LONDON, Uingereza
PAMOJA na Porto kufungwa wakiwa ugenini bao 1-0 dhidi ya Sevilla Jumatano katika mechi Kombe la Europa, lakini wamesonga mbele kutokana na
sheria ye goli la ugenini.
Klabu hiyo ya Ureno katika mechi ya awali ya mzunguko wa timu 32 iliibuka na ushindi wa bao 2-1, wakati juzi Sevilla ilipata bao lake pekee dakika ya 71 kupitia kwa Luis Fabiano katika Uwanja wa Estadio Do Dragao.
Porto ilionekana kama ingeweza kuvuka katika mzunguko huo mwanzoni mwa mchezo wakati Hulk, alipokuwa ana kwa ana na kipa wa Sevilla, Javi Varas lakini alikosa.
Fabiano alifunga goli baada ya mapumziko na mlinzi wa Porto, Alvaro Pereira katika dakika 72 alipewa kadi nyekundu kutokana na kucheza faulo ya kurukia miguu miwili, kitu kilichoongeza matumaini ya timu hiyo ya Hispania kutinga hatua ya mtoani ya timu 16.
Sevilla nayo ilianza kukata tamaa ya kusonga mbele kutokana na mchezaji wake, Alexis naye kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 77 lakini matokeo hayakubadilika.
Sevilla imeweza kuifunga kwa mara ya kwanza dhidi ya Porto kwenye uwanja wake katika mechi 29 za mashindano yote msimu huu, Porto wanaongoza Ligi ya Ureno kwa tofauti ya point nane mbele ya mabingwa watetezi Benfica na wanaizidi pointi 23 timu iliyo nafasi ya tatu Sporting Lisbon kwenye msimamo.
No comments:
Post a Comment