Na Gladness Mboma
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Bw. Pius Msekwa amewataka mwananchi mwenye mawazo Katiba kuwa na subira hadi
pale Rais Jakaya Kikwete atakapounda tume yake ndipo wayapeleke na si vinginevyo.
Bw. Msekwa aliyasema hayo jana wakati alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka mjini Arusha baada ya kuombwa kutoa maoni yake kuhusu Katiba hiyo akiwa mmoja watu walioshiriki kuandika Katiba ya sasa.
"Rais ameshazungumza yote kuhusiana na Katiba mimi siwezi kuzungumza lolote mawazo yangu na ya kwako pamoja na watu wengine yanayohusu Katiba tuyapeleke katika tume itakayoundwa na Rais na siyo kuhoji mtu mmoja mmoja,"alisema na kuongeza;
"Sasa hivi tusubiri tume na siyo kusubiri maoni ya mtu mmoja mmoja, kwani haitawezekana kusikiliza maoni ya mamilioni ya watu wote kwa kuhoji mtu mmoja mmoja. Haitawezekana, ila tume itakwenda kila wilaya na kijiji kuchukua maoni ya wananchi," alisisitiza.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais Kikwete alitangaza mchakato wa katiba mpya katika hotuba yake ya kufunga mwaka 2010 na kukaribisha 2011, ambapo alieleza kuunda tume maalumu itakayoratibu maoni ya wananchi ili waamue jinsi wanavyotaka katiba hiyo iwe.
Katika hotuba hiyo, Rais Kikwete aliwataka Watanzania kutokuwa na jazba katika madai mbalimbali ya katiba na kuweka wazi kuwa tume atakayounda haitabagua chama, rangi, dini na kwamba itaunganisha makundi yote ya jamii.
Rais Kikwete alisema kuwa ameamua kuunda tume hiyo itakayoongozwa na mwanasheria aliyebobea, itakayokuwa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali katika jamii kutoka pande mbili za muungano.
Hata hivyo pamoja na Rais Kikwete kuvunja ukimya kuhusu mjadala huo wa Katiba ambao uliwakuna Watanzania, baadhi yao walimeshauri kuhusu utaratibu unaofaa kwa utekelezaji.
Mh.Msekwa,wewe kaa kimya hakuna unachokijua.Mwache boss wako aongee.Vinginevyo utakua kama kama Mh.Werema mdomo ulivyo mponza.
ReplyDeleteWe Mheshimiwa Msekwa, sasa unasema hutoi maoni yako kuhusu Katiba mpya kwa kuwa rais kashasema. Hivi sisi watanzania tutakuwa lini na uhuru wa maoni yetu hata baada ya rais kusema?
ReplyDeleteMsekwa ni kama mtu ambaye haifahamu katiba na kazi yake. Nashangaa kumbe alishiriki kuiandika! Watu wanapenda madaraka jamani! Tangu 77 mtu anang'ang'ania tuuuuuuuuuuuu uongozi. mpaka kifo kiwaondoe? Ndio maana Kikwete anawaburuza tu! Hawajui chochote kinachoendelea. Afadhali waachie ngazi.
ReplyDeletenashindwa kuwaelewa hawa wazee akina Msekwa na wengineo wa aina yake,unaposubiri mpaka Kiongozi aliyopo juu atoe tamko baada ya msuguano mkali ambao hata yeye mwenyewe anajua tu kuwa asingeukwepa ndipo wanajitokeza.nimuulize Msekwa je yeye na mheshimiwa nani kalitumikia taifa hili kwa muda mrefu hata kama hukuwahi kuwa Rais wa Tz,lakini baado hukustahili kumsubilia Rais ndipo na aje na hoja ya ubabaishaji wake kuhusiana na katiba.siamini kama alihusika serious katika kutunga katiba inayoisha muda wake huenda alichoshiriki na ambacho tutawatahadhalisha WaTZ wakati wa mchakato wasiwe na staili ya kuchangia kama ya maswali ya KIPIMAJOTO cha ITV
ReplyDeletebadala yake washiriki kikamilifu.