13 January 2011

Waliouawa na polisi waagwa na halaiki

*Viongozi wa dini wasema wamekufa wakitetea taifa
*Freeman Mbowe adai mauaji hayo yalikuwa yamepangwa


Na Glory Mhiliwa, Arusha.

MAELFU ya wakazi wa Arusha na mikoa ya jirani jana walijitokeza katika kuaga miili ya
watu waliouawa na polisi kwa risasi kwenye maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yaliyofanyika Januari 5, mwaka huu.

Ibada za kuaga miili ya Denis Shirima na Isimal Omar ilifanyika jana katika Uwanja wa NMC baada ya maandamano yaliyotokea katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, saa nane na robo.

Ibada hiyo iliongozwa na viongozi wa dini wa madhehebu ya kikristo na kiislamu, ikiwashirikisha viongozi wa Taifa wa CHADEMA, wabunge wa chama hicho, wanachama,  rafiki, ndugu, jamaa na wananchi wengine.

Katika ibada hiyo alianza Ustadh Alawi kuuombea dua mwili wa marehemu Ismail Omar kwa kusema  amekufa kutokana na kupigania haki ya taifa kuwa na katiba mpya.

Alifutiwa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini Dayosisi ya Mjini Kati Askofu Thomas Laizer  ambapo alisema kuwa chanzo cha vifo hivyo  ni  kupigania haki ya Watanzania.

"Sisi viongozi wa dini tutaendelea kuishauri serikali na kutoa maoni yetu maana na sisi pia ni sehemu ya jamii namshangaa Bw. Makamba anapotukejeli kwa kauli anazozitoa huku akitumia vifungu vya kwenye biblia,  uelewa wake kwenye biblia kwanza ni mdogo sana, haelewi hata maana ya neno tiini mamlaka iliyo juu yenu," alisema Askofu Laizer.

Alisema kuwa inashangaza kuona hata Katibu wa Mkoa wa Arusha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Mary Chatanda kuambukizwa na Bw. Makamba ambaye amekuwa akiwakejeli  viongozi wa dini.

Aidha katika ibada hiyo pia alikuwemo Diwani wa Kata ya Sombetini kupitia TLP, Bw. Michael Kivuyo ambaye hivi karibuni alijivua unaibu meya na kuungana na CHADEMA  kwa madai ya kuwa hawezi kuongoza manispaa hiyo ikiwa katika dimbwi la damu.

Ndugu wa marehemu pamoja na viongozi wa CHADEMA pekee ndio walioruhusiwa kuwaaga miili ya marehemu hao  baadaye mwili wa Isamil Omar ulikwenda kuzikwa Lekitatu, Usa River Arumeru na mwili wa Dennis Maiko Shirima  ulisafirishwa kwenda Rombo Kilimanjaro kwa mazishi yanayofamyika leo.

21 comments:

  1. serikali ya jakaya kikwete itambue ina deni kubwa sana la kumwleza m,wenyezi mungu juu ya uozo wanaoufanya.Wametuchakachua kuanzia BOT,UMEME,mpaka UCHAGUZI.Na sasa wanakwenda kuchakachua roho za watanzania masikini kama sisi?Jakaya kuwa makini na team yako tofauti na hapo majibu utayapata,na serikali inatakiwa kujua kwamba mnaongoza watu waelewa kwa sasa

    ReplyDelete
  2. Nasema kila mara kwamba amani itapatikana tu pale wananchi watakapotendewa haki, tofauti na hivyo neno amani halitasikika masikioni mwa wanyonge! Jamani tutendee wananchi haki Bei ya umeme imepanda, Gesi Tsh 50,000/= hata maana ya kuwa na Songosongo gesi sijui, bei ya mkate Tsh. 1,500/= wakati mkate ndicho chakula cha mwisho cha kuliwa na mtu mnyonge ambaye anaishi chini ya dola moja ambapo bei ya mkate iko juu ya dola moja. Mwanzoni nilikuwa naipima serikali utendaji wake kwa miaka miwili lakini sasa nawapima kwa wiki mbilimbili. Ishara zinaonyesha kwamba wizara tatu zitatimiza malengo nyingine zisipozinduka haraka 2015 shughuli ipo. Kwaheri!

    ReplyDelete
  3. hivi unajisikiaje kikwete kwa haya mauji yako yaliyofanywa na police arusha, kwani inaonyesha wazi kabisa ni mipango yako na kabinet yako kwani kukaa kwako kimya kunamaanisha nini? na kwa nini mnataka sana Arusha? haya maovu yenu yatawakosti halafu mtoe makamba tena ajiuzulu kwani ubongo wake umezeeka kama yeye, hana kazi tena acheni vijana wafanye kazi.kwani anaongea ujinga tu.

    ReplyDelete
  4. Serikali ya awamu ya tatu ya Mkatoliki Mkapa itambue ina deni kubwa sana la kumwleza m,wenyezi mungu juu ya uozo wanaoufanya.Wametuchakachua kuanzia BOT,UMEME,mpaka UCHAGUZI.Na sasa wanakwenda kuchakachua roho 21 za Wapemba,watanzania masikini kama sisi?JMkapa kuwa makini na team yako tofauti na hapo majibu utayapata,na serikali inatakiwa kujua kwamba mnaongoza watu waelewa kwa sasa.

    ReplyDelete
  5. Ama kweli chadema mna matatizo. Mnachanganya mambo. Nyie mnadhani akina Slaa wakija madarakani hakutakuwa na matatizo? Ndivyo alivyokuwa anawadanganya lakini watanzania walimshitukia. Baada ya kushindwa akaanza kubwatuka eti ameibiwa kura. Nani angempa urais mzee asiye na busara? Eti anawaambia watu waende kuwatoa viongozi polisi. Slaa ana kesi ya kujibu. Mropokaji mbowe anadai eti kikwete alipanga mauaji. Give me a break. Watu wameshawajua hawa watu ni akina nani, na matokeo yake mtayaona 2015. Hata kidogo mlichopata mtanyanganywa hata uchaguzi ukisimamiwa na Umoja wa Mataifa

    ReplyDelete
  6. Hivi unajisikiaje Mkapakwa haya mauji yako yaliyofanywa na police Pemba, kwani inaonyesha wazi kabisa ni mipango yako na kabinet yako kwani kukaa kwako kimya kunamaanisha nini? na kwa nini mnataka sana Pemba? haya maovu yenu yatawakosti halafu mtoe Mbowe na Slaa tena wajiuzulu kwani ubongo wao umezeeka , hawana kazi tena wacheni vijana kina Zitto kabwe wafanye kazi.kwani Mbowe na Slaa wanaongea ujinga tu.

    ReplyDelete
  7. ushauri wangu kwa mary chatanda, kwanza amwogope Mungu huwezi kuingia madarakani kwa kumwaga damu,maana chanzo cha watu kupoteza maisha ni yeye kukubali kugombea umeya arusha hali akijua ya kuwa yeye ni mbunge viti maalumu Tanga. pili ajiuzulu yeye mwenyewe kama alivyofanya naibu meya wa arusha. kung'ang'ania itadhihilisha kuwa kweli ilikuwa serikali na chama tawala kilidhamilia kuchukua umeya arusha kwa njia yoyote ile hata kama ni kwa kumwaga damu.

    ReplyDelete
  8. Idadi kubwa ya waliojitokeza kuaga miili ya wahanga wa siasa za CCM imekwenda kinyume na matarajio na malengo ya polisi na serikali ya kuzima maandamano kwa mtutu wa bunduki. Nadhani serikali ilitumia nguvu kubwa ili kutisha wananchi waogope kushiriki shughuli zinazoratibiwa na vyama vya siasa vya upinzani siku zijazo. Maana yake wanachi wasijitokeze tena wanapotakiwa na wapinzani kujitokeza kupinga jambo linalofanywa na serikali vinginevyo watahatarisha maisha yao. Umati uliojitikeza jana umedhihirisha kuwa wananchi hawahofu kuuawa na polisi wakati wakitetea ukweli, mimi na wengine tulidhani wananchi wengi wasingejitokeza kwenye shughuli ya jana iliyoratibiwa na CHADEMA tena. Watu walikuwa wengi sana na amani ilikuwepo pia, jambo linaloonyesha kuwa hata yale maandamano yaliyo sitishwa kwa risasi yangekuwa ya amani na utulivu ungekuwepo pia. Intelejensia iliyotumika kusitisha maandamano yale ilikuwa feki iliyoongozwa na hisia tu badala ya evidence. Namuomba IGP Mwema na viongozi wengine wa serikali na taasisi zake watumie taaluma zao katika kutimiza kazi zao. Wawe na waangalifu na wanasiasa, taarifa zenye harufu ya siasa wawe makini nazo. Mambo yanapokwenda kombo wanasiasa ni rahisi na wepesi kuwakana na kuwatoa kafara watendaji wao kwa lengo la kuficha nyuso zao, chama na serikali. Ona sasa Makamba anamtwisha zigo msimamizi wa uchaguzi wa Meya Arusha kuwa yeye ndiye alaumie, kana kwama CCM haikujua kilichofanyika kwenye uchaguzi ule. Bora ujiuzuri kuliko kutekeleza jambo lisilo na evidence. Rais Kikwete alitufunza wanchi wote tutumie akili zetu katika kutenda mambo badala ya kufuata ushauri usio na ushahidi wa kutosha pale alipotoa hadithi ya ndege wawili, mbayuwayu na Kong'ota. Nchi hii ni yetu sote.

    ReplyDelete
  9. Unapowatuma wafuasi wako waende polisi kuwatoa viongozi wako unategemea nini? Huyo Mbowe ndiye atakayekuuwa Slaa ili yeye awe Rais na baadaye wataisingizia CCM,KAA CHONJO NA HAO,NI MAFIA. MBOWE NI MZUSHI HUYO

    ReplyDelete
  10. Wanataaluma tufanye kazi zetu kwa mujibu wa taaluma zetu nchi, watu, rasilimali na mustakabali wetu utategemea wanataaluma wake. Tuache kufanyakazi kama maroboti ya wanasiasa. Tufikirie taifa letu zaidi kuliko kutii mamlaka zilizo juu. Hatuwezi kutii mamlaka zilizowekwa kwa njia zisizokuwa za wazi. Mfano, majeshi yetu yote ni ya ulinzi wa wananchi na mali zao, yanalinda mipaka dhidi ya adui kutoka nje ndani ya nchi, lakini ona, madini yanaibwa, magogo yanaibwa, samaki, wanyama, kodi zinaibwa sasa tunalinda nini? tunasubiri tu akina Idd Amini tuwapige wakija lakini hatumpigi adui anayevuka mipaka na kuja kupora mali zetu, tunalinda nini kila kitu kinaondoka? Amini akija tena tutampiga na nini wakati hatutakuwa na pesa za kununua silaha za kisasa? Ajenda ya ukombozi wa nchi sio ajenda ya raia tu ni ajenda ya watanzania wote bila kujali sehemu unayofanyia kazi. Iko haja hata majeshi yetu kuhoji vitendo vya wanasiasa na mamlaka iliyojuu, vinginevyo iko siku mtalinda nchi hii kwa silaha duni kuliko za adui na kuhatarisha maisha yenu kwenye uwanja wa vita. Wanasheria wetu wanalifanya taifa lifanane na lile taifa la akina Mangungo wa Msovero walidanganywa na akina Karl Peters kwa kutojua sheria. Nchi inavyokwenda sasa utadhani hatuna wanasheria nchini. Tulitegemea wanataaluma waongoze harakati za mageuzi ya kisiasa nchini lakini hali ni tofauti kabisa, wanaohangaika kuweka huru mifumo ya demokrasia na utawala bora nchini ni wananchi wa kawaida nchini na wanafunzi, huku maprofesa nchini wakiendelea na miradi yao ya ufugaji wa kuku, bata, nguruwe, uyoga, na kufanya tafiti uchwara zenye lengo la kupata hela kuliko kutatua matatizo halisi ya wananchi. Wasomi wetu ni wanafiki wakubwa wanalinda wasichokuwanacho, wanalinda kazi wazizokuwanazo. Ona wahadhiri wetu wanavyohangaika na kazi za day waka, wanazunguuka vyuoni kupata kazi za kutwa kuongeza kipato, wamekuwa wamachinga huku taifa lao likiporwa na watu wachache kutoka nje na ndani ya nchi, huku kazi ya ukombozi wa taifa ikiachwa mikononi mwa wanahabari wachache na wananchi wasio na taaluma japo kwa kujitokeza kwenye maandamano.

    Taifa likiangamia tutaangamia wote bila kujali kazi wala taaluma, tusitii mamlaka iliyojuu tu mali tujiulize tunatii mamlaka inayotufanyia nini na iliyopatikana vipi.

    ReplyDelete
  11. RAIS KIKWETE UNAMLEA WA NINI HUYO BABA YAKE NA JANUARI YAANI YUSUPH MAKAMBA ANA MAWAZO MGANDO TENA YALIYOPAUKA FIKRA CHAKAVU ANAWABEZA HATA VIONGOZI WA DINI SAMBAMBA NA MARY CHATANDA HAWAMWOGOPI MUNGU HUYO MAKAMBA ANAJIFANYA ANAIJUA BIBLIA ANKARIRI MSTARI MOJA SASA NDIYO KILA SIKU JAMBO NI HILO UPEO WAKE NI MDOGO SANA.

    ReplyDelete
  12. Tutafakari na kuhoji kwa kurejea taarifa na kauli za viongozi wa serikali kuhusu sakata hili la Dowans.
    Kuvunjwa mkataba wa Dowans
    Msingi wa kuvunjwa mkataba kati ya TANESCO na Dowans ni ushauri wa wanasheria kutoka kampuni ya Rex-Attorneys. Ni Kampuni hii ya kisheria iliyonadiwa bungeni kuwa, imebobea katika masuala ya sheria za kimataifa.
    Agosti 28, mwaka 2008, Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda (mwanasheria kitaaluma) aliimwangia sifa kampuni ya Rex-Attorneys bungeni.

    Hukumu hii inatoka katika wakati ambao ushauri wa Rex-Attorneys (wazoefu wa mikataba ya kimataifa) ukiwa katika makabati ya TANESCO.
    Lakini pia ashinikize uchunguzi wa uhusiano kati ya kampuni hii na viongozi wa serikali, ikiwamo ofisi ya Waziri Mkuu iliyoipamba kampuni hiyo bungeni.
    Ikumbukwe, kwa mara nyingine kampuni hii imefuatwa tena baada ya hukumu ya ICC ili kushauri kama Dowans ilipwe au la. Wameshauri ilipwe.
    Ni kama vile kampuni hiyo mwanzo ilitoa ushauri wenye malengo ya kuandaa mazingira ya Dowans kushinda kesi na kulipwa.
    Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema; “Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO ilishauriwa na kampuni ya Rex Attorneys Advocates kukubaliana na hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Usuluhishi bila kuipinga endapo itasajiliwa kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania.”
    Hapa, Rex Attorneys ndiyo iliyosifiwa na Waziri Mkuu bungeni, ikatoa ushauri wa kuvunja mkataba. Baada ya kuvunja mkataba, TANESCO ‘imehukumiwa’ kulipa mabilioni.
    Lakini baada ya hukumu kutoka, TANESCO imerudi kwa kampuni iliyotoa ushauri wa kuvunja mkataba, kampuni hiyo inashauri tena TANESCO ifanye malipo?!
    Je, vigezo vya awali vya Rex Attorneys kushauri mkataba uvunjwe vimepotelea wapi hadi wakimbilie kushauri TANESCO ifanye malipo? ? Je, kuna mgawo wa malipo hayo baadaye?
    Kwa nini kampuni iliyoshauri kwa vigezo vya kisheria mkataba uvunjwe, baadaye igeuke ikipuuza vigezo hivyo na kutoa ushauri mpya wa kulipa mabilioni? Kwa mbunge makini bila shaka hapa kuna jambo la kuhoji.
    Serikali kupitia TANESCO imevunja mkataba kwa ushauri wa kampuni hii, leo inakwenda kulipa faini kwa ushauri pia wa kampuni hii, je, kuna nini?

    MY COMMENT: REX ATTORNEYS NI KAMPUNI AMBAYO FISADI EDWARD NGOYAI LOWASSA AMEKUWA ANAITUMIA KWA SHUGHULI ZAKE ZA KISHERIA KAMA ALIVYOSEMA HADHARANI MWENYEWE. MPANGO MZIMA WA KINA JK NI KUJIPANGA KIUHUJUMU NCHI. KESI IKIENDA MAHAKAMANI, ATAPANGIWA JAJI WA KUINYONGA HAKI YA NCHI HII WA WANANCHI.NDIO MAN ACHADEMA ARUSHA HAWATAKI OPTION YA MAHAKAMA KATIKA SUALA LA UMEYA ARUSHA KWA KUTAMBUA KWAMBA HAKI HAITATENDEKA. JAJI MKUU OTHMANI ATA INFLUENCE JAJI WA KUTOTOA HAKI. PEOPLES POWER NDIO DAWA PEKEE. CHADEMA TUSAIDIENI JAMANI!

    ReplyDelete
  13. Ni kweli watu wa ARusha kwa ujumla tumeonyesha Umoja, Ujasiri, Upendo, AMani,Utlivu pale tulipokubali kujipanga wenyewe katika kufanikisha mazishi na zoezi zima la maandamano ya haki, tunamshukuru Mungu kwa kuwaonyesha ccm kuwa hatupo kwenye dunia ya zamani ya kutishiwa na kukimbia bali kukubali kufa kwa ajili ya haki na kusimamia demokrasia nchini ili iheshimiwe na ccm wajue tu kuwa hata jimbo la Arusha na kuingine hawatapata tena maana watu wamewajua na kuwaogopa kama ukoma kwa ajili ya ukatili wao. jana nilihudhuria kwenye maandamano nilisikia watu wengi wakiuaga ccm na kukaribisha CHADEMA miyoyoni mwao kwa upendo na umoja waliouonyesha viongozi wa CHadema kwa kukubakubali kupigwa , kuteswa, kumwagwa damu na kudhihakiwa na ccm kwa ajili ya haki ya walio wengi.

    ReplyDelete
  14. Darwin,

    Ndugu zangu Watanzania Popote pale mlipo, Watu waliokufa iwe ni Polisi au wafuasi wa chama fulani tukumbuke kuwa hao si Polisi au Wanachama wa CHADEMA au CUF nk, bali hao ni Watanzania wenzetu. Wangeweza kuwa ni mimi au wewe.

    Roho za Watanzania zimetutoka,roho za watanzania zimelazimishwa kutolewa ili kuhalalisha madai ya Serikali na CCM kuwa mlikaidi amri halali ya Polisi.

    Ipi bora kuuwa watu au kukaidi amri inayojichanganya ya Polisi. Kwa bahati nzuri namfahamu kamanda Andengenye, ni mtu mcha Mungu kweli kweli na hata hapa sijuwi kaingiaje! Na kwa jinsi pia ninavyomfahamu Kamanda Mwema yeye ni mwema kuliko hata hilo jina lake.

    Sasa kimetokea nini mpaka Jeshi la Polisi kulazimishwa kufanya hicho walichokifanya dhidi ya Raia wasio na silaha wala sijuwi, kwa jinsi tunavyofahamu "taarifa za kiinteligensia" hakusanyi yeye (mwema) na wala hajuwi zinapatikana vipi, bali hulazimishwa kuamini kile anachoelezwa kutoka "Intelligence Agency"

    Tusilitumbukize jeshi la Polisi katika kadhia hii, waanzilishi wa machafuko haya wapo na wanajulikana Rais na wananchi kwa ujumla tunahitaji mabadiliko makubwa sana si ya Katiba tu bali hata na Intelligence Agency yenyewe.

    Usalama wa Taifa ikae ikijuwa hii si enzi ya kukumbatia Chama tawala na serikali yake, bali ni enzi ya kusikiliza matakwa ya wananchi na kumshauri Rais inavyostahili kulingana na hali halisi.

    Mwema na Andengenye nawapa pole kuingia mkenge huu,ila najuwa moyoni mwenu hampo hivyo! Hata leo hii naamini nikiwaita nikawahoji kiundani mtanieleza kitu tofauti na zaidi hata kutoa machozi!

    Ushauri wangu ni huu tu tuache siasa iendeshwe na wanasiasa, watu wa Usalama mratibu tu shughuli za kiusalama bila kukumbatia chama chochote! Kesho ikiingia Ikulu CHADEMA au CUF au chama chochote cha siasa mtaficha wapi sura zenu?!

    Vyama vyote ni vya watanzania vinahitaji haki sawa!

    ReplyDelete
  15. Kwa nini hamtaki ukweli? hao waandamanaji waliamriwa na Padri Slaa waende kituo cha polisi wakawatoe watuhumiwa ambao ni viongozi wao,kama wasingekwenda kule hayo yangetokea? mauaji hayo tuambieni yalifanyika kabla au baada ya mkutano? HAPA PADRI SLAA ANA KESI YA KUJIBU

    ReplyDelete
  16. SASA WE BWANA MJINGA AMBAYE HUNA HAYA WALA CHEMBE NA MJINGA MWENZIO MBOWE NA SLAA MNAMUINGIZAJE lOWASA KWANYE UJINGA WENU HUU KWANI ALIWAAMBIA MUANDAMANE?MNATUDANGANYA KUWA MNADAI HAKI ZA WATANZANIA KUMBE NI UONGO TU MNATAKA UMAARUFU WENU KWA FAIDA YENU NA LEO MMEUA WATU WASIO NA HATIA MNAWASINGIZIA CCM NA POLISI NA BWANA WENU MBOWE BILA HAYA ANASEMA IGP MWEMA NA WAZIRI NAHODHA WAJIUDHURU THUBUTU UU,WAANZE WAO KUJIUZURU NAFASI ZAO KWENYE CHADEMA WAWAPISHE AKINA ZITO ILI NCHI ITULIE VINGINEVYO HAMASISHENI WAJINGA WENZENU WAANDAMANE MUONE KAMA TUTAWAACHA ILI MUWAUE WATANZANIA WASIO NA HATIA MSINGIZIE CCM JARIBUNI MUONE KAMA TUTAWAACHA.

    ReplyDelete
  17. NAWAOMBA WATANZANIA WENZANGU KUWA MACHO SANA NA PADRE SLAA NA WAKUBWA WAKE WA KAZI YAANI MAASKOFU HAWANA NIA NJEMA NA WATANZANIA HAO HIVI PADRE SLAA KAPOLA MKE WA MTU MAASKOFU MBONA HAWASEMI?JE HIYO SIYO DHAMBI?SIYO UFISADI MBONA WAO AKO KIMYA WANA MASLAHI GANI NAO JAMANI INAUMA SANA JAMANI ,HIVI KANISA KATOLIKI ANALIAHARIBU NANI?AHAA

    ReplyDelete
  18. Chama Cha wachaga na wenzao tunawaonya sisi watanzania hatutaandamana kwa ujinga wenu sawa?

    ReplyDelete
  19. Mimi nadhani kwa akili zangu za kibinadamu,ni bora kama mtu huna hoja wala cha kuchangia basi unyamaze usipoteza muda wako kukaa kwenye mtandao kuandika vitu ambavyo hata mtoto wa drs la kwanza hawezi kuvisema wala kuviandika,kama unapinga hoja fulani jenga hoja yako ili watu wakuone kweli hoja hii ina nguvu na inafaa kuchangiwa ,lakini kutoa kauli ambazo kwamimi (uelewa wangu mdogo)hazifai kusomwa na watu maana tujue haya maoni tunayoondika hapa yanasomwa na watu wa lika mbalimbali ,hivi wadogo zetu wanatuonaje tunavyondika upuuzi usio na kichwa miguu,halafu mjadala hapa ni mauji ya Arusha je hayo mamabo ya sijui udini yanatoka wapi?,mchangiaji emu chukulia hayo mambo yapo kwako,dada yako au mama yako au kaka yako au baba yako mzazi yeye alikuwa ametoka kwenye mihangaiko yake ,lakini ktk kupita mjini kulikuwa na vurugu hizo za kisiasa kapigwa risasi na polisi na amefariki dunia je ungepokeaje huo msiba?,inamaana kama baba huna tena,kama mama huna tena au kaka huna tena,jamani mimi naomba sana kabla ya kuandika chochote tuwe tunafikiri kwanza je hichi ninachoaandika kingetokea kwangu ningeandika haya ninayoyandika?,halafu la mwisho wachangiaji wenye hoja zenu naomba msiingie kwenye mtego wa kujibu matusi,kwani ukimjibu mtu humu anakutoa kwenye maada iliyopo hapo juu,mtu akiandika upuuzi jaribuni kumpuuza,simamieni maada ilyopo basi, hata kama atandika nini msimjibu baadae atajiona yeye yuko peke yake ataacha ,mkijbu mnapa nguvu ya kuendelea kuandika upuuzi
    Asanteni

    ReplyDelete
  20. nachokiona ni kwamba serikari ya awamu 4 kupitia JK na CCM wameshindwa kusimamia ujenzi wa taifa hili. pia wapo kwa masilai yao binafsi na chama chao. HONGERA CHADEMA KWA MAPINDUZI

    ReplyDelete
  21. JE?,MAKAMBA ANAFAHAM KWA NINI?, WATU WALIKUWA WENGI KTK VIWANJA VYA KUAGA MIILI YA MAREHEM,WAFAHMU KUWA WATANZANIA SASA WAKO TAYARI KUPIGANIA HAKI ZAO HATAKAMA WATATISHWA KWA MABOM NA RISASI.CCM TUMECHOKA NA UTAWALA WENU ULIOJAA UFISADI ,ANGALIA BEI YA UMEME,MAFUTA,NA BIDHAA MBALIMBALI ACHIENI INCHI KWA WATU WENYE UCHUNGU NA INCHI HII

    ReplyDelete