*Prof Safari asema kuilipa ni kukiuka katiba
Na Waandishi Wetu
KAMATI ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana limeopendekeza kurudishwa
bungeni suala la Kampuni ya kufua umeme wa Dowans/Richmond ili Watanzania wajue nani alisababisha serikali kubeba mzigo wa kutakiwa kulipa sh. bilioni 94 na awajibishwe.
Kwa hatua hiyo, UVCCM wamesema endapo Kamati ya Dkt. Harrison Mwakyembe ililidanganya bunge, mbunge huyo ambaye sasa ni Naibu Waziri wa Ujenzi awajibishwe na kama kuna mtu yeyote alijiuzulu bila hatia, asafishwe.
Tamko hilo lilitolewa na Mjumbe wa Kamati hiyo na Mwenyekiti wa UV-CCM Mkoa wa Arusha, Bw. James ole Millya kwa niaba ya kamati hiyo, ilipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari jana kuhusu maamuzi ya kikao chake kilichofanyika juzi.
Alisema endapo kosa hilo ni la serikali, basi itamke ni nani mmiliki wa Richmond, aliyehamishia mkataba wake kwa Dowans ambayo inatakiwa kulipwa mabilioni ya fedha za walipa kodi.
"UV-CCM inaitaka serikali kuwataja rasmi wamiliki wa Richmond. Haiingii akilini mmilikishwa (Dowans) ajulikane na alipwe fidia ya sh. bilioni 94, wakati mmilikishaji (Richmond) asijulikane.
"Hao Dowans waliotajwa na serikali ambao ndio walinunua mali za Richmond waisaidie serikali yetu kuwataja wamiliki halali wa Richmond ili wao ndio wawajibike kulipa pesa hizo badala ya serikali," alisema Bw. Millya.
Katika mkutano huo ambao wajumbe wa kamati hiyo walizungumza kwa zamu kila mmoja na mada yake, UV-CCM iliitaka serikali kuwa na msemaji mmoja ambaye atatoa ufafanuzi na maelezo juu ya masuala makubwa yanayogusa maslahi ya taifa, na kulaani hatua ya sasa ambapo mawaziri wamekuwa wakitoa maoni tofauti hadharani.
Kwenye suala la hali ya CCM na UV-CCM lililotolewa tamko na Bw. Marwa Mathayo ambaye pia ni mwenyekiti wa jumuiya hiyo mkoani Mara, umoja huo uliwakemea baadhi ya viongozi wa chama chao na serikali kwa kutopendana na kujenga uhasama na chuki, jambo ambalo walisema ni aibu na urithi mbaya kwa vijana.
"Watambue kuwa wao walipokuwa vijana hawakurithishwa chuki na uhasama miongoni mwao. Vitendo hivi haviwezi kuvumiliwa. UV-CCM inawataka sasa wale wote wanaoendekeza uhasama na chuki iliyojengeka katika msingi wa ubinafsi, waache mara moja. Vinginevyo tutawataja kwa majina na kuwataka vijana kote nchini kuandamana na kuwalaani, maana uhasama na chuki zinaleta mipasuko katika jamii na chama kwa ujumla," alisema. Bw. Mathayo.
Akiwasilisha hoja ya mikopo ya elimu ya juu nchini, Bi. Zainab Kawawa alisema kuwa bodi ya mikopo haijafanya kazi yake vizuri na hivyo kupendekeza ipinduliwe ili kunusuru vijana wa Tanzania wanaoteseka kwa kukosa mikopo.
"UV-CCM imebaini kwamba kuna urasimu unaofanywa na watendaji, na haiingii akilini Mkwawa University wagome kwa kutolipwa posho zao na baada ya siku moja walipwe. Jambo hili si utamaduni wa vijana wa Kitanzania na halikubaliki popote duniani. Wale wote wanaohusika, CCM ichukue hatua ili serikali iwawajibishe mara moja ili tabia hii isijirudie.
"UV-CCM haiko tayari na katika historia yake haijawahi kuwa tayari kuwaona vijana wa vyuo wakigoma ndipo matatizo yao yanatatuliwa. Wale wote wanaotaka kuanzisha utamaduni mpya wa utawala wa kwamba mpaka vijana wagome au kundi fulani ligome ndipo ufumbuzi wake upatikane wapishe ofisi za umma, wawajibike mara moja na serikali iwafikishe mahakamani kwa kuisababishia hasara," alisema Bw. Kawawa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia vyama vya wafanyakazi.
Katika hatua nyingine, mmoja wa wanasheria mahiri nchini, Profesa Abdallah Safari amemuunga mkono Waziri Samuel Sitta, akisema hoja zake ziko dhidi ya malipo ya Dowans ni sahihi kwa kuwa kulipa tozo hiyo ya sh. bilioni 94 ni kukiuka katiba ya nchi.
Prof. Safari aliyasema hayo jana Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari, waliotaka kujua maoni yake kama mwanasheria juu ya mjadala huo unaoendelea nchini.
"Msimamo wangu juu ya Dowans mbona uko wazi, nakubaliana na Waziri Sitta moja kwa moja, naunga mkono hoja za mzee yule, yuko sahihi kabisa, nafikiri ninyi hoja zake mnazijua...lakini mbali ya hilo, kuilipa Dowans ni kukiuka katiba ya nchi, katika ibara yake ya tisa.
"Katika ibara hiyo imeelezwa kuwa serikali italinda rasrimali za nchi hii si kuzitapanya...kuwalipa Dowans inakiuka ibara hiyo...hili ni sawa na lile suala la nyumba za serikali ambalo nashangaa vyama vya siasa haviliongelei kabisa...pia mikataba yenyewe ya kimataifa inasema wazi kuhusu kuheshimu mikataba," alisema Prof. Safari na kuongeza;
"Lakini inasisitiza mikataba inayopaswa kuheshimiwa ni ile iliyo halali tu, si mikataba inayoonekana kuwa na rushwa ya wazi wazi kabisa. Nakumbuka Mwalimu aliwahi kumwambia Kabila mkubwa (Rais Laurent) kuwa asilipe mikataba yote ya feki iliyoingiwa na Mobutu...Mwalimu Nyerere pia aliwahi kupinga mikataba ya kikoloni kama ule wa Nile Basin."
Mara kwa mara Bw. Sitta ambaye alikuwa spika wa bunge la tisa wakati mjadala wa kampuni tata ya Richmond ulipoibuka bungeni, amenukuliwa mara kadhaa akisema kuwa Dowans ni kampuni ya wajanja wachache wanaotaka kujichotea fedha za walipa kodi wananchi maskini wa nchi hii, kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Masikini UV-CCM ile kamati ilikuwa ya bunge na haikuwa ya Mwakyembe..mwakyembe hawezi wajibishwa ila bunge zima kama mnataka hivyo, masikini mmedandia ajenda/hoja, kama hamjatumwa na mafisadi basi mnatakiwa kujenga hoja upya, hayo maono na ndoto zenu mbona mmechelewa kutuambia hivyo mapema?Hata sidhani kama mna uchungu na nchi yetu tukufu ila mna uchungu na CCM yenu, naamini kwa 100% mmetumwa na Lowassa! kwa hio mnataka nani asafishwe?Lowassa?hapana haiwezekani...mmetumwa na tunafahamu hilo.
ReplyDeleteWANAFIKI WAKUBWA NYIE HAMNA LOLOTE MLIFANYALO ZAIDI YA KUTEKELEZA MLIYOTUMWA NA BABA YENU JK. MNGEKUWA NA BUSARA MSINGEANZA NA KUMTUKANA MATUSI YA NGUONI DR. SLAA AMBAYE NI SAWA NA BABA YENU WA KUWAZAA. TUNAJUA MMETUMWA KWASABABU WOTE NI WALEWALE, MNAKITEKELEZA KILEKILE KATIKA SURA TOFAUTI NA HATA SIKU MOJA HAMUWEZI KWENDA KINYUME NA WAFDHILI WENU. SO IT IS BETTER IF YOU STAY OF THIS COZ CCM MTOTO HAWEZI KUMPINGA CCM MZEE, WAACHENI WAPIGANAJI WAENDELEE NA KAZI YAO NYIE HAMUIWEZI.
ReplyDeleteUVCCM Hebu angaliene maslahi ya taifa na wala si ya chama kama kweli mnauchungu na nchi yenu. nani alisababisha vurugu na mauaji ya Arusha kama sio polisi? Achani ushabiki wa chama na muongee ukweli toka mioyoni mwenu na tutawaunga mkono.
ReplyDeletePongezi Uvccm kwa tamko lenu,lina mvoto lakini CCM sio wasi kivu wanamajivuno yasio ya kawaida.Kwa mfano.Mtu kama Mh.Makamba anaweza kupokea Tamko lenu wakati amelewa madaraka?Uvccm jitihada zenu hazitakuwa na nguvu kwa sababu ya viongozi wenu wa ngazi za juu ni matajiri sana.
ReplyDeleteMIMI NADHANI SERIKALI AIDHA HAIJAJIPANGA, AU NI KWA MAKUSUDI IMESHINDWA KUWEKA PRIORITIES ZAKE KISAWASAWA KATIKA KUINUA MAISHA YA WATANZANIA. KUNG'ANG'ANIA KUILIPA DOWANS PESA ZOTE HIZO, HAITAKUWA NA HAKI YOYOTE MACHONI PA WATANZANIA WENGI AMBAO WAMEENDELEA KUKANDAMIZWA NA UGUMU WA MAISHA NA SINTOFAHAMU YA MUSTAKABALI MZIMA WA TAIFA KATIKA KUWAWEZESHA KUBADILISHA HALI YAO YA KIMAISHA.
ReplyDeleteSIO TU KATIKA HILO, BALI KUNA MENGI AMBAYO KWA MACHO YA WATANZANIA YANAHITAJI KUANGALIWA UPYA. KWA MFANO, HIVI NI LAZIMA WABUNGE WAKOPESHWE MAGARI NA SERIKALI? KWA KIPATO WALICHONACHO, KWA NINI WENYEWE WASINUNUE KWA PESA YAO, NA PESA HIYO INAYOTUMIKA KUAGIZA MAGARI HAYO IKAPELEKWA KWENYE HUDUMA ZA WANANCHI? KUNA UHALALI GANI KWA WANANCHI KULIA NA HUDUMA DUNI ZA MATIBABU, SHULE NK., WAKATI MABILIONI YANATUMIKA KUCHUKULIA MAGARI HAYA KWA WATU AMBAO WENYEWE WANA UWEZO WA KUNUNUA?
SERIKALI YA CCM IMEWEKWA NA WANANCHI WA NCHI HII, LAKINI KADIRI SIKU ZINAVYOKWENDA, NI KAMA INAJISAHAU NA KUFANYA MAMBO AMBAYO HAYAWASAIDII WALIOIWEKA, NA IMEWAGEUZA KUWA WATAWALIWA, IKIFANYA MAMBO AMBAYO HATA KATIBA HAIJAYAPA UHALALI.
OMBI LANGU KWA AWAMU HII, HEBU TUANZE UPYA. KAMA MUELEKEO ULIKUWA UNATUPELEKA KUSIKO, INABIDI KUBADILIKA. BABA ASIYESIKILIZA KILIO CHA WANAE HAFAI HATA KUITWA MZAZI. TUANGALIE PRIORITIES ZA KITAIFA, TUACHE KUPELEKESHWA.
Umoja wa Vijana CCM mmelala na mmechelewa,CCM haisimamii serikali wala inavyoendeshwa,viongozi wamejikita katika ulaji zaidi kuliko maadili ya chama,kumbukeni enzi za Mwalimu ilikuwa hachaguliwi kiongozi bila kujulikana tabia yake,leo kuna kina Karamagi hata hatujui walipotokea wanapewa uongozi na matokeo yake ndio hayo mnayoyaona. watizameni kina marehemu Mzee Kawawa,Warioba,Salim na viongozi wa zamani nani tajiri? hawa watu walikuwa waadilifu mno kwa serikali,leo wako wapi,ukienda mahakamani ni uoza mtupu,jaji au hakimu wanatoa hukumu kinyume na sheria hakuna wa kuwakemea na hata ukipeleka malalamiko yako utazungushwa mpaka uchoke maana yule aliyepewa jukumu la kufanya kazi hiyo anaona kama anakupa hisani,nchi imeoza viongozo hawawajibiki ndio maana nasema kuwa NYERERE ALISEMA "ITAFIKA WAKATI WANANCHI WATAMCHAGUA HATA SHETANI ILIMRADI WAONDOKANE NA CCM" NA SASA NAONA WAKATI UMEWADIA,hata nyie vijana mmelala usingizi wa pono,hamko active,mambo mengi ya hovyo yanafanyika nchini mnakaa kimya ndio maana mnaona mashambulizi yanaelekezwa kwenu na watoa maoni
ReplyDeleteHabari feki ni kama hiyo waliyokuja nayo hawa Uvccm, hivi wao wameona mgomo peke yake na wamesahau kama kuna watu walikufa pale Arusha? Sisi tunataka watu wenye moyo wa dhati katika kulikomboa taifa na sio wenye polojo. Mnataka kulipa kisasi kwa kina Mwakyembe, na kusahau kuwa wahusika wa Richmond ndio wa Dowans kwa mlango wanyuma! Acheni upuuzi wenu huo kwani watanzania tunaelewa kamchezo kenu na kutokuwa na busara kwa chama chenu kizima na laana zitawapata kwani mmefikia hatua ya kuwatolea watumishi wamungu maneno machafu mkisaidiana na Chitanda na Baba yenu Makamba. Ana maneno machafu bila kuangalia athari zake hana hata chembe ya busara.
ReplyDeleteKaazi kwelikweli. James Ole Milya ni swahiba mkubwa wa Lowassa. kamtuma!!! Ndo maana kapewa kipengele hicho akisome. UVCCM hawajatueleza ni hatua gani watachukua matakwa yao yasipotekelezwa zaidi ya kuandamana. maana watapigwa mabomu na watawala waliogeuka madikteta. Hayati Mwalimu angekuwepo angekuwa amehamia CHADEMA, maana hii si CCM aliyoiasisi. Serikaoi inatenda mambo isiyoyaamini, na kuyaamini mambo isiyo yatenda. Kwa mara ya kwanza vijana mnatanua midomo yenu, mnataka kuvaa ngozi ya kondoo wakati ndani yenu mu mmbwa mwitu wakubwa. Shigella huyo huyo ndo alikuwa akimtukana Dk. Slaa, mkombozi wa wanyonge, hadharani, leo eti, wanaimba wimbo mmoja ambao chorus yake lazima itakuwa tofauti, maana wanataka kuwasafisha mafisadi. Uchaguzi mkuu ungerudiwa leo, nasema leo, ccm wangeambulia viti maalumu tu vya kupewa katika serikali ya umoja wa kitaifa. Lakini yenyewe, mmmh, imepoteza mvuto. wazee huku vijijini wanailaumu, wanailaani, wanailaumu kuichagua tena, maana vichwa vyao vimefunguka. Mungu ibariki Tanzania, Mungu wasaidie vijana kutambua uzalendo wa nchi yao bila kujali itikadi za vyama vyao.
ReplyDeleteMAFISADI NYIE NA MLAANIWE NA MUNGU.KWANI HAMJUI MMILIKI WA DOWANS NI ROST-AM LA AZIZI NA WHITE HAIR NA CHAIRMAN WA CHAMA CHENU KILICHOOZA?MANYANG`AU NYIE HAMNA LA MAANA NENDENI SHAMBANI MKALIME TUMECHOKA NA MATAMKO YENU YASIYONA VICHWA WALA MIGUU.TUNAJUA MMETUMWA NA KINA LOWASA KUTOA MATAMKO YA AJABU ETI LOWASA ASAFISHWE?HOW?YOU IDIOTS,PUT YOUR OWN HOUSE IN GOOD ORDER KABLA HAMJADANDIA HOJA ZA MSINGI KAMA HIZO.JK,AZIZ,LOWASA NDO WAMILIKI WA DOWANS.SHERIA YA MAKAMPUNI YA MWAKA 2002 HAIRUHUSU KAMPUNI YA NJE AMA MTU TOKA NJE KUFUNGUA TAWI TZ BILA KUWA NA SHAREHOLDER MZAWA,MBONA DOWANS NI YA WAGENI WATUPU?HUYO NAIKO NAYE ASEME PAMOJA NA BRERA WALISAJILI VIPI DOWANS?
ReplyDeleteIDIOTS IDIOTS IDIOTS UVCCM NA CCM YENU WOTE WASHENZI NA WEZI WAKUBWA,MLAANIWE NYIE MAPAKA
HAWA VIJANA KAZI YAO KUTUMIWA TU NA MAFISADI NA WATAWALA WA CCM AMABAO HAWANA MVUTO TENA KWA JAMII SHAURI YA KIKOSA UADILIFU NA DIRA, KUSHIRIKI WIZI WA MALI ZA TAIFA, KUBEBESHA WANANCHI MIZIGO HIVYO KUWATUNUKU UMASIKINI, KULINDANA NA KUTOWAJIBIKA KWA HALI YA JUU. LEO NDIO WANAAMKA!!NILIDHANI MTASEMA CHENGE HAFAI KUWA NDANI YA KAMATI YA MAADILI YA CCM; ROSTAM HASTAHILI KUWA CC MEMBER, MAKAMBA AME EXPIRE ATOKE; LOWASSA AFUKUZWE CCM;NK. ENDELEENI KUTUMIWA NA HAO WAZEE, TUTAONANA 2015. HIVI CHADEMA HAWANA UMOJA WA VIJANA? ITS HIGH TIME. TENA UANZIE KUSINI MWA TANZANIA.
ReplyDeleteAma kweli tusiosoma tunachakachuliwa. Ina maana Richmond hakujulikana ni mtoto wa nani, na ni mtoto wa kwanza, ila mtoto wa pili Dowans anajulikana na analipwa mafao? Na baba mmoja maana wameachiana ziwa.
ReplyDeleteHakuna haja ya unafiki,wanaosema ukweli ni Kina Sita na wengine na wanaonyesha uchungu wa kweli, ni kama sisi tunaolipia luku na mita kwa gharama kubwa za ziada bila sababu zaidi ya wenye akl kutuzidi maarifa.
kama kweli ccm ni ya taifa hili wamtaje huyo boss wa richmond aliyemwachia dowans,ndo tujue ccm si mali ya watu bali ni chama cha taifa hili.walipoona slaa anaenda kusema kuhusu mabilioni ya dowans kule arusha wakawapiga na kuuwa wengine.Slaa is our hero, na ngojeni akutane na wana-habari atatoa moja hadi jingine,lipeni mwaniukwe vizuri.
nyie watoto wa chama,hamyawezi haya,achieni baba zenu watamke. aliyewatuma mwambieni kachelewa.
NGOJA CHADEMA WAJIPANGE VIZURI,SI WALIWATIBUA JUZI NA MABOMU YAO,WE NGOJA BUNGE LA FEBRUARY HOJA IPELEKWE KAMA HAIJAWA KAMA BUNGE LA KENYA,CCM HAWATAKI KUAMBIWA UKWELI,SASA WANAENDA KUPEWA LIVE BUNGENI NA VIJANA WA CHADEMA,SAFU IMETULIA HAINA WASI NA KILA KITU WANACHO,PLUS KINA SITA, MWAKYEMBE NA WALE WOTE WABUNGE WENYE UCHUNGU NA NCHI HII, MBONA HAKUNA MALIPO YA DOWANS HAPO? NANI APITISHE HAYO MALIPO DOCUMENT IPATIKANE HAJIPENDI TAIFA HILI,WANANCHI WANAKATAA NA BUNGE LITAKATAA MAANA WENYE AKL WAMEKATAA NA USHAHIDI WANAO,HAO WENYE DOWANS WAJE BUNGENI KUDAI MADAI WAWEZE KUHOJIWA KAMA WANA UCHUNGU NA MALIPO YAO.UCHAGUZI UMEISHA NDO WANAIBUA MENGINE BAADA YA KUWIN MAISHA.ANAYEDAI AJE INDIVIDUAL APAMBANE NA MALIPO YAKE.
ReplyDeleteKATIBA YA SASA ITAWEKA MAMBO MENGI HADHARAN,YALE YANAYOSABISHA RUSHWA YATAFUTWA.TUTAFIKA TU
Ndugu mlio katika cham twawala!!, kumbukeni kuwa historia itawahukumu siku moja. Mifano iko mingi dunia wala sihitaji kuisema hapa, ila cha maana ni kwamba, ipo siku ukweli utajulikana kuhusu hiyo dowans na mafisadi wote mtahukumiwa. hata kama itachukua miaka mingi lakini mtahukumiwa. Mambo ya muhimu kama umeme (mgao umekuwa ni maisha yetu???), mikataba ya madini na mengineyo mengi. Chama twawala tumieni busara, someni alama za nyakati!!!!
ReplyDeleteUV-CCM, hakuna aibu iliyopo kama kijana tena msomi unaye tegemewa na familia na taifa kwa ujumla ukubali kutumiwa kama kibaraka katika zama hizi ambako ukweli uko wazi kwa kila kitu kinacho endelea Tanzania, hasa katika kuyumba kwa utawala wa nchi na udhalimu wa rushwa kwa viongozi wenye dhamana ya nchi kuendelea kufilisi taifa kwa kutumia ujinga wa walio wengi na katiba dhaifu inayoruhusu mianya ya Rushwa kwa viongozi wadhalimu wa CCM.
ReplyDeleteAibu kwa hao vijana kutumika kama kinga ya kusafishia njia kwa hao wanao haribu taifa letu teule.
Hao uv-ccm ni vibaraka wa wale waliosaliti viapo walizo kula kuwaongoza wananchi.
Tuuwapuze na tuwatupilie mbali maana ni kuundi la aibu na hatuwataki kwa maendeleo ya taifa hili.
DOWANS wakawa ulize hao wanao walea UV-CCM.
upuuzi mtupu wa tamko la uvccm walikuwa wapi kusema mpaka jana wanadandia mijadara makini ya watu prudent and righteous uwe wewe kusema madubwana kama jk white hair na rostam azizi waulize mapolisi ndugu zake na slaa au mapolisi wanaotoka kwa slaa wote wametupwa nje njoo shinyanga umuone aliyekuwa ocd yuko pembeni kwa sababu tu anatoka mburu hivi wote wa iraq ni chadema jk acha inteligensia ya kijinga ya kinasaidi mwema wa benk kuu zamani usiipelekee nhi hii kwa visasi rais mwenye kisasi hatufai watanzania umemfanyia kisasi bobu seya umemfanyia kisasi mahalu wote hawa kwa sababu ya mademu acha hayo hata salima utamwacha nawatu watakula tu acha grudge haikufai charity for all malice for none ............be careful acha udini wewe ni mdini sana wanakuficha hufai mbona umekaa kimya tu hata mambo makubwa yanayo hitaji kauli nzito we kimya tu kama paka nyauuuuuuuuuuuu
ReplyDeleteJamani UVCCM nyie ni vijana tena wasomi tuliokuwa tunawategemea kwenye chama.It does not make sense kwa watu kama nyinyi kukaa chini na kutukana watu wazima kama mlivyomtukama Dr.Slaa mambo yake binafsi yanawahusu nini? Hivi tukianza kumchunguza kila mwanasiasa kihivyo tutaona mangapi? Tanzania tuna matatizo mengi mno mngetumia muda wenu kuieleza serikali na kuishauri kuliko kukaa chini na kuandika kashfa na matusi kama watu ambao hamjaenda shule.Yani katika mambo mliyoboronga hilo mmeboronga na msitegemee kupata suport kutoka kwa vijana wenzenu
ReplyDeleteMi nawashangaa makauzu wote hao kwani ukianza kuwatolea kasoro kila mmoja utajua wametumwa, nimtolee mfano huyo Marwa Mathayo ambaye ni mwenyekiti wa Uv-ccm Mara, Yeye kaka yake alikuwa mbunge katika bunge lililopita Vedastus Manyinyi Mathayo - Mbunge Musoma Mjini, angalia mambo waliyokuwa wanatenda, 1. Waliwahi kubainika wanawachukua wanachuo kutoka chuo cha maendeleo ya jamii Buhare, Jinsi ya kike, wanakwenda kuwalipa Tsh. elfu sabini (70,000) wanawanywesha madawa kisha kuwafanyisha mapenzi na mbwa huku wanawarekodi mikanda ya ngono na kwenda kuiuza nje wakishirikiana na mfanya biashara wa kijaruo (Mtanzania) anafahamika kwa jina la Oberto. waandishi walipobaini uozo huo wakaenda kuandika katika gazeti moja makini na la uhakika, habari ilipotoka, wahusika wakalilangua kwa mawakala wa gazeti husika na kwenda kzichoma moto copy zote kabla hazijatapakaa. 2. Marwa na ndugu yake waliwahi kumteka mkenya mmoja aliyekuwa meneja katika Min Super Market moja inaitwa Kotra, ambayo ina kituo cha kuuza mafuta (Filling Station) kisa ni wivu wa kibiashara kwani Vedastud (Mbunge) ana Kituo chake pia (Filling Station) na ni Wakala wa kampuni ya Hans inayojishughulisha na usambazaji wa mafuta husika = Diesel, Petrol, Mafuta ya taa, walimtesa kwa Pasi ya umeme sehemu mbalimbali za mwili hadi sehemu nyeti hatimaye kumuuwa Marwa akidai amemfumania Mkenya huyo na mke wake yeye Marwa, kwasababu wana hela hawakufanywa kitu na serikali ya wakati huo ya Mkapa, Marwa amegonga watoto wadogo na magari yao ya kifisadi zaidi ya mara mbili lakini wakifika polisi hakuna kinachotokea zaidi ya kuyamaliza kifisadi. Yeye na kaka yake ambaye alikuwa mbunge wanamchezo wa kuwatisha watu na bastola kila mara, hawafanywi kitu wenye hela zao. Hadi majuzi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu Marwa alimtisha kwa bastola mwandishi wa habari (George Malatu, nini kilitokea zaidi ya kuyazima kishkaji zaidi pale polisi? Nahisi hata muhusika hakuambulia kitu chochote. Sasa hizo chuki alizopewa kuziongelea alikumbuka kwamba na yeye ni muhusika? Waache kutufanya wananchi kuwa hatujui, bali tunakosa pakuwasemea zaidi ya hapa, na kama maoni haya yangekuwa yanachapishwa wazi, naamini wangekuwa wanajifungia katika nyumba zao kwa aibu. hayo ni machache yapo mengi tunayoyafahamu ila tumefumba midomo kuwahofia na utawala wao wa kidharimu. Wakomeeeee.
ReplyDeleteSasa hivi tunajifunza kuwa kama una mapungufu yako nchi hii usijaribu kuongea hadharan mambo ya unafiki,watakuumbua wanaokujua vibaya sana.maskini ya alah kina malisa wametumwa kusema,km vile katolewa kafara,mbona asiseme ridhiwan au january,nao si kamati kuu ya watoto ccm?kashfa zote kazibeba yeye,kama alikuwa hajui ajifunze.hakuna maandamano yoyote ya kupinga dowans ni porojo tu za kifissadi. tungoje tuone, tumwombe alah atupe matumaini ya kuongokona na ufissadi huu. Amin!
ReplyDeleteUVCCM acheni kufurahia jenge la mafisadi kama wamewatuma kudandia hii mada ya DAWANS mlishachelewa na serikali ikatoa tamko kwamba ilipwe. Sasa ni kipi kimewakwaza mpaka mkaona ya kuwa sisi watanzania hatutendewi haki na wanafunzi tuna nyanyaswa. Kupiga kura tumenyimwa haki yetu vijana wenzenu na mkaa kimya mikopo mpaka kwa shinikizo la mgomo leo hii kuna nini kimewauma. Mtafanya kazi sana mpaka mushawishi tuiamini hii CCM. Nakama na nyinyi mnakerwa basi tunawasubiri tushirikiane kumwondoa huyu mdudu aliyepo CCM. Mh Rais ni mvumilivu sana na anamwelekeo mzuri ila watendaji na wanaompa ushauri wanaimarisha upande wao zaidi kama mlivyotoa mfano kwenye secter ya mkopo kuna uzembe. Sasa msubiri baba yenu Makamba awajibu. Kuhusu suala la viongozi wa dini mimi ninaona hawana matatizo kukemea maovu na uzembe inapobidi. Hawa watu ni watu ambao wapo makini sana na ndio wasuluhishi kwa dira iliyopo sasa hivi. Kwa sababu mahakama ndio hivyo tena. Hilo la viongozi wa dini halikwepeki na serikali ikisha jenga tabaka na dini tayari nchi lazima iyumbe. Viongozi wa dini wanafanya kazi kuliko hata mafsa wa CCM.
ReplyDeleteMLIOTOA MAONI WOTE NI MAPIMBI
ReplyDeleteHAHA NJAA TU ZINAWATESA MTASEMA MENGI KULIKO MAELEZO,HAMNA JIPYA NYIE WAONGO TU PUMBAVU ZENU ALA MSIRUDIE TENA MMETUMWA NA SLAA NYIE WAPUUZI KWENDA ZENU HAMNA POINTI YA MAANA
ReplyDeletehivi nyie watoto wa mafisadi lengo lenu nn? hamna jipya inaonekana mmetumwa,dhambi ya udhalimu ipo mikononi mwenu,pumbavu zenu.......
ReplyDeleteYaani nyinyi vijana wa UVCCMna Makamba wenu na hulo limama gani ambalo halia hata aibu huko Arusha mlitukana sana watanzania, moja wapo wakiwepo viongozi wa dini mpaka baba yenu Makamba anachukua biblia anafundisha viongozi wa dini ikiwa na maana siasa imemshinda, mkaua raia wasio ha hatia, mkamtukana Mh Slaa, Mbowe, Ndesamburo nk. Leo hii mnaongea hayo maneno hapo juu, kweli CCM hamna mwelekeo. Tunafikiri barabara na viwanja ni vyeupeee!!!!! havija pata wateja wa mapambano. Sasa mapambano yataanza rasmi maandamano yatakapo anza rasmi kama TUNISIA ndio mtapata uchungu wa maisha. Sasa mkitaka kujua hali ya hewa ya nchi angalini upepo unako kwenda. Yaani wamefikia hatua ya kukata tamaa ya kuishi kwa sababu ya hali ya maisha.
ReplyDeleteUVCCM NI WATOTO WA CCM, SASA WANACHOTAKA KUTUAMBIA SIYO KIPYA KWA JAMII YA TANZANIA. MBONA HAWAZUNGUMZI MAMBO YA KATIBA AMBAPO NDIYO MSINGI WA KUFUTA UFISADI WOTE NCHINI?? WAMEANZISHA HOJA ZAO WALIZOTUMWA NA MAFISAI WENZAO KWA KUSUDI LA KUWAYUMBISHA WATANZANIA WASIENDELEE NA MJADALA WA KIKATIBA!! PILIMBONA HAWAZUNGUMZII SUALA HATA LA UMEME AMBALO NI JAMBO LINALOWASUMBUA WATANZANIA WENGI HASA WALE WA MJINI?? WATANZANIA WENZANGU MLIYOTOA MAWAZOYENU MWANZONI MUWE MACHO NA HAWA WATOTO WA MAFISADI!!!!!!!
ReplyDeleteUmoja wa Vijana wa CCM kweli utoto unawasumbua. Mnakashifu na kumtukana Slaa wakati tayari mnaunga mkona harakati zake alizoanzisha. Hamieni upinzani kama serikali ya baba zenu imekwama. Tutawafukuza kwa mawe kama ilivykuwa Tunisia muda si mrefu nyie na wazazi wenu mafisadi.
ReplyDeleteMh Dr Slaa, Mbowe na viongozi wote wa Chadema muwe macho sana bado Tanzania tunawahitaji kwa nguvu zote na mungu aendelee kuwaongoza. Hawa wajamaa walivyo na hasira wakimkamata Dr Slaa sijui. Lakini mungu atamlinda mja wake na ataendelee kupambana mpaka mwisho wa safari. Amen.
ReplyDeleteVJCCM kwisha habari yake baada ya kutekwa na matajili wa CCM wanatumiwa kama punda tu hao. Zamani kujiunga na VJCCM ilikuwa ni kwa ajili ya uzalendo siku hizi ni kuganga njaa tu hawana kitu hao. Vijna ndio wana mapinduzi lakini sasa wao wanaingia ili kumsindikiza Riwadh Kikwete amuwezeshe baba yake kutawala. Sasa vijana wa CCM mtaendelea kutumiwa kama punda mpaka lini? Sasa hivi mnapigana kufa na kupona kumsaidia Lowasa aingie Ikulu na kwa sasa mnamsaidia Lowasa na Rostam wapate fedha za Dowan ili ziwasaidie kwenye kampeni 2015. Ni lazima muwelewe Lowasa hawezi kupata urais. Tena itakuwa njia rahisi sana kwa Chadema kuchukua nchi. Yeye na Rostam ni mafisadi wa kutupwa Tanzania. Wakishirikiana na baadhi ya wahindi. Vijana wa CCM eleweni sisi vijana wenzenu wa Tanzania tena tulioenda shule tunasema ya kwamba Tanzania bila CCM inawezekana. Kwa taarifa yenu wale tutakaoshiriki uchaguzi 2015 robo tatu hatuipendi na wala hatutaki kuisikia CCM. Maana CCM ni genge la wanyang'anyi wanaotaka kutafuna kila kitu kilichoko Tanzania. CCM ya kizalendo ilishakwenda na Nyerere na Kawawa. Hii ya wakina Rostam, Premji na Karamagi hatuihitaji hata kidogo itokomee kuzimu kwenye shimo la uharibifu.
ReplyDeleteHuwezi kuwa ndani ya CCM ukawatetea watanzania bali kuwafuja na kuwaibia. Hawa wasiwadanganye. Ni mashindano ya mitandao na kutapatapa baada ya kuhofia CCM inaweza kupigwa kibuti 2015 iwapo tutaandika katiba mpya. Wanaanza kujaribu kutafuta jinsi ya kujikosa huku wakiwapigia debe mafisadi ambao ni baba zao au kaka zao. Hapa naona harufu ya Ewassa na Nchimvi. Hata hivyo wote ni wachafu sawa na hao watoto wa mafisadi waliowatuma. Shame on you and may you perish come 2015.
ReplyDeleteSasa tuone hayo malipo ya tapeli dowans yatalipwa vp, benki zote za hapa ziko macho kusubiri hiyo transaction,km ulaya watu wako macho pia,mbona transaction ya mtoto wa lowasa ya mabilioni iliwashtua uingereza. watakavogawana itajulikana tu mgao umeenda kwa nani,watu wako macho hawalali.nchi hii ni wizi tu,watu hawana huruma na wengine, yaani kama wewe hujulikani na mafisadi ya ccm,usubiri kuwa ombaomba!!!ndo maana rushwa katika huduma za jamii zimeota matawi,wizi katika sekta mbalimbali haukwishi,unapamba moto kila kukicha,mtu anaona akikwapua ml.20 zitapunguza matatizo yake kuliko kuendelea kuona mafisadi wanavogawana nchi na watoto wao.
ReplyDeleteNimesoma comments zote leo bila kuacha hata moja! Sasa najiuliza, hivi kweli katika hali halisi UVCCM wamekosea kutoa tamko lao kihivyo ama? Kama wamekosea ni nini dhamira yao? Kama hawajakosea mbona hapa watoa maoni karibu wote wanawasuta tena vibaya kwa maneno ya kashfa na matusi!
ReplyDeleteNaanza kuamini kuwa siasa zetu zimeshaanza kuwa si za kistaarabu hiyo moja, lakini pili ipo chuki ndani ya siasa zetu! Kwa mantiki ya kawaida mtu hawezi kutuo maoni yake asilimia 100 yakawa mabaya, ama kuna chuki kwa waliyapokea au .....!
Mimi naamini si kweli UVCCM wamekosea hata kwa asilimia 3 tu kuwa hawana ukweli katika walichokizungumza na kukitolea tamko! Mimi ninaamini kuwa hata kama 97% ya maoni yao hayaaminiki basi kwa hizi tatu wanastahili pongezi! Vinginevyo tutajiingiza kwenye malumbano yasiyo na tija kwa Taifa letu! Na hata sisi wasomaji wa Comments zenu tutaanza kuona kuna upungufu wa kufikiri miongoni mwetu.
UVCCM pamoja na mapungufu waliyonayo,labda pengine kama ni kweli walimtukana DR. Slaa huo ni upungufu, lakini hatujuwi labda na Baba yao naye alitukanwa wakashindwa kuvumilia hatujuwi kwani hatuna mkanda mzima wa matukio ya kuunganishwa ya mchakato wa uchaguzi Mkuu!
Hivi ni kweli UVCCM wamekuwa wapumbavu kiasi tunachotaka kuaminishwa na wasomaji wetu wa haya maoni? Mimi sitaki kuamini hivyo, ila nachowaomba watoa maoni tuache jazba, tuondowe ushabiki na tuzungumze taifa letu!
Nikiangalia UVCCM katika taarifa ya Habari walipotoa Tamko lao ni tamko lenye utashi wa kisiasa na mtazamo wa Kidiplomasia ila wanaonekana wamekatishwa tamaa na mwelekeo wa chama chao! Hivyo ndiyo maana wanatoa matamko makali kama hayo! Kwangu mimi nawatazama kama watanzania wengine na si tu kama wana CCM! Maana siku hizi inaonekana ukitoa maoni kama si mwana chama wa chama fulani basi maoni yako hayana maana kabisa! Hata kama ni CCM wametoa maoni mkumbuke kwamba si wana CCM woote wanakubaliana na mambo yanavyokwenda ndani ya Chama chao, au Wana CHADEMA woote wanakubaliana na mambo yanavyokwenda ndani ya CHADEMA yao. Kwa mantiki hiyo UVCCM kutoa tamko hili ni kielelezo tosha kuwa hawawezi kuvumilia uozo wa maamuzi na utendaji ndani ya chama na ndani ya Serikali kw ujumla.
Tunapohitaji Demokrasia lazima tuheshimu pia maoni ya watu wengine hata kama yanaudhi kiasi gani!
Sitaki kuchambuwa mantiki nyuma ya UVCCM kwani ipo wazi kabisa na nadhani ni wakati wa kuwaunga mkono kwa maslahi ya Taifa! Na hasa kama tutaondoa ushabiki wa vyama, kwamba wapigania demokrasia na haki ni lazima watoke, ama wasikike wakitoka chama fulani na fulani tu. Nje ya hapo wote ni wanafiki! Hii si kweli!
Carwin 1
Hivi ni lini hiki chama cha majambazi kitatoka madarakani, ni lini tu mungu wangu. Walivyo na tabia mbovu nchi zote Africa wanasikiliza taarifa za habari waliopo nje ya nchi kwenye Internet lakini Tanzania hakuna hata moja ni Radio maria na Bongo ambao wanapiga miziki tu, Wanataka hela za kutongoza tu na madisco usiku na kugandamiza vyombo vya habari. Huko Zanzibar wanakiredio chao cha mzalendo wanavyotukana nacho utafiki imetoka sijui wapi. Hata hamu ya kukisiliza hakuna. Kenya wanazo nyingi tu. Rwanda usiseme, Uganda hazihesabiki. Sijui hapo CCM pana mdudu gani au TZ ni koloni la Mkenya mbona ofisi zote za kupata na kusambaza habari zipo Kenya.
ReplyDeleteKATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa, amesema yupo tayari kupimwa akili nzuri alizonazo za kupambana na wanaotafuna rasilimali za taifa.
ReplyDeleteAkizungumza na Tanzania Daima Jumapili juzi, Dk. Slaa alisema kuwa yeyote mwenye kutetea rasilimali za taifa zisitafunwe na walafi wachache waliopo ndani ya Chama Cha Mapinduzi hawezi kuwa na matatizo ya akili.
Kauli hiyo aliitoa baada ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), kuitaka serikali imkamate kiongozi huyo na kumpeleka katika hospitali kumpima akili.
Katibu Mkuu wa UVCCM (taifa), Martin Shigela, alisema wameamua kutoa kauli hiyo baada ya kujiridhisha kuwa kiongozi huyo wa upinzani hakutakiwa kukataa matokeo ya urais kwa kudai kura zake zimechakachuliwa (kuibwa).
Aliongeza kuwa Dk. Slaa ni miongoni mwa vinara waliochangia kuhamasisha vijana wafanye maandamo yaliyopigwa marufuku na Jeshi la Polisi mkoani Arusha, ambako vijana watatu walifariki dunia na zaidi ya 20 kujeruhiwa.
Umoja huo ulisema Dk. Slaa amekuwa akitoa kauli mbalimbali za kichochezi ili kuwafanya wananchi wasiiamini na kuipenda serikali ya CCM chini ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete.
Akijibu mashambulizi hayo ya UVCCM, Dk. Slaa amesema yuko tayari kupimwa akili zake nzuri alizonazo kutokana na kuwa mstari wa mbele kuibua hoja nzito dhidi ya serikali.
“Unakwenda kunipima akili kwa kitu gani? Mimi naona nipimwe kwa akili nzuri, maana siku zote nimekuwa nikisimama kidete kutetea rasilimali za nchi, likiwamo suala la Dowans kutolipwa.
Sasa kati ya mimi, Shigela na vijana wenzake wa CCM, nani akapimwe akili zisizofaa?” alihoji Dk. Slaa.
Alisema umaarufu wa mtu na umakini wake unatokana na ujengaji wa hoja na anavyozitetea pamoja uungwaji mkono wa jamii, hivyo haoni sababu kwa watu wa aina hiyo wapimwe akili.
CCM fisadi imezaa na kuendeleza serikali fisadi.
ReplyDeleteViongozi wanadhani kwamba kwa kuwa viongozi maana yake wameshikilia akili za wanaowaongoza. Angalia sasa Waziri Mkuu anataka Wabunge wa CCM wawasikilize viongozi wao na kisha wabwabwaje maneno ya viongozi kwa wananchi. Maana yake ni kwamba Wabunge hawa wa CCM hawana uwezo wa kufikiri na kutafakari! wanawekewa maneno ya kusema midomoni mwao!
Wananchi na wazalendo tuwe macho. HAKUNA KULALA HADI KIELEWEKE.
Hapa tumeliwa watani kwa uroho na njaa zetu. Nani UVCCM, Msuya, Sitta nk? jaji Bomani ameshamaliza kila kitu... Lipeni deni mara moja vyenginevo mtanikiona cha mtema kuni!
ReplyDeleteBiashara za baharini na angani, rasilimali zilizoko nje na misaada ndio sekta za kwanza kushambuliwa. Riba ya mamilioni itatozwa kwa saa ndio itayotufata.
MIMI NASEMA HIVI HAWA SI UVCCM KWELI, NI WALE WALIOKOSA MGAO WA DOWANS. KAMA WATAFANAYA KITU BASI NITAJUA KUWA TANZANIA TUMEKOMAA.
ReplyDelete