*Asisitiza kuondoka nchini
Na Mwandishi Wetu
SIKU chache baada ya kudaiwa Kocha Mkuu wa Yanga, Kostadin Papic kukubali kuendelea kuinoa timu hiyo, kocha huyo
sasa amezua jipya ambapo sasa amesema hataki kufanya kazi na aliyekuwa msaidizi wake, Salvatory Edward na kusisitiza kwamba ataondoka leo nchini.
Papic hivi karibuni alitangaza kujiuzulu kwa kile anachodai hataki kufanya kazi na kocha aliyeletewa na uongozi, Fredy Felix 'Minziro' kwa madai kwamba hataki kusaidiwa na kocha aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa timu inayocheza Ligi Kuu.
Minziro awali kabla ya kuitwa Yanga kumsaidia, Papic alikuwa akiifunza Ruvu Shooting inayocheza Ligi Kuu Tanzania Bara.
Lakini kabla ya siku moja kucheza Dedebit ya Ethiopia katika mechi ya Kombe la Shirikisho, vyombo vya habari viliripoti kuwa Papic ameamua kurejea Yanga baada ya kuzungumza na Mdhamini wa Yanga Yusuf Manji kwa kina.
Kocha huyo anadaiwa alikuwa akisubiri kauli ya Manji, ambaye awali walifanya naye mazungumzo kuhusu hatima yake lakini hadi jana alikuwa hajaonana naye tena.
Katika mechi hiyo ambayo timu hizo zilitoka sare ya mabao 4-4, Papic hakuwepo kwenye benchi la ufundi ambalo lilikuwa chini ya Minziro.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Yanga, Llody Nchunga alisema baada ya kusikia Papic amebadilisha uamuzi wake aliamua kukaa naye chini kujadili hatma yake.
"Nilizungumza na tukakubaliana amalizie mkataba wake, lakini hata hivyo aliendelea na msimamo wake wa kuondoka na pia si kung'ang'ania kuondoka tu hivi sasa hamtaki tena Salvatori (Edwrad) kufanya naye kazi," alisema Nchunga.
Alisema wanashindwa kumwelewa kocha huyo kwanini anakuwa na masharti mengi ambapo awali alikataa kufanya kazi na Minziro na sasa hataki kufanya kazi na Salvatory.
Nchunga alisema kutokana na hali hiyo amemwandikia barua ya kutaka kujua baadhi ya mambo kabla hajaondoka.
Hi
ReplyDeleteKwani kuna ulazima wa kumng'ang'ania? huyu mzungu?