Na Grace Michael
SERIKALI imetakiwa kuangalia uwezo wa watendaji hasa walioko kwenye Halmashauri na Manispaa kwa kuwa mambo mbalimbali ya kimaendeleo
yanakwama kutokana na uwezo mdogo walionao.
Rai hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mbunge wa Jimbo la Temeke Bw. Abasi Mtemvu kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala wakati akichangia mambo yanayotakiwa kuboreshwa katika Wizara ya Menejimenti na Utumishi wa Umma.
Bw. Mtemvu alikwenda mbali zaidi kwa kutoa mfano wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ambayo yeye ndiyo ya kwake kwa kusema kuwa mambo mengi yanayotakiwa kufanywa kwa ajili ya maendeleo yamekwama kutokana na kukosekana uwezo wa kiutendaji.
“Wizara iangalie hata uwezo wa watendaji wetu hasa katika Halmashauri na Manispaa, matatizo mengi yanasababishwa na watendaji hao, mfano hapo kwangu Temeke mambo mengi yamekwama kutokana na hilo na ndio maana tunamkumbuka sana Marehemu Nyundo (Idd, aliyekuwa DED)ambaye aliifanya Temeke ikakimbia na sasa imesisima kabisa,†alisema Bw. Mtemvu.
Hata hivyo, Waziri wa Wizara hiyo, Bi. Hawa Ghasia alisema kuwa jukumu la kumwajibisha mtumishi asiyekuwa na uwezo liko ndani ya mamlaka husika lakini kwa kuwa limefikishwa mbele yake amelichukua na atalifanyia kazi.
Suala jingine ambalo lilisisitizwa na wajumbe wa kamati hiyo ni kuhusu maadili hasa uvujaji wa nyaraka za siri za serikali ambapo waliitaka serikali kuangalia namna ya kulidhibiti.
Jambo jingine ambalo lilihojiwa na wanakamati hao ni tatizo la kulipa mishahara wafanyakazi hewa ambapo Bi. Ghasia alieleza kuwa suala hilo linashughulikiwa na kwa sasa kinachofanyika ni kusafisha data ambapo kazi hiyo itakamilika ndani ya miezi miwili ili wabaki wanaotakiwa kulipwa.
Akizungumzia tatizo la upungufu wa wafanyakazi, alisema kuwa sekta zinazokabiliwa na tatizo hilo ni pamoja na elimu, afya na kilimo ambazo hata hivyo serikali imejipanga kulifanyia kazi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bi. Pindi Chana alisema kuwa wanachofanya kwa sasa ni kuangalia kazi na namna wizara zinazoangaliwa na kamati hiyo zilivyojipanga katika kufanya kazi zake.
kweli ndugu muandishi watumishi wengi wa serikali uwezo wao ni mdogo kiutendaji,inafikia wakati wanajiona kama wao ndio wamiliki wa hizo halmashauri kana kwamba hakuna utawala.leo hii utakuta hizi wilaya zipo nyuma sana hususani hio temeke ni aibu tupu ndugu muandishi.dhana mzima za hizi halmashauri imepotea na matokeo yake kama yanavyoonekana.wakati umefika sasa wa kuwaondoa watendaji wote wasowajibika na kuwaajiri vijana wapya ambao wapo wengi wenye sifa za kuweza kuongoza.leo hii ukienda katika nchi za wenzetu hayo unayoyaona unashangaa sana kwa hatua wanazopiga lakini kwetu sisi kila mmoja anataka kujiimarisha yeye binafsi.kwa mtindo huu hatufiki popote itakuwa kila kitu ni wahisani tu.tubadilikeni jamani hii ni nchi yetu sote na maendeleo yakipatikana ni yetu sote.TUAMKE SASA.
ReplyDeleteNamuunga mkono huyo ndugu yangu alotoa maoni yake kuhusu uwajibikaji wa halmashauri zetu.ni kweli sio siri hakuna uwajibikaji na sana sana watu wanasubiri mwezi ufike wavute mishahara pamoja na vikao vingi tu vya kupeana posho.leo hii wao ndio wa mwanzo kupinga uondowaji wa mabango kwa sababu posho za vikao hawatazipata tena.katika uendeshaji wa halmashauri serikali kuu huwa inatoa ruzuku kwa hizi halmashauri lakini ajabu hakuna kinachofanyika.basi afadhali wangekuwa wanatudanganya labda mwaka huu wangefanya kitu hiki na kile na mwaka mweingine vivyo hivyo lakini wapi!!!!!!!!!!hakuna wao kula tuuuuuuuuuuu.
ReplyDelete