31 January 2011

Wanaoshindwa kulipa wasifukuzwe shule-DED

Na Raphael Okello, Bunda

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara, Bw. Cyprian Oyier amewaagiza wakuu wote wa shule za sekondari wilayani humo
  kutowafukuza wanafunzi wanaoshindwa kulipa ada na michango mingine ya shule badala yake wawasiliane na wazazi au walezi wao.

Alisema kuwa endapo wataendelea na vitendo hivyo atawachukulia hatua kali za kisheria wakuu wa shule za sekondari kwa kile alichoeleza kuwa serikali ilishatoa waraka inayowataka wasiwafukuze wanafunzi badala yake wahakikishe kuwa wanawasilina vizuri na wazazi ili kuona ni jinsi gani mzazi mwenyewe anaweza kulipa michango hiyo iliyopitishwa kisheria.

“Nimeshazungumzia suala hili la wakuu wa shule kutowafukuza wanafunzi kwa sababu wenyewe hawana fedha za kulipa michango isipokuwa ni wazazi, hivyo wakuu hao wakutane na wazazi wa watoto husika wapeane mkakati wa kulipa michango hiyo lakini sio kumfukuza mwanafunzi,” alisema Bw. Oyier.

Naye Ofisa Elimu Sekondari wilayani humo, Bw. Michael Macha amewataka wazazi na walezi ambao watoto wao wanafukuzwa kufika ofisini kwake ili aweze kuwasiliana na wakuu wa shule husika pamoja na wazazi hao namna ya kuwasaidia katika suala zima ya madai hayo ya michango ambayo baadhi ya wazazi wamekuwa wakikosa kwa wakati maalumu.

Tangu shule za sekondari zifunguliwa wilayani humo, kumeibuka
malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wazazi na walezi kuwa baadhi ya wakuu wa shule wamekuwa wakiwafukuza wanafunzi kwa kigezo cha kukosa

No comments:

Post a Comment