Na Elizabeth Mayemba
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mserbia Kostadin Papic jana waliwaaga wachezaji wake, na kutoa sababu zilizomfanya aachie ngazi kuinoa timu
hiyo.Akizungumza na wachezaji hao jana katika mazoezi ya asubuhi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam Papic alisema hana budi kuwaaga wachezaji wake kwa kuwa alikuwa nao vizuri tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2009, ambapo alirithi mikoba ya Dusan Kondic.
"Wito wangu mkubwa kwenu nawaombeni jitumeni katika ligi, ili mtwae ubingwa wa Bara ikiwa na kufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Shirikisho na wapeni ushirikiano makocha ambao mtakuwa nao," alisema Papic.
Alisema sababu kubwa iliyomfanya ajiondoe katika timu hiyo ni kuona viongozi hawamuhitaji kwa kuwa wamekuwa wakifanya mambo bila kumshirikisha.
"Wamekuwa wakifanya maamuzi ya benchi la ufundi bila ya kunishirikisha, hiyo ni wazi kwamba walikuwa hawanihitaji, mimi ni kocha mzoefu kama miaka 20 ninaimani nitapata klabu nyingine, ambayo watanipa heshima yangu kama kocha," alisema.
Alisema hana sababu nyingine yoyote zaidi ya kutengwa kwa kila maamuzi na pia ameiombea kila la kheri timu hiyo katika kibarua chake cha kwanza katika michuano ya Kombe la Shirikisho, dhidi ya Dedebit ya Ethiopia Jumamosi.
Awali kabla ya kuachia ngazi Papic, tayari Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Davis Mosha na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Ahmed Seif, walipewa jukumu la kumtafuta mbadala wa Mserbia huyo.
kwakweli uongozi wa juu wa yanga LYOD NA MOSHA mnatualibia timu yetu toka mmeingia full migogoro tumechoka sasa ...........tafadhari hebu achieni ngazi
ReplyDeleteMkoba Said; inaonyesha viongozi wa yanaga mna ummelo, wachachezaji bado wanampenda sana kocha wao Parpic lakini ninyi ndio mnafanyia mtima nyongo, wachezaji wakigoma na kucheza chini ya kiwango mtafanyaje? ilikuwaje muanze kutafuta kocha mwingine?
ReplyDelete