LONDON, England
LICHA ya kuwa na hisia za kuchanganyikiwa kutokana na kuwa mara kwa mara kugombana na mashabiki wake, beki wa timu ya taifa ya
England, Ashley Cole ameshinda tuzo ya mchezaji Bora wa mwaka jana, baada ya kuibuka mshindi katika kura zilizopigwa kwa njia ya mtandao na mashabiki wa soka nchini humo.
Cole, ambaye ameshachezea timu ya taifa ya England mechi 86, alitangazwa juzi, baada ya kupata taarifa hizo alisema kipindi hiki kilikuwa kigumu kwake, lakini baada ya kupata tuzo hiyo anadhani kwa sasa anaaminika.
Picha ya beki huyo wa kushoto wa timu ya Chelsea, mbele ya umma iliingia matundu kutokana na tamaa yake kimwili jambo ambalo lilisababisha kuvujika kwa ndoa yake na mwanamuziki mashuhuri Cheryl Cole.
Alisema ana uhakika mashabiki walikuwa wakimzomea alipokuwa akiboranga uwanjani, lakini akakiambia kituo cha televisheni cha FATV kuwa jambo lile lilikuwa ni jambo binafsi zaidi, ila lilimuumiza mno, lakini kila wakati aliweka jitihada zake kwa timu hiyo ya taifa na alijaribu kufanya kila aliwezalo kuipa mafanikio.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya England, ambacho kilifika hatua ya pili ya fainali za Kombe la Dunia mwaka jana.
No comments:
Post a Comment