyo alisema lazima nchi itawalike kwa amani, hivyo kitu chochote kinachowasilishwa kwa ajili ya kufanya nchi isitawalike kwa kuwepo kwa migomo na mauaji lazima kikataliwe.

Alisema Watanzania wanataka kambi ya upinzani yenye nguvu, kama kuna vipengele vya kudhoofisha hivyo vinakwenda kinyume na kanuni, aliwaomba CHADEMA kupunguza hasira watengeneze bunge litakalotegemewa na wananchi, wasiendeleze uadui.

"Nanyi chama tawala mambo ya kura myaache, mtawale nchi, Rais Jakaya Kikwete tawala nchi baada ya miaka mitano wengine wapigiwe kura," alisema.

Mbunge wa Singida Mashariki, Bw. Tindu Lissu (CHADEMA) alisema waliowasilisha maombi hayo lengo lao kupata madaraka wakati Watanzania hawakuwapa nafasi katika vyama vyao.

Alisema chama cha upinzani chenye viti vingi bungeni ndio chenye nafasi ya kushika nafasi za uenyekiti katika kamati za kusimamia fedha za umma, chama chenye kiti kimoja kupata nafasi hiyo ya ulinzi wa fedha za umma haiwezekani.

"Hatuko tayari kuwa na ndoa na chama chenye ndoa na chama kingine ukivuka Bahari ya Hindi, sheria inaruhusu ndoa ya wake wengi lakini si ndoa ya wanaume wengi," alisem na kuongeza kwamba hawako tayari CHADEMA kuburutwa katika hoja hiyo ya mabadiliko.

Bw. Kafulila akichangia alisema upinzani kutofautiana wenyewe kwa wenyewe ni jambo la aibu, wale wanaopinga mabadiliko hayo haoni sababu zaidi ya ubaguzi.

"Tunashinda kwa asilimia 20 tunakataa mseto, tukipata asilimia 60 hali itakuwaje, ukipata kidogo uoneshe una busara ya kufanya kazi pamoja, kwa hali hiyo ukipewa kikubwa huwezi kuaminika," alisema.

Naye Bw. Mohamed alisema kuna dhana kwamba kuna watu wanabebwa na CCM, hakuna anayebebwa na chama hicho kufanya mabidiliko pale panapoonekana kuna haja, ni jambo la kawaida, hizo tofauti za ubaguzi zinazojengwa si wanazotaka Watanzania kusikia.

"Mkuki kwa nguruwe kumbe, CUF mbona hatukulalamika? Tushirikiane tumepata ridhaa kwa wananchi," alisema na kuunga mkono azimio hilo.

48 comments:

  1. Baadhi ya wananchi hatujaelewa kwanini bunge limefanyia marekebisho ya hicho kifungu! Kwa mdomo wake spika makinda alisema haitawezekana kwa kile alichopendekeza kafulila na rashid (CUF) kuwa kuwe na kambi ndogo ya upinzani bungeni na kwamba CHADEMA wana haki ya kuunda kambi rasmi kwakuwa wamekidhi vigezo hivyo, sasa imekuwaje spika ukaruhusu hiyo haki itengeliwe? huoni unajichanganya mwenyewe badala ya kusema kuwa chadema wamepotoka kwa kutoka nje? either hujui kanuni mwenyewe au unaburuzwa au unapata shinikizo kutoka mahali vipi ufanye kazi zake ambapo hautofika kwa mpango huo mama bora angekuwepo SITTA hata kama hutopenda hilo tutalisema kwakuwa unaonekana kujichanganya na maneno yako na wewe usipoangalia utakuwa mwanzo wa vurugu usidhani tumelala wananchi tunaangalia na kusikiliza na kupima sie sio wa mwaka 47 mnatudanganya, huko misri na tunisia etc unadhani wananchi wana uroho wa madaraka wanavyoshinikiza watawala wao waondoke madarakani? Hapna, wamechoshwa na utendaji wa kubahatisha kama huu, naomba mtende haki na mwenye haki apewe haki yake na si kutumia wingi wengi kuwanyima haki watu wengine

    ReplyDelete
  2. Jamani chadema wapo sahihi CUF ana ndoa na ccm na ndio maana jana walipigiwa debe na wenzao ccm ili kuuyumbisha upinzani bungeni.

    wakae wakijua wananchi hatuungi mkono hatua ya ccm kutoa tafsiri tata kuwapa wenzao nafasi ya kuingia upinzani kama hatua ya kupunguza makaLI YA UPINZANI, WAKIWEMO KENGE KWENYE MSAFARA WA MAMBA AMBAO NI NCCR MAGEUZI,TLP,UDP wasio na mtazamo mpana wa nini watanzania tunataka.

    ReplyDelete
  3. Wakati kambi rasmi ya upinzani ilipopitishwa kwa vigezo vilivyowekwa, CUF walikuwa walifurahia kwa kuwa ndio walikuwa wengi, baada ya kushindwa kwa vigezo, huyohuyo aliyependekeza vigezo hivyo viwekwe anageuka na kutaka vigezo hivyo vivunjwe huoni kama nimvurugaji anayetaka madaraka. Chadema kaza buti msikubali kwani wanataka kuwadhoofisha.hata sisi wananchi tunaona hilo

    ReplyDelete
  4. cuf inajifariji na wabunge wa zanzibar ambao ni wawakilishi wa watu 7000-10,000 kwenye jimbo hii ni aibu. ndio maana tunataka tuwa na serikali moja au tatu tumechoka na ubabaishaji huu wa muungano

    ReplyDelete
  5. Kafulila ana hoja ya Richmond anasubiri kuileta bungeni.CCM wameshampa rushwa.Kwa msingi huo atakaa kimya.Yaani atafyata mkia,jamani njaa hizi!!!!!

    ReplyDelete
  6. Chadema kaza buti! Ukiona kitu ccm wanashabikia ujue hapo kuna kitu. Na wanainchi wengine walivyo mambumbumbu yanawaponda chadema. Hivi kweli unategemea kambi ya upinzani ipi hapo wakati cuf na ccm wao lao ni moja, haya Mrema yeye ni ccm damu hilo siyo siri. Mzee mwenzangu cheyo, utakumbuka bunge liliopita ni kwanini ulivuliwa uwaziri kivuli baada ya kushabikia ccm. Yaani hakuna kambi ya upinzani zaidi ya chadema wengine ni wanafiki tu hakuna upinzani hapo. chadema kazaa butiiiiiiii tweeeeeeeeeeendeeeeeeeee!

    ReplyDelete
  7. chadema wana hoja za ubinafsi, washirikiane na wenzao, wanaowaunga mkono chadema kwa hili wanalenga kugawa nchi, huu ni ubinafsi Mbowe aache tabia hii hivi akipewa nchi si atawapiga risasi watakaopinga serikali yake ?, niliwapenda chadema lakini sasa wananitia mashaka kwa hili.katika bunge la 2005 Cuf ndio ilikuwa na wabunge wengi wakati chadema walikuwa wachache sana, lakini kwa kuwa Cuf iliwathamani na uchache huo katika kambi la upinzani kazi ilikuwa nzuri wakati hoja nyingi za ufusadi zikiibuliwa.iweje leo chadema kwa kuwa wamepata wabunge wengi katika kambi la upinzani wawakatae wenzao kwa mwamvuli kuwa wako kwenye muafaka,hivi wana hofu gani?wakati wananchi ndio wenye uamuzi sasa wao wanataka kulazimisha mambo, huo ni ubabe na ubinafsi, chadema wanayo ajenda ya siri na kwa hali hii mjadala bungeni itawashinda na watawaboa wananchi kwa migomo yao kwani hadi sasa asimia yao ya kukabidhiwa nchi imeanza kushuka tena kwa sababu wananchi wanaona leo kura ikipigwa tena kura za chadema zitapungua tena kuliko wakatim wa uchaguzi mkuu, ninawaomba chadema wawe na busara kwa masuala ya kitaifa sio hivyo jamani mnataka kupita kiasi.

    ReplyDelete
  8. Mama Anne Makinda mtihani wako wa kwanza umefeli. Hapa ndipo wananchi wanapoona wazi kabisa kuwa ulipandikizwa na chama chako kwa maslahi zaidi ya chama na si kwa kile walichokisema ni fursa sawa kwa wananwake.

    Hamadi ndiye aliyeweka maneno Kambi rasmi ya upinzani wakati huo akitaka CUF wawe vinara. Leo hii Hamad huyu huyu analiondoa na kumkubalia. You are weak madam, tena umewadhalilisha sana wanawake wenzake. HUFAI ANNE! Uko kwenye kiti cha uspika kimaslahi ya chama zaidina si kwa maendeleo ya nchi.

    Ole wenu CCM, wananchi wa leo si wa miaka ile ya ujinga wa kikondoo. CHADEMA kina dira sahihi ya ukombozi. CUF mnadanganywa ili muwatumikie CCM daima. Mnafikiri ndoa ya visiwani na huku bara itakubalika? Mna ndoto za ndaria. Hamad wewe mwenyewe unakiri Zanzibar ni nchi kamili, sasa huku bara mnafuata nini?

    Wananchi tuamke, saa ya ukombozi ni sasa. Tukiunge CHADEMA mkono - MAANDAMANO NCHI NZIMA TUFIKISHE UJUMBE KWA JK!!!!

    ReplyDelete
  9. nisaidien jaman eti hivi chadema ni chama tawala au ni chama cha upinzani kwenye bunge la jamhuri ya muungano? kuna mbunge yeyote wa CUF kateuliwa na JK kuwa waziri? hii inanfanya nikumbuke maneno ya mtikila kuhusu serikali ya tanganyika

    ReplyDelete
  10. huyo mboe msimlaumu sana kwanza anadaiwa hela nyingi sana na mabenki pili simtumwenyebusara ya kutawala nchi pili anachuki binafsi ninadhani sabau ya kukosa uraisi kwani walijitahidi kushawishi sana watu kuwachagua sasa wanafikiria pumzi walioifanya 2010 wataweza 2015?sasa tumewashtukia kuwa mnataka tu kutumaliza wezi wakubwa nyie nae mzee slaa hushituki tu upo na manyonya damu hayo? yatakumaliza

    ReplyDelete
  11. CHADEMA TUKO PAMOJA NANYI,TUKO NYUMA YENU TUNAWASAPOTI ASILIMIA 100. HAIJATUINGIA AKILINI SISI WANANCHI KUONA KWAMBA KANUNI ZINABADILISHWA BAADA YA CHADEMA KUSHIKA KAMBI YA UPINZANI,KWANINI WASIBADILISHE WAKATI CUF WAKIWA WAPINZANI RASMI?
    HAKUNA KULAZIMISHANA KUUNGANA,HIYO NI HIYARI YA CHAMA,.
    MSIJE MKASAHAU CHADEMA NI NGUVU YA UMMA,HATA KUTOKA NJE JANA HIYO NI NGUVU YA UMMA!!!!
    HAKIKA HATUTAKUBALI KUDHALAULIWA NA MAKINDA TUNAMWACHIA MUNGU,KAMA ULIWEKWA UWE SPIKA WA KUKANDAMIZAA CHADEMA NA MUNGU AKUADHIBU!

    ReplyDelete
  12. hapo mwanzo mnasema kanuni ilibadilishwa ili chama chenye 12% kiwe kiongozi wa upinnzani, leo hii wanafikia kiwango chadema, ccm wanaona chadema itawazid hoja bungeni,bi anna anashinikizwa na hao waliomweka kitin abadili kanuni, jaman, haji hata kwa mjinga, yote haya kufanya chadema isiwe na nguvu bungeni hata kama wana wabunge makini na wasomi. Yaleyale ya kusema wanabadili kanuni kumtoa sitaa eti wanataka kuweka jinsia ya kike katika ngazi ya spika,kumbe janja ya kumtoa spika maana hatetei mafisadi.Huyo maza hapo kwenye kiti atayumbishwa na walimweka inabidi afate masharti yao.hawezi kanuni.kanuni alizijua sitaa,hapindishi.chadema wako imara,wametulia,kila wakisema cha ukweli,wanaonekana hawafai,hayo ya richmond,hadi dowans,kama si chadema,kikwete kigugumizi angekipata wapi,mwenyewe kasalim amri.hawafahamu maswahiba zake na wakwe zake, jamani? Chadema kaza buti,tutafika,barabara ina kona lakin mwisho wa siku safari inafika mwisho wake!!!.kila kukicha mkiona kanuni inabana mnataka kupinda,ongeeni ya maana.

    ReplyDelete
  13. Madam Anne Makinda umechemka, nafikiri umetumika na wenzako wa ccm, you are not free in that seat,ni juzi tu umeongea juu ya uhalali wa chadema kuunda kambi ya upinzani na kuwashangaa CUF and then over the sudden umegeuka na kusahau kauli yako. CCM wamefanikiwa kwenye nia yao ya kuweka boya lao la kuligeuzageuza. Mpango mzima ni kuwadhoofisha chadema but hamtaweza kamwe, watanzania wa leo si wa mwaka 47, tuko nyuma ya chadema, chadema kaza buti, tutafika tu kwenye nchi ya ahadi ya maziwa na asali ingawa safari ni ngumu.

    ReplyDelete
  14. WATANZANIA WENZANGU, NAOMBA NIWAAMBIE JAMBO MOJA! MHESHIMIWA PHILEMON NDESAMBURO NA MHESHIMIWA HAMAD RASHID WALIFANYA MAZUNGUMZO SIKU MOJA KUHUSU SABABU ZINAZOKWAMISHA KUUNDA KAMBI YA UPINZANI YA PAMOJA, MHESHIMIWA NDESAMBURO ALIMWELEZA MHESHIMIWA HAMADI RASHID BILA KUMFICHA KAMA WANAVYOFANYA KINA MBOWE, SABABU KUBWA YA KUTOTAKA KUUNGANA NA C.U.F NI:
    ''nyie C.U.F waislaam ni wengi sana, na hilo ndilo linalotupa sana taabu kuungana na nyie''HAMAD NAE BILA KUMUONEA HAYA WALA KUMCHELEWESHA AKAMWELEZA: ''Na nyie CHADEMA mbona wakatoliki ni wengi sana??''
    KUTOKANA NA MAZUNGUMZO HAYA, TUNAPATA PICHA YA WAZI KABISHA KWAMBA KINACHOWASUMBUA chadema NI UDINI, UROHO WA MADARAKA, UBINAFSI, KUTAKA UMAARUFU KWA NGUVU, UTOTO, PAMOJA UMBUMBU WA KISIASA WALIONAO VIONGOZI WA CHADEMA, WATANZANIA NAOMBA TUWAFAMU KWA UHALISIA WAO HAWA CHADEMA, HAWATAIPELEKA NCHI YETU PAZURI KWA TABIA HIZI CHAFU WALIZONAZO!! TUWAZOMEE NA KUWAEPUKA KAMA UKOMA!!!!

    ReplyDelete
  15. Ukipenda chongo utasema kengeza.

    Kizuri kipi ambacho viongozi, wanachama na washabiki wa CHADEMA wamekifnya zaidi ya ukabila, uongo, ubinafsi na ufisadi wa kisiasa.
    POLE.

    ReplyDelete
  16. me mtazamo ni kwamba hizi hoja za wadau ziwekwe ktk gazeti lako,wadau wengine wasome,wajue nchi inavyoyumbishwa,kuna watu redio,tv hawazipati,japo gazeti baada ya wiki akipata ajue wajanja wa mjengoni wanavotaka kupinda mambo,hivi mbona sijamsikia site kauli zake,nataka nitafute nafasi nimfate ofisini kwake anipe ukweli wa hoja hizi,huyo maza simwamini hata.sita mwanasheria no.1, mambo yote yako akilini.haya majambo kama hujui sheria wala usijisumbue kutoa hoja,maza hilo angesema alijibu leo,maana lina sheria,asingekurupuka nalo.na akitaka kazi iende makini,awe anaomba ushauri kwa boss wake ayemnyanganya kidoga? kama uliwekwa bila ngozi ya watu, mfate mwombe ushauri,ana hekima zake atakuongoza.wala hakatai.mambo mazito hayo.Kama hivo kila kukicha kanuni zitabadilishwa kwa faida za watu,itakuwa yale yale ya viraka vya kariba!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  17. Huo ni mwanzo tuu ukweli utabainika kwani wenye nia swafi na ukweli utawagunduwa na wenye nia ya ubinafsi pia watajitokeza, hao wataanza hata wenyewe kwa wenyewe kutengana na kufukuzana ktk chama,kwani si wote wanaokubali huo utoto wa hao chadema. leo hiyo kambi ya upinzani sasa hawa wengine wakajiunge wapi? au wao wapinzani B watakuwa ktk kamati ipi? hao ni wabinafsi, wakabila na wapenda fitna tusubiri ndani ya miaka 2 tutaona

    ReplyDelete
  18. wabunge wengine njaa ya madaraka. chadema tuko pamoja wananchi wa sasa si wa miaka ile ya 42. Chadema kazeni buti hao wa vyama vingine keshokutwa utawakuta ccm tu, yote njaa ya madaraka

    ReplyDelete
  19. People's Power!

    Moshe Dayan

    ReplyDelete
  20. Kufulila na Hamadi ni wauwaji, kumbukeni watanzania wanateseka kwa ajili ya uroho wenu wa madaraka, mnawaibia wananchi kura kwa ulagai wenu. Nyinyi mnasema CHADEMA ni wabinafsi hakuna nyinyi ndio mamluki. Kufulila umejichafua sana ndugu yangu umeshaanza kasumba za M/kiti wako MBATIA HUFAI HATA KIDOGO. Hamadi peleka unafiki wako kwa wapemba wenzako hatukuhitaji. Nyinyi kila kitu ni vurugu tu tunawajua nyinyi wapemba. Nyinyi mna wivu umewazidi hakuna lolote mnalofanya na mtakuwa wasindikizaji mpaka mwisho.

    ReplyDelete
  21. eng. Mwakapango,E.P.AFebruary 9, 2011 at 12:03 PM

    ukiritimba wa chama kimoja bado kabisa baadhi ya makada wa CCM wanauota. ni mfumo pandikizi wa max wa kujaribu kutawala ukiwafanya wengine ni mambumbumbu ukitumia vya usalama wa taifa kuhahakikisha nchi inatawalika. poleni sana ndungu zangu wa CHADEMA lakini nataka ni waambie kitu kimoja CHADEMA msibweteke na mafanikio mliopata piganeni watanzania wako nyuma yenu. nilikuwa naangalia kipindi cha Bunge nilimwona mpiganaji Samwel Sitta kidogo mchozi umtoke aliona mliotendewa CHADEMA wametuondolea wakata nondo wote maarufu wa CCM kama Lucas Selelii, mwakyembe, Sita wetu na wengineo sasa wameingia upande wa shilingi ambako ni CHADEMA sisi mnavyotoka nje tunawaelewa sana na endeleni pale manapoona haki zenu ziachukuliwa kwani hata alipokuwa anavunja DUSO 1978 mwalimu JK Nyerere aliwaambia wanafunzi kuwa 'kama mnaona milango ya haki imefungwa na hamuwezi kufungua basi ivunjwe! vile vile Raisi wa marekani John Kenedy akiwahutuba wanafunzi wa moja ya chuo kikuu nchin humo alisema 'the hotest place in hell will maintained for those who during moral crissis maintain their neutrality'
    Anna Makinda dada yangu sina maneno naye sana anaelewa nguvu za CHADEMA lakini punguza kuwasikiliza baadhi ya mafisadi ambao wamepenyeza mianya yao NDANI YA CCM waache CHADEMA waisafishe CCM kwenye kamati hizo tatu za fedha za wananchi.
    JOBU NDUNGAI ameibuliwa na kutayalishwa na mafisadi ili awachanganye watanzani kwani nani asiyejua jin si alivyotumia pesa kuhakikisha anapita bila kupingwa? mchana anajifanya kumjadili Rostam aziz jioni anaenda kuchukua uchache,ni mnafiki sana na hafai kushika madaraka makubwa na nadhani hichi Rais JK ameliona. tumemstukia ndungai na 2015 angojee adhabu stahili kwake. anasema Freeman Mbowe anadaiwa na mabenki heri ya huyu anayedaiwa na mabenki kuliko utitiri wa wabunge wa CCM wamafisadi ambao wanayajaza matumbo yao kwa fedha za EPA na richmond.
    CHADEMA waachieni hizo kamati tatu nyinyi imarisheni intelejensia yenu hakikisha ufisadi wowote haufanyiki wanatafuta hela za kuwalipa wanachama wao walochakachua matokeo ya uchaguzi kwani ruzuku yao mmeipunguza. Halima JAMES Mdee usikate tamaa mamaangu ongoza mapambano mmeanza vizuri sana big up!
    rafiki yangu Tundu lisu kijana shupavu mpiganaji toka utoto wake pale Galanos na baadaye mlimani tuponye majeraha watanzania, ondoeni wizi huu, together we stand.
    naomba kuchukua nafasi hii kuwa tafadhalisha wabunge wa CCM dua la kuku halimpati mwewe msije mkadhani maneno mnayozungumza juu ya CHADEMA wananchi wanawasikiliza DAMU YA WATANGANYIKA inawalilia nyini msiona uchungu wa nchi yenu , mnapata ubunge kwa kuhonga mapesa mengi mlioibia watanzania.

    ReplyDelete
  22. WATANZANIA WENZANGU, NAOMBA NIWAAMBIE JAMBO MOJA! MHESHIMIWA PHILEMON NDESAMBURO NA MHESHIMIWA HAMAD RASHID WALIFANYA MAZUNGUMZO SIKU MOJA KUHUSU SABABU ZINAZOKWAMISHA KUUNDA KAMBI YA UPINZANI YA PAMOJA, MHESHIMIWA NDESAMBURO ALIMWELEZA MHESHIMIWA HAMADI RASHID BILA KUMFICHA KAMA WANAVYOFANYA KINA MBOWE, SABABU KUBWA YA KUTOTAKA KUUNGANA NA C.U.F NI:
    ''nyie C.U.F waislaam ni wengi sana, na hilo ndilo linalotupa sana taabu kuungana na nyie''HAMAD NAE BILA KUMUONEA HAYA WALA KUMCHELEWESHA AKAMWELEZA: ''Na nyie CHADEMA mbona wakatoliki ni wengi sana??''
    KUTOKANA NA MAZUNGUMZO HAYA, TUNAPATA PICHA YA WAZI KABISHA KWAMBA KINACHOWASUMBUA chadema NI UDINI, UROHO WA MADARAKA, UBINAFSI, KUTAKA UMAARUFU KWA NGUVU, UTOTO, PAMOJA UMBUMBU WA KISIASA WALIONAO VIONGOZI WA CHADEMA, WATANZANIA NAOMBA TUWAFAHAMU KWA UHALISIA WAO HAWA CHADEMA, HAWATAIPELEKA NCHI YETU PAZURI KWA TABIA HIZI CHAFU WALIZONAZO!! TUWAZOMEE NA KUWAEPUKA KAMA UKOMA!!!!


    NDUGU MWANDISHI -NAOMBA UANDIKE HAYA MAONI KWENYE GAZETI LAKO TUKUFU ILI WANANCHI WAIJUE CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO(CHADEMA)VIZURI

    ReplyDelete
  23. CHADEMA ni chama cha WA...GA malizieni wenyewe.
    Wameona biashara imekuwa ngumu sasa wamewekeza kwenye siasa. FUJO ZIKITOKEA HAKUNA BIASHARA WALA SIASA.

    Wanafunzi mnajiangaisha tu kuwa support CHADEMA namjue wa kichukua nchi mnakwenda na maji.
    Wakati wa Mwalimu sasa hivi mgekuwa vijijini
    shukruni sana JK. Sababu na migomo yenu jiulizeni kwanza wazazi wenu wanalipa KODI?

    ReplyDelete
  24. nami naungana na mpinzani namba moja wa CDMA, wakati wa mdahalo wa RASHID NA MBOWE, mheshimiwa RASHID alidokeza jambo hilo, tuwe na tahadhari kubwa na hiki chama cha WACHAGGA

    ReplyDelete
  25. Wewe mpinzani No 1 wa CHADEMA. Ondoa upupu wako hapo juu hata haueleweki kimtizamo. Unaweza kulinganisha chama cha CHADEMA na CUF. Chadema inamchanganyiko wa wabunge na dini na makabila sio Cuf ina wapemba watu.

    Hao wapemba tuwapeleke wapi? Mnafikiri TZ ni soko la mitumba hakuna kitu hicho kwanza wasomaji wakiona point kama hiyo hata hawasomi kwa sababu walishawajua. Unajisumbua.

    ReplyDelete
  26. chadema ni chama kinachoongozwa na maaskofu na mapadri, angalieni hata wabunge wao ni maaskofu na mapadri, kuungana na chama chenye muonekano wa kiislaam si jambo jepesi!!!watanzania tuimarishe tu chama chetu (CCM) ndicho chama kisicho na ubaguzi wa kidini wala ukabila, CHADEMA NA CUF hawatufai, naungana na mpinzani NAMBA moja wa chadema!!

    ReplyDelete
  27. NYINYI CUF NI CHOGO WA CCM, SISI HATUTAKI MALAPULAPU YA CCM. HAPO HAJAPATIKA MTU, MTAONA AIBU WENYEWE.

    ReplyDelete
  28. KWELI MIMI NINAJIULIZA SIPATI JIBU, UPANDE WA UPINZANI HAWA CCM WANAPIGA KURA KAMA WAPINZANI UA KAMA NANI. SASA KAMA NI KAMBI YA UPINZAI WANGEPIGA KURA WAO WENYEWE KAMA WAPINZANI SIO KUSHIRIKISHA WABUNGE WA CCM. NA KAMA BUNGE LILIKUWA LINATAKA KUSIMAMIA HAKI KAMA WANAVYO SEMA WANGESIMAMIA ILI HAKI ITENDEKE.

    SPIKA ANALIAIBISHA BUNGE LA TZ KWELI JAPOKUWA ANAHAKI NA MAMLAKA ZA BUNGE LAKINI HAJATENDA HAKI KWA UPANDE WA WAPIZANI. SASA HAPA DEMOKRASIA IPO WAPI KWA UPINZANI?

    ReplyDelete
  29. uuuwiiiiiiii, jamani mbona wachangiaji mnatudhalilisha wachagga, kwani hatuna haki ya kuongosa nji hii, hii ni nji yetu sote na tuna mchango mkubwa kuliko makabila yote hapa TZ, Kwakuwa tumesoma na tuna pesa kuliko makabila yote hapa TZ, sasa kuwa mkuu wa upinzani bungeni tu inawatoa roho!!!! acheni ubaguzi wapumbavu nyie, mbona C.CM mwenyekiti hajawahi kuwa mchagga tangu kianzishwe, CHADEMA iko juu na tutaendelea kususia bunge hadi kieleweke, na budget ya mwaka huu Haipiti -lazima tutoke nje wakati wa kupitisha vifungu!!

    ReplyDelete
  30. Kuna mamluki wa vyama kwenye mitandao kazi yao ni kutukana na kupinga mawazo yanayotofautiana na mabwana zao. SASA NYIE CHADEMA TUAMBIENI PEOPLES POWER NI IPI? HAMNA WINGI WA KURA BUNGENI NA NDIO MAANA MKAKIMBIA HAPO NA HATA ARUSHA HAMKUWA NA KURA ZA KUMPATA MEYA NDIO MKAKIMBIA. ANNA MAKINDA ALIVYOKATAA KAMBI NDOGO YA UPINZANI BUNGENI MLIFURAHIA SANA LEO MKIKATALIWA NYIE MNAKIMBIA BUNGENI,MKIPEWA NCHI WANANCHI WAKIANDAMANA KUWAPINGA SI MTAGEUKA IDD AMIN WA PILI. HICHO CHAMA HAMNA KIONGOZI HICHO NI KIKUNDI CHA WAFANYABIASHARA WA KICHAGA NA MAOPPORTUNIST WENGINE WENYE KUANGALIA UPEPO UNAVUMA WAPI. MMEJIFANYA WAJANJA KUWAKATAA WENZENU,OK KAMA CUF HAMUITAKI NCCR,TLP AU UDP NAO WANA KOSA GANI. UONGOZI NI BUSARA NA SIO JAZBA, CHADEMA PUMBA TUPU,NA NYIE WABUNGE WA CHADEMA MSIO NA UAMUZI OLE WENU SIKU MTAPOKATAA YA HAO WENYE CHAMA.MNAPANDA BANGI MTAVUNA BANGI HIYOHIYO. PEOPLES POWER NDIO HIYO ILIYOWAKIMBIZA BUNGENI MLIYONAYO NI MBOWESLAANDESA POWER

    ReplyDelete
  31. wewe mchaga unaelia kisenge hapo juu, usijifanye unauchungu sana na CHADEMA kuliko watu wengine ili kujenga picha kwamba ni kweli CHDMA ni chama cha wachagga, usiwapoteze wasomaji, CHADEMA ni chama cha watanzania wote wapenda maendeleo bila kujali dini wala kabila, kama huwezi kuchangia point ya maana acha kuandika upupu kwenye hii blog- na wewe URIO ondoa uchafu wako hapo hakuna askofu wala padri CHADEMA

    ReplyDelete
  32. JAMANI WAPENZI WA CHADEMA ACHENI KUTUKANA WACHANGIAJI WENYE MTIZAMO TOFAUTI NA NYIE , TUMIENI LUGHA ZA KISTAARABU, TUNAJUA KWAMBA, MATUSI,UONGO, UCHOCHEZI,UBINAFSI,UKABILA,UDINI,UCHOYO, UGOMVI NA UCHAFU WOTE UNAOWEZA KUUJUA NDIYO SERA ZA CHADEMA,SASA TUSITUMIE UKURASA HUU KUTANGAZA UOZO WENU, CHANGIENI MADA KISTAARABU, MTAZIDI KUTUFANYA TUZIDI KUICHUKIA CHADEMA NA PIA HATA WANACHAMA WACHACHE MLIONAO MTAWAPOTEZA KWA MTINDO HUU!!!!

    ReplyDelete
  33. HEBU NIWAAMBIENI WACHANGIAJI WANAO TAJA UDINI NI WAPUNGUFU WA AKILI AMBAO HAWAWEKI MASLAHI YA NCHI MBELE. HATA AWE MWISLAM AU MKRISTO KINACHOTAKIWA NI HAKI YA WANANCHI IPATIKANE, ANAYENYONYWA MWISHO WA SIKU NI MWANANCHI MWENYE HALI YA CHINI. UMEONA WAPI MTU ALIEFIKIA MUAFAKA (CUF NA CCM) HALAFU AWEZE KUPINGA MAAMUZI YATAKAYOTOLEWA NA CHAMA TAWALA IMPOSIBLE HAIWEZEKANI. BAADA YA CHADEMA KUWAPELEKA MBIO SASA WANATAFUTA NJIA YA KUWADHOOFISHA KISIASA KULE KUNA VICHWA BWANA CHA MSINGI NI CHADEMA KUJIPANGA. nA KAMA KANUNI HIYO ITAPITISHWA UFISADI TENA BYEBYE MAANA HUYO SPIKA KAWEKWA TU ILI AKIDHI MASLAHI YA MAFISADI. UKWELI UTABAKI PALEPALE

    ReplyDelete
  34. Wewe Lissu funga mdomo wako huna unalojua bungeni hapo kuna kanuni za bunge,mlikuwa watatu au wanne na Slaa na Zitto wakapata nafasi hizo,hapo si pahala pa...........

    ReplyDelete
  35. Kuna watu wenye tabia ambayo sio ya kistaarabu ya kuheshimu watu wengine. Aliye toa hiyo Comment ya UUUWIIII!!!!!!, KIMTAZAMO NA KIUELEWA SIO MCHAGA. HUWEZI KUTOA COMMENT YA KISHAMBA NAMNA HIYO. NAOMBA TUICHUKUE TUIWEKE KWENYE KAPU LA TAKA KWA WAELEWA. ASANTENI.

    ReplyDelete
  36. Msg zinazotolewa zinapima ni jinsi gani watanzania wanavyoelewa siasa au la mi nadhani kinachotakiwa ni uzalendo na si vinginevyo. Ili chama tawala kiweze kuongoza vizuri wananchi lazima kambi yenye upinzani wa kweli iwepo kwa ajili ya kukosoa chama kilichopo madarakani. ukiondoa utofauti wa sera zilizopo ni dhahiri kuwa kama kuna chama ambacho kwa njia moja au nyingine kina masilahi na chama kingine ukweli ni kwamba inapofikia masuala ya utata ni dhahiri kuwa CUF haitaenda kinyume na chama tawala. na kama wataungana kwenye kambi ya upinzani watasababisha mgawanyiko ndani ya upinzani hasa kwenye hoja. upinzani utadhoofishwa ni bora wale wenye msimamo mmoja waendelee kuwa peke yao tu ili kuleta ufanisi katika kulilinda taifa.

    ReplyDelete
  37. mamboooookwelikwelikweli Tanzania ya leo ipo kazi mpaka Kwete akisalim amri mambo yatakuwa shwari la! jamani tuahamie Zanzibar tukimbie ccm

    ReplyDelete
  38. Chama cha ccm na cuf ni wabinafsi na wamejaa uisilamu mtupu,ndio maana viongozi wa dini wakikemea maovu waislamu wanakuja juu,tulishawajua.

    wabunge wote wa ccm wameingia bungeni kwa kuhonga fedha lukuki kununua madaraka hivyo ccm haipo kwa ajili ya wananchi.

    CUF nao wamefulia kuungana na ccm huo ndio mwisho wao kuungana na ccm kushangiliwa itawagharimu,walicheka wakakebehi lakini wananchi watawacheka zaidi 2015.

    Makinda umepwaya mapema na nikuhakikishie kama utaachia bunge kubadili kanuni ili kukidhi matakwa ya mtu fulani umekwishaaa!!!!!!!!!!!lakini sikulaumu maana hata katiba mlikuwa mkibadilisha kimyakimya ili kukipendelea ccm.

    Kafulila umechesha kuungano na wanafiki CUF kwani hao ni upemba tu tu na hawana lingine jipya kiboko yao ni katiba mpya tutakayoweka serikali tatu au moja kwani mbili ni kiini macho.

    ReplyDelete
  39. Hongera chadema mmebanwa na chama tawala na vyama vingine vya upinzani bungeni, watz tumeona mmetoka nje ili msishiriki maamuzi hayo tata. tunachowaomba bunge likimalizika mrudi kwetu wapiga kura tena mjipange vizuri muwashtaki kwa wapiga kura,nasi tutawaadhibu muda utakapofika wala si mbali 2015. WATANZANIA WENGI, MASHULENI, MITAANI MAKAZINI,SERIKALINI,NDANI YA MAJESHI YETU WAPO NYUMA YENU WANAWAPIGA MABOMU HUKU WANASIKITIKA KAMA WATZ WENGINI.MUNGU AWENANYI

    ReplyDelete
  40. CUF, TLP na NCCR walimpigia kura Makinda wakati wa uchaguzi wa spika bungeni na hata katika chaguzi za mameya walikuwa upande wa ccm, iweje leo waingie kwenye ushirikiano na chadema, hii ni janja ya ccm ya kuwavuruga chadema, wapinzani wa kweli kwani katika ndoa hiyo ya mkeka pindi watakapo shindwa kuelewana ccm itawaambia wananchi "watazameni hao wanavyogombana, hao ndiyo wanaotaka kuwaongoza" Chadema ni bora msusie uundwaji wa kambi na kujitenga nao ili ccm A na B waendelee kutawala, mwendelee kujijenga kwa uchaguzi wa 2015 ambao ni lazima tuwatoe mafisadi hawa.

    Haiingii akilini CUF kuwepo kwenye uongozi wa serikali ya kitaifa ya jamhuri ya Zanzibar na kutaka kuwa mpinzani tena kwenye serikali ya muungano, watawezaje kupinga mambo ya serikali ya zanzibar yakiletwa bungeni? huu ni uhuni wa kitoto.

    Makinda nawe bora ungewakatilia mafisadi walipokufuata ugombee ili kumpinga boss wako Sitta, ungestaafu vizuri binti yetu kuliko kuingia katika laana hii, naona huruma kwani kuna siku utalia bungeni kama MTOTO WA MKULIMA PINDA, kiti ulichokalia ni cha moto, hutaweza kuendesha bunge kwa ridhaa yako, mafisadi watasema tusikilize sisi tuliokuweka, mfano ni juzi tu ulipotoa ufafanuzi juu ya hiyo kanuni kwamba chadema wana haki na pia ulimshangaa Hamad ukisema kwamba ni yeye aliongeza neno RASMI na si "kambi ya upinzani" na sasa ulipooelekezwa juu ya mpango wa kuwavuruga chadema umesahau yote hayo, OLE WAKO na pole sana ni bora ukaungame.

    ReplyDelete
  41. Nyie Wabunge, mnaaanza malumbano na misongamano bungeni, hamjui siku zinaenda na mnakula pesa za walalahoi/wavuja jasho ambao ni sisi wananchi??

    Wote ni wababaishaji tu, kila mtu atetee jimbo lake tunataka maendeleo, si msongamano bungeni

    Madowans tupu nyie

    ReplyDelete
  42. CHADEMA wasimame kidete kuwatetea wanyonge kwani CCM imetuchosha. Kuwa makini na hao wanafiki yaani CUF na vyama vingine kwani ni washabiki wa CCM. Watanzania nasi tupo nyuma yenu. MUNGU ibariki CHADEMA, MUNGU ibariki Tanzania. By Thomas.

    ReplyDelete
  43. CHADEMA NA SIASA ZA UKABILA, UCHOCHEZI, UONGO FITINA NA UFISADI WA SIASA ZIMEKULA KWENU.

    KETE YENU NI WIMBO WA UFISADI HAKUNA JIPWA
    HABARI ZA WIZI NA UFISADI NI KWENYE MAHAKANI
    NA SI KWENYE MAJUKWAA YA KISIASA.

    ReplyDelete
  44. mimi naunga mkono madai ya chadema kwa vile hata last time kambi hiyo ilikuwa inaundwa na CUF waliokuwa na viti vingi vya ubunge wa upinzani. sasa kwa nini over the suddenly kanuni ibadilishwe? naona sio fair hapo kuna kamchezo mchafu hususan kudhoofisha upinzani. CCM wanafanya ndivyo sivyo kwa mtaji huu. watanzania sasa imefikia wakati watu wawe na uwezo wa kuhoji kwa mantiki na sio kukubali tu hata kama tunaburuzwa.

    ReplyDelete
  45. Kweli mafisadi hawawezekani. Wanataka hata kupindua nguvu ya wananchi. Nibora tuje tufanye kama Tunnisia ama Egypt. Nyie watawala mnaotuburuza mnajisahau na kuona tunastahili kuwa nyasi za kurupushani zenu. Tangu lini kanuni zinabadilishwa mnapoona mwiba mchungu. Subiri next time mtapokuwa wapinzani tutawakumbusha hili. Msidhani mtaongoza daima, na hivi ndiyo kujimaliza kwenu. Na nyie wachangiaji acheni kupandikiza fikra za udini ama ukabila, mbona hamtetei DOWANS, RICHMOND, MEREMETA etc kwa udini ama ukabila? Tunaumia sisi wa hali ya chini, na sasa TUMECHOKAAA...

    ReplyDelete
  46. PONGEZI ZENU WAKEREKETWA WA CCM NA USALAMA WA TAIFA KWA MATUSI MNAYOYATOA ILI KUCHONGANISHA WATU. PAMOJA KUWA MNALINDA VITUMBUA VYENU, KUMBUKENI KUWA ATHARI YA MATENDO YENU INATIRIRIKA KWA NDUGU/FAMILIA ZA KOO ZENU.

    MNAFANYA HIVYO KUTOKANA NA KUWA MYOPIC. MNA MACHO YANAYOTAZAMA, LAKINI HAYAONI MBALI.

    NI KUTOKANA NA HALI HII KAMATI YA KUUKOMBOA MKOA WA RUVUMA NA KUUFANYA NCHI HURU INAYOJITEGEMEA IMEUNDWA RASMI. MCHAKATO UMEANZA, NA KAZI RASMI ZA UKOMBOZI ZITAANZA HIVI PUNDE.

    ReplyDelete
  47. ANNA MAKINDA UMECHOKAACHA KAZI
    RAIS ANASEMA HAWAJUI DOWANS WALA HAWAMFAHAMU, HASARA ILIONGIZWA NA DOWANS NI BAJETI KARIBIA YA MWAKA, ELIMU INAYUMBA, WANAFUNZI VYUONO WANAFUKUZWA,VIJANA HAWANA AJIRA. HIVI KWELI NYUMBA YAKO ONAIBIWA HUFAHAMU INAWEZEKANA?
    HILO SI KWELI MI NAONA KAMA MTU UMESHINDWA KUONGOZA SI VIZURI KUNG'ANG'ANIA MADARAKA
    KWANZA CCM NI WEZI WAKUBWA
    WANANCHI WA SASA SIO WA 1995 MZE WA TAIFA ANGEKUWEPO ANGEWACHAPA VIONGOZI WETU BAKORA SASA WANANCHI WAMECHOKA HATUTAKI IFIKIE MISRI,NAONA MUONDOKE UMEME MGAO,VYAKULA VINAPNDA BEI PESA MTUMIE HALAFU SISI NDO MTULIPISHE HILO DENI KWA KUTUPANDISHIA BEI
    ENOUGH NOW ONDOKENI MADARAKANI

    ReplyDelete