05 January 2011

'Watanzania wafahamishwe umuhimu wa elimu huria'

Na Mwandishi Wetu

VIONGOZI wa serikali na vyama vya siasa wameombwa kutambua mchango mkubwa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambacho sasa kimefikia udahili wa
wanachuo 35,000.

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Tolly Mbette wakati wa maafali ya chuo hicho yaliyofanyika mwishoni hivi karibuni kampasi ya Mbeya.

Prof. Mbwete alikipongeza chuo hicho kwa mchango wake mkubwa kikiwa chuo cha tatu kuanzishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

"Inafaa sasa, kwa maslahi ya Taifa wao wawe mstari wa mbele kuwajulisha watanzania kuhusu umuhimu na nafasi ya elimu huria katika kufikisha elimu yenye ubora chanya na ya ana kwa ana kwa watanzania badala ya kuwafanya wadhani elimu bora ni ya ana kwa ana tu,” alisema Prof. Mbwette.

Katika hotuba yake, Makamu Mkuu wa Chuo aliwapongeza wahitimu kwa kuchagua serikali mpya ya wanachuo kwa kuhitimu.

Mkoa wa Mbeya ulitoa jumla ya wahitimu 96 katika shahada mbalimbali ambayo ni asilimia 4 ya wahitimu wote 2373. 

No comments:

Post a Comment