*Wahofia 'ya Tunisia, Misri' endapo italipwa mabilioni
*Lipumba ataka waliosababisha kashfa hiyo wawajibishwe
Na Heri Shaban
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimefanya maandamano makubwa jijini Dar es Salaam na kutoa tamko la
kupinga malipo ya sh. bilioni 94 kwa Kampuni ya Dowans na kutaka waliosababisha kashfa hiyo kuwajibishwa.
Maandamano hayo yaliyoongozwa viongozi wa ngazi ya juu wa CUF na kumshirikisha Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Bw. Ambar Haji Khamisi, yalianzia Buguruni Sheli hadi Viwanja vya Kidongo Chekundu jirani na maeneo ya Mnazi Mmoja.
Walikuwa wamebeba mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali wa kupinga malipo hayo, yakiwamo, 'CCM chama cha mafisadi', 'Yaliyotokea Tunisia yatatokea hapa kwetu endapo fedha hiyo italipwa' na 'Bei ya mkate 750/ badala ya 300/ baada ya bei ya umeme kupanda'.
Maandamano hayo yaliongozwa na polisi wa kawaida na wale wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakiwa hawana silaha.
Akitoa tamko hilo baada ya maandamano hayo Mwenyekiti wa chama hicho, Prof Ibrahim Lipumba alisema CUF inapinga kulipwa kwa fedha hizo kutokana na kuwa zinahitajika katika matumizi mengine kama elimu, afya, maji ufuaji na usambazaji wa umeme.
"Nchi yetu hivi sasa inakabiliwa na mgao mkubwa wa umeme ambao ni mkali kuliko ule 2006, umeme unafuliwa haukidhi mahitaji. Tunaambiwa maji katika mabwawa yanayofua umeme yamepungua sana.
"Tatizo hili ni la muda mrefu Watanzania wana kila sababu kukasirishwa na mgao huu wa umeme kwa miaka mitano baada ya mgao wa 2006 na kuahidiwa na serikali kuwa mgao huo utakuwa ni historia," alisema Prof Lipumba.
Alisema athari za umeme ni kubwa kwa kuwa wananchi wanasumbuka vyombo vya umeme maofisini na viwandani vinaharibika kwa sababu ya ukataji wa umeme wa mara kwa mara shughuli za uzalishaji bidhaa na utoaji huduma zimeathirika na ajira zimepungua.
Alisema kuwa wawekezaji wa ndani na nje wanasita kuwekeza vitega uchumi na hivyo kuongeza ajira kwa sababu ya kutokuwa na umeme wa uhakika, umeme ambao ndio nishati kuu kwa kuwa matumizi ya mitambo viwandani na majumbani ili kupunguza matumizi ya nishati ya mkaa kwa lengo la kulinda mazingira.
Prof Lipumba alisema uzalishaji wa umeme nchini kwa asilimia 90 unategemea maji ya mvua hivyo isingekuwa tatizo iwapo kungekuwa na hifadhi ya maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme yangekuwa ni ya uhakika kwa bahati mbaya uhakika huo haupo kwa sababu ya maji
"Nchi yetu imejaliwa vianzo vingi vya nishati ya umeme maeneo ya maporomoko ya maji yakitumiwa yote yanaweza kufua umeme wa MW 5,000 ilinganishwa na uwezo wa sasa wa MW 562 na umeme wa gridi ya taifa MW 791 makaa ya mawe yamegundulika yanaweza kufua umeme wa MW 1,000 kwa zaidi ya miaka 50 ijayo," alisema Prof Lipumba.
Alisema kuwa gesi iliyogundulika Mnazi Bay, Mtwara; Mkuranga, Pwani na Songosongo, Lindi inaweza kufua umeme wa zaidi ya MW 1,000 kwa zaidi ya miaka hamsini ijayo, pia madini ya urani (uranium) yaliyogundulika Namtumbo na Manyoni nayo yana uwezo pia wa kufua umeme.
Chimbuko la Dowans
Akielezea chimbuko la kampuni hiyo, Prof. Lipumba alisema kuwa Dowans Holdings SA ni Kampuni iliyoanzishwa Julai Mosi 2005 chini ya sheria za Costa Rica.
Alisema kampuni hiyo haina raslimali nyingine isipokuwa Dowans Tanzania Ltd, iliyoianzisha Novemba 28 2005 na ilimpa mamlaka ya kisheria (Power of Attorney), Bw. Rostam Azizi kuendesha shughuli zote za Kampuni ya Costa Rica ikiwa ni pamoja kufungua, kufunga akaunti za kampuni na kutia sahihi hundi za kampuni.
Alisema mamlaka aliyopewa Bw. Aziz ni makubwa kwa kuwa yanampa uwezo wa kusimamia na kuendesha kampuni hiyo kama mali yake.
Alisema kampuni hiyo ilisajiliwa Costa Rica siyo kwa madhumini ya kufanya biashara bali kuitumia kampuni hiyo nje ya nchi hiyo na wamiliki wao wasijulikane.
Na nyie sasa hayo maandanmano yenu hayana maana, juzi Raisi ameshafafanua kuhusu suala hilo, au hamna kazi za kufanya.
ReplyDeleteNaunga mkono maandamano ya CUF, Vinginevyo Rostam ataimaliza nchi yetu. Keep it UP. Hakuna kurudi nyuma.
ReplyDeleteCUF nyie wanafiki mara CCM mafisadi wakati chadema walipotoka bungeni mlishangilia na wenzenu wa ccm na mkahamia viti vyao..............nyie hamna jipya kwani nawaona kama wote MAFISADI kwani mngekuwa si mafisadi msingeungana na ccm kuishambulia CHADEMA AMBAE NI MKOMBOZI WETU watanzania
ReplyDeleteMimi naona CUF wanafuata bendera ya fuata upepo kwani Chadema walishaomba maandamano hayo wakanyimwa , mimi ninomba isiwe CUF wala CHadema kuandamana bali watu wote wenye nia na kuipenda nchi kuwa wote tuandamane mpaka rais aondoke maana anasema eti hawajui wamiliki wa Dowans kama kweli ni rais kuna kitu hakijui. inamaana yeye hashirikiani na viongozi wengine wa juu ambao ni wazaidizi wake. basi aondoke na tufanye uchaguzi upya au Dr Slaa aapishwe kama mshindi halali wa uchaguzi 2010 maana nchi haitakalika endapo kikwete aliingia kwa njia ambayo inamchukiza Mungu lazima apate cha moto na kuondolewa na Mungu mwenyewe.
ReplyDeleteRais Jk Naomba uwaachie nchi maana miaka mitano tumekupa ndio majuto tunayopitia na sasa umeingia kwa mara ya pili ukame na matatizo mengi yameongezeka, ina maana hamsikii sauti ya Mungu anapowaonya kwa mifano au mnataka awafanye kama Nebukardresa ndio muende madarakani?
ReplyDeletewatanzania wa bara tuwemakini na cuf,au kuwepo na cuf zanzibar na cuf tanzania bara wala haitaji elimu ya darasa la saba kujua hili, kwa hivi sasa cuf ni chama cha ccm B,mhe lipumba wewe ni msomi ni aibu kufahamu ukweli na hukaunyamazia,siku inakuja wana cuf wataunda cuf yao ya bara.ndoa yenu na ccm ni shinigizo kwa manufaa ya cuf zanzibar.hivi sasa mnawabeza chadema kwasababu mko na ccm...yetu macho haya...
ReplyDeleteHivi nyie wendawazimu wa Chadema,mlitaka nyie mkitoka bungeni na cuf wawafate,CUF sio makondoo wa Slaa,Mbowe na Ndesamburo na baba yao Mtei,kila chama kina maamuzi yake na kama kweli wazo la mjinga mmoja hapo tuandamane kwa ajili ya umeme tusiangalie chama tuwe kama wazalendo ulikuwa na haja gani ya kuishambulia CUF.KWA TAARIFA YENU CUF NDIO CHAMA MAKINI PEKEE HAKINA HARUFU YA UFISADI KATIKA NYOYO ZA VIONGOZI,HIVI WAJINGA NYIE MNAWEZA KUMFANANISHA MBOWE NA LIPUMBA? MBOWE NA JAMAA ZAKE WANATAKA IKULU KWA BIASHARA ZAO KWANI TAYARI WAO NI WAFANYABIASHARA KAMA WALIVYO CCM, CUF HAMNA WAFANYABIASHARA NA HAPA PAKIPATIKANA KIONGOZI KAMA LIPUMBA BASI MAMBO YANAWEZA YAKABADILIKA,TUKAPATA NYERERE MWINGINE LAKINI HAO NYAMAUME WA CHADEMA HAWANA TOFAUTI NA CCM WANAGOMBEA KWENDA KUPEANA TENDA HUKO IKULU. WEWE UKIONA MCHAGA ANALIA NA KUSIKITIKIA WIZI UJUE HAPO KAZIDIWA KETE. PROFESA LIPUMBA HANA HAJA NA UTAJIRI,ANA FAHARI NA USOMI WAKE AOENYESHE NJIA,NI MTU ANAEPEWA KAZI HATA ZA KIMATAIFA ZA RESEARCH,TUAMBIENI MBOWE KAFANYA JIPI,TABIA YA KUJARIBUJARIBU VIONGOZI NDIO ILIOIANGUSHA NCHI HII,SASA MTU KAMA MBOWE TUMPE UONGOZI KWA LIPI LA KITAIFA AU LA KIMATAIFA ALILOLIFANYA? SASA HIVI NDANI YA MITANDAO YA INTERNET KUNA UMAFIA MKUBWA UNAFANYWA NA WANASIASA HASA WA CHADEMA KWA KUWEKA WATU WAO SAA ZOTE KUWASHAMBULIA WATU WALIO AGAINST NA MAWAZO YA MABWANA ZAO.
ReplyDeleteWEWEEE!!!!! acha kupotosha umma na upupu wako. Nyie fajilieni CCM tu, yetu macho. Mimi sina chama lakini ukiniuliza kama kuna chama cha upinzani kinachoitwa CUF mimi sijui. Ila jana niliwaona wanaserebuka taarabi na mdundiko kule kodongo che kundu.
ReplyDeleteCUF ni popo, huku bara wanalilia kambi ya upinzani bungei, kule visiwani wana ndoa na CCM. Vipi, mbona mmepoteza mwelekeo?
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteWANAOPINGA MAANDAMANO NI MAKATIBU KATA. MAKATIBU KATA NI WAAJIRIWA WOTE WA SERIKALI AMBAO AJIRA ZAO NI KUTOKANA NA KUWA NA BABA, MJOMBA, SHANGAZI, BINAMU N.K. AMBAO WANAWATENGENEZEA POSTI HATA KAMA SIFA HAWANAZO.
ReplyDeleteHAWA MAKATIBU KATA HAWANA HILI WALA LILE, WANA HOOF KUBWA KUWA MAMBO YAKIGEUKA HAWATAKUWA NA PA KUJISHIKA. HAWANA ELIMU YA KUTOSHA, WALA UWAJIBIKAJI. WANAOGOPA WIMBI LA MABADILIKO AMBALO AIDHA LITAWASHINIKIZA KUACHIA NGAZI AU KUWAFANYA WAWAJIBIKE KITU AMBACHO HAWAKIPENDI.