11 February 2011

Mbunge wa Arusha matatani bungeni

*Alitaka aelezwe adhabu waziri mkuu akidanganya
*Makinda amtaka kuwasilisha vielelezo Jumatatu


Na Kulwa Mzee, Dodoma

MBUNGE wa Arusha Mjini, Bw. Godbles Lema (CHADEMA) amemkoroga Spika wa
Bunge, Bi. Anna Makinda pale alipomuomba mwongozo wa nini mbunge afanye ikiwa kiongozi mwenye mamlaka makubwa bungeni kama waziri mkuu atasema uongo.

Mwongozo huo uliombwa muda mfupi baada ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kutoa taarifa ya mauaji yaliyotokea Arusha na Mbeya hivi karibuni, wakati akijibu maswali ya papo kwa papo na kukihusisha CHADEMA.

Kutokana na kauli hiyo, Spika Makinda alihamaki, akisema wabunge lazima wawe na nidhamu, kwa kuwa waziri mkuu ni mtu mkubwa, na kumkalisha chini, lakini baadaye alitoa alikampa mbunge huyo siku 4 kuanzia leo hadi Februari 14 awe amethitisha kauli yake kwa maandishi.

Tukio hilo lilitokea bungeni jana mara tu baada ya maswali ya papo kwa papo yaliyokuwa yakiulizwa na wabunge na kujibiwa na Waziri Mkuu, Bw. Pinda.

Swali lililoibua kasheshe hiyo liliulizwa na Kiongozi wa Kambi ya upinzani, Bw. Freeman Mbowe kwamba polisi wamekuwa wakipiga raia risasi na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa na serikali, na kutolewa mfano wa mauaji yaliyokea Arusha na Mbeya na hivyo kutaka kujua kama serikali inaweza kutoa tamko la kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Shamsi Vuai Nahodha na IGP Said Mwema.

Akijibu swali hilo, Bw. Pinda alisema serikali iko makini sana na jambo likitokea, wasikimbilie kusema serikali, ni vizuri kuulizana nani kasababisha.

Alisema katika mauaji hayo ya watu watatu, waliosababisha kutokea ni CHADEMA ambao walikataa kufuata makubaliano ya kufanya mkutano badala yake wakaelekeza wanachama kufanya maandamano.

Bw. Pinda alisema walikubaliana kufanya maandamano kwa kutumia ruti moja, CHADEMA walikataa ndipo serikali nayo ilipokataa kufuata wanavyotaka wao, waliruhusu kufanyika mkutano peke yake.

"CHADEMA walikaidi makubaliano hayo wakafanya maandamano ndipo baadhi ya viongozi wakakamatwa. Matamshi yaliyotolewa katika mkutano si ya chama chenye kujenga nchi, waliwaongoza wanachama waende kuwakomboa wenzao waliokamatwa kituoni wakati kituo
hicho ni kikubwa na kuna silaha," alisema.

Alisema katika purukushani za kuzuia kukifikia kituo hicho, ndipo mauaji hayo yalipotokea na kwamba endapo utaratibu waliokubaliana ungefuatwa mauaji hayo yasingetokea.

Majibu hayo ya Waziri Pinda ndiyo yaliyofanya Bw. Lema kwa kutumia kanuni namba 68 (7) kuomba mwongozo kwamba mbunge anawezaje kuchukua hatua kama mtu mwenye nafasi kubwa kama Waziri Mkuu anapodanganya Bunge.

Spika alimkatisha kwa mara ya kwanza kwa kumtaka aweke hoja hiyo kwa maandishi na kuonya kwamba wabunge wanatakiwa kutoa hoja kwa adabu.

Akifafanua suala hilo baada ya kipindi cha maswali na majibu, Bi. Makinda alirudia akisema, bunge linaanza kukosa adabu, alitumia kanuni ya 63 (6) inayosema mbunge atawajibika kuthibitisha aliyosema kwa muda aliopewa au kwa muda atakaopanga.

Bi. Makinda alisema katika kanuni ya 63 (8) inasema kwamba hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa atashindwa kuthibitisha ukweli spika anatakiwa kutoa adhabu ya kumsimamisha asihudhurie vikao visivyozidi vitano.

Baada ya kusema hayo aliinuka Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Bw. John Mnyika (CHADEMA) na kusema kwamba Bw. Lema aliomba mwongozo kwa kutumia kanuni ya 68 (7) hakusema kuhusu utaratibu, bali aliomba mwongozo ikiwa taarifa ya waziri mkuu si ya kweli, atumie utaratibu gani.

Bi. Makinda alijibu: “Nilisema atoe taarifa kwa maandishi, ndio hivyo nasema hadi Februari 14, mwaka huu kipindi cha asubuhi cha bunge awe ametoa maelezo ya waziri mkuu kusema uongo.”

Akizungumza nje ya Bunge, Bw. Lema alisema alichokisema ni sahihi yuko tayari kutoa maelezo Jumatatu.

Katika hatua nyingine, akijibu swali kuhusu uchaguzi wa meya uliosabisha mauaji hayo lililoulizwa na Bi. Martha Gumbula, Bw. Pinda alisema uchaguzi ulikuwa sahihi na matokeo pia yalikuwa sahihi.

Alisema kwa hesabu za kawaida hata kwa mtoto wa darasa kwanza wangewezaje CHADEMA kushinda wakati CCM ilikuwa na wajumbe 16, wenyewe 14 na TLP mjumbe mmoja.

Waziri Pinda alisema wajumbe wote walikuwa na taarifa kwamba Desemba 18 mkutano utaendelea lakini siku hiyo wajumbe walifika 17 ambapo CCM walikuwa 16 na TLP mjumbe mmoja, wajumbe kutoka CHADEMA walikuwa wakifika na kuondoka wakati taarifa na barua kuhusu mkutano huo walikuwa nazo.

Alisema katika mkutano huo, CCM ilishinda kwa nafasi ya meya na TLP walishinda unaibu meya, ilipofika saa saba mchana, Bw. Lema aliingia kwa ukali akitaka wafanye uchaguzi kumweka meya, ndipo polisi walipoingia kuwaondoa na mkutano ukaahirishwa. Baada ya hayo ndipo yakawepo maandamano ya kupinga matokeo hayo.

Tulisikia naibu meya alijitoa katika magazeti, hatujapata taarifa rasmi, tukipata taarifa rasmi kwa maandishi hatua zingine zitachukuliwa, alisema.

Wakati huo huo, Mbunge Samson Kiwia (CHADEMA) alimuuliza swali Waziri Mkuu kwamba wakuu wa mikoa na wilaya watawezaje kuwatendea haki wabunge wa upinzani wakati wao ni makada wa CCM.

Alisema Waziri Pinda kwamba mfumo wa serikali ulivyo ndivyo ulivyo, wakuu wa mikoa na wilaya watatekeleza ilani ya chama kilichoshinda.

Huwezi kuwalalamikia wakuu wa mikoa na wilaya, hawa wanatakiwa kusukuma maendeleo kwa ahadi zilizotolewa, alisema.

Akizungumzia hali ya chakula nchini, Bw. Pinda alisema itakuwa mbaya kwani bei zitapanda kutokana na kupanda kwa gharama za mafuta lakini serikali imejipanga vizuri kukabiliana na tatizo hilo, wakuu wote wa mikoa walishapelekewa taarifa, chakula kitumiwe vizuri na mbegu za muda mfupi zitapelekwa.

Waziri Pinda alisema hayo akijibu swali la Mbunge wa Wawi, Bw. Hamad Rashid Mohammed aliyetaka kujua hatua iliyochukua serikali kukabiliana na hali mbaya ya chakula inayosababishwa na hali mbaya ya upatikanaji wa mafuta ili kupunguza makali ya maisha kwa Watanzania.

44 comments:

  1. SERIKALI INGEKUWA MAKINI DOWANS ASINGEINGIA WALA MIKATABA MIBOVU KAMA YA RITES ISINGEKUWEPO. MATATIZO KAMA YA MFUMUKO WA BEI, UMEME,MAJI YANAONYESHA KUWA TUNA SERIKALI YA MAKANJANJA NA SIO WATU WALIOPO KWA AJILI YA MASLAHI YA TAIFA. NI WATU AMBAO WAPO KUJICHUKULIA CHAO MAPEMA.

    ReplyDelete
  2. spika wa bunge la tisa alionekana anaikoroga kwa kuibana serikali juu ya richmond, epa, na BOT; spika wa sasa anabariki akijaribu kuwaridhisha waliomuweka; ajihadhari hali itakuwa nguvu na baadaye atasalimu amri. amesababisha kuwepo kwa bunge lisilo na heshima, kuzomea ni kazi ya watoto wa shule za awali si wabunge. cha ajabu humo ndani ya bunge kuna wachungaji, na wenye elimu za uimamu lakini wanaruhusu kuwepo kwa uongo bila uoga na wanadhani wanaweza kuwaburuza watanzan; wakati huo umekwisha wasijidanganya.

    ReplyDelete
  3. Hivi kweli ikugundulika waziri mkuu amelindanganya bunge atafanywa nini? au anayetafutwa ni aliyesema PM amelidanganya bunge? sidhani kama kutatoka majibu ya kueleweka hapo kwakuwa madam spika mwenyewe alipandwa na jazba baada ya kuambiwa PM akilidanganya bunge inakuwaje, sidhani kama kutakuwa na hukumu ya kweli kwa hilo jambo.

    ReplyDelete
  4. Si huyo tu waziri mkubwa aliyetudanganya wananchi hata boss wake JK alitudanganya wananchi kwa kusema kuna maendeleo mengi yamefanywa na serikali yake ambayo hatuyaoni mathalani swala la umeme limekuwa kizungumkuti tuna miezi miwili tu ya kuwa na huo mgao wa umeme wataalamu wamesema hali ni mbaya sana tunakaribia kuwa gizani totoro wao wanasema kuna maendeleo ngeleja alisema mgao wa umeme kwisha, aah wapi mbona ni tabu na balaa tunashangaa unafanya nini badala ya kujiengua maana kazi ilishakushinda siku nyingi. Miaka 50 ya uhuru tunajifunia giza, maisha magumu watu hawana uhakika wa mlo hata mmoja kwa siku, elimu duni watoto wetu walalahoi wamefeli kwenye hizo shule za kata zisizo na walimu na maabara hapo ndio tuwapongeze eti mmetufanyia makuu nchi hii? nitoe angalizo kwa serikali amani ya nchi hii inadumishwa na wananchi wenyewe na sio nyie ccm mko wachache sana nchi hii tusio na vyama ndio tuko wengi kwahiyo amani ni sisi watz tulioidumisha na sio nyie na msiwe mnapenda kusema kuwa nyie ndio mnafanya amani iwepo, angalieni nchi za tunisia na misri wanacholalamikia wa rais wao ni sawa na matatizo tuliyonayo hivyo msiwe mnatudanganya wananchi kwakuwa tuna masikio na macho ya kuona kuwa nyie mnaishi ikulu, oysterbay, masaki, mikocheni na mnakula na kusaza wakati wengine hata hayo makombo hawajui watayapataje, tumechoshwa na uongo wenu wajibikeni na sio kutufanya sie hatuna akili mnapoomba kura (kula vizuri) kwa kuwagawia wananchi chumvi, kitenge au unga hayo ni matusi na hata haimpendezi MUNGU, au mnadhani Mungu wenu ni pesa zenu?

    ReplyDelete
  5. spika aliyeko bunge hili ni kama sanamu ya mwanasesele. hawezi chochote zaidi sana wabunge wataishia kupigana ndani ya ukumbi.

    ReplyDelete
  6. hivi mbunge kauliza utaratibu au kasema , maana mimi naelewa kauliza ikitokea suala kamahilo taratibu zinasemaje? mama apunguze munkari asihofu hao ni wabunge tu hata kama wanatoka upinzani na hasa Chadema asihofu. Angemjibu tu utaratibu and then huyo mbunge aseme sasa.
    Duu! kazi ipo

    ReplyDelete
  7. Inajulikana wazi kwamba watanzania tuna matatizo ya uchumi (Umasikini), lakini nadhani sasa tunaanza kuwa na matatizo ya akili, nadhani spika wa bunge hili ana tatizo la akili, mtu akiomba muongozo endapo spika endapo Waziri mkuu atalidanganya bunge ni kosa?, kwani haiwezekani kwa waziri mkuu kulidanganya bunge?, mbona ilitokea kwa mzee malicella hadi mwl. Nyerere akashindikiza ajiuzulu ? Kwa uelewa wangu wa darasa la saba (Lakini la zamani), Bwana Lema alisema "Endapo Waziri mkuu atalidanganya bunge" hakusema kwamba waziri mkuu amelidanganya bunge, kwa nini Annie Makinda akasirike kiasi hicho na kusema watu hawana adabu?.Atafanya hata sisi ambao ni wagumu wa kuamini maneno ya mitaani kwamba Sitta ameondolewa na yeye kupewa Uspika ni kwa Maslahi ya chama tawala tuanze kuamini. Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  8. mama makinda ni kero tu, mtu kaomba mwongozo, yeye anamwekea maneno mdomoni kwamba amesema Waziri mkuu kalidanganya bunge! Very stupid, nani kasema?. Nchi hii kero tupo bora kuwa mbwa ulaya kuliko kuwa mtz

    ReplyDelete
  9. Jana maza spika kalipuka,mbena yule kwa jazba ndo mwenyewe,bora angekuwa mama mongela huwa anacheka ndio anatoa kauli.ile hasira yote ya nini.kwani waziri mkuu hawezi kukosa,mtu mkubwa ndo nani nchi hii.wakubwa hao ndo wanatumaliza sisi wa chini,hawafikirii maslahi ya taifa,wanachuma wenyewe,hata huyo jk mwongo sana,eti hawahui dowans,baada ya kuona kina sita wamemkomalia ndo anadanganya wananchi hata yeye hawahui dowans,hayo ya akili kweli?si anatudanganya,sasa mwelezeni huyo maza spika hata raisi ni mwongo atafutiwe mwongozo,japo kura za kumtoa alipo.huyo maza asitishe watu.hasira za kukosa jimbo la arusha,kama waziri mkuu hasemi kwani polisi waliua watu,anapinda kama jina lake,mbona raisi alisema ni bahati mbaya?si aliona polisi walichemka,tusubiri hiyo jumatatu,apunguze mukari wa kibena sijui wa kihehe vile,atafute ushauri nasaha kwa walimtangulia hicho cheo.ngoja wazipige wabunge ndo atajua mbichi na mbivu.!!!!

    ReplyDelete
  10. kuweni na busara hujaambiwa kutukana toa maona wala hujaambiwa umkashifu mtu huo ni umasikini wa fikira wabongo mtazidi kuwa nyuma tu ya wenzenu kwa kujifanya mnajua sana na kubisha wakati hamjui kitu huondio ukweli mmezoea kuongea tu kama madem

    ReplyDelete
  11. Huyo jamaa hapo juu anasema eti tumezoea kuongea tu kama madem,hivi hajui hata huyo spika anayesemwa ni dem? Au akili za mchangiaji huyo ameziwekeza kwa mtu amshikie?

    ReplyDelete
  12. Huyu Godbless Lema ana ndoto za kula mchicha wakati unakula maharage. Yeye anadhani atakuwa waziri au katibu mkuu siku moja. Anafikiri nchi hii haina watu wenye diplomasia. yeye hana diplomacy hata chembe, kauli zake huwa ni zile za watoto wa vijiweni, majigambo, majisifu, dharau na kadhalika. Mpelekeni chuo cha Diplomasia ndipo atafaa kukaa bungeni otherwise, mnatwanga maji kwenye kinu cha mbao. Huyu kijana hafai shimoni wala mtini ni mhuni wa mitaani tu. Mtoto wa vijiwe, ndiyo maana akikaa na watu wenye hekima anajilingalisha nao maana hajui wenzie wako mbele yeye yuko nyuma. Elimu yake nayo naona ni ya kubabia maana mtu ukisha staarabika kwa kusoma au kuishi na watu wastaarabu huwezi ku-behave kama yeye. nimesha msikiliza sana sehemu sehemu kwenye vijiwe, yuko out spoken and he is too vocal, Bunge lote (mchanganyiko CCM na wapinzani) na Mama Makinda, kaeni chonjo na huyu jamaa. Ndiyo maana alisababisha watu kadhaa kufa Arusha na yeye na wenzie kuruka eti ni CCM, kweli Inzi anaweza kurukia kwenye tanuru la moto? mwana CCM gani angeweza kwenda au kukaribia kwenye maandamano ya chadema tena akiwemo yeye Lema? Hakuna, ni wao kwa wao. Mwogopeni kama ukoma huyu jamaa, I swear in the name of God, Lema is more than Tsunami. Yeye ni lethal injection kwa watu wenye hekima na busara.Watu hawajamjua huyu jamaa, wakimjua hawata msogelea kamwe. Believe you me.

    ReplyDelete
  13. huyo anayesema ni madem,kafilisika mawazo,huyo maza ni dem,na yeye ana dem,na sister zake ni dem,sasa dem wote ni feki, nammuliza.mtu akichemka anapewa ukwel na si kusema madem,una maana wote jinsia madem hawana point au,jipime,then pangua.

    ReplyDelete
  14. kwan madem(wanawake) sio watu? uliyetoa maoni kwamba "wabongo mmezoea kuongea kama madem" na wasiwasi na akili yako, wewe mwenyewe umezaliwa na madem(mwanamke) haafu leo una mkashif, ji heshim bwana.

    ReplyDelete
  15. wewe liotoa maoni kwamba "Huyu Godbless Lema ana ndoto za kula mchicha wakati unakula maharage. kijana hafai shimoni wala mtini ni mhuni wa mitaani tu" mbona baba salma ambae wewe unamwita rais ni muhuni wa mitaani?, tumecheza nae sana disko sinza, bilcanas, na kamnyany'anya mshikaji wang demu wake kisa alikuwa waziri, leo unasema lema muhuni. muhuni mwenyewe na rais wako.

    ReplyDelete
  16. NASHINDWA KUELEWA KWA NINI CCM WANASHINDWA KUELEWA KUWA KUCHAGUA NI UHURU WA MTU. CCM KUWA NA WAJUMBE ZAIDI YA CHADEMA SIYO KIGEZO CHA USHINDI. KWANI ALIYECHAGULIWA KUWA NAIBU MEYA ALIPITAJE? KWA KURA YAKE MOJA? MBONA HILI LIKO WAZI ZAIDI KULIKO HILO LA WAZIRI MKUU? NI AIBU KWA CCM, CHAMA AMBACHO KIMEKUWA MADARAKANI KWA MUDA MREEEFU, KUENDELEA KULAZIMISHA USHINDI MPAKA KWA KURASIMISHA MAMLUKI, HUO NI UVUNJIFU WA AMANI.

    ReplyDelete
  17. ndo hivo tena penye moto tunapenda kuongeza petrol, sishangAI

    ReplyDelete
  18. huyo anayekashifu madem,yeye kama dume ana demu au ana mke dumu na analala nae,na kama hana dem nae ni dume basi yeye ni SHOGA.ana maana anamwita mamake dem!asilete ushamba wa kudhalilisha jinsia,anatukana kuanzia maza wake,hadi nesi alomdunga chanjo,hadi mwl wake wa chekechea wote ni madem,asiduridie tena kudhalilisha mama zangu.kaishiwa point!

    ReplyDelete
  19. Wakati Anna Makinda anapewa Uspika nilijua hivi ndivyo atakavyoongoza, Tutalalamika sana, lakini ukweli utabaki palepale Makina uwezo wake ni mdogo sana, JK uwezowake pia mdogo, Watanzania kwa sasa kazi tunayo. Sikuzote mtu asiyekuwa na uelewa huwa anatumia nguvu zaidi, Ukitaka kuhoji risasi zinatumika, bungeni mtu anaomba muongozo kama kunaudanganyifu kifanywe nini kiongozi anasema hakikisha kama kunaudanganyifu, badala ya kujibu swali lililo ulizwa. Lazima tufike mhali tuamua Kusuka au Kunyoa. nchi yetu inaongozwa na watu wenye ulemavu w Fikra.

    ReplyDelete
  20. Haya! haya! Huyo ndiye Makinda bwana, mama wa hasira nyingi. Tafadhali! Mama, Uspika si lelemama. Ulipopandikizwa ukafikiri umeula, kumbe umeliwa. Bunge la safari hii lina changamoto si mchezo. Punguza lugha kali, hapo ni bungeni.Utafoka sana, ni vijana hao, na wana uchungu na nchi inavyopelekwa kifisadi -fisadi kwa maslahi ya jK, Lowassa, Rostam, na WEWE kama ahadi ulizopewa zinavyotanabaisha. Utakataa kuwa hukuahidiwa makubwa? Rostam alifuata nini Iringa kama si kukupa mkakati wa Uspika kwa vile walikwisha kuku-earmark!

    Mzee wa viwango na spidi alifiti kabisa kwa bunge kama la safari hii. Mhe. Lema ameomba mwongozo, Spika anasema ni utovu wa nidhamu, kisa, ni mbunge wa CHADEMA. Basi Anne, jitayarishe, kuna siku utaanguka kwenye kiti sababu ya jazba. Vijana watakukimbiza kweli safari hii. We haya tu, mimi nimekupa ushauri wa bure kabisa. TAFAKARI!

    ReplyDelete
  21. mAMA Anna Makinda punguza jazba!
    Chedema wajipanga vizuri tumia akili zaidi kuliko jazba na u-ccm. kwani waziri mkuu hawezi kusema uongo? yeye si mwanadamu kwa wewe tu?

    ReplyDelete
  22. CHADEMA WAO WANAONA WAKO JUU YA SHERIA.
    WABUNGE WA CHADEMA, WANACHAMA NA WAPAMBE WAO
    NI GEGE LA WAHUNI. RAIS FANYA KILA LINALOWEZEKANA KUPAMBANA NA GEGE LA WAHUNI WA CHADEMA.

    ReplyDelete
  23. Haya naona mmemaliza,naomba nitoeushauri japo kuwa siyo mama ushauri,wengi mliochanga mawazo yenu mna ushabiki ndani ya michango yenu.
    1.Spika pengine hakufurahishwa na Approach aliyoitumia mh.Lema labda naye aliuliza kwa jazba au kejeli.
    2.Kiuhalisia spika alitumia jazba kujibu hoja ya mbunge.[a]mbunge ana haki ya kuomba mwongozo juu ya asichokifahamu japo ana maandishi yake[mwongozo wa Bunge]
    3.Kama kiongozi mkuu wa bunge [impartiality and Justice]kwa wabunge ndiyo sifa kuu ya spika wa bunge.
    4.Ushauri kwa spika-Heshimu wabunge wote bila kujali tofauti za kisiasa.
    5.Siku zote simamia kwenye ukweli na haki.
    Mwisho usipofuata huu ushauri uongozi bungeni utakuwa mgumu na jumuia ya kitaifa na kimataifa tunahisi kuwa umeshindwa kuongoza Bunge letu.

    ReplyDelete
  24. Tatizo la nchi hii kwa kipindi hiki ni kumpata rais mwenye akili finyu. Tanzania imepotea muelekeo na sifa duniani kote tangu Kikwete alipoingia madarakani, huu ni mwanzo tu wa kipindi chake cha pili tumeanza kutukanana ndani na nje ya Bunge, sijui kama miaka mitano hii itaisha salama. mungu tusaidie tuvuke sala, hatuna rais wa kutuvusha. (Ikulu imeingiwa na Mhuni)

    ReplyDelete
  25. Wewe ndio mwenye akili finyu,Kikwete yuko safi,hivi mtu anayechangia mawazo kama mla unga ati anaita makinda "Maza" hawa ni pumba tupu. Zamani niliisha sema huyu Lymo hamna kitu humo na hafai kuwa kiongozi,huyu ni mhamasishaji tu kwa hilo anaweza lakini penye siasa hawezi huyu,alihojiwa na mwandishi wa habari kuhusu sakata hili la kuleta kwa maandishi ushahidi,ati anasema mimi siogopi mtu,looh aibu hii hana hata diplomasia,mambo ya kihuni aliyokuwa anafanya Arusha anafikiri bungeni anaweza kufanya? hao wachaga wawili Mbowe na huyo Lymo ni pumba tupu, ni wafanyabiashara wanaotafuta urahisi wa kupata mali kupitia siasa,cheo alichopewa ni kwa ajili ya uchaga wake tu lakini si kwa ajili ya uwezo wake,hapo bungeni kunaendeshwa na taratibu zake. nchi hii imeongozwa na Mzanaki kisha Mzanzibari kisha Mzaramo mpaka sasa tupo salama na Mungu apushe mbali hawa watu wa Kaskazini wakishika nchi tumekwisha tena hawana lolote zaidi ya kiburi na wizi kwa kisingizio ni wafanyabiashara wakubwa nchini,ni Mafia inaliandama Taifa letu,hawa itafika wakati watu watapotea kama Kenya kisha mnakuta maiti milimani,si watu wa kuachiwa nchi,subirini miaka mitano muone ndani ya chama chao moto utavyowaka

    ReplyDelete
  26. Wewe unaemkandia Lema ndio huna lolote ni sawa na Makinda ambaye hajui kishwahili. mh. Lema ameuliza endapo Waziri Mkuu atalidanganya Bunge kanuni zinasemaje alita mwongozo wa Spika. Sasa huyu madam anang'aka utafikiri Lema ametukana. Hata hivyo ni kweli kuwa Waziri Mkuu amedanganya kuwa watu waliouwawa walikuwa wanakwenda kuteka kituo. Hili si kweli kabisa hao polisi wake wamempa uongo. Waliouwawa wote hawakupo kwenye maandamano ya kwenda polisi bali mtu wa kwanza alipigwa lisasi akiwa eneo la jogoo House umbali wa kilomita 2 kutoka kilipo kituo cha polisi, wa pili aliuawa Kaloleni kwenye baa akinywa pombe umbali wa kilomita 1 kutoka polisi, na watatu yule mkenya aliuuawa eneo la Golden Rose akiwa na Kidumu chake cha mafuta ya kula. Hapo ni umbali wa kilomita zaidi ya 3. Hivi hawa ni kweli walikuwapo kwenye maandamano ya kuteka kituo? NILIMWAMINI SANA NA KUMHESHIMU MTOTO WA MKULIMA MH. PINDA LAKINI KWA HILI LA KUSHABIKIA DAMU ZA WATU WASIO NA HATIA NIMESHAMTOA MAANANI KABISA. SASA OLE WENU MWENZENU MBARAKA AMEONDOKA LEO BAADA YA SWALA YA IJUMAA KWA NGUVU YA UMMA. AMEBAKIA KIKWETE NAE ATAONDOKA MCHANA KWEUPE HIVYO PINDA UITAMBE SANA.

    ReplyDelete
  27. sasa tumeanza kuwa na wasiwasi na chadema kweli wapo kwa maslahi ya taifa hili na raia zake ,tunamashaka na viongozi wa chadema kama kweli wapo makini na sio waropokaji tu mwanzo wao unaashiria mabaya waswahili wamesema dilili ya mvua ni mawingu .waziri mkuu wa nchi ni kiongozi mkubwa wa nchi inawezekana kabisa kukosea sababu ni binadamu au inawezekana pia kuw amepewa wrong information, hio ikitokea sio mbunge kumtukana waziri ,kumwita waziri muongo hilo ni tusi kubwa kwa jamii yetu ya kitanzania labda ni seme hatujui mila na desturi za wenzetu wahuko kaskazini.dawa ya kosa si tusi bali nikuonyesha ukweli ulivo .Heshimuni watu ni nyinyi mta heshimiwa.chadema mnatupa mashaka sasa wapi mnaelekeo .upinzani sio matusi wala ngumi bali ni nguvu ya hoja .

    ReplyDelete
  28. Hivi kuuliza kwamba endapo waziri mkuu atakuwa amedanganya bunge ni zipi hatua za kufuata ni tusi? kama unakubali kwamba hata waziri mkuu ni binadamu anaweza kukosea, sasa Lema angeulizaje? hebu tusaidieni wengine kiswahili tulikutana nacho tulipoingia mjini.

    ReplyDelete
  29. Ulitegemea nini kutoka kwa spika ambae kawekwa hapo na mafisadi. Tunajua kwamba aliagizwa kuchukuwa fomu; binafsi hakuwa na ubavu wa kushindana na Sitta. Lakini kwa kuwa CCM inaendeshwa na akina Rostam; waliweza kumweka kwa maslahi yao. Sitta alikuwa mwiba ubavuni mwao.

    Madam spika iko siku tutakuuliza wewe unafanya haya kwa niaba ya sisi wananchi au kwa niaba ya nani? Siku hiyo hawatakuwepo waliokuweka bali wewe mwenyewe. Zinduka usitumiwe bila kujijua, ghadhabu ya wanachi na laana visikushukie.

    ReplyDelete
  30. WABUNGE CHADEMA MSIFE MOYO, WATANZANIA TUNAJUA MAFISADDI WANA CCM NA KIONGOZI WAO FISADI JK WANAHILA, WAMESOMA UJUMBE WA EU WAMESHIKA VIDOMO VYAO VYA CHINI, SASA NGUVU TUNAYO YAKUPAMBANA NA MAFISADI CCM, HATAKAMA NI KWAJASHO, MILIIBA KURA NA KUJAZA MATUMBO YENU KWA KUWAGANDAMIZA WANYONGE. HERI KUPOTEZA AMANI YA KUJISINGIZIA HUKO WALALA HOI WAKITESEKA KULIKO KUENDELEA KUWA NA MAFISADI WA CCM WASIO FAA WALA KUONA UCHUNG KWA VIFO VYA RAIA WASIO NA HATIA. HATA WAZIRI WAO KUSUBUTU KUUNGA MKONO KUUWAWA KWA RAIA NI AIBU KWA SERIKALI BUTU YA CCM. TUTAWATOA MADARAKANITUUUU.

    ReplyDelete
  31. jambo nzuri ninaloliona hapa jamvini ni kwamba angalau wengi wetu tunakubaliana kimsingi kwamba ni muhimu kuiondoa serikali iliyopo madarakani, pia kimsingi tunakubaliana kwamba njia ya kisasa "and most effective and safe way" ni kutumia Nguvu ya umma kwa maandamano si ndio watanzaia wenzangu? kama mnakubaliana na sisi kuhusu hili naomba mseme ili tuanze hatua nyingine ya kufikia hazma yetu.
    Quote

    ReplyDelete
  32. the time has come;
    Wapendwa WATANZANIA wenzangu, tumeona haya yanawezekana, kama mmekuwa mkifuatilia comments zangu, mimi naomba jambo moja tu kwa wasomaji wa Gazeti hili, we can encouraging people to the big issue through a number of ways, karibia wanafunzi wote siku hizi wanaosoma ama waliomaliza vyuo wana email ama wako facebook, lets start spreading the news and open forum how best we can ask the government to step down, and give our Tanzania back. Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  33. tutahakikisha nchi hii haitawaliki,hayo yalikuwa maneno toka mdomoni mwa kiongozi wa kitaifa wa Chadema mheshimiwa sana Ndesamburo Arusha walipowaua watanzania wasio na hatia. Huyo Lema kwakweli anasikitisha sana lakini ni kijana wa kijiweni tu, hata maneno anayotumia nikama ulimbukeni fulani, kama watanzania ni wafuatiliaji wa mambo hasa haya ya kisiasa mtakubaliana na mimi kwamba Chadema wapo kwa ajili ya kundi fulani ambalo lipo nje ya nchi likitoa maelekezo na kufadhili kile kinachotolewa maelezo, kilichowaumiza zaidi ni kule kuikosa ikulu 2010. iwe isiwe agizo lililokuja ni kuhakikisha nchi haitawaliki. watanzania tuwe macho sasa amkeni Upole Ukimya wenu mwishowake damu itamwagika. Huko Bungeni ndiko kwenye kushikishana Adabu kwanza na 2015 tunaagana nao kwa amaNI.

    ReplyDelete
  34. Hivi hawa wanafiki wanaoikandia CHADEMA ama viongozi wake ni watanzania kweli? Nilidhani watakosoa hoja na siyo mtu ama chama. Kweli wengi wetu tunaufinyu wa kufikiri. Nchi hii si ya CHADEMA, CCM ama chama chochote, hivyo kila mtu anahaki ya kuhoji maswala yenye mustakabali kwa taifa. Tuache ushabiki na tuijenge nchi yetu

    ReplyDelete
  35. CCM ina hasira kwani wanajua hii miaka mitano ndio mwisho.

    Lema yuko sahihi,serikali yetu imelala fofo ,umakini ni zero kama wangekuwa makini EPA,BOT,RICHMOND&DOWANS zingetupata? wangekuwa makini mbona wanapindisha sheria kila siku hasa za uchaguzi? wangekuwa makini uchafu usingezagaa mitaani vibao vimelala barabarani hadi tumekuwa nchi ya takataka wanabaki kusifia nchi za wengine mara o rwanda pasafi mara uchumi wa rwanda uko juu!!!!!!!!!!!ccm hao tulishawajua!!!!!!!!!!!!!!Acheni jazba pinda unapoteza mwelekeo kiasi cha kutojua hata sheria za uchaguzi wa meya!!!!!!!!!! KATIBA MPYA NDIO DAWA YA KUWANYOA................

    ReplyDelete
  36. achane kuongea,fanyneni kazi.

    ReplyDelete
  37. 0 #76 Evance 2011-02-13 08:09
    kinachoonekana hapa ni wananchi kuchoshwa na maisha magumu ya kutokuwa na maendeleo ya mtu mmoja mmoja hasa vijana hali hii inasababisha vijana kuvaa ngozi ya chui na kuamua chochote kitakachokuwa na kiwe hivyo wanaamua kuanza kuingia mtaani ili kudai maslai ya kwa nguvu hali ambayo inakuwa ngumu kukubalika kwa mara ya kwanza lakini jinsi mda uanavyozidi kwenda ndo hali inavyoonekana kukubalika na watu wengi na kuungwa mkono na makundi yote ya kijamii sasa mimi kwa upande wangu naona hali kama hii inaweza hata kutokea katika nchi zetu kwakuwa watu maisha ni magumu hasa vijana itafika mahali watu wataamua kuingia mtaani ili kutafuata mabadiliko kama serikali yetu itendelea na mambo jinsi yanavyoendelea basi tusishangae kuona kilichotokea Misri kutokea hata hapa kwetu kinachotakiwa kwa seriukali yetu ni kuhakikisha kinazitumia rasilimali za nchi yetu kwa ajili ya maslahi ya nchi yetu na si vinginevy haya mabadiliko yamewaonyesha watanzania kuwa kumbe nguvu ya umma ni kubwa kama kila mtu taamua kutafuta madadiliko kwa nguvu.

    ReplyDelete
  38. nahisi mzee pinda anapinda siku hizi. nilitegemea atoe majibu yenye kumsaidia mtanzania, na sasa anatoa majibu yenye kuisaidia ccm pasi na kuleta tija kwa watanania. wacha kupinda mzee pinda. nilidhani utaweya, kumbe hakuna kitu.

    ReplyDelete
  39. Watanzania wenzangu mbona mnalumbana kufikia hatua ya kukashfiana? tatizo ni udini miongoni mwa viongozi wakuu wa nchi.Ni kwamba ukristo unataka utawale nchi zote duniani kupitia sera za nchi za Magharibi na sio kitu kingine, hakuna kibaya zaidi alichokifanya Rais Kikwete na serikali yake kuliko serikali ya Marekani inayoua watu bila makosa kila siku .ni kwamba majasusi wa kikristo waliojipenyeza kushika uongozi ndani ya serikali na vyama vya siasa ndio wanaochochea vurugu katika nchi nyingi duniani ni mashetani wakubwa wanaopenda kuchukua madaraka kwa kuchochea fujo ndani ya jamii zetu.kama hutaki ubishi kwa hili fanya utafiti katika serikali zote duniani, ajabu baadhi ya wasomi wanakuwa na haraka ya kuwaunga mkono kwa ubaguzi mkuu wa aina hii, nchi zile zinazofuata sera za magharibi hazina fujo.hivi kama leo Tanzania tatizo ni umaskini ndiyo sababu za fujo,Misri kuna nini? hata haya masuala ya ufisadi yanapikwa kupita kiasi utadhani wenyewe ni wasafi, wanafurahi kugonganisha watu ili wauze silaha zao wamwage damu, mashetani wao wafurahi lakini wote watafikiwa na hukumu wa Mungu,ndugu zangu mimi ni mkisto lakini siungi mkono jinsi ambavyo World christian Council(Wcc)na jumuiya zake za National Christian council(Ncc)katika kila nchi inavyoshiriki kwa siri katika mapinduzi ya kisiasa duniani hasa kwa nchi ambazo serikali yake haitokani na Ukristo, hii ndiyo siri iliyoingia Tanzania. tabia yao moja kuu ni kujipendekeza kwa umma iwaunge mkono kwa mambo ya kupikwa kwa ustadi wa ujasusi wao ndani ya serikali jambo hili ni sharti itokee ni lazima itimie kwa sababu yametabiriwa katika vitabu vitakatifu.wanaoshabikia Mapinduzi hayo watashuhudia matokeo ya yale wanayochochea.hii ndio siri ya Chadema kwa Tanzania ndio sababu haitaki kuwa pamoja na vyama vingine.

    ReplyDelete
  40. Mtoa comment hapo juu hujasema kitu chochote cha maana kinachoeleweka cha kuweza kumsaidia mtanzania wa leo. Hakuna kitu kibaya kama kutokumdhamini mwenzio kama mzalendo. Afrika ya leo sio Afrika ambayo mungu aliibariki akaipa kila kitu kwa ajili ya maisha ya watu wake. Ndugu yangu unaposema udini hujajenga bado unazidi kupotosha jamii ya watanzania kutoka na ninavyoijua na tunavyoishi kama ndugu na mungu atakuhukumu kutokana na ushawishi wako unavyoutumia kuwanyima fursa ya kutafuta tonge ambalo wameshanyimwa wakachukua mafisadi.

    Hakuna mtanzania anaweza kukujibu lakini mungu atakujibu kutokana na hali ya maisha yalivyo sasa hivi. Fikiria mtu anakubali kusoma ili akijua atapata kazi na kuitumia elimu aliyoipata kwa watu wengine lakini kwa serikali yetu nini kinachofanyika hakuna. Tuchukue mfano mzuri tu ambao JAPANI waliweza kuutumia na waliweza kufanikiwa kwa asilimia mia moja na wanatikisa dunia. Sasa hivi wanasema ni kuiba TECHNOLOGIA sio kuonyeshana ubabe au kukomoana hatumkomoi mtu ila tunajikomoa wenyewe.

    Mfano tu mtu anamaliza masomo hapa nchini au nje ya nchi anaona kuliko kurudi TZ niafadhali kubeba mabox kuliko kurudi nyumbani sasa ile elimu amesamo kufanya nini. Tunataka Tz ijenge na kila mtu aitamani kusiwe na tamaa ya kufanyia watu wengine kazi wakati nchi yetu inahitajika kujengwa.

    Kubadilisha chama sio ugomvi wote wanatafuta kuifufua TZ yetu wote. Ugomvi wa watanzania sio kwa Kikwete kwani kikwete kafanya nini? Tatizo ni chama sio Kikwete muelewe. Mh Kikwete hana kosa lolote ila nyinyi watendaji wake mnaotuandikia Comment kama hizi. Sisi tunamlinda Mh Kikwete na wala asikimbie ila tu kibadilishwe chama. ASANTENI.

    ReplyDelete
  41. Poleni wana-jamvi wote. Mmeyaona ya Musa tu, subirini ya Firauni mwaka 2015 atakapopewa nchi mtoto wa Kimeru aliyekimbilia Monduli akitokea sehemu inayoitwa "Kwa Pole" (Chama cha Ushirika Nkoanrua, barabara ya kwenda Arusha ukitokea Moshi). Si mmeona kaanza na u-wenyekigoda wa kamati ya kumdhibiti na kumwadabisha Mzee wa Spidi na Standards! Hivi mnafikiri kawekwa kwa ajili ya nini? Ki-strategically zaidi!

    ReplyDelete
  42. Waziri Mkuu simuelewi anaposema CCM walikuwa kumi na sita na TLP mmoja kwa hiyo chadema wasingeshinda.Huyu wa TLP alipata kura za nani mpaka kupata Unaibu Meya wakati alikuwa mpinzani.Wapende wasipende waliharibu uchaguzi makusudi na ili kuweka mambo sawa uchaguzi urudiwe tu.Wanaogopa nini na wao wapo wengi?

    ReplyDelete
  43. Pumba tupu Bar ya Goldern Rose iko kilomita tatu toka kituo cha polisi? Pumbavu mmoja wewe au hujui vipimo?

    ReplyDelete
  44. Wewe unayejua idadi ya madiwani hebu tupe takwimu zako utuambie Chadema ina madiwani wangapi? ututajie na sehemu. mficha uchi hazai

    ReplyDelete