03 January 2011

Watanzani watakiwa kuthamini filamu za wazawa

Na Amina Athumani, Zanzibar

WATANZANIA wameombwa kununua nakala halisi za filamu za wasanii wa ndani, ili kuwapa moyo wa kuendelea na kazi hiyo. Kauli hiyo imetolewa mjini Zanzibar jana na Meneja wa nembo halisi za filamu zinazojulikana kama
Steps Entertainment, Kambarage Ignatus, alisema kama watanzania wataendelea kununua filamu ambazo si halisi, wataua fani hiyo.

Alisema wasanii wengi wanategemea kazi zao, hivyo wakihujumiwa, watakuwa wakikatishwa tamaa. Ignatus alisema kazi nyingi za filamu zimekuwa zikihujumiwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitoa nakala ambazo siyo halisi na kuziuza kwa bei nafuu.

Hali hii ikiendelea, wasanii  watakata tamaa ya kuendelea kutengeneza filamu, gharama ya kutengeneza filamu ni kubwa,  lakini malipo yanakuwa madogo.alisema.

Alisema wakati umefika kwa watanzania kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na wasanii kwa kununua kazi zao ili kuwaongezea ari na mwamko wa kuipenda kazi hiyo.

Naye, Mkurugezi wa  Zanzibar International Film Festival (ZIFF), ambayo ndiyo inayoandaa tamasha la filamu nchini Martin Mhando, alisema ZIFF itaendelea kuunga mkono kazi za wasanii wa Tanzania kwa kuwaandalia matamasha ili kazi zao zionekana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchini.

Mhando alisema mwaka huu, ZIFF imejipanga katika kuzipeleka filamu za watanzania nje ya nchi, ili kushiriki katika matamasha makubwa ikiwemo tamasha la Afrika litakalofanyika nchini Burkina Faso Februari mwaka huu.

Filamu mbili zitakazoshinda leo (jana), kwenye tamasha dogo la ZIFF (Mini-Festival),  zitaiwakilisha nchi kwenye tamasha la filamu la Afrika litakalofanyika Burkina Faso,  tunaendelea na taratibu zitakazowezesha filamu zetu kuonekana sehemu nyingi duniani,¡± alisema.

Tamasha la ZIFF la Mini-festival lilitarajiwa kumalizika jana usiku katika ukumbi wa Ngome Kongwe mjini Zanzibar.

2 comments:

  1. HII TABIA YA KUWEKA PART 1 NA 2 KTK MOVIE MOJA NDIO INATUBOA KUNUNUA! HADI MREKEBISHE

    ReplyDelete
  2. kweli kabisa, filamu moja inagawanywaje ktk parts 2? kama sio kutuibia jamani. labda ingekuwa zote mbili ktk bei hiyo hiyo bt unalipa mara mbili, why? hatutaki wizi wenu

    ReplyDelete