13 January 2011

Mauaji Arusha ya kupanga-Mbowe

Na Grace Michael

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa mauaji yaliyofanywa na Askari Polisi mkoani Arusha yalipangwa na Rais Jakaya Kikwete pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) walihusika moja kwa moja katika
umwagaji huo wa damu.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe kwenye ibada ya kuwaombea waandamanji waliouawa na polisi kwa risasi, wakati wa maandamano ya amani yaliyofanyika Januari 5, mwaka huu.

"Rais Kikwete na serikali yake na chama chake cha CCM wanahusika moja kwa moja na damu iliyomwagwa kwa makusudi Arusha...Kikwete ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama. Aidha, chini ya Sheria ya Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi – ambaye ni mteuliwa wa Rais – anawajibika kufuata amri na maelekezo ya Waziri wa Mambo ya Ndani – mteuliwa mwingine wa Rais kuhusiana na udhibiti wa shughuli za Jeshi la Polisi.

"Kwa hiyo, kikatiba na kisheria, Jeshi la Polisi liko chini ya mamlaka ya Rais na wateuliwa wake kama Waziri wa Mambo ya Ndani na Inspekta Jenerali wa Polisi. Pamoja na mamlaka ya Rais juu ya Jeshi la Polisi, Kikwete mwenyewe alikwishatoa kauli na matamko hadharani ambayo yaliashiria kwamba Jeshi la Polisi la Tanzania lilikuwa linajiandaa kumwaga damu ya Watanzania ili kulinda utawala wake na wa chama chake," alidai Bw. Mbowe.

Mbali na hayo pia chama hicho kilitoa mapendekezo kwa kuitaka serikali kuwajibika kwa wananchi kama ilivyotamkwa na Katiba ya Tanzania kwa Waziri wa Mambo ta Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha na Inspekta Jenerali wa Polisi, Saidi Mwema wajiuzulu mara moja ili kuwawajibisha kama viongozi na wasimamizi wa juu kabisa wa Jeshi la Polisi la Tanzania.

Alisema kuwa kujiuzulu kwao kutapisha uchunguzi huru na wa kina wa matukio yote yaliyosababisha wananchi kuuawa, mamia kujeruhiwa na mamia wengine kukamatwa bila sababu yoyote na kuwekwa rumande na baadaye kufunguliwa mashtaka ya uongo ya jinai.

Aidha alisema kuwa Ispekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye na wale wote walioamuru au kutekeleza amri ya kuvunja maandamano na mkutano halali, wafunguliwe mashtaka ya jinai kwa matumizi mabaya ya madaraka na kwa kusababisha mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia.

Kwa mujibu wa Bw. Mbowe, CHADEMA kinataka ilipwe fidia stahili kwa mujibu wa sheria husika za nchi kwa ndugu na kwa wale wote walioumizwa kwa namna yoyote ile au kuharibiwa mali zao kutokana na vitendo hivyo.

"Lakini pia tunataka mashtaka ya uongo ya jinai yaliyofunguliwa dhidi ya viongozi wa ngazi zote wa CHADEMA, wanachama, wafuasi na wananchi wengine wote yafutwe bila masharti yoyote kwa sababu maandamano na mkutano wa hadhara uliozuiliwa ulikuwa halali kwa mujibu wa sheria husika za nchi yetu," alisema Bw. Mbowe.

Alisema kuwa kwa vile uchaguzi wa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ndio chanzo cha mauaji ya wananchi na kwa kufahamu utaratibu haramu uliotumika kumpata Meya wa Jiji hilo, matokeo ya uchaguzi huo yafutiliwe mbali na uchaguzi mpya uitishwe haraka iwezekanavyo kwa kufuata sheria husika za nchi.

Aidha CHADEMA kimeendelea kusisitiza kuundwa kwa tume huru ya kimahakama kwa sababu historia ya tume nyingine ambazo zimeundwa kwa utaratibu wa rais kuteua watu anaowataka inaonesha kwamba zimefanya kazi zao za uchunguzi mafichoni bila kushirikisha wadau wengine na bila wananchi kufahamu kitu kinachoendelea.

Alisema kuwa ili kuhakikisha madai hayo yanatekelezwa, alielekeza viongozi, wanachama na wafuasi wote mikoani na wilayani kuandaa maandamano ya amani nchi nzima ili kulaani mauaji ya wananchi wa Arusha na kudai utekelezaji wa madai haya.

Akifafanua zaidi kuhusika kwa Rais Kikwete katika mauaji hayo, alisema kuwa pamoja na mamlaka ya Rais juu ya Jeshi la Polisi, yeye mwenyewe alishatoa kauli na matamko hadharani ambayo yaliashiria kwamba Jeshi la Polisi la Tanzania lilikuwa linajiandaa kumwaga damu ya Watanzania ili kulinda utawala wake na wa chama chake.

"Kwa mfano katika hotuba yake ya Mwaka Mpya aliyoitoa usiku wa Desemba 31, 2010, Kikwete alidai kwamba 'wapo baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa wamepanga kuchochea migomo vyuoni na maandamano ya wananchi mara kwa mara. Wao hasa wanachotaka ni ghasia kutokea na vyombo vya dola kuingilia, ati waiambie jumuiya ya kimataifa jinsi serikali yetu ilivyo katili...katika hotuba hiyo, Kikwete alizungumzia kile alichokiita wananchi kugeuzwa kuwa mbuzi wa kafara'," alinukuu baadhi ya maneno ya Rais Kikwete.

Bw. Mbowe alisema kuwa mauaji hayo yamedhihirisha wazi umuhimu wa kuwa na katiba mpya kwa ajili ya nchi na hii ni kwa sababu, 'katiba viraka' inayotumika sasa hivi haiheshimiwi hasa na watawala wenyewe kama ilivyoonekana kwenye uhuru wa kufanya maandamano ya amani na mikutano ya hadhara.Alisema kuwa matukio yaliyosababisha mauaji ya Arusha yanaonesha kwamba mfumo mzima wa kisheria na kitaasisi wa kuendesha chaguzi katika nchi unahitaji mabadiliko makubwa.

"Sasa ni muda muafaka wa kuhakikisha tunapata katiba mpya itakayohakikisha kwamba vyombo vya ulinzi wa wananchi vinakuwa chini ya udhibiti halisi wa wananchi au vyombo vyao vya uwakilishi. Sasa ni muda muafaka kuhakikisha kwamba tunapata katiba mpya itakayohakikisha kwamba mfumo wetu wa uchaguzi ni huru na wa haki kwa watu na vyama vyote," alisema Bw. Mbowe.

Alisema kuwa utaratibu ambao CHADEMA itauunga mkono na kushiriki kikamilifu ni ule utakaowezesha kufanyika kwa Mkutano wa Kitaifa wa Katiba ambao utawakilisha makundi yote ya kijamii katika uundaji wa Katiba mpya.

"Utaratibu wa kusubiri fadhila za Kikwete za kuteua wajumbe wa Tume ya Katiba haukubaliki tena na CHADEMA haitaubariki kwa kushiriki... CHADEMA itatumia uwezo wake wote kuhamasisha wananchi nchi nzima kuhakikisha wanapinga utaratibu unaopendekezwa na Kikwete na kuunga mkono utaratibu wa kidemokrasia wa kupata katiba mpya kwa kupitia Mkutano wa Kitaifa wa Katiba," alisema.

Alihusisha mauaji hayo na kisasi cha Uchaguzi Mkuu kwa viongozi wa CHADEMA wa ngazi zote na kwa wananchi wa Arusha kwa kudiriki kuisambaratisha CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Alisema Jeshi la Polisi la Tanzania limelipa kisasi kwa niaba ya CCM kwa sababu wananchi wa Arusha wamediriki kutumia haki zao za kisheria kupinga mipango ya mafisadi kuingiza Meya wa Jiji la Arusha atakayelinda maslahi ya mafisadi na chama chao.

"Wananchi wa Arusha wamelipiziwa kisasi kwa sababu mafisadi wanajua wangeruhusu haki itendeke katika uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha CCM ingesambaratishwa kama ilivyosambaratishwa katika Uchaguzi Mkuu," alisema.

Alisema kuwa mauaji hayo hayakuwa kisasi cha CCM dhidi wananchi wa Arusha tu bali ilikuwa ni kisasi pia dhidi ya wananchi wa Tanzania na dhidi ya CHADEMA, kwa sababu, kwa mara kwanza tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa urudishwe mwaka 1992, Uchaguzi Mkuu wa 2010 ulionesha wazi kwamba CCM imeanza safari yake ya mwisho kuelekea ukingoni.

Alisema kuwa mara ya kwanza, CCM ilipoteza miji mikubwa karibu yote ya Tanzania, licha ya uchakachuaji wa kura, rushwa na uharamia wa kutisha, ilipoteza Jiji la Dar es Salaam, Jiji la Mwanza, Jiji la Arusha, Jiji la Mbeya na miji mikubwa kama vile Moshi, Iringa na Musoma.

Kutokana na hali hiyo Bw. Mbowe aliitangaza Januari 5, 2011 kuwa siku ambayo haitasahaulika katika historia ya Jiji la Arusha, na historia ya Tanzania.

"Ni siku ambayo Jeshi la Polisi la Tanzania ambalo limepewa wajibu wa kisheria wa kulinda amani, sheria na utulivu, kugundua na kuzuia uhalifu, kukamata na kudhibiti wahalifu na kulinda mali za wananchi; liliamua kwa makusudi kuacha kutimiza wajibu wake kisheria na kujipa wajibu mwingine wa kuwa ni Jeshi la kuvunja amani, kukiuka sheria, kuvuruga utulivu, kufanya uhalifu na kuharibu mali za wananchi.

30 comments:

  1. Kwa viongozi kama Mbowe tutafika kweli? Ipo kazi.

    ReplyDelete
  2. Kwa nini tusifike tutafika tu, au wewe ndio miongoni mwa polisi waliowaua watu wasikuwa na hatia. Kama huna maoni si afadhali kunyamaza. Acha kuumiza roho za watu

    ReplyDelete
  3. Kuna Baadhi ya watanzania kama wewe ni maji nga maji nga kwisha kazi. Yaani unasubiri Yesu arudi ndio akupe ukombozi.

    1. Unajua Mchakato wa Dowans?
    2. Unajua unatakiwa kulipa umeme kiasi gani?
    3. Unajua kuna watu kilosa wanalalia Mahindi na sukari tu?
    4. Unajua ndege za ATCL zimenunuliwa ngapi na kwa kiasi gani?

    5. 6. 7. Haina haja kama hayo hapo juu huya jui.

    AMKA WEWE!!!!

    ReplyDelete
  4. Ni kweli tutafika tuu!! Ni hapo tutakapo kuja jutia maneno aliyoyatamka na matokeo yake, na wakati huo wao watakuwa wapo Merekani au vatican wakipata hifadhi ya kisiasa, na sisi tukiuwana hovyo kama kuku. Liko linalotafutwa na hawa Chadema, lkn Mungu atatunusurisha nalo Inshaallah.

    ReplyDelete
  5. sijui kinachachangiwa hapa. Mauaji ya Arusha au ufisadi?

    Tubakie kwenye mada. Mbowe na Slaa lazima washitakiwe kwa kuchochea wafuasi wao kuvuruga amani iliyopelekea watu kupoteza maisha na mali za kuharibika.

    Nahodha, ambaye ufanyaji kazi wake tokea Zanzibar ulikuwa wa kubebwa amaedhihirisha kuwa hawezi uongozi na hivyo aungane na IGP Mwema wajiuzulu kushindwa kudhibiti maandamano bila kuleta upotevu wa maisha.

    Vingozi wa kidini waache kuongeza chumvi kwenye kidonda kwa vile haitasaidia kitu zaidi ya kuleta sitofahamu zaidi.

    CHADEMA kwa kuutumia na kuuzuwia mwili wa marehemu muislamu usizikwe ndani ya kipindi kinachokubalika na sheria za Kiislamu,yaani kusizidi kuzama majua matatu (three sunsets) kwa ajili ya propaganda za kisiasa ni kuudhalilisha uislamu na kuufanya mwili wa marehemu kuwa kama mzoga tu.

    Shehe alieshiriki kuusomea dua mzoga anaonesha haijui dini yake kama alivyo Makamba kwa Biblia

    Ya kaizari tumwachie kaizari

    ReplyDelete
  6. Mh.mbowe CCM,wamekwisha habari yao.Cha msingi ninaomba usilipize kisasi ni juu ya Bwana.Kuanzia hivi sasa ninaomba usamehe mara saba wa sabini.

    ReplyDelete
  7. MBOWE NA SLAA LAZIMA NANYI MSIMAME KIZIMBANI KUJIBU SHUTUMA ZA UCHOCHEZI. KIKWETE TUNAYE HADI 2015,MBONA UNADANGANYA WATU MKOA WA DAR-ES-SALAAM MMECHUKUA CHADEMA,UNADHIHIRISHA UONGO WAKO MBELE YA JAMII,MEYA WA JIJI LA DAR ANATOKEA CHADEMA? UBUNGO NA KAWE NDIO DAR NZIMA,HAPO NDIPO MNAPOWAPATA WAJINGA.

    ReplyDelete
  8. chama tawala ccm na serikali yake anzeni kusoma alama za nyakati. huu sio wakati wa ujinga.tuko kwenye ulimwengu uliostarabika.acheni mambo ya mwaka 47.damu mnazozimwaga zitawasumbua huko mnakoelekea.kwanza ndani ya chama hakutakuwa na mshikamano.zitawatesa pia ktk uzee wenu.katika nchi anayoendelea inathamini sana uhai wa raia wao kuliko kitu chochote lakini kwenu mnajali madaraka kuliko waliowaweka madarakani.angalieni ni aina ya kizazi kipi mnachokiongoza.angalia mnaowatendea ndio hao mtakao kwenda kwao 2015 kuomba kura.someni alama za nyakati.

    ReplyDelete
  9. wewe huna hata chembe ya akili rudi darasaniukasome fala wewe huna tofauti na hawa wanaokejeli watumishi wa mungu, wewe na shehe nani mwenye akili?unadiriki kumtolea mtu wa Mungu maneno kama hayo ndugu yangu umekwisha kwa hiyo kasomea dua mzoga kana kauli yako unacheza na moto. halafu yaelekea kwenu wote ni mataahira sana huna elimu kabisa.peleka ujinga wako huko.

    ReplyDelete
  10. kuna watu wanaongea kama wamekatwa ulimi hususan huyu wa pili juu kutoka mimi,Mbowe, slaa,sio waongo wewe ndo mjinga. kabisa huna hata chembe ya akili.Fataki wewe.

    ReplyDelete
  11. wapo watanzania wajinga sana wanatoa maoni kwa ajili ya kujipendekeza ka serikali ya ccm na jeshi la polisi watu wanauwawa unasema ni mzoga hi heri mimba hiyo ingeharibika usingezaliwa huna maana hapa duniani,uliona wapi risasi za moto wanamiminiwa raia wasio na hatia mbona wakati wamaombolezo hakuna gjasia yoyote acheni ukuda,mnashabikia vitu vya kijinga sana.

    ReplyDelete
  12. Najiskia kuumia badala watu wengine konyesha masikitiko kwa watu waliopoteza uhai na wengine kujereuhiwa na serikali ya Jk kiwete bado wanakiunga mkono chama hicho katili na serikali yake isiyomwogopa Mungu kwa kutoa uhai wa mtu aliyeumbwa kwa Mfano wake na kwa gharama ya hali ya juu na hakuna kiumbe kilichoweza kuumbwa kama mwanadamu na kupewa heshima kubwa aliyopewa mwamnadamu wao wanawauwa na kutoonyesha uanadamu huu ndio mwisho wa CCM na uongozi wake wa kideteta. hata kama CHadema walikataa kutii maagizo wakiwa kwenye maandamano ilikuwa haki yao ya msingi na waliwajulisha hao walinzi (polisi kwa ajili ya uimarishaji wa ulinzi wao lakini wakageukwa na kuuwawa kama wanyama wasio na haki ya kutetewa.ila KIKwete Hiyo damu itakulilia na familia yako kwa kuwa uliingia nmadarakani kwa kutumia uovu wa kuiba kura na ndio maana yote mabaya yanaendelea kukutokea na bado mapigo ya farao yatakupata na familia yako maana ulisikaia sauti ya Mungu ukaacha kuyafanya ukafanya moyo mgumu na kukubali matokeo yalichakachuliwa na usalama wa taifa na wajumbe wa NEC na wale wataalamu wa computer. tunawapo poleni sana wafiwa na waliojeruhiwa .na tusiogope kutoa maoni maana ni haki yetu.

    ReplyDelete
  13. Tunahitaji viongoz wenye msimamo kama Mbowe ndio ukombozi utapatikana cha msingi walaumuni wanaoanzisha mgogoro sio wanaopigania haki hivi uchaguzi wa meya ungefanyika kwa utaratibu haya yangetokea nani asiyejua kwamba utaratibu ulikiukwa na CCM walienda kufanya uchaguzi pekeo yao kabla ya siku ya waliyokubaliana huku wakiwekewa ulinzi na OCD kama mtu uelewi kitu gani kinachoendelea Arusha ni bora uka kaa kimya au uulize lakin mbona vyombo vya habari vinaeleza kila kitu
    Ole waenu ambao mnaingiza udini mkifikiri kwamaba propaganda hiyo itaiangusha CHADEMA kumbe itakuja kuleta maafa kwa Taifa lakin uhudhuliaji wa Sheikh kwenye uaga wa marehemu pamoja na maaskofu umeonyesha pigo kubwa kwa wanaoendesha propaganda za udin ndio maana mchanga akili na tathimin akimtuhume sheikh huyo lakin pia kuhama kwa diwan wa sombetin kwenda CHADEMA na kujiudhuru kwa naibu meya kwa tiket ya TLP umeonyesha hali halis bado we mpumbavu unaongee nin....

    ReplyDelete
  14. Demokrasia ndio hii jamani. Tuwaelekeze tu hawa watanzania ambao hawaelewi, tusiwatukane. Wengine wanasema kwa kutokujua, wengine wamelipwa ili watukoroge, n.k.

    Tusiingie wote kwenye kukosa umakini, na kupoteza muda na nguvu zetu zaidi kuwatukana badala ya kutoa mawazo ya kujenga.

    Kwa vile serikali na makada wa chama tawala nao wanasoma maoni haya, tuwape tu vidonge vyao. Wakimeza wapone, wasipomeza wafe wao kwa ujinga wao.

    1. Tatizo lao kuu ni kuwa inaelekea hawajui kusoma au kuchanganua sheria zilizopo. wanafanya kazi kwa amri ya bwana mkubwa tu. Kwa vile mkubwa kasema staki maandamano, jamaa anazua sababu za uongo ili asitishe maandamano.
    2. Serikali hii haioni mbali. Wanatumia nguvu nyingi kuwakandamiza wananchi, badala ya kuwaongoza walete maendeleo. Wanasahau kuwa sisi ndio ndio tunawalipa mishahara yao. Hata akina Dowans na wenzake wasingetaka kuja kufua umeme TZ kama sio michango yetu.
    3. CCM oneni aibu, mtaumbuka vibaya. Tumewapa kula miaka mingi, tuheshimuni hata kwa unafiki.
    4. Hivi vyombo vya dola mnavyoringa navyo ni watoto wetu, wakichoka watawageuka na kuwamaliza.

    ReplyDelete
  15. La, sikubali kwamba tunahitaji "viongozi kama Mbowe. Mbowe na wenzake wanaleta hatari kubwa nchini. Mwanzo wanafanya maandamano,halafu watu wanatokomea,halafu wanafanya maandamano mengine,halafu wanatangaza maandamano kote nchini. Yeye katika hotuba yake amekiri kwamba nia ya maandamano kote nchini ni kuwahamasisha Watanzania. Isitoshe anasema hawataenda mahakamani yaani wale waliofunguliwa mashtaka Arusha. Hizi zote ni mbinu za vurugu, uharibifu na ukaidi ambao waweza kuiletea Tanzania balaa. Mbowe anasema hadharani kwamba hawezi kutii amri ya mahakama! Fikiria iwapo kila mtuhumiwa nchini akiamua hivyo, Tanzania itakuwa wapi! Anakebehi sheria na kuwachochea watu kufanikisha hali ambayo sheria haitawali (anarchy). Yeye na wenzake wanatafuta kila udhuru kufanya shari. Lazima wakomeshwe la sivyo Watanzania tutajuta. Hata kama makosa yakifanyika ufumbuzi ni kutafauta suluhisho, sio kuchochea moto.Wao kwani hawakuhusika na maafa ? Na sasa wameanza kutumia maiti katika ulowezi wa siasa.

    ReplyDelete
  16. Poleni sana ndugu zangu mliopatwa na matatizo.
    Kwa kweli ninamsifu Mbowe na Slaa na uongozi wote wa CHADEMA. Tuache unafiki wamemsaidia sana Rais kujua mambo mengi yanayo vurundwa huko chini na ndio maana mashirika yanakufa. Lingine kubwa na la kihistoria ni kuwavalisha watanzania ngozi ya ujasiri bila kuogopa hoja. Tungekuwa hivi anzia mwanzoni mashirika yetu yasinge fikia hapo yalipo sasa hivi.

    Sisi watanzania tusingekuwa watu wa kukimbia na maduka mkononi, ungekuta watanzania tunafanya kazi kwenye nchi yetu kwa amani, na kila mtu anauhakika wa maisha. Ninacho mshauri Rais Kikwete aache kufanya kazi kwa chama kimoja kama anataka kufanikiwa. Sisi tunachotaka ni maendeleo sio sifa ya mtu haitusaidi kitu chochote. Yaani pale jana serikali ingetuma hata mtu mmoja wa kutoa rambirambi.

    ReplyDelete
  17. Wewe unayesema kuwa kama viongozi ni kama kina Mobwe tutafika? I think akili zako zimeenda likizo.So kwa uongozi wa kina IGP na Makamba ndo tutafika kwa kupiga risasi za moto raia? Think of millions of Tanzanians who are extremely poor! think of Dowans, Richmond,Meremeta, and many other scandals.. then uache huo ujinga uliojipakia!

    ReplyDelete
  18. Siwezi kuamini kwamba kuna wasomi ambao hawawezi ku-control akili zao. Kweli tunakipenda chama cha chadema lakini hizi jazba hazitufikishi popote kwani ina maana tukisha chukua hii nchi ndiyo tutakuwa kila mtu ni akikosea ni wa kufunga, kupiga, kufukuza kazi au kuumiza na kulipiza visasi kila siku na kuummbua watu bila kujali utu wa mtu. Mi naona bora kama jazba zingepungua au kungekuwa na diplomacy kuanzia ngazi ya viongozi hadi kwetu sisi Wanachama. Inatisha kuona kama kutakuwa na sodoma na gomora inayo tokana na sisi na si wenzetu. Kukosa ni ubinaadamu hata nzi anakosea kuingia kwenye mchuzi wa mtu bila idhini. Sasa iweje kila kukicha malumbano?? Jazba, mihasira, kutaka kufunga watu, kuwashitaki, kulipa visasi, kuataka watu waachie ngazi za kazi zao, huu ni uongozi kweli?? Viongozi wa ngazi za juu wa chadema, jirekebisheni na kauli zenu. Kama hamuwataki viongozi wenzenu wa vyama vingine, vile vile nasi wanachama wenu wa chini mbeleni tutakiona cha moto kama tutafanya makosa bila kukusudia. Mnatisha kwa mihasira na mijazba jamani. Kila kukicha malumbano, yataisha lini? Subira huvuta kheri, 2015 haiko mbali, anaye lilia uraisi ataupata, anaye lililia uwaziri ataupata muda ukifika, anaye taka umeya, atapewa tu Mungu si mjinga, mbona mnalazimisha vitu bila kusubiri muda muafaka?? Au mnataka vita nchini?? Tunachokigombea kila siku ni nini? Uhuru, dowans, uraisi, amani, maendeleo kwa wote, hasira za kuukosa uraisi, vyeo au nini? mwishowe tutaonekana kama vile watu wa ajabu kugombana kila leo na wenzetu. Tujaribu kuwa wastaarabu na wenye subira kama watu walio kwenda shule. Hata wanao tutetea wakisikia tunagombana kila siku matusi na makelele hawatatuelewa.Kila jambo na wakati wake, tuzingatie kwamba mijadala ya kampeni ilisha pita, ya nini kila siku maneno jamani??

    ReplyDelete
  19. MSAIDIENI HUYU JAMAA ANAKIU YA KUELEWA.
    Jamaani nisaididieni tafadhali chonde chonde nimekwama, mimi nimechaguliwa au nimechagua kuwatumikia wananchi wa mkoa wa Tanga kama mbunge wao, na nimeapa "Mimi nipotayari kuwatumikia wananchi wa Tanga kwa nguvu zangu zote, sinta kwenda kinyume na sheria za nchi yangu", na ninajua ile ni nafasi kwa ajili ya kutetea watu wa Tanga hakuna tena nyingine zaidi ya hiyo na ninajua serikali imetenga hiyo nafasi kwa ajili yao wawe na wawakilishi wa kutosha bungeni na tume ya uchaguzi imeniona ya kuwa ninaweza kushirikiana na watu wa Tanga na kuwatatulia matatizo yao, leo ninakiuka ninakipeleka kile kiti Arusha ambako hata serikali imewapelekea wawakilishi kama waliotumwa Tanga, hamuoni kama mimi ni tapeli, au mimi ni mwizi. Kwanza nimedanganya umma, pili serikali, tatu nimevunja sheria niliyo apa.

    Sasa watu wa Tanga nafasi yao waliyonayo ya viti maalumu ndio hiyo je nitakuwa nimewatendea wananchi wa Tanga haki au nimewanyanganya kofia yao ninaipeleka sehemu nyingine. Hicho kiapo nitakuwa nimekipata wapi au huo uhalali wa kuwatumikia wananchi wa Arusha kama mbunge wao wakati sijatumwa na serikali wala sijachaguliwa na wananchi. Nitakuwa nimeupata wapi? Ingekuwa ndani ya mkoa sawa lakini nimeenda kuwanyang'anya watu wa Tanga nikapeleka Arusha. Hata kama chama kitapanga hakiwezi kunitoa ndani ya mkoa mimi ninavyo jua ni makosa. Lazima niwe mle ndani ya mkoa hatakama kuna jambo limetokea serikali na wananchi wanajua mimi nipo pale.

    Kama kuna hii sheria kwa kweli tunawadanganya wananchi kwa akili yangu. Na ndio maana zuluma, ufisadi, rushwa, utapeli haviishi. Serikali itupie jicho hapa au ifafanue zaidi hili lieleweke. Hii ni mara ya kwanza ninaisikia. Sasa Rais uone jinsi watu wako wanavyovurunda wakikosolewa wanakuwa wachungu kama pilipili. Tunarudi kule kule kwa baba wa Taifa Mw/J. K. Nyerere aliposema, kila mtu anapanga sheria za nchi kama ratiba ya nyumbani kwake.

    ReplyDelete
  20. SWADAKTA MBOWE MAUAJI YA ARUSHA NI YA KUPANGA NA MLIOPANGA NI WEWE,SLAA,NDESA NA LYMO ILI MJINUFAISHE KISIASA. DAMU ILIYOPOTEA HAITAKWENDA BURE NA ITAKUWA LAANA KWENU HAMTAIONA PEPO MILELE HAPA DUNIANI NA KESHO KWA MUNGU

    ReplyDelete
  21. mliochangia huko juu wote majuha tuu,ngekua mnaakili msingechangia kwenye vitu ambavyo mnajua hamuwezi kuvibadilisha hata iweje!!!

    ReplyDelete
  22. Juha wewe unayefanya mambo kama kondoo kwa maana mmoja akielekea huko basi wote humfata huko,hatubadilishi kitu hapa,hao wachaga walipanga hilo jambo kwa manufaa yao ya kisiasa,na kamwe Ikulu hamta iona. TOKA LINI MCHAGA AKAJALI UHAI WA MTU KWENYE PESA?

    ReplyDelete
  23. Ukabila tunaondekeza, ujinga tulionao ndio vitakuwa msiba mkubwa sana hapa nchini.... lijitulizima linafsmilia kila siku ya mungu kuanzia wanawe mpaka lenyew wanachangia mafisadi...leo halioni ....bado lang'aniza tu ccm ccm ccm kwanza utakufa maskini pili, machafuko yatakayo fuata hayata kupitia mbali bali hapo hapo kwenye shingo yako na itakula kwako mazima... amka wewe Tunahitaji TANZANIA MPYA..... FREE OF CORRUPTION... SUCKER

    ReplyDelete
  24. ukombozi gani atautoa mtu mwenye makengeza?kwetu sisi ni mtu aliyelaaniwa na mungu tena shetani mkubwa baba yake ndie aliyekuwa mkurugenzi wa kwanza wa tume ya ubinafsishaji wa mashirika ya uma alikuwa mwizi tu na baada yahapo akaja mwizi mwingine samueli sita leo hii eti watu hao wanauchungu na nchi msiojua kaenikimya sita alikuwa na masi kibao ya msavu company lmt aliitoawapi hela ya kupata magari hayo tena enzi ya nyerere?

    ReplyDelete
  25. chadema hamna akili kumpa uenyekiti mtu mwenye malyenge mlifikiria nn?mzee slaa vipi mtumishi wa mungu muombeeni huyo shetani aliyenae huyo mboe atoke ili machoyake yawe sawa ndipo atakuwa na akili

    ReplyDelete
  26. tatizo la mboe linaeleweka machoyake yalivyo ndio naakili zake zilivyo msimlaumu sana wachungaji watumishi wa mungu muombeeni huyo pepo alilonalo limtoke na arudi kwao moshi hii nchi sio ya wachaga wala wameru tafadhalini sana tunawaomba wasukuma tupo theluthi ya watanzania mbona hatupigi kelele kamanyie wachaga?ukizingatie elimu tunayo yakutosha mikoa yetu yote nitajiri zaidi ya mikoa yenu tupo kimya nyie vichaa?

    ReplyDelete
  27. watanzania sasa tufanye kama tunisia tuiondoa ccm kwa maandamano kupinga udhalimu wao.. ufisadi, umeme,shida za walimu,ajira hakuna,madini yananufaisha waliomadrakani, watanzania tusidanganywe na kuwa hii ni nchi ya amani! amani wapi hali wengine wanafaidi nchi, matajiri wachache, wengi wetu ni hohe hahe, tunadanganywa na hii ni nchi ya amani!!!YALIFANYIKA TUNISIA HATA SISI TUNAWEZA!!!

    ReplyDelete
  28. Tunisia matako yako mpumbafu wewe hii nchi si ya kifalme inautawala wa kisheria mungu ajalie damu ya kwanza ya kumwagika zikija hizo vurugu iwe yakwako,Amen.

    ReplyDelete
  29. Kwa Mtazamo wangu Viongozi wa CHADEMA kweli washitakiwe mahakamani kama Kiongozi mkuu wa CCM Yusuph Mkamba alivyowaelekeza viongozi na wanachama wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA pale HAKI itapatikana japo itachelewa kwani mahakamani hakuna Upuuzi kama wanaofanya Viongozi wa aina ya Yusuph Makamba.yeye anadhani kila kitu CCM itashinda pale chama hicho kinaenda kupata aibu kubwa kuanzia Kiongozi wao Mkuu hadi mwanachama wa mwisho kujiunga na chama hicho kwa sababu ya kupewa fulana ya ccm ya mwaka 2010.pia tumuombe naye makamba aje ahudhurie kesi hiyo kwa niaba ya chama.mwenzetu yeye rambirambi yake amesikitishwa eti na mali ya chama ya chama cha mapinduzi iliyoharibika wakati wa vurugu hizo.ndugu zangu Tukubali tusikubali CCM hadi leo hawajakubali Mfumo wa vyama vingi.

    ReplyDelete
  30. KAMWE WACHAGA HMTAPATA KUWA RAIS WA NCHI HII HATA HUYO SLAA AKAE SAWA IKIFIKA WAKATI WATAMNYOFOA ROHO,HIVI WEWE MBOWE NANI AKUPE IKULU? TUTAKUWA WEHU. UCHAGUZI UMEISHA BADO TU MPO NA UCHAGUZI,HUKO IKULU KUNA NINI JAMANI? CHAMA CHENU NI CHA KIIMLA HATUTAWAPA,MTAISHIA KULALAMA KILA SIKU,NYIE NI MAFIA PENGINE HATA HUYO MKENYA ALIYEUWAWA NA POLISI MLIMLETA NYIE,ATULETEE MACHAFUKO KAMA YA KWAO? KWANI HAMUONI GAZETI LA MWANANCHI LINAMILIKIWA NA WAKENYA NA HABARI ZAO SIKU ZOTE NI MBAYA KWA SERIKALI,WANATAKA WATULETEE MACHAFUKO YA KWAO,POLISI CHUNGUZENI HUYU MKENYA ILIKUWAJE AWEPO KWENYE MAANDAMANO? HAO WACHAGA NI MAFIA HAWAJALI ROHO ZA WATU KWENYE PESA

    ReplyDelete