10 February 2011

Cole aweka rekodi kucheza mechi nyingi

LONDON, Uingereza

ASHLEY Cole usiku wa kumakia leo ameweka rekodi ya kuwa beki wa kushoto aliyechezea mechi nyingi zaidi timu ya taifa ya England.Mchezaji huyo
alicheza mechi yake ya 87 na kuivuka rekodi ya Kenny Sansom.

Cole mwenye miaka 30, ambaye alianza kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Albania 2001, sasa amekuwa na mtazamo wa kufikisha mechi 100.

Alisema: "kwangu mimi itakuwa ni mechi ya kawaida, lakini bila shaka nyuma ya mawazo yangu nitakuwa nawazia, nimevunja rekodi.

"Lakini sitaki kukomea hapa ninataka kucheza mechi zaidi za kimataifa. Nilikosa mechi nyingi kutokana na umajeruhi pengine hadi sasa zingeweza kuwa mechi 90. Kuchezea nchi ni ndoto nilikuwa nikiota tangu nimefanya hivyo kwa mechi 86.

"Ninataka kucheza mechi nyingi kadri ninavyoweza hadi kocha aone, sina uwezo wa kucheza au ni wakati wa kuwapisha vijana kuja na kucheza. Sitakata tamaa na kustaafu.

"Ninatumaini, siku moja wachezaji kama Kieran Gibbs watapata nafasi. Sitaki kuwazuia wachezaji wengine ni mchezaji mzuri kijana anayekuja.

"Ninakumbuka kumuona, Kenny Sansom miaka yangu ya mwanzo nikiwa Arsenal. Aliniambia siku moja utavunja rekodi."

No comments:

Post a Comment