21 January 2011

Wabambwa wakitengeneza noti 'gesti'

Na Cresensia Kapinga, Songea

JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukutwa wakiwa wanatengeneza noti bandia kwenye nyumba ya kulala wageni ya Kisale iliyopo
mjini hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Bw. Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea jana saa tano usiku huko katika nyumba ya kulala wageni Kisale iliyopo mtaa wa Matomondo eneo la misufini mjini hapa.

Kamuhanda aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Daniel Lukinja  (66) Mkazi wa Namtumbo, Emmanuel Eruka (29) Mkazi wa Manispaa ya Morogoro na Fransis Soko (54) Mkazi wa Bombambili Songea Mjini.

Amesema kuwa siku iyo ya tukio Askari Polisi wakiwa kwenye doria waliwakamata watuhumia hao wakiwa na makaratasi yanayodaiwa kutumika kutengenezea noti bandia

Alieleza kuwa makaratasi hayo yaliyokamatwa ambayo yalikuwa yameifadhiwa kwenye box yalikuwa yatumike kutengenezea noti bandia ambazo idadi yake haikuweza
kufahamika mara moja kwa ajili ya kutaka kumuibia mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa uchunguzi zaidi.

Watuhumiwa hao walikutwa kwenye chumba kimoja ambamo ndio walikuwa wakifanya shughuli hizo kwa muda  mrefu hadi taarifa zikawafikia raia wema ambao waliiarifu polisi hadi kukamatwa kwao.

Alisema kuwa polisi inaendelea kufanya uchunguzi wa kina
ili kubaini ukweli wa jambo hilo na kwamba watuhumia hao watafikishwa mahakamani mara tu upelelezi utakapo kamilika.

4 comments:

  1. "HONGERENI WAJASIRIAMALI WETU.NDULU WACHUKUE HAO JAMAA WAKUSAIDIE KUTENGENEZA NOTI MAANA NASIKIA HUKO MNAZOZITENGENEZA MNALIPYA VIJISENTI VINGI.MSIWASHITAKI ILA WAENDELEZENI LABDA NA SISI TUTAFUNGUA BIG INDUSTRY YA NOTI.HONGERA WAJASIRIAMALI"

    LAKINI KWA NOTI MMECHEMSHA LAZIMA MTASOTA JELA HAKUNA NJIA NYINGINE

    ReplyDelete
  2. MAISHA MAGUMU ISIWE SABABU YA KUTAFUTA NJIA YA MKATO/

    ReplyDelete
  3. noti aina gani? we mwandishi hujui kuripoti. lazima ueleze ni noti za shillingi mpya au za obama dola?

    ReplyDelete
  4. wew hawa polisi nao walikosa dili ndio maana hali ipo hivi wangekamatishwa kwa vinjaa vyao hata 500 tou wangeishia

    ReplyDelete