LONDON, Uingereza
KIPA wa Liverpool Pepe Reina, mwenye thamani ya pauni 20, juzi alifungua milango kwa Manchester United.Reina alikataa kuhamia Old Trafford
mwishoni mwa msimu uliopita.Wakati Edwin van der Sar anatungika glovu zake, kumekuwa na uvumi kwamba kocha wa United, Alex Ferguson atajaribu kumchukua Reina kwa pauni milioni 20 kwa kutumia kipengele kilichopo kwenye mkataba wake.
Kipa huyo alisema kuwa milango iko wazi kwa United, wakati akizungumza na kituo cha redio cha Onda Cero, ambapo alisema uhamisho unaweza kutokea.
Alisema: "Ndiyo, Van der Sar atatungika glovu."Siwezi kufanya chochote, siwezi kusema kwa kuwa nina mkataba wa Liverpool.
Reina pia alishindwa kueleza kuhusu uwezekano wa kuondoka Anfield, kama Liverpool itakuwa nje ya timu nne za juu.
Alisema: "Siwezi kuongopa, ninataka kucheza katika Ligi ya Mabingwa na kuwania makombe.
No comments:
Post a Comment