26 January 2011

Shein ateua wakuu idara za SMZ

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amewateua wakuu wa taasisi mbalimbali serikalini.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na
Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee ilieza kuwa uteuzi wa watendaji hao ulianza rasmi jana.

Walioteuliwa katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Mkurugenzi Idara Mipango, Sera na Utafiti, Fauzia Mwita Haji, Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi Is-hak Ali Bakari, huku Sheha Mjaja Juma akiteuliwa kuwa Mkurugenzi Idara ya Mazingira.

Wengine ni Mkurugenzi Idara ya Watu Wenye Ulemavu, Abeida Rashid Abdulla, ambapo Dk. Omar Makame Shauri anakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya UKIMWI na Fatma Mohammed Omar anakuwa Ofisa Mdhamini wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Pemba.

Katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Sera na Utafiti ni Khatib Said Khatib, huku Hassan Khatib Hassan akiteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi.

Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali ni Ahmada Kassim Haji, huku Issa Ibrahim Mahmoud akiteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa.

Wengine ni Ali Juma Hamad anayekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, ambapo Iddi Suleiman Suweid anakuwa Mkurugenzi wa Idara ya Upigaji Chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali.

Ofisa Mdhamini wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba ni Amran Massoud Amran.

Katika Ofisi ya Rais (Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo), aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ni bw. Idrissa Abeid Shamte, ambapo Bw. Ramadhan Senga Salmin ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi.

Bw. Omar Hassan Omar ameteuliwa kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali, ambapo Msaidizi Mhasibu Mkuu wa Serikali ni Mwanahija Almasi Ali.

Rais pia amemteua Bw. Khatib Mwadini Khatib kuwa Kamishna wa Bajeti, ambapo Bw. Said Mohammed Hussein ameteuliwa kuwa Kamishna wa Uhakiki Mali na Mitaji ya Umma.

Aidha, Saada Mkuya Salum ameteuliwa kuwa Kamishna wa Fedha za Nje ambapo Mkurugenzi wa Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dar es Salaam ni Shumbana Ramadhan Taufiq, ambapo Ofisa Mdhamini Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Pemba ni Bakari Haji Bakari.

Rais pia amefanya Uteuzi katika Tume ya Mipango ambapo Ahmed Makame Haji ameteuliwa kuwa Kamishna wa Mipango ya Kitaifa, Maendeleo ya Kisekta na Kupunguza Umasikini.

Kamishna wa Ukuzaji Uchumi, aliyeteuliwa ni Mwita Mgeni Mwita ambapo Seif Shaaban Mwinyi ameteuliwa kuwa Kamishna wa Mipango na Maendeleo ya Watenda Kazi.

8 comments:

  1. ZNZ hamna mkristo hata mmoja mwenye sifa ya kuteuliwa?

    ReplyDelete
  2. Waislamu ndio hao hao wanaopiga kelele kwamba wanabaguliwa na kumbe wao wenyewe ndio wabaguzi wakubwa. Siku hizi tutabadilisha majina tuitwe wakina Ali ili tupate kazi Tanzania. Sasa wewe angalia hata uteuzi wa Kikwete unaangalia zaidi dini ya mtu badala ya sifa za mtu. Hivi ebu mtu ajiulize hivi kweli haiwezekani hata siku moja mkristo akawa balozi wa Tanzania Irani, Misri, Libya, Saudi Arabia to name few! Mbona Waislamu wanapangwa katika nchi za kikristo kama Uingereza, Ujerumani, Marekani, Italy, Ufaransa to name few. Iweje iwe dhambi mkrito kupangwa nchi za kiislamu. Hivi mbona jamani waislamu wanamatatizo ya ubaguzi sana. Halafu wao wenyewe ndo wa kwanza kulalamika kwamba wanabaguliwa nia waendelee kupendelewa kuliko wakristo. Ukweli ni kwamba wakati huu wa Kikwete wakristo wamebaguliwa sana. Na ifike mahali tuseme hapana sasa. Watu wapewe kazi kulingana na taaluma yao na uwezo wao na si kwa vigezo vya dini zao. Wakristo kule Zanzibar wamenyanyaswa usiseme hata imefika mahali wananyang'anywa hata viwanja vyao na kupewa wakubwa waislamu. Hebu tazama mtoto wa Karume akitumia kofia ya baba yake ya kuwa rais anakwenda kunyang'anya kiwanja cha kanisa. Mimi hata wakati mwingine ninasema hata hili limuungano na life kabisa. Ukifa Muungano siku hiyo nitafanya sherehe kwani ukweli haina maana kuwa na ndoa ya kubembeleza upande mmoja. Kwan Zanzibary kuna nini mpaka tuendelee kuwang'ang'ania. Ikiwa ni usalama dunia imebadilika kabisa hakuna haja ya kuwabembeleza zaidi. Waacheni wauane ndo watakoma.

    ReplyDelete
  3. Maoni yote mawili ya hovyo,mnafikiri muungano ukifa ndio mnaweza kuawakandamiza Waislam huku Bara? ujinga wenu ndio huo na ndio maana mmemshupalia Kikwete wakati manyago yote ya ufisadi wa nchi umefanywa na Mkristo mwenzenu,mbona mlikuwa hamshambulii kama sasa? Bandari,EPA,Reli,migodi,Kiura,Rada,Ndege ya Rais vyote hivi na vingine vyingi vilifanywa na Mkristo mwenzenu mkafunga makaro yenu.

    2. Wakristo wenyewe hawataki kwenda kwenye nchi ulizozitaja kwa sababu wamezoea mambo machafu na starehe za kupindukia hivyo huko kuna limitation.huko pia hakuna nguruwe. na wa nini huko? mbona Israeli hapelekwi Muislamu au nitajie balozi Muislam aliyeko au aliyewahi kuwa huko,nchi za Ulaya ulizozitaja si za kikristo wala dini hazina nguvu huko,ukienda makanisani wengi ni wa umri mkubwa,ni afadhali kwenye misikiti utakuta watu wa umri wote,Ulaya hakuna dini iliyoshamiri ndio maana unakuta wazungu wanafanya ngono hadharani,na wanyama,baba na mama wanavua nguo mbele ya watoto wao bila aibu au ndio mwongozo wa dini ya kikristo?

    3. Zanzibar haina haja ya huo muungano hata nyerere alifanya hivyo kwa sababu maaulum ambazo Waislamu wanazielewa na tunaamini hilo la muungano halipo mbali,mtakuja kuona Paris ya pili huko Zanzibar.

    ReplyDelete
  4. mh mbona tunaenda kubaya km tukianza mambo hayo ya udini? jamani chondechonde

    ReplyDelete
  5. Sikilizeni nyie wabongo. Siku utaovunjwa muungano nyinyi mutakufa njaa, mutabaguana, mutapunguziwa misaada, mutakosa ustaarabu na kuna hatari nchi kugaiwa vipande kama Yugoslavia.

    Wacheni kasumba za kijinga; you are inclined to lose while Zanzibar prospects of dev. is pretty clear!

    Musizungumze kama mnatoka porini.

    ReplyDelete
  6. wewe kafiri nani aliyekuambia zanzibar tunahitaji kuongozwa na kafiri,wewe angalia asilimia 99.99 ni waislamu ipo haja ya kuongozwa na mkiristo

    ReplyDelete
  7. hao jamaa inawezekana kabisa hawaijui zanzibar wanaropoka tu ni miongoni ya wale wasioitakia mema zanzibar lakini ''Alhamdulillah'' zanzibar tunakwenda vizuri hakuna udini hakuna ukabila siasa yetu ya kimaendeleo sio ya chuki si kama ya wabongo waaacheni watafunane wenyewe kwa wenyewe na kuhusu uchaguzi wa viongozi wanaoulalamikia haiwahusu wasitake kutuletea balaa mbona wakati wa nyerere waislamu walipuuzwa katika kila nyanja na waislamu walikuwa wastaamilivu kikwete ana kila haki ya kuwanyanyua waislamu kwa kuwa walipuuzwa siku nyingi na serikali zilizotangulia.

    ReplyDelete
  8. Ebwana wewe elewa kuwa hakuna mzanzibari hata mmoja ambae ni mkiristo, hao wakiristo walioko Zanzibar wote ni wageni kutoka huko kwenu Bara, kwa msingi huu bado hatujawa na upungufu wa watu wenye sifa za kushika hizo nafasi. Tutakapopungikiwa na watu basi tutawasiliana na wewe ili utueleze hao wakiristo unaodai wanasifa za kushika nafasi za uongozi zanzibar. Pia tunakuanya kuwa mambo ya Zanzibar hayakuhusu ndewe wala sikio kwa hio hapo ulipofika iwe ndo mwisho usithubutu tena kuingilia wala kuzungumzia mambo ya zanzibar, natamani kukwambia ukome kuingilia mambo ya zanzibar, lakini nahofia hii inaweza kuwa sio lugha ya kiungwana kwa watu wazima kuambizana.

    ReplyDelete