MELBOURNE, Australia
BINGWA mtetezi, Roger Federer ameongeza rekodi nyingine katika orodha yake kwenye michuano ya wazi ya Australia kwa kumfikia mchezaji, Jimmy Connors
baada ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo ya Grand Slam kwa ushindi wa seti 6-3, 3-6, 6-3, 6-2 dhidi ya Tommy Robredo.
Kwa ushindi huo wa jana, Federer anakuwa ametinga hatua hiyo kwa mara ya 27, tangu alipopoteza mchezo wake raundi ya tatu ya michuano ya wazi ya Ufaransa mwaka 2004, rekodi ambayo inakuwa ni sawa na iliyokuwa inashikiliwa na Connors.
Mbali na Federer, bingwa wa michuano ya wazi ya Ufaransa, Francesca Schiavone vilevile naye aliweka rekodi ya michuano hiyo ya Grand Slam kwa upande wa wanawake, baada ya kuhitaji saa nne na dakika 44 kumchapa, Svetlana Kuznetsova kwa seti 6-4, 1-6, 16-14 katika duru ya nne.
Kwa ushindi huo, mwanadada huyo anatarajia kukutana na mchezaji anayeshika nafasi ya kwanza kwa ubora, Caroline Wozniacki katika hatua ya robo fainali.
No comments:
Post a Comment