10 February 2011

Sitta 'kuwajibika' kwa Edward Lowassa

Pia wamo Bernard Membe, Mwinyi na Nahodha

Na Waandishi Wetu, Dodoma

UCHAGUZI wa wenyeviti wa Kamati za Bunge umemrejesha Mbunge wa Monduli, Bw. Edward Lowassa kwenye uongozi ndani ya mhimili huo
akishika uenyekiti wa Kamati muhimu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayosimamia wizara nne nyeti, zikiwamo zinazoongozwa na aliyekuwa spika wa Bunge, Bw. Samuel Sitta na Bw. Bernard Membe.

Ukiacha Wizara ya Afrika Mashariki inayoongozwa na Bw. Sitta na ile ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa inayoongozwa na Bw. Membe, pia kamati hiyo ya Lowassa inazisimamia Wizara za Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa inayoongozwa na Dkt. Hussein Myinyi na ile ya Mambo ya Ndani ya nchi inayoongozwa na Bw. Shamsi Vuai Nahodha.

Bw. Lowassa aliyekuwa mjumbe wa kawaida wa kamati hiyo katika Bunge la tisa lililoongozwa na Spika Bw. Sitta, alilazimika kujiuzulu uwaziri mkuu baada ya kutajwa katika kashfa ya Richmond, hatua iliyosababisha Rais Jakaya Kikwete kuvunja Baraza la Mawaziri na kuliunda upya Februari 2008.

Kutokana na sakata hilo, Bw. Sitta na Bw. Lowassa wameendelea kuwa katika pande mbili hasimu, zenye mafuasi wanaopingana, hadi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanachotoka kikaamua kuunda Kamati iliyoongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi kuwapatanisha, hatua ambayo inaonekana haikuzaa matunda.

Kwa upande mwingine, Bw. Lowassa ambaye amekuwa akitajwa kusaka urais mwaka 2015, uchaguzi wa jana utakuwa umemkutanisha moja kwa moja na Bw. Membe ambaye pia anatajwa kujiandaa kuwania nafasi hiyo, safari hii wizara yake ikisimamiwa na kamati inayoongozwa na mshindani wake.

Kama harakati hizo za kwenda ikulu ni za kweli, Bw. Lowassa kwa nafasi hiyo atakuwa amelamba dume kwa kuwa itamwezesha kupata taarifa muhimu za Usalama wa Taifa, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Jeshi la Polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.

Mbali na Bw. Lowassa wengine waliochaguliwa kuongoza kamati ni pamoja na Bw. Mshirika wake wa karibu, Bw. Peter Serukamba atakayeongoza Kamati ya Miundombinu inayosimamia wizara za ujenzi na Miundombinu, Bw. Januari Makamba (Kamati ya Nishati na Madini) na Bw. Zitto Kabwe anaendelea kuongoza Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma.

Kamati nyingine ni ya Hesabu za Serikali za Mitaa itakayoongozwa na Bw. Augustino Mrema akichukua nafasi iliyokuwa ya Dkt. Willibrod Slaa kipindi kilichopita, Bi. Margaret Sitta atakayeongoza Kamati ya Huduma za Jamii na Bw. John Cheyo ataendelea kuongoza Kamati ya Hesabu za Serikali.

Kwa upande wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala mwenyekiti ni Bi. Pindi Chana na Kamati ya Maliasili na Utalii, Bw. James Lembeli.

14 comments:

  1. Ama kweli tumekwisha kama wenyeviti ndio hao wabunge tuliowachagua wameamua kuwapa sehemu nyeti mafisadi ok! wananachojali wabunge hao ni matumbo yao na si wananchi.
    yaaani wanadanganywa na pesa kwa ajili ya kuuza utu.

    ReplyDelete
  2. Changia hoja za msingi, hizo kamati ni za kawaida ndani ya bunge,wacha chuki binafsi wewe kama humpendi mtu bs ungetushauri au kutushawishi watu wa monduli tusimchaguwe kuwa mbunge wetu,Bw Lowassa ni mtu makini, mchapa kazi hodari,mwerevu na asiyependa makuu.wacha hizo fikra zako potofu haya mambo ya siasa tuachie wanasiasa na ikiwa ww ni vuvuzela kapigie uwanja wa fisi au wa mpira

    ReplyDelete
  3. jamani tunaipeleka wapi tanzania yetu yenye amani tujadili hoja na sio kupakan amatope kwamba maisadi sijui wanasiasa na mengineyo tuchangie hoja za msingi tuangalie uwezo na umakini wa viongozi hawa na sio kujadili upuuzi tuwachie wanakamati waendelee na kamati zao na matunda tutayaona. tusiwe na haraka ya kutoa yanayokuja mbele wala hatujajua hapa tulipo.

    ReplyDelete
  4. eng. mwakapango, E.PAFebruary 10, 2011 at 9:24 AM

    Ama kweli kina JOB NDUNGAI mnaipeleka nchi pabaya sana. mimi nilidhani kuwapa wapinzani kamati za fedha mnataka kutatua tatizo sugu la matumizi mabaya ya fedha za umma. aidha nilidhani wangechaguliwa watu makini na wenye uwezo,sauti na mamlaka ya kuhoji. tukianza kutoa hizi posts ambazo ndiyo checklists za utawala bora kwa watu ambao nynyi memewaandaa ni sawa na kumwandalia mtu leading questions na baadaye ukasema amefaulu vizuri jamani muwe na uchungu na inji hii. mtu kama Augustino Lyatonga amechoka sana lakini anatatizo kubwa sana lakuwa anapenda mno madaraka (power monger) na anapenda asikike yeye tu naikumbukwe alipokuwa waziri wa mambo ya ndani alijaribu kushinda madaraka ya rais wakati wa mrema umekwisha wananchi wa Vunjo walichofanya ni kumlipa fadhila na yeye sasa hivi haishi kutamani kwenda ikulu ya Dar kumpa data anayemwita rafiki yake Kikwete (sijui lakini) hivi kwa kumpa wadhifa ataweza kuhoji wakati ni mtoto wa CCM na analelewa naikulu ya DaresSalaam.CCM mmejiwekea kisu tumboni mkiyumba tu kitawachoma nyinyi wenyewe.
    mmejitahidi kuweka watu wataowasaidia msiyumbe tena na kudhoofisha nguvu za bunge kwenye utendaji. nimemsikia mtu mmoja anaitwa Geoge Simbachawene ni mchanga mno kwenye siasa anajaribu kuwakatisha tamaa wapambanaji na wanaharakati kama Tundu Lisu ambao hata ingekuwaje wasingeruhusu wapewe kamati hizo. simbachawene anadai yeye ni mwanasheria hajulikani lakini si hivyo tu wansheria wote huwaingii kwenye malumbano na mtu anayetetea hoja za msingi. angalie washeria makini inchini kama samwel sitta, Harrison mwakyembe,werema na wanakaa na wanapoambiwa watoe maoni regardless na tofauti za kiitikadi huwa wanasimamia ukweli Geoge Simbachawene au alisoma Lushoto nimejaribu kutafuta cv yake nimeikosa , usituharibie nchi kwa kuclaim unachosema. mwisho niwape pole CHADEMA hizi ndizo siasa za Tanzania na ndiyo maana hatuwezi kutatau matatizo kama ya Dowans, wachapa kazi wote wamekuwa wakiwekewa mizengwe na wengine kupoteza maisha yao kama Horrace Korimba na Edward moringe sokoine mungu azilaze roho zao mahali pema peponi. muwe wapya sasa na msikate tamaa Job Ndungai atashangaa mwaka 2015.

    ReplyDelete
  5. Fisadi ni fisadi tu hata umpake rangi ya kuvutia,lini Lowasa kaacha ufisadi?wananci wa Monduli wanamchagua kwani hiyo wilaya inaongoza kwa kiwango cha iliteracy ,hao wafugaji hawajui hata kinachoendela nchini wakiambiwa ukichagua upinzani nchi itaingia vitani wanaamini,unadhani Lowasa akigombea sehemu yenye watu wenye upeo atapita?nadhani hukumu ya wabunge wa CCM ni 2015,TUNAFUATILIA bUNGE ILI KWA MAKINI NA KUCHAMBUA NA KUJADILI HOJA WANAZOTOA. Mfano kwa kila aliyeangalia bunge la jana atakubaliana na mimi kwamba mbunge wa Nkenge hana chake 2015,huyu mama kwa kweli kachemsha alipochangia hoja na kuonyesha jinsi asivyo na uwezo kabisa,somtimes silence speaks louder than words,kuliko kuchangia upupu na kujidiscredit ni bora ukae kimya na changia pale unapokuwa na hoja nzito na za msingi,mfano mama Tibaijuka na elimu yake anakaa kimya na kuangalia hoja zinazotolewa.Mama Nshashu naona miaka mitano ni mingi mno sijui tufanyeje na kosa tumeisha lifanya wana Nkenge.

    ReplyDelete
  6. JAMANI TUMEKWISHAAAA!!!!!!!!!!MAKINDA NA NDUGAI MMETUMALIZA WATANZANIA...........HIVI ROSTAM ANAKUWA KWENYE KAMATI? MWIZI MKUBWA ATATUSAIDIA NINI KAMA SI KUWAZA KUHAMISHIA PESA ZETU OMANI!!ANGALIA HAYA MADUDU KWENYE KAMATI ZA FEDHA WOTE WALE WAPO HOI KWA CCM -ZITTO,MREMA NA CHEYO WOTE VIBARAKA WA KIKWETE AMA KWELI HUU MUHIMILI SASA KWENDA KUFA LALA!

    ReplyDelete
  7. Mungu ibariki Tanzania! Dumisha Uhuru na umoja, wake kwa waume na watoto, Mungu ibariki, Tanzania na watu wake, ibariki, Tanzania ibariki, Tanzania, tubariki, watoto wa Tanzania!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  8. Nguvu ya pesa inaonekana na jeuri ya pesa siyo lelemama. Hakuna lisilowezekana kama mtu unazo 'chenji'. Maumivu ya Wananchi yataendelea tu mpaka pale Watanzania watakapoamka na kusema INATOSHA. Kwa taarifa yenu tu leo hii Mheshimiwa sana Lowassa akisema anataka kuwa Rais wa Tanzania wenzake wa CCM watampitisha tena kwa kishindo kuliko hata 'Mheshimiwa sana'. Lowassa bado anazo busara ambazo zinawakuna sana wana CCM kwa hiyo ni lazima aendelee kutumika. Mwenye macho haambiwi tazama uozo uliopo nchini. 'Maumivu ya kichwa huanza polepole' Bei za bidha juu kwa juu, maisha ya Mtanzania mwendo mdundo. Tukimbilie wapi na Wabunge tumewapa wenyewe mamlaka ya kutowakilisha? Ebu tuamini japo kwa shida kuwa uteuzi wao ni wa 'Busara ya Nyoka'. Mungu atusaidie. Waliosababisha matatizo ya Umeme ni Richmond na Dowans na wamiliki wake tunawafahamu ndiyo hao waliowekwa ndani ya Kamati muhimu (Mambo ya Nje na Usalama). Sina Chuki na mtu yeyote ila ukweli ni lazima usemwe. Mheshimiwa Lowassa ni Mchapakazi kweli tena mtu makini sana, lakini pia ni Fisadi Mzuri tu kwani alihusika na uchakachuaji wa Umeme kwa kutuletea Richard MONDULI (RichMond) ili itupeleke tulipo. Hatujutii kwa kuwa tuliyataka wenyewe kwa kutokuwa makini katika maamuzi yetu na Wajanja wakajipatia 'MULO' kwa kutumia mgongo wa ujinga wetu. Well ni vizuri kwani msamaha upo kwa ajili ya wakosefu na huenda anaweza kuwa raia mwema iwapo chembechembe za kifisadi zitaombewa ba kumtoka vinginevyo maumivu yapo palepale tena kwa kasi maana ana usongo na wale waliomchafulia kujipatia Milioni 152 kwa kila siku iendayo kwa Mungu. Kumbukeni nini alichosema Mzee wetu wa Busara Mwalimu Nyerere kuhusu mtu huyu!! Alisema akimaanisha maana alikuwa na upeo wa kuona mbali sana. Wabunge wetu msituletee majonzi jamani tunahitaji kuhurumiwa na sasa ifike mahali tuseme inatosha kubebeshwa mizigo mizito na misalaba mizito namna hii.

    ReplyDelete
  9. Yangu Macho tu, nasubiri nione utendaji makini sio ubabaishaji-Mungi Ibariki Tanzania!!

    ReplyDelete
  10. Wabunge wa CCM kama hamna hoja za msingi za kuchangia bora mkae kwenye viti mbembee tu maana mnatuudhi sisi wananchi kwa vijembe na kejeli zisizo na maana wenzenu wa upinzani walichangia mambo ya maana na sio nyie mliokalia vijembe na kebehi ipo siku yenu na nyie mtakuwa mkizomewa kama wananchi msidhani kila mtu haelewi kinachoendelea tunawaunga mkono hao chadema kwa kutoka nje kwakuwa hawakukubalina na hayo yaliyokuwa yakiendelea au nyie mlitaka wanyanyue viti na kuwarushia kama kwenye bunge la KENYA? Hiyo ni demokrasia tena ya ustaarabu kabisa ambayo wameionyesha. Hivyo basi kama hamna la kuchangia mkae kimya tumechoshwa na kila anae simama kusema jambo hilohilo msidhani wananchi wote wanawapenda CCM la hasha hatuwapendi kwakuwa miaka 50 ya uhuru wachache mnaneemeka wengi tuna shida na wananchi wengi hawajui kukikuchwa watakula nini hivyo msijidanganye kuwa mnapendwa na hizo laana zenu mnazozitoa ziwarudie wenyewe kwa kutufikisha hapa watanzania (kwenye umasikini ulikithiri)

    ReplyDelete
  11. we mtu hapo juu nani ataondoa shida zako kama si ww mwenyewe mdomo unaumba utaendelea kuwa na shida mpaka kufa kwako mungu hajatuleta humu duniani tuwe nashidi huna dini soma neno achana na siasa utazikwa pekeyako huzikwi na mm shaurizako pole sana hayo siomaneno unayoyaumba kwako jisemee nafsi yako usisemee nafsi ya mwingine

    ReplyDelete
  12. Asalaam Aleykum wachangiaji wa mawazo murua kabisa katika gazeti hili la majira ambalo ni huru na linachaposha michango yote ya wasomaji.
    Kwanza nianze kuchangia kwa wale wanaomtukana na kumpinga Lowassa. Kumpinga mtu inaruhusiwa maana si wote mtampenda. lakini nataka niwambie ukweli tu kuwa hata mbingu zije mpya Lowassa ataendelea kuwa mbunge wa Monduli maana huko wamasai wanampenda, wanamwamini na kumwabudu. Muulize Sendeka atakwambia. Huyu ni kiongozi safi na ninauhakika kamati hiyo ataiweza sana.

    2. Pili nyie mliompa Ndugai onyo, mimi nawaunga mkono kabisa. Naibu spika huyu anamapungufu kidogo. Bahati nzuri mie natoka jimbo hilo la Kongwa. Nasikitika wale wakaguru na wagogo wa watu katika jimbo lile hawana mbunge. Isipokuwa wana mtetezi wa ufisadi. Fuatilia mivhango na kauli yake utagundua kuwa huyu hamnazo. Sasa mimi ndio namalizia shule hapa Sheffield nawaahidi na kumtahadharisha Bw. Ndugai anapaswa kunipisha 2015. Hee! nimo, naja, changamoto hiyo.

    3. Simbachawene nae alimwondoa bure Prof. Mwaga. Unaona hatari ya wapiga kura hawa wa kibakwe ambako hakuna maji, baraabara, hospitali wanamwacha Prof. wanamchagua huyu aliyefeli FTC pale Arusha Tech, akaishia kusaidiwa na Open University. Mtu anayesoma elumu Masafa siku zote anakosa mambo mengi kutoka kwa wanazuoni kwani yeye huishia na karatasi tu. ona hata michano yake ukiwamo huu wa juzi anaonyesha ni hamnazo, waingereza hapa wanaita "stupid"

    ReplyDelete
  13. NA LUWASA, TENE FISADI CCM MNA LENU, HAMNA MAANA MAFISADI WOTE

    ReplyDelete
  14. mambo ya ccm huyawezi,wamewin kutosa sita asiwe spika,eti wanataka jinsia.kumalizana tu,hawana jipya.huyo mmsai atakuwa kuwa tu mwenyekiti wa kamati,wala hawezi kumkontor sita kihivyo,hiyo rimoti hana,mwinyi kashindwa atayeweza wapi,siku zitaenda tu kiaina.

    ReplyDelete