04 January 2011

Pinda awaomba radhi Wakatoliki

Na Sammy Kisika, Sumbawanga

WAZIRI Mkuu, Bw. Mizengo Pinda amewaomba radhi viongozi wa dini hasa Kanisa Katoliki kutokana na kitendo cha baadhi ya wafuasi na wagombea wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutumia kauli zinazokinzana na imani zao wakati wa kampeni za uchaguzi uliopita.

Bw. Pinda ambaye pia Mjumbe wa halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM, aliomba radhi hiyo katika kikao baina yake na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini na baadhi ya wazee maarufu wa mjini hapa jana, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Libori mjini Sumbawanga.

"Najua tulimkwaza Mhashamu Baba Askofu (Damian Kyaruzi), tumekejeli imani ya dini yake, tunaomba radhi. Mimi naomba radhi kwa niaba ya CCM na serikali. Si hapa tu (Sumbawanga) lakini ni maeneo mengi nchini kama vile majimbo ya uchaguzi ya Hai na Same ambapo baadhi ya wagombea katika kuomba kura ya ndiyo, walilazimika kutumia baadhi ya maneno yanayotumika katika Injili.

"Uchaguzi mkuu uliopita haukuwa laini kama ilivyotarajiwa na kutazamiwa, lakini badala yake ulikuwa na changamoto nyingi ikiwemo tofauti za kimtizamo na kiimani, hivyo kwa yale yaliyojitokeza ya baadhi ya waliokuwa wagombea kugusa imani za dini za watu, halikuwa lengo lao kufanya hivyo na tunaomba mtusamehe kwa yote yaliyojitokeza na kukwaza imani za dini zenu," alisema Bw. Pinda.

Kauli hiyo ya Bw. Pinda imekuja wakati Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga likiwa limewasimamisha na kuwatenga baadhi ya waumini kwa kukashifu Utatu Mtakatifu kwa kuufananisha na kaulimbiu ya mafiga matatu, yaani rais, mbunge na diwani; wakifananishwa na Mungu, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu wakati wa kampeni.

Vile vile waumini hao ambao ni wafuasi wa CCM wanadaiwa kukashifu alama ya kanisa, msalaba, kwa kuuzika wakati wa kushangilia ushindi wa mgombea wao.

Wakati Bw. Pinda akikiri makosa hayo na kuomba radhi, baadhi ya viongozi wa CCM mkoani humo wamekuwa wakissitiza kuwa waumini hao wametengwa kutokana na kushabikia chama hicho na mgombea wake wa Ubunge, na hivyo kutofautiana na mgombea wa CHADEMA wanayedai alikuwa anaungwa mkono na kanisa hilo.

Akitoa maoni ya jumla ya uchaguzi huo, Bw. Pinda alisema kuwa kutokana hali iliyojitokeza, CCM na Serikali yake imepata fundisho, na hivyo kuomba katika chaguzi zijazo viongozi wa dini, serikali na vyama vya siasa wakae pamoja na kuweka angalizo ili wagombea wajiepushe na kukejeli imani za dini za watu wengine.

Waziri Mkuu aliwasihi viongozi hao wa dini nchini nzima kuanza ukurasa mpya na kutumia muda mrefu kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo.

Akizungumzia suala la rushwa, alikiri kukithiri kwa vitendo hivyo katika uchaguzi mkuu uliopita na kuongeza kuwa ipo haja ya kuangali upya mfumo wa uchaguzi kuanzia ndani ya CCM ambayo inajiandaa kwa uchaguzi wa viongozi wake mapema mwakani, ili kuhakikisha hautatoa mianya ya rushwa.

Aliwaomba viongozi wa madhehebu ya dini na wazee kukemea kwa nguvu zote vitendo vya rushwa.

"rushwa ni rushwa tu, hakuna haja ya kusema kuna rushwa ndogo hata mtu anapotaka kutimiza haja zake fulani kwa kutoa kitu kidogo bado ni rushwa. Pia kwa mgombea anapotoa doti ya khanga ili apigiwe kura hilo ni tatizo, hivyo naiomba CCM ibadilike, najua ni jambo gumu lakini lazima tupigane nalo kikamilifu. Wagombea nao taabu tu, hasa kwenye chama, safari hii tujirekebishe," alisema Pinda.

Akitoa neno la shukrani, Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo Tanzania mkoa wa Rukwa, Mchungaji Israel Moshi alisema kuwa madhehebu ya dini yamesamehe, na kuwataka viongozi kusameheana kwa kuwa wote ni binadamu.

16 comments:

  1. sasa kiko wapi?nani alitumia dini kupiga kampeni?wao au upinzani?na ni upinzani upi?CUF, NCCR,TLP au CHADEMA?tunashukuru mmelifahamu hilo, badala ya kusema udini umeingia, kumbe nyufa ya udini mmeinza nyie

    ReplyDelete
  2. ccm hawafai kabisa kutokana na ulangai wao ambao sasa unakwenda kwenye mabadiliko ya katiba wanataka nako wawadanganye watanzania. CCM chama hakifai kabisa ni ufisadi mtupu ulipo hapo.

    ReplyDelete
  3. Sasa sikiliza basi, si unaona hata hao wanaomba samahani eti anaomba samahani na Serikali inaomba samahani. Upumbavu gani huu. Ikiwa ni chama kilofanya makosa basi ni chama kiombe samahani sio serikali iombe samahni. Munatutia aibu wana siasa. Vipi kiserikali atoke mtu binafsi aombe samahani kwa niaba ya srikali - Hakuna mwny power hio ila ni Raisi tu, kwani yeye pekee pale anarepresent leadershipo ya serikali na sio ajili ya chama kwa wakati anapokuwa madarakani. Kwa hio mweny kuomba msamaha kwa niaba ya chama basi asiitie serikali hata ikiwa wakati ule chama hicho kiko madarakani. Kwa maana, iwapo chama kingine kikifanya kosa wakati kimo madarakani, tuilaumu Serikali???

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli inafurahisha, iwapo sote tukubaliane hilo: kuwa hakuna Udini wala Ukabila wala urangi kwenye kampeni zetu. Na pia Watanzania sote tuwe wamoja katika maadili ya serikali, kundeleza serikali yetu. Hii ni dalili njema ya kuendelea kisiasa Tanzania. Tuendelee hivo. Kuna ubaya gani mtu kuomba radhi unapokosa. Mimi binafsi nampongeza muomba radhi hapa. Inafurahisha kwamba yapo makubaliano mema.

    ReplyDelete
  5. Kwa kosa hili la CCM: ni la KIKATIBA ( uhuru wa Mwananchi kuamini dini anayochagua ),Anyaeyeweza kuomba radhi kwa Wananchi ni Rais wa Nchi na siyo Waziri Mkuu.Kwa hiyo Pinda amwambie Rais aifanye hiyo kazi na siyo yeye, kwani yeye ni Waziri mchaguliwa tu.

    ReplyDelete
  6. pinda acha waliokosa waombe radhi kwa midomo yao usifuge vilem vy ccm,

    ReplyDelete
  7. Hakika Dini imeonyesha mfano wa msamaha. lakini hili lingetokea kwa waislam hata kikwete angelivalia njuga kushinikiza koa lakini kwa wakatoliki kikwete kimya, eti kamsakizia pinda, jamani acheni tu, tayali wamesha anza tutamshauri kikwete achague waislam, maro oooo tunaunda tume ya kupendekeza wajumbe wa kuunda katiba, mara hooo mahakama yakadhi ithaminiwe. kanchi ni yawaislam basi mhakama ya kadhi na ikubaliwe

    ReplyDelete
  8. WE wakome waislamu kama ulivyokoma ziwa la mama yako. sisi tunaongozwa na maadili ya dini yetu na siasa zenu chafu na za ulaghai hazina nafasi kwenye UISLAMU.

    ReplyDelete
  9. ndugu zangu hamna kazi za kufanya?mambo yenu ya siasa yana tukera tumechoka uchaguzi upo 2015 subirini siombali sasa tunahitaji kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo mboe kwao wanahela slaa wabunge wa chadema wanamchangia anahela ya mboga tu tunahitaji kuwaza na kujituma ktk maendeleo ya taifa letu

    ReplyDelete
  10. We koma kuwasakama Waislam, kama ulivyo unatakiwa kuangalia nini kimesemwa, kama wewe ni Mkatoliki basi ujue watu wa madhehebumengine wanajua janja yenu, Pinda ameomba msamaha wajibu wa muungwana kukubali na sio kuanza kuhoji kwanini CCM isiombe msamaha, je katika Kanisa Katoliki mtu anaruhusiwa kuiba Mke wa mtu? Je kuna talaka katika Kanisa lako, Waache Waislamu na mambo yao, wao ndio walihangaika kudai Uhuru wakati Kanisa Katoliki likiandamana kupinga Uhuru, Chukua picha ya TANU uangalie waanzilishi na wadhamini wa TANU ni kina nani, Jiulize wakati huo wewe uko wapi na ulikuwa unafanya nini? ndio utajua historia ya nchi hii. ukiombwa msamaha ni wajibu kusema tusameheane kama kweli wewe ni Mkristo, Hata Yesu alikuwa akisamehe, Je umesahau kuwa ukipigwa kofi shavu lakushoto Geuza na la kulia upigwe vilevile?

    ReplyDelete
  11. Huyo Mjinga anazungumzia mambo ya Waislam katika tukio la Sumbawanga wakati walioshututumiwa na kanisa ni wakiristo wenyewe kwa kuingia kanisani na jeneza na mslaba kwisha kwenda kuzika. Ni vyema usichanganye Uislam na laghai zenu,sisi tunaongozwa na maadili ya dini yetu kama dini na mwenye interest na siasa ni zake mwenyewe na si mwongozo wa dini na ndio maana unaona tunapambana na Wamerakani katika Saudia Arabia,Afghanista,Iran,Palestina na kwingineko kwa sababu hatukubali kulazimishwa kitu kilicho against na dini yetu. Wewe hujui historia ya nchi yako na pale unapoambiwa ulikuwa wapi wakati huo wa kupigania uhuru,huenda wewe au wazazi wako mlikuwa mnachunga mbuzi.

    ReplyDelete
  12. mimi nashangaa hao waislamu wanavyomshambulia mtoa mada hapo juu,yeye ameongea kweli,CCM iliwakosea sana wakristu wakati wa kampeni kwa kuendesha kampeni kwa misingi ya udini na baadae kuwatuhumu maaskofu kwa kuendesha kampeni za kidini,tatizo utawala wa kikwete unaegemea sana upande wa waislamu,na kama wanataka amani katika nchi hii basa hiyo mahakama ya kadhi wakaifungulie bagamoyo tu.

    ReplyDelete
  13. Tunakuambia na wewe koma kuitaja Uislamu,mambo ya Sumbawanga yaliwahusu Wakristo wenyewe waliokwenda kanisani na jenaza na msalaba na baadaye kuuzika,mahakama ya kadhi itafunguliwa huko kwenu vijijini kwenye ukandamizaji mkubwa wa haki za kina mama zenu mliowageuza ngombe wa kuwalimia na mahakama hiyo itawakomboa tu,mnaiogopea nini wakati haiwahusu?

    ReplyDelete
  14. SASA NYINYI WAISLAM MNATOWA MAONI AU MNATUKANA, HUKO NIKUJIONYESHA MLIVYO, JAMA WATOA MAONI MBONA MNAONYESHA KUTOKAMAA, WAWEZA KUANDIKA LUGHA ZA NAMNA HII GAZETINI AU MNATANIA. MBONA MMELIWEKA MBELE HILI LA UISLAM, INAMAANA TANZANIA NI YA WAISLAM AU WKRISTU TU. KAMA MNALUMBANA KWA VIGEZO VYADINI HAMNA KAZI, ISIPOKUWA KUFUNGUA INTERNENT NA KUKODOLEA YASIYO NA MAANA. ACHENI UPUUZI MMETUCHOSHA.

    ReplyDelete
  15. inasikitisha kuona watanzania wamefikia hatua hii. viongozi wa kiislam na wakristu kaeni pamoja mfikilie nini muwashauri watu wenu ili yasisa yasihusishwe a udini. watanzania wenzangu acheni malumbano kwani hapa wengine ni ushabiki tu kuandika ili waonekane kuwa wameandika. haifai acheni jamani nawasihi, acheni mitafaruku tujenge nnhi yetu. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  16. Hovyoo unawaona Waislam ndio wanatukana?,sisi ni wastaarabu sana.Chokochoko ya nchi hii ni kila muislamu anaposhika madaraka,milifunga midomo yenu wakati nchi inasulubiwa na Mkapa ati sasa ndio mnaona.

    ReplyDelete