NA Amina Athumani
VYAMA vyote vya michezo vinavyoshiriki mashindano ya Afrika 'All Africa Game' vinatarajia kukaa meza moja na Baraza la Michezo Taifa (BMT) ili kuelezea mikakati
waliojipanga kwa ajili ya ushiriki wao katika michezo hiyo.
Michezo hiyo ya All Africa Game hufanyika kila baada ya miaka minne na kushirikisha michezo mbalimbali ikiwemo soka, netiboli, kikapu na riadha.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa BMT, Henry Lihaya alisema michezo hiyo inatarajia kufanyika Oktoba, mwaka huu huku Tanzania ikiwa ni moja ya nchi shiriki zinazoshiriki michuano hiyo.
"Tutakaa na vyama vyetu ili kuona tunashirikiana nao vipi katika maandalizi ya kuandaa timu zao katika michezo hii kwani sisi ndio wenye dhamana ya kuhakikisha timu zetu zinafanya vizuri na kuliletea sifa Taifa,"alisema Lihaya.
Alisema kuhusu lini watakutana na vyama hivyo bado hawajapanga kwa kuwa mchakato bado unaendelea wa kutaka kujua zaidi kwa mwaka huu ni michezo gani iliyojidhatiti kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo.
Mara nyingi kwa Tanzania michezo inayoshiriki mashindano hayo kwa mara nyingi ni riadha, ngumi na kuogelea ambapo kwa mwaka huu michezo hiyo inatarajiwa kuongezwa.
No comments:
Post a Comment