09 February 2011

Twanga Pepeta yajibu mapigo

Na Addolph Bruno

UONGOZI wa Kampuni ya African Stars Entertaiment Tanzania (ASET), jana imemtangaza rasmi mwimbaji mahiri Khadija Mnoga 'Kimoteli', kujiunga na
bendi ya Twanga Pepeta akitoa Extra Bongo.

ASET imemtangaza mwimbaji huyo ikiwa ni siku chache tangu, Extra Bongo kuwanyakua baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo, hatua inayoonekana ni katika kulipa kisasi.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka alisema kuondokewa na wanamuziki katika bendi yake ni changamoto kwao na kamwe hawezi kuingia katika malumbani kwa kuwa kampuni yake ina utajiri wa wanamuziki.

Wanamuziki wa Twanga waliochukuliwa na Extra Bongo ni Rogert Hega 'Catapila', Saulo John 'Furgason' na kiongozi wa wanenguaji Hassan Mussa 'Nyamwela'.

Asha alisema yupo katika kazi ya muziki ili kuwasaidia vijana kuwapa ajira kwa kuwa bendi yake ni ya jamii.

"Siwalaumu wanamuziki waliondoka kwa kuwa ni sehemu ya kutafuta maisha, lakini nazishauri bendi zinazochipukia kuiga mfano wa Twanga kufufua vipaji.

Alisema bendi yake kwa sasa ina wanamuziki 32 ambao wanafanya kazi katika sekta tofauti, ambao wana mikataba na wanalipwa vizuri tangu bendi hiyo ilipoanza ikiwana na wanamuziki nane.

Kimobitel baada ya kutambulishwa alimkandia Choki kwa kudai kuwa ameamua kurudi Twanga Pepeta baada ya kuchukizwa na kiongozi huyo Extra Bongo kuikamia Twanga Pepeta badala ya kutoa burudani.

"Sikuwa napata raha nilipokuwa kule licha ya kuwa nilikuwa kiongozi wa bendi, nilitumiwa katika mambo mabaya kama kuwafukuza wanamuziki akiwemo Greyson Semsekwa kitu ambacho kiliniumi sana, mambo mazuri sikishirikishwa na maslahi ndiyo balaa," alisema Kimobitel.

No comments:

Post a Comment