Na Addolph Bruno
TIMU ya soka Simba ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, imemaliza vizuri hatua ya makundi na kutinga robo fainali ya Kombe la Uhai, kwa kuikung'uta African Lyon mabao
4-1.
Mchezo huo wa kundi B, uliochezwa jana asubuhi katika Uwanja wa kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam, Simba ilikuwa ya pili kukata tiketi ya robo fainali katika michuano hiyo, ikitanguliwa na AFC Arusha na kuongoza kundi lao kwa pointi tisa.
Wakicheza kwa kasi na kujiamini, Simba ilipata bao la kwanza dakika ya 20, kupitia kwa Kelvin Charle, baada ya kupokea pasi nzuri ya Miraji Athumani.
Bao hilo liliwafanya Lyon kuongeza kasi, lakini walijikuta wakipigwa bao la pili dakika ya 36, kupitia kwa Marcel Bonventure alipokea pasi ndefu ya Athumani.
Timu hizo zilishambuliana kwa zamu, lakini African Lyon ilipata nafasi nyingi za kufunga kupitia Hamis Thabit, mikwaju mingi ilidakwa na kipa wa Simba, Mohamed Azizi.
Dakika ya 34, Charle aliipatia Simba bao la tatu, baada ya kushirikiana vizuri na Miraji, ambaye alikuwa mpishi mkubwa wa mabao.
Chale ambaye pia alifunga bao la nne dakika ya 71, baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa wapinzani wao.
Mabeki wa Simba, walishindwa kumdhibiti Abuu Mwasekaga, aliyeifungia bao African Lyon dakika ya 89 .
Michezo ya hatua ya makundi ya inamalizika leo kwa mechi za kundi C, Mtibwa Sugar itaumana na Kagera Sugar asubuhi na jioni JKT Ruvu na Majimaji 'Wanarizombe' ya Songea.
No comments:
Post a Comment