MADRID, Hispania
TIMU ya Real Betis imevuruga rekodi ya Barcelona ya kutaka kufikisha mechi 28 bila kufungwa, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika michuano ya
Kombe la Copa del Rey, lakini mabingwa hao wa Hispania wakafanikiwa kusonga mbele hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa jumla ya mabao 6-3.
Mechi hiyo ambayo ilifanyika usiku wa kuamkia jana, Jorge Molina alifunga mabao mawili dakika saba za mwanzo wa mchezo huo na kuwapa matumaini mashabiki waliofurika kwenye Uwanja wa Benito.
Hata hivyo timu hiyo ya Betis ilifanikiwa kuwadhibiti vilivyo wachezaji, Lionel Messi na Xavi Hernandez wasielewane hadi dakika ya 38 wakati Muargentina huyo alipofunga bao dakika ya 32.
Hata hivyo, Messi alishindwa kufikisha bao lake la 33 baada ya shuti lake la penalti alilopiga dakika ya 54 kupaa juu ya lango huku mchezaji Arturo 'Arzu' Garcia, akiifanya timu yake iwe mbele kwa mabao mawili zaidi baada ya kuwahi mpira uliokolewa kizembe na mlinda mlango, Jose Manuel Pinto.
Kwa ushindi huo, timu hiyo inayoongoza ligi daraja la pili itakuwa imelipiza kisasi cha kufungwa kwenye Uwanja wa Camp Nou, ambako Barcelona ilipata kipigo chake cha mwisho cha mabao 2-0 dhidi ya Hercules iliyofanyika Septemba 11, mwaka jana.
No comments:
Post a Comment