14 January 2011

Liverpool mwaka wa shetani

LONDON, Uingereza

LIVERPOOL imekuwa kama sikio la kufa ambalo halisikii dawa.Msemo huu imejidhirisha usiku wa kuamkia jana ambapo, Liverpoolikiwa ugenini imekubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Blackpool, ikiwa ni mechi ya
10 kupoteza katika msimu huu.

Hiyo ni mechi ya pili kupoteza tangu kuingia kwa kocha mpya wa muda, Kenny Dalglish ambaye alichukua mikoba wiki iliyopita baada ya klabu hiyo kumtimua Kocha Roy Hodgson, baada ya klabu hiyo kupata matokeo mabaya.

Baada ya kipigo kutoka kwa Blackpool, ambacho kimeifanya timu hiyo kushinda mechi zote mbili msimu huu, King Kenny  alisema: "Wazi ni changamoto kubwa, hutokea kupata kazi wakati haipo."Kila timu ambayo inafanikiwa inahitaji kuwa na bahati, lakini inapotokea kushindwa nahisi kujisamehe wenyewe, tulipata nafasi nzuri.

"Lakini si hivyo tu, tuna kazi kubwa ya kufanya."

Fernando Torres alianza kuifungia Liverpool lakini Gary Taylor-Fletcher  na DJ Campbell, walikuja kufunga magoli ambayo yaliibeba Blackpool na kuifanya kushinda mechi zote mbili katika msimu dhidi ya Liverpool kwa mara ya kwanza katika miaka 64.Lakini Dalglish aliongeza kuwa wachezaji walionesha kujituma sana na kuongeza kuwa ana imani bahati itakuja baadaye.

Liverpool sasa iko katika nafasi 13 kwenye msimamo, ikiwa na pointi 25 huku timu zilizo kwenye eneo la kushuka daraja zina pointi 21.Kocha Ollie alisema timu yake ilicheza kwa kujituma na amefurahi kwamba imeshinda."Tulihitajika kusawazisha goli, tulijituma na kufanya hilo. Niliwaambia watulie kwa kuwa goli la pili ni muhimu kama tutalipata... tulikuja kupata.

Katika mechi ijayo Liverpool itacheza nyumbani Jumapili dhidi ya Everton, huku Blackpool yenye pointi 28 itakuwa ugenini kuchuana na West Brom Jumamosi.

No comments:

Post a Comment