Na Shufaa Lyimo
UONGOZI wa Klabu ya Toto Africa, umesema umejipanga vizuri kuhakikisha wanaifunga timu ya JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu unaotarajiwa kupigwa Jumamosi katia Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi juzi kwa njia ya simu akiwa Mwanza Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Choki Abedi alisema kikosi chake kinaendelea vizuri na hakuna majeruhi hata mmoja.
"Baada ya kuifunga Polisi Tanzania mabao 2-0, tulipumzika jidogo lakini kwa sasa tumeanza mazoezi huku, ili tuweze kufanya vizuri katika mechi inayofuata Jumamosi," Alisema Choki.
Katika mechi hiyo vijana wake wamepania kuwafunga wapinzani wao ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi hiyo.Choki aliwataka mashabiki wao kuendeleza ushirikiano kwa kuwa bila wao, timu haiwezi kufanya vizuri uwanjani.
"Naomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi siku hiyo, ili watushangilie pindi mashujaa wetu watakapokuwa wanapambana na wapinzani wetu," alisema.
No comments:
Post a Comment