Na Daud Magesa, Mwanza
HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza imeridhia wamachinga waendelee kufanya shughuli zao katika baadhi ya maeneo katikati ya jiji.Mvutano baina ya
halmashauri hiyo na wamachinga ulimalizika Alhamisi wiki iliyopita baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Abass Kandoro, na viongozi wa halmashauri ya jiji la Mwanza kukutana na uongozi wa wamachinga na kufikia makubaliano hayo.
Muafaka wa kufanyia shughuli zao katikati ya jiji ulifikiwa kwa amani na utulivu baada ya uongozi wa serikali ya mkoa, halmashauri ya jiji kukutana na viongozi wa wamachinga na kubainisha maeneo yanayofaa kwa wafanyabiashara hao bila kuchafua
mazingira wala kuvunja sheria zilizopo.
Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango miji wa halmashauri ya jiji, Bw. Henry Matata alikiri kufikiwa kwa muafaka kati ya uongozi wa jiji na wamachinga hao, muafaka ambao uliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Abass Kandoro.
Bw. Matata alisema maeneo sita yameruhusiwa wamachinga kuyatumia kufanyia biashara zao na kuyataja kuwa ni Mirongo Community Centre na Mlango Mmoja ambako kuna baadhi ya wamachinga wameendelea kufanyia shughuli zao tangu yalipotengwa.
Magari yote yaliyokuwa yakitumia eneo la Mirongo Community yamezuiwa kutumia eneo hilo tena, huku Mlango Mmoja ambako mmoja wa maofisa wa jiji aliyeziba choo na kukigeza vyumba vya maduka akiamuliwa kuyavunja na kuacha kitumike kwa
wafanyabiashara.
Maeneo mengine yaliyoruhusiwa kutumiwa na machinga ni pamoja na eneo la soko la vitunguu (nje ya soko kuu), Miti Mirefu (nyuma ya nyumba ya wageni ya Zimbabwe) na Mkuyuni kuelekea relini. Eneo jingine ni la mtaa wa Makoroboi (kuacha eneo la Misikiti ya Wahindi)
Matata alisema kuwa kulingana na makubaliano hayo wamachinga hawataruhusiwa kufanyia biashara zao katika barabara kuu za Nyerere, Kenyatta, Pamba, Lumumba, Nkuruma, Rufiji, Uhuru na nyinginezo kama ambavyo wamekuwa wakifanya kabla ya mazungumzo hayo kufanyika umpya mwishoni mwa wiki.
Vile vile wamachinga wanaweza kwenda kufanyia
biashara zao katika maeneo ya Buhongwa, Sabasaba, Igoma, Igogo, Nyakato NHC, Kitangiri, Kiloleli, Kayenze, Mkolani na Magomeni Kirumba ambayo awali walipangiwa.
Mbali na Kandoro kuongoza zoezi hilo ambalo lilizua vuta nikuvute kati ya wamachinga
na uongozi wa jiji, Meya wa Jiji Bw. Josephat Manyerere na Naibu wake Bw. Chales Chinchibera, walihudhuria shughuli hiyo, wakiwemo Wabunge wa majimbo ya Nyamgana na Ilemela, Bw. Ezekia Wenje na Highness Kiwia na Mwenyekiti wa Mipango Miji Bw. Matata na baadhi ya Madiwani.
Hatimaye wamachinga wameanza kuthaminiwa,asanteni Chadema.
ReplyDeletecongratulation all chadema and kandoro kwa hili na ccm muige msifikiri mafisadi ndio wenye nchi tu
ReplyDeleteHongera sana Chadema Mwanza, mmeonyesha umuhimu wa kuthamini kila binadamu unavyoweza kuleta amani na maendeleo katika nchi yetu.
ReplyDeleteNadhani bado huu si ufumbuzi madhubuti wa swala hili, mi nadhani kuwepo na mkakati endelevu wa kujenga machinga complex angalau 3 yaani moja katika kila bara bara kubwa ya mwanza (Makongoro, Kenyatta na Nyerere) Kwa makongoro road wajenge complex pale Pasiansi, Nyerere wajenge Mlango mmoja na Kwa Kenyatta wajenge Mkuyuni. HII itasaidia kupanua mji, kuuweka safi na pia kuunguza msongamano mjini.
ReplyDelete