Na Shaban Mbegu
CHAMA cha Michezo ya Jadi Tanzania (CHAMIJATA), kimesogeza mbele Uchaguzi Mkuu wake uliopangwa kufanyika mwishoni mwa
mwezi huu kutokana na ukata wa fedha uliokikumba chama hicho.
Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa chama hicho, Mohamed Kazingumbe alisema uchaguzi huo sasa utafanyika Agosti mwaka huu.
Alisema wameamua kufanya hivyo pia, ili kuwapa nafasi wajumbe wa mikoani pamoja na kusubiri chama kijipange kikamilifu kwa ajili ya uchuguzi.
"Tumeamua kusogeza mbele uchaguzi na sasa utafanyika mwezi wa nane, wakati wa mashindano ya kimataifa kwa sababu mpaka sasa baadhi ya maandalizi bado hayajakamilika," alisema.
Wakati huohuo, Kazingumbe aliwaomba wadhamini mbalimbali kujitokeza kudhamini chama hicho, ili kiweze kufikia malengo yake kama walivyojipangia na si kila siku kuendelea kudhamini mchezo wa soka pekee.
"Mara nyingi tumekuwa tukipata ahadi kutoka kwa wafadhili mbalimbali, lakini wamekuwa wagumu kutekeleza pia tunawaomba wabadilike na kudhamini hivi vyama vidogo vidogo, kuliko kila siku kuendelea kufaidisha soka pekee," alisema.
No comments:
Post a Comment