24 February 2011

Sumatra yaonya daladala kupandisha kauli

Na Agnes Mwaijega

MAMLAKA ya Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imewataka madereva na makondakta wa daladala mkoa wa Dar es Salaam kutokupandisha
nauli kiholela mpaka hapo itakapowatangazia rasmi.

mamlaka hiyo imesema mpaka sasa nauli ya daladala nchini imebadilika kwa mikoa mitatu ambayo ni Tanga, Mwanza na Kagera tu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja wa Mawasiliano wa SUMATRA Bw. David Mziray alisema maombi ya kupandisha nauli ya daladala jijini bado yanashughulikiwa.

"Bado hatujatangaza nauli mpya, za zamani zitaendelea kutumika na tunaomba wawe wavumilivu mpaka SUMATRA itangaze rasmi.

"Tunaomba waandishi wa habari mtusaidie kuwatangazia ili waweze kutuelewa," alisema.

Alisema nauli ambazo mabadiliko yake yamekamilika ni za mabasi makubwa yanayoenda mikoani, ambazo zilianza kutumika juzi.

No comments:

Post a Comment