Na Agnes Mwaijega
MTANDAO wa Asasi za Kiraia za kuangalia Chaguzi Tanzania (TACCEO) unaoratibiwa na Kituo Cha Haki za Binadamu (LHRC) umesema Tanzania inatakiwa
kujifunza kutokana na utaratibu uliotumika katika Uchaguzi uliofanyika nchini Uganda ili kuweza kuboresha chaguzi zake.
Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Mtandao huo, Bi. Martina Kabisama alisema pamoja na kwamba uchaguzi huo ulikuwa na upungufu wa aina mbalimbali wao kama waangalizi wangependa mambo yote mazuri Tanzania iyachukue na kuyafanyia kazi.
"Tumejifunza kitu kutokana na uchaguzi uliofanyika nchini Uganda na tungependa nchi yeu kujifunza jinsi ya kuratibu na kuendesha chaguzi ndani ya nchi," alisema.
Alisema kutokana na mchakato mzima wa uchaguzi wamegundua kuwa kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa wapiga kura, mfumo wa watendaji wa Tume ya Uchaguzi unakuwepo katika ngazi ya taifa hadi kata na mafunzo kwa wataalamu mbalimbali wa kusimamia na kuratibu uchaguzi kufanyika haraka.
Bi. Kabisama alisema katika uchaguzi huo matumizi ya makubwa ya rasilimali za umma yalioneshwa kwa kiwango kikubwa na rais aliyeko madarakani.
"Kwa mfano fedha ziligaiwa kwa wananchi ili kuwashawishi wapiga kura, ujumbe mfupi kwa njia ya simu kwa kila mwananchi ulikuwa katika lugha mbili ambazo ni Kiganda na Kiingereza ili kurahisisha mawasiliano," alisema.
Pia alisema matumizi ya Teknohama katika uangalizi wa uchaguzi huo yalisaidia kuonesha mchakato mzima wa uchaguzi jinsi ulivyoenda na kufanya ushiriki mpana wa wananchi katika zoezi zima la uchaguzi ambapo taarifa za matukio yaliyokuwa siyo ya kawaida yaliripotiwa kwa wakati.
Aliongeza kuwa Katiba ya Uganda imepanua wigo wa demokrasia na ushiriki wa wananchi katika masuala mbalimbali.
Aliyataja mambo hayo ambayo ni pamoja na mgombea binafsi, viti vya wanawake kushindana katika majimbo, katiba kuruhusu mtu yeyote ambaye hajaridhika na matokeo ya rais kupinga pamoja na katiba hiyo kutamka wazi kwamba rais mteule lazima akubaliwe na walio wengi.
Wewe Kabisama usitudanganye, kama ni kibaraka wa Museveni useme tu. Vyombo mbalimbali vya habari dunia nzima vinasema uchaguzi haukuwa huru na haki, maana yake kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi, sasa tutajifunza nini katika hali ya namna hiyo?Hata kunafikiriwa watu kuingia mtaani kama ilivyo kwa Libya, Misri na Tunisia
ReplyDeleteTuache usiasa, tufanyekazi ya kweli kwa manufaa ya Waafrika Wazalendo.
Nitakubaliana na Kabisama ktk category moja tu! "System iliyotumiwa kuhesabu na kutoa matokeo" Tanzania ilitakiwa iige system hiyo, si kusubiri wiki unusu kukusanya matokeo yote! Vinginevyo Museveni ni fisadi tu!
ReplyDeletewanatudanganya tuu;huyo jamaa kaisha pewa chake anaropoka pumba tu ni wale wale tu,tuige vitu gani vizuri Uganda Museveni dictator tuu.
ReplyDeleteUchaguzi wa hapa Uganda wameiga mbinu zote za CCM za wizi wa kura. Juzi uchaguzi wa Meya wa jiji la Kampala umeahirishwa kwa sababu watu walikwenda asubuhi saa 1.00 kamili kupiga kura lakini walipofika tu vituo vilipofunguliwa kila kituo masanduku yalikuwa yamejaa kura zilizotikiwa tayari. Baada ya wapigakura kugoma uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa kura zilizokuwa zimetikiwa zilikuwa ni za mgombea wa chama tawala cha NRM Peter Sematimba. Sasa fikiria wizi huu. Mama Kabisama nimemwelewa sana amesema yale ya kujifunza ambayo hata mimi nakubaliana nayo ni:- Mfumo wa kuhesabu kura, Mgombea binafsi (kwani hata rafiki yangu hapa Keneth Kiyingi- ameshinda ubunge kwa mgombea binafsi), Viti vya wanawake kushindaniwa kimajimbo au kiwilaya, wenyeviti wa Halmashauri na mameya kuchaguliwa na wannchi wote na si lazima wawe madiwani. Haya ndio mambo mazuri tunayotakiwa kujifunza. Lakini kwa wizi wamekubuhu hawa jirani zetu. Nakumbuka andiko la mwalimu wangu Kamanzi - Crazy Gods of Tanzania a Lesson to Uganda. Sasa Dr. Kamanzi utabiri wake umefanikiwa maana jamaa hawa wamepata somo la kuiba kura na wamewazidi Miungu wajinga wa Tanzania.
ReplyDeleteDavie
Tunajaribu kutangaza kuwa tunamwelekeo mzuri wa kisiasa,hapana hatupo mia kwa mia nafikiri tupo asilimia 45% tu.Hatuwezi kuiga Uganda au kufananisha naMisiri,Libya Tunisia na kote kule kuliko na watawala wa maisha sawa na Uganda,mabadiliko ya viongozi ni muhimu na sio utitiri wa vyama uchwarana visio na muelekeo zaidi ya kuanzisha vurugu.Ukitaka kuona mabadiliko ya siasa tunahitaji angalau vyama viwili au vitatu hakuna wizi wa kura utatokea
ReplyDelete