Na Reuben Kagaruki
MBUNGE wa Singida Magharibi, Bw. Tindu Lissu, amesema Tume ya Maalumu ya Katiba itakayoundwa na Rais Jakaya Kikwete, ni mbinu ya miaka yote ya
kuteka mijadala hatari kwa CCM na serikali na kuielekeza palipo salama.
Katika maoni yake kwenye mtandao wa Wanabidii jana na baadaye kulithibitishia gazeti hili kuwa hayo ni maoni yake binafsi na si msimamo wa chama, Bw. Lissu amesema mara mjadala unapoanzia nje ya chama au dola ni hatari kwa watawala, hasa pale ukiachwa ujiendee wenyewe bila kuingiliwa.
"Hapa ndipo watawala wanaingia kwa 'gear' ya Tume ya Katiba. Tume hiyo inajengewa hoja yenye maneno matamu na rais, inakolezwa utamu kwa kuwekwa mtu mmoja au wawili (kwa mfano 'mwanasheria aliyebobea)," alisema Bw. Lissu na kuongeza;
"Kwa hiyo, maneno kama 'Tume yenye uwakilishi wa makundi mbalimbali ya kiraia' ni chumvi tu inayopakwa kwenye mhogo mchungu ili ulike kirahisi."
Alisema wananchi wanaambiwa tuwe na subira hadi Tume ya Rais itakapomaliza kazi yake.
"Tunaaswa tuwe wavumilivu ili tule mbivu na katu tusiwe na jazba, munkari au kelele wakati mjadala unauawa pole pole kwa kupitia tume," alisema Bw. Lissu.
Alisema watu wachache wanaoendelea kupiga kelele kuwa mjadala umetekwa nyara, wanashambuliwa kuwa wanaonea wivu wale walioteuliwa kwenye Tume ya Rais, au wanaitwa walalamikaji tu wasiokuwa na lolote la kujenga au ni wakosoaji wa kila kitu kinachofanywa na mtukufu Rais hata kama kina maslahi kwa nchi.
Bw. Lissu alitoa mfano wa tume nyingi ambazo ziliwahi kuundwa, lakini ripoti zake hazijawahi kutekelezwa.
Lissu yuko sahihi kabisa. Uundwaji wa tume ni danganya toto, ili wapitishe masuala yatakayochelewesha kifo chema cha CCM. Sisi tunasema hatudanganyiki, katiba siyo ya CCM, Rais au mtu yeyote, Katiba ni Watanzania wote.
ReplyDeleteUshauri wangu ni kuwa kwanza itengenezwe sheria ya Bunge ya kubadilisha katiba halafu ndio mchakato uanze, ukiwa unasimamiwa na Bunge ambalo ni chombo cha juu kabisa cha wananchi. nawasilisha
Tundu Lisu tunajua umejitosa kwenye siasa ili upambane. Unakatishwa tamaa baada ya kukuta wote unaopambana nao hawana gloves. Sisa siyo mapambano ndugu yangu ni majadiliano. Mojawapo ya kazi ya serikali ni kuchukuwa mijadala yote na kuifanyia kazi. Tundu anaita kuteka mijadala. Badala ya kutumia jina tume mnataka baraza la katiba. Je, hilo baraza litateuliwa na nani? Tukumbuke kuwa kiongozi pekee chaguliwa na watanzania wote ni Rais, wengine wote wanachaguliwa na baadhi ya watanzania. Katika maana kamili mtu anayewakilisha watanzania wote ni Rais. Ni sahihi kabisa Rais kusimamia zoezi hili, ila lazima ahakikishe anasimamia maslahi ya wote. Tukishaona Rais anapendelea watu wachache katika kusimamia mchakato huo basi hatuna budi kuja juu kwa gharama yoyote ile kutetea maslahi ya wantanzania wote. Ningewashauri akika Lisu na wenzake kuwa na subira kuona utendaji wa rais katika hili kabla hatujamhukumu. Tanzania sasa inageuka kuwa kila mmoja ni kiongozi kitu ambacho ni hatari kwa taifa letu. Huu mchakato wa kupata katiba usiposimamiwa na kuongozwa utageuka kuwa vurugu. Rais ana mamlaka ya kusimamia mchakato huu tumpe nafasi.
ReplyDeleteNaomba mjadala wa katiba ujadiliwe kwa umakini zaidi bila jazba, tusubiri tuione hiyo tume itakayoyeuliwa na rais ikoje ndipo tukosoe au kuikataa. Naamini nguvu ya umma siku zote hushinda
ReplyDeleteNina muunga mkono Lissu kama watanzania hawatashirikishwa kwenye katika hiyo kamati ni bure watanzania tunapoteza muda. Katiba itakayotengenezwa bado niya chama kimoja. Ninashindwa kuelewa lengo la serikali kuchagua mwanasheria bingwa, ambaye anaelewa zaidi ya watanzania wanaotaka utawala wao. Mimi ningemuomba Mh Rais kuliacha hili suala la kamati huru kutokana na fani za watanzania. Mf wanasheria, wafanyakazi, wanafunzi, wakulima, wafugaji, waliopo nje na balozi zao, taasisi mbalimbali, vyama vya siasa nk. Hapa ndipo itatengenezwa katiba inayoendana na maisha ya huyu mtanzania na tutajua anataka nini na nini kiboreshwe zaidi. Mh Rais akiteuwa kamati bado malalamiko yatakuwepo na watu hawatasoma kilichoandikwa ila ni kuanza kupiga makelele. Wabunge wakae wa wananchi wao, wachaguane kutokana na hali iliyopo kwenye jimbo lao. Baada ya kupata hizi kamati kwenye mjimbo kuwe na kamati chini ya wizara ya sheria na katiba ambayo itachaguliwa na mkutano wa katiba. Ikiwezekana hapa pawe na barua za maombi na zipitishwe na mkutano huu wa katiba.
ReplyDeleteHivi, wanao sema kuwa Katiba si ya rais, au CCM au serekali na ni ya watanzania mbona wanakosea sana. Je Kikwete, na wana CCM si watanzania au ni ubaguzi unaonyeshwa na hawa ndugu zetu wa Chadema? Neno 'WATANZANIA' isitumike kana kwamba wanacho sema wana Chadema ndio matakwa ya wote. Hiyo sio kweli na chadema wasidanganyike kuwa wana mamlaka ya kuwasemea wote.
ReplyDeleteYa pili ninge omba Chadema hasa Dr Slaa amuheshimu Rais wa jamhuri wa Tanzania. Kila kukicha anatokea na mambo hayasaidii. bado anafikiri kwamba kampeni zinaendelea. Na muomba sana ajiheshimu na kuheshimu watanzania waliomchagua JK kuwaongoza. Yeye asubiri hadi wakati mwingine wa uchaguzi ili aombe kura.
Alichoeleza Tundu Lisu ni sawa Raisi Kikwete ni mwenyekiti wa CCM kwa vyovyote vile anaiwakilisha CCM na sera zake, hivyo hatuwezi kutarajia mtu kama huyu aunde tume itakayosimamia haki ya watanzania wote pamoja na masilahi ya vyama vya upinzani, tume ya Kikwete haiwezi kuwa kinyume na CCM na serikali yake. Tunataka tume itakayoteuliwa na Bunge letu la wananchi na itakayowajibika Bungeni. Mfano halisi ni Tume ya akina Mwakyembe ilifanya vizuri pasipo woga kwa sababu haikuwa inawajibika kwa Raisi bali kwa Bunge na kulindwa na kanuni za Bunge Watanzania wa leo sio mbumbumbu tena.
ReplyDeleteNa kwa nini Bung la wanachi peke yao wawakilishe pand zote? Huko nyuma mangapi wanajifanyia kwa masilahi ya vigogo na wao wnyewe. Tunataka mabadiliko dhahiri!! Hata kama tume hamsini na ziundwe lakini kuwe na uwazi tu. Tumechoka kudanganywa...
ReplyDeleteJamani Tunaelewa vyema kwamba CCM iko madarakani kuendesha SERIKALI - Sio kuendesha CHAMA CHA CCM ndani ya serikali. Hapa mujifunze kwanza. Sera za CCM na Katiba ya SERIKALI ni vitu viwili tofauti. Sera zitapitishwa ili zijenge Taifa. Katiba ipo tayari, kwa hio imeshawagusa wengi tangia huko nyuma, watu wanataka mabadiliko.
ReplyDeleteSera mara nyingi ni vitu vipya. Iwapo Katiba (contitution) inawagusa wanachi wote bila kuchagua mwanachama, basi ipo haja ya wengine kuingizwa kusikilizwa nini wachotaka kibadilike. Si lazima wafatwe, lakini iko haja iwapo tunaelewa nini maana ya demokrasia. Iwapo Chama kinaamua tu, basi hata hilo Bunge hamulihitaji kwani Raisi si mwanachama wa CCM, basi akurupuke tu siku moja aseme "mimi" nataka hivi!! Ah! kwa kuwa yeye ni Kiongozi wa CCM?? Yakowapi majukumu yake ya Uongozi wa serikali ndani yao wako waraia wanaotetea vyama tofauti. Jifunzeni siasa, ili Raisi yeyote awe na Amani Madarakani.
Hata huko majumbani hamuamui tu, bila ya kuzungumza na mama wa nyumba, familia memba, hata baadhi ya wakati unahitaji opinion za jirani au rafiki - nje ye familia.
Lakini nyinyi CCM (Chukua Chako Mapema) munazani mukipata serikali ni yenu nyinyi tu. Wajinga sana!!!
kwako DR. ANDERSON WA CHICAGO,
ReplyDeleteKujibu swali lako nani mwenye mamlaka ya kuundwa tume? ni BUNGE la TZN chini ya ibara ya 98 imepewa mamlaka ya kuunda kitu kinaitwa National convention kwa ajili ya kushugulikia swala la katiba. kwahiyo bunge liunde national convention ambayo itayokutanisha wawakilishi wa makundi yote ya kijamii halafu hao ndio waandae hadiju za rejea na kuunda tume ya kukusanya maoni ya wananchi nchi nzima kabla ya kuyawakilisha bungeni kuwa adopted halafu kurudi kwa wananchi kwa ajili ya kura ya maoni (referendum) na kama wananchi wengi wakiunga mkono basi yanakuwa ndio katiba mpya.hii ndio katiba itakayokuwa imetokana na wananchi maana haikuundwa wala haitakuwa na mkono wa kikwete ndani yake kumbuka ndugu anderson ukimpa mamlaka JK kufanya basi ni sawa na methali ya amlipaye mpiga zumari ndio atakayechagua wimbo kwahiyo huyo mteuliwa siku zote atawakilisha na kulinda interest za wale waliompa kazi na siyo mimi na wewe.
RAIS kuunda tume ni kutupotezea muda na matumizi mabaya ya fedha za walipakodi,kwani tume itahudumiwa na serikali kwa fedha zetu,wakati kuna viporo viwili vya tume ya nyalali na kisanga hazijafanyiwa kazi,alafu mnataka tume nyingine ya tatu ya nn?,swala liko wazi katiba mpya ni lazima sio ombi wala maamuzi ya rais hii nchi ni yetu sote,tunataka mchakato wa kuandika katiba mpya,na si blablah za tume.tunakosa subira kwa sababu kunawatu hawavumiliki kama ccm,anayeona lissu kakosa subira basi,ccm imekosa subira kwa kufuja pesa ya walipa kodi katika tume mbili bila kuzifanyia kazi,na wote wanaoridhikia na hii danganya toto ya ccm,wanamaslahi yao binafsi au ni wavivu wa kufikiri,
ReplyDeleteTumechoka kuburuzwa kama ming'ombe. Tunaiomba hiyo TZ ya Ikulu iache watanzania huru watafute maendeleo na jinsi ya kuondokana na huu umasikini. Tumechoka na blabla za CCM. Wanashindwa kuwaamini watanzania eti kwa sababu ya CHADEMA. Hivi CCM ni nini na chadema ni nini?Sisi watanzania masikini tunaomba tujiwekee sheria zetu kutokana na uwezo wetu. Kama hamtaki basi wapeni hao watanzania wenye nchi huko Ikulu.
ReplyDeleteLISSU AMESEMA SAWA. LAKINI PIA HAPA NDIYO MAHALI PA RAIS KUJIPIMA. HANA BUDI KUSIMAMA KAMA RAIS NA SIYO MWENYEKITI WA CCM KWANI SWALA LA KATIBA SI LA CHAMA BALI NI LA WANANCHI NA NCHI YOTE. KWA HIYO ANAPOKWENDA KUCHAGUA TUME, IWE KWAMBA ANACHAGUA TUME AMBAYO TANGU KUUNDWA KWAKE HAITAUNDWA KISIASA WALA WATU WAKE WASIINGIZE ITIKADI HIZO. NI VIZURI IKAWA TUME YA WASOMI WALIOBOBEA KWENYE SHERIA ZAIDI KULIKO SIASA. KATIKA HILO, TUME PIA IWAJIBIKE KUFANYA KAZI KUONDOA HISIA MBAYA ZINAZOENDELEA KUJENGEKA JUU YA RAIS KUTEKA MJADALA, NA KWAMBA WAO WAMECHAGULIWA KWA UPENDELEO ZAIDI ILI KU-UHODHI.
ReplyDelete