Na Rabia Bakari
CHAMA cha Uzalishaji na Mandeleo Tanzania (TAMADA) kwa kushirikiana na wafanyabiashara ndogondogo wameandaa maandamano makubwa ya
kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kutoilipa kampuni ya kufua umeme ya Dowans, na kudai kuwa anayetaka kuilipa kampuni hiyo atoe fedha zake mfukoni.
Maandamano hayo ambayo yapo katika maandalizi ya hatua muhimu ikiwemo ya kisheria, yanatarajia kufanya wakati wowote kuanzia sasa, ambapo yataanzia katika majengo ya Machinga Complex kuelekea Ikulu, na sambamba na suala la Dowans, pia yatabeba na ujumbe wa wafanyabiashara hao jinsi wanavyoumia na maisha.
"Tumesikitishwa na kauli ya Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda, ya kudai lazima Dowans ilipwe, anatoa fedha zake mfuko?
Hizo fedha ni za walipa kodi, na ni bora ziende kwenye huduma muhimu kuliko kuilipa kampuni hewa...kama kuna umuhimu wa kulipa basi watoe fedha zao mifukoni,"alisema Mwenyekiti wa TAMADA, Bw. Abel Mwakabenga.
Alidai kushangazwa na hatua ya serikali kutaka kulipa fedha hizo haraka haraka bila hata kushughulika na hukumu iliyotolewa na mahakama ya kimataifa ya ICC na kudai kuwa hakuna sheria isiyo ruhusu kukata rufaa.
"Hawataki hata kukata rufaa, wanaharakisha kutaka kuilipa tu, wananchi tumechoka kubebeshwa mizigo mikubwa, kwanini kodi zetu wafaidi watu wachache, tumekaa kimya tumechoka, na sasa ngoja tutoe sauti zetu,"aliongeza.
Aliwataka viongozi kuwa wasikivu, na kujua wananchi wanataka nini, na kuhoji ni kwanini serikali haitaki kupinga wala kutetea wananchi, na kushabikia mambo ya kihuni kama Dowans.
"Maandamano yetu hayapo kisiasa, na wala hatutaki mkono wa wanasiasa, ila tumeamua kusema baada ya kuwa sisi kuumia zaidi na madeni ya serikali, kwa kuwa hizo fedha zikilipwa, hazitoki mifukoni mwa mtu bali ni kodi zetu,"alidai.
Aidha Bw. Mwakabenga akisaidiana na viongozi wenzake wa TAMADA waliokuwa katika mkutano huo, walionya nchi kuwa inapoelekea pabaya, kwakuwa hata machafuko duniani kote yalianza kidogo kidogo kama Tanzania.
"Hakuna aliye salama katika nchi hii, hasa sisi tulio katika hali ya chini, tukiwa na matarajio kuwa sasa mambo yatakuwa mazuri, inakuja hali mbaya zaidi. Inabidi tuseme ili tusiendelee kuburuzwa inafika wakati tunaona uchungu jinsi mambo yanavyoenda.
"Lakini zaidi tunasikitishwa na ukimya wa Rais Kikwete, maana yeye ndio alitakiwa aseme na kuokoa wananchi wake waliomuweka madarakani,"alisema.
Aliongeza kuwa hawategemei maandamano hayo kuzuiwa na polisi kwani wameshatangaza kuwa ni maandamano ya amani, yenye kutaka amani ya nchi, si ya kisiasa wala vurugu.
"Hatutegemei polisi kupinga maandamano kwani tumeshatangaza kuwa ni ya amani, wakipinga wanaficha uovu gani?Wenyewe wanashiba na matumbo yao hivyo wawaache walalahoi wadai haki zao,"aliongeza.
Akisistiza katika hilo, Bw. Mwakabenga alisema kuwa hawaogopi chochote, na nchi nzima waelewe hivyo kwamba hawataogopa chochote kwakuwa wao wametumwa na maelfu ya wafanyabiashara ndogondogo ambao wamekata tamaa kutokana na hali ngumu wanayokumbana nayo kila siku.
"Mabilioni ya pesa yaende kwa watu wachache katika nchi hii wakati sisi tunakula mara moja kwa siku, haiwezekani,"alisisitiza.
Kwa upande wa Machinga Complex, ambapo wanachama wengi wa TAMADA wamepanga, alisema kuwa tayari serikali imeshaonesha nia ya kutaka kuwalipisha wafanyabiashara hao zaidi ya bilioni 12 inazodaiwa na Mfuko wa Hifadhi za Jamii (NSSF).
"Fedha hizo zilitolewa ili kujenga majengo hayo, lakini walipaji ni sisi wajasiriamali, maana jinsi kodi zilivyokuwa nyingi ni wazi tunalipia sisi deni lote bila kutonea huruma.
"Sehemu ni ndogo sana na tunalipa fedha nyingi na kodi mfululizo, lakini kama haitoshi tulipewa vyumba ambavyo tunatakiwa sisi ndio tunafanye ukarabati, hivi huyu Mtanzania atainuka lini?
"Sasa badala ya kodi zetu kutusaidia katika mambo muhimu kama hayo, wanataka kupewa watu wachache walionacho, na sisi masikini tupokonywe kabisa, kama si kutaka kutuua au kuondolea amani iliyopo nchini humu, ni kitu gani wanataka?"Alihoji.
Alitaka mabilioni ya Dowans yaelekezwe katika huduma za elimu, afya na katika sekta zisizo rasmi.
"Hili jambo hatulishangai kwani hata watu tuliowachagua na kuwapa madaraka wanalipigania jambo la Dowans kulipwa, badala ya kushughulikia matatizo ya watu wa chini.
"Huduma za afya ni mbovu, elimu ina matatizo makubwa, wasionacho wanapata tabu, hebu tufikiri kitendo cha kupandishwa gharama za umeme.
"Gesi haikamatiki, vyakula vimepanda, mafuta kadhalika, haya yote yatasababisha na kuleta machafuko na hatimaye umasikini mkubwa katika taifa lenye amani,"aliongeza.
Aliwataka wananchi wote ambao wanaunga mkono maandamano hayo kujitokeza mara moja mara yatakapotangazwa siku maalum ya kufanyika, na kudai kuwa kila mmoja ni muathirika wa tatizo la Dowans.
HUYU RAIS WENU MWENYEWE YAWEZEKANA NI MWIZITU.TENA IKIWEZEKANA TUMFANYE KAMA YULE MWIZI MWENZAKE WA TUNISIA KWANI TUNA SHINDWA NINI KWANI SISI HATUNA UCHUNGU AU WANAOJILIPUA KWANI NAO WALIVUMILIA ,HIVYO UVUMILIVU UKIISHA NI KUMLIPUA TU. TUNAWEZA SANA.
ReplyDeleteMFIKISHIENI UJUMBE KUWA TUNAWEZA.
Idadi ya watu wanaokufa katika maandamano ni ndogo kuliko watakao kufa kwa ajili ya umaskini na maumivu yanayotokana na maisha magumu yanayosababishwa na unyonyaji.
ReplyDeleteSauti zetu zitapaa na hiyo ni nguvu yetu, wao na watumie risasi na mabomu, yataisha mwisho wataishia mikononi mwetu.