Na Zamzam Abdul
SHAHIDI wa tatu upande wa mashitaka Bw. Michael Wage ametoa ushahidi wake katika kesi ya kudai rushwa ya sh. milioni kumi kinayomkabili
mtangazaji wa TBC, Bw. Jerry Muro.
Akitoa ushahidi wake Bw. Wage alisema Januari 28 mwaka 2010 jioni akiwa nyumbani kwake alipigiwa simu na mtu ambaya alijitambulisha kuwa yeye ni Jerry Muro, mtangazaji wa TBC.
Alinitaka Januari 29 mwaka 2010 nifike Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano ili aweke sawa taarifa alizonazo kuhusu mimi, za ufisadi na ubadhilifu wa mali za serikali.
"Siku hiyo nilitoka Bagamoyo kuja Dar es Salaam ambapo aliniambia tukutane Calfonia Restaurant saa 5:00," alisema Bw. Wage.
Alisema alimpigia simu Bw. Muro kumjulisha kwamba tayari ameshafika kwenye eneo hilo, naye akaja akiwa na gari yake ndogo aina ya saloon.
Alikuja mpaka nilipokuwa nimekaa mimi pamoja na dereva wangu ambapo alinitaka tuongee pembeni katika meza iliyofuata ili dereva wangu asijue nini anataka tuongee.
"Tulihama na kuingia ndani, na ndipo aliniambia kuwa nakabiliwa na tuhuma za ufisadi na ubadhilifu wa fedha na anaandaa kipindi cha kueleza tuhuma na biashara zangu katika kipindi cha usiku wa habari," alisema Bw. Wage.
Alinieleza mahojiano hayo yatafanyika katika Hotel ya Sea Cliff ambako yuko bosi wake wanamsubiri na kutaka nimuache dereva wangu ili tupande gari lake kuelekea huko.
"Tukiwa njiani alimpigia mtu simu katika maongezi yao alinitaja jina langu na nikamuuliza huyo ni nani akanijibu Mkurugenzi wa PCCB, naye anataka kuonana na mimi kabla sijapelekwa mahakamani," alisema.
Bw. Wage anaeleza kuwa wakiwa wanaendelea na safari, Bw. Murro alimwambia yeye ni Ofisa wa Jeshi na ana nyota tatu amesoma Uingeraza na Marekani na ana uwezo wa kumkamata.
"Akafungua 'dash board' akatoa pingu akaniambia nikileta mchezo atanifunga na hizo pingu baada ya hapo akatoa tena bastola na kuniambia kama pingu zitashindikana angenipiga risasi.
"Baada ya hapo tulifika Sea Cliff tulipokewa na mwanaume aliyejitambulisha kwa jina la Mgassa, kuwa yeye ni Mkurugenzi wa PCCB kwa hiyo jumla tukawa watatu tukaingia hotelini hapo.
Baada ya muda mfupi akaingia mtu mwingine alijitambulisha kama Kaimu Mkurugenzi wa PCCB, anaitwa Edmund Kapama.
"Ndipo Bw. Muro aliniambia kuwa mimi ni fisadi, hivyo anaandaa kipindi kwa ajili yangu na kama nahitaji msaada niseme. Niliwajibu mimi sio fisadi na sijawahi kuiba fedha yeyote kutoka serikalini.
"Msaada wenyewe waliniambia nitoe sh. milioni 10 niliwajibu pale sikuwa nayo, hivyo nikaomba niwapatie kesho yake ndipo waliniambia nionane na mmoja wapo akiwemo Muro," alisema.
Vitu alivyokamatwa navyo mshtakiwa huyo, bastola na pingu, vilifikishwa mahakamani hapo kama utambulisho.
Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa Januari 29, mwaka jana jijini Dar es Salaam, Bw. Murro na wenzake walikula njama ya kuomba rushwa ya sh milioni 10 kutoka kwa Bw. Wage ambapo Bw. Kapama na Mgassa walijifanya ni maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Mimi ni yule yule Hafidh - mpenda mageuzi , mwanaharakati kutoka Zanzibar.napenda nichangie hapa mana naona kuna usanii !! kwa mujibu wa maelezo haya yaliotolewa na Majira.
ReplyDeleteBw. Wage anasema yeye alipigiwa simu na Bw.J. Muro kua akifika Dar amjulishe ili wakutane wazungumze kuhusu sakata la Rushwa kwa Bw. Wage.walikutana Restaurant na wakaongea lakini cha kushangaza ni kwamba Bw. Muro alimuomba watoke waende Seacliff kwa ajili kipindi cha Biashara zake za kifisadi na yeye akakubali akaenda wakati katika maelezo yake anakataa na kusema yy hajawahi kuwa fisadi na hajawahi kuibia serikali !! hii haingii akilini hata kidogo maana kama kitu unapinga kua mimi sijafanya na kuna mtu anakuambia umefanya na anataka aandae kipindi kwa ajili yako na ww unakubali kwenda !! haiwezekani.
Wakati wa safari anasema kua Bw. Muro alijitambulisha kua yy ni askari mwenye cheo!! hapa pia pana mushkeli !! mana Bw. J.Muro watanzania wengi wanamjua ni mwana habari lkn tuseme pengine ni askari kanzu wakati huo huo ni mwanahabari basi hawezi kumtishia kwa kusema nitakufunga pingu au kukupiga risasi ! maana kwa mujibu wa maelezo ni kwamba Bw. Muro anachotaka kujua ni ukweli juu ya kashfa sasa ikiwa ndio mana yake kama ni askari mpelelezi huwezi kutumia njia hiii ya vitisho vya kukupiga risasi kwa sababu utapoteza malengo ya kazi yako ya upelelezi!
Na walipofika Hotelini anasema kua alipokelewa na Afisa wa PCCB na baada ya mazungumzo bw. Muro akataka amsaidie kwa kumsafisha katika kipindi chake lkn kwa masharti ya kumpa rushwa ya pesa kadhaa. YY Bw Mage akamkatalia kua yy si fisadi kwa mara nyengine lkn hicho walichotaka kasema hana ila anaweza kuleta badae !! sasa kama ww hujafanya kosa na unamini hujafanya kwa nini utake kuhonga kwa eti kutishiwa kua kitaandaliwa kipindi !! hapo wasisi pia mm naona hii kesi ni usanii lkn acha tuone mwisho wake utakuaje mana ipo ktk vyombo vya sheria ambavyo tunaviheshimu.
Hafidh
ReplyDeleteMaelezo yaliyopo hapa sio kamili. Ukisoma magazeti mengine ya leo unaweza kupata picha tofauti kidogo.
Mwisho wa siku ukweli utajitenga na uongo.