05 January 2011

Polisi yazua maandamano CHADEMA

Na Agnes Mwaijega

JESHI la Polisi limesitisha maandamano yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha kushinikiza kurudiwa uchaguzi wa
Meya wa Halmashauri ya Jiji.

Hatua hiyo imetokana taarifa ambazo jeshi hilo limedai za kiintelijinsia, na tetesi kwamba maandamno hayo yanaweza kuambatana na vurugu na kusababisha uvunjivu wa amani.

Hata hivyo, jeshi hilo limeruhusu chama hicho kufanya mkutano wa hadhara na kuahidi kutoa ulinzi wa mkutano huo.

Awali, CHADEMA ilipeleka maombi ya kufanya mkutano na maandamano ya amani, hata hivyo jeshi liliwaomba kusubiri mpaka lifanye majadiliano juu ya maombi hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema alisema kuna viashirio vingi ambavyo jeshi hilo limegundua kwamba endapo litaruhusu maandamano kutatokea vujo na vurugu.

"Ufuatiliaji wa kiintelijinsia unaonesha wazi kamba kama tutaruhusu maandamano basi tutarajie hali isiyokuwa ya kawaida, ndiyo maana jeshi limeamua kusitisha maandamano hayo," alisema IGP Mwema.

Alisema katika mkutano huo jeshi litaimarisha ulinzi wa hali ya juu ili kuzuia uvunjifu wa amani mkoani humo.

"Jeshi litahakikisha mkutano unafanyika katika hali ya amani na utulivu," alisema. 

Alisisitiza kuwa jeshi hilo limeamua kutolea taarifa hizo jijini Dar es Salaam kwa sababu kuna vyombo vingi vya habari hivyo zitawafikia kwa haraka.

22 comments:

  1. Polisi acheni woga hizo taarifa za kiintelijensia ni uzushi mtupu. Polisi mnafanya kazi ya CCM, nawaambia nguvu ya umma ni zaidi hata jeshi zima la nchi hii haiwezi kuzima nguvu ya umma. Kaeni chonjo

    ReplyDelete
  2. NGUVU YA UMMA INAITESA CCM NA SERIKALI YAKE, NI SILAHA YA MAANGAMIZI KWA UTAWALA WA KIDIKTETA

    ReplyDelete
  3. SAUTI YA UMMA NI SAUTI YA MUNGU JAMANI MBONA HAMUELEWI, ACHENI KUTUMIA NGUVU KUZIMA NGUVU YA MUNGU SASA TUNASUBIRI NA MWANZA NA MIKOA MINGINE...

    ReplyDelete
  4. Polisi wa kuzia maandamano wapo lakini polisi kwa ajili ya kulinda watu wakati wa maandamano hawapo... mimi yangu macho na maskio mpaka nione ukomo wa hii serikali ya kiditeta..

    ReplyDelete
  5. SAIDI MWEMA Ukiwaacha wananchi wakaandamana unaumia nini mwilini mwako au ndio unalinda ugali wako kwakuwa aliyekuteua amesema hataki maandamano ya CHADEMA hivyo nawe unatuzuga kwa kusema kuwa umepata taarifa kuwa kutakuwa na vurugu?! vurugu ailete nani kama sio polisi wako wanaoleta vurugu hapa nchini, watu wameshakuchoka wewe na na polisi wako iko siku yenu watanzania watawatolea uvivu na kuwaambia imetosha sijui mtakimbilia wapi au unadhani cheo hakitakuacha hicho kumbuka cheo ni dhamana utakawa mtaani na sie siku si nyingi sijui utajificha wapi MKUU

    ReplyDelete
  6. WANACHADEMA NA VIONGOZI WENU ACHENI UJINGA,USIFIKILI SERIKALI NI CLUB YA MUZIKI KILA MTU ATACHEZA,kAMA KWELI HAMKUWA NA NIYA YA FUJO SIMGEENDA MKUTANDONI KWA AMANI MPAKA MANDAMANO? kAPU LA MJAJA MJINGA HATII MKONO CHADEMA WAHAWANA MPANGO SERIKILI IMEKUBALI KUHUSU KATIBA MPYA SASA NYINYI KELELE ZA NINI?

    ReplyDelete
  7. Polisi acheni huo unyama, acheni kuwanyima raia haki yao. Kisheria maandamano hayazuiliki katika nchi yeyote. Inatakiwa polisi wawe na utaratibu wa maandamano kwa usalama wa raia na kuwalinda. Kama hawajui waombe wafundishwe sio kutumia silaha, mabomu kwa madhara ya raia. Sasa mbona utaona ya kuwa wananchi hawajaleta madhara yeyote ila ndio hayo ya polisi kuwaingilia. Hii serikali ya Kikwete ina mkosi inabala. Halafu serikali inasema haina hela, hizo pesa za kununua mabomuya ya kuwaweka wananchi vilema zinapatikana wapi.


    Wewe SAIDI MWEMA hufai kuwa mkuu wa polisi aliyekuweka hapo alikosea. Unashindwa kuwaelimisha vijana wako jinsi ya kulinda amani. Hawa wanauadui na viongozi wa CHADEMA sio bure. Kikwete amka huko uliko kumesha kucha.

    ReplyDelete
  8. hivi watanzania wanaoshabikia siasa kumbe ni malimbukeni,hivi mnaamini vyama ndio vinaoleta maendeleo upuuzi mtupu.Badala ya kuishi kwa amani ili tutafute namna ya kujikwamua na huu umasikini kila siku imekuwa majigambo tu ya kipuuzi tanzania haiwezi kujikwamua kutoka kwenye umaskini kupitia chadema ,au ccm au cuf nk,ni jukumu letu kuchapa kazi tuache kushinikizwa na viongozi wa vyama hasa chadema wanaopenda malumbano na maandamano.hebu fikiri mtu aliyegombea urais anafikia hatua kuruhusu wananchi wapambane na polisi.wajinga ndio waliwao mtapoteza maisha wananchi then huyo boss wenu slaa anaendelea kupeta tu.kabla hujatenda kitu fikiri kwanza faida na hasara kwa hicho unachokifanya.polisi wanahaki kuzuia maandamano endapo watagundua kuna hitilafu fulani.nawahurumia watanzania wenzangu.

    ReplyDelete
  9. chadema msika riri siasa sio ugomvi mboe baba yako alikuwa mwizi tu kauza mashirika ya umma nawe sila rudi kwe parukia yako ukachunge ktk siasa hakuna jazba wasomi wote wameisha washitukia mbona wenzenu wajanja hawakuwepo? zito na mnyika?na msijifanye kigoma wanawapenda kigoma hata ukisimamisha shati tupu ligombanie litashinga

    ReplyDelete
  10. chdwma msiutumie ujinga na umasikini wa watanzania wengi ambao hawajaenda shule kuwa kielelezo chenu cha kupendwa niayenu ni kutaka madarakatu nayo hamtayapata kwanza hammaanishi chochote msijifanye mnauchungu na nchi hii unafiki mtupu nawe slaa kachnge na uzee wako unakujia vibaya umeisha pagawa mboe we babayako ameiibia serikali leo unajifanya unauchungu na nchiyetu muongo mkubwa na makengeza yako nasema kwa uchungu sababu kila kukicha vyombo vya habari chadema chagema hamuoni kuwa mnatukera?tumeishaanza kuwachoka bara werikali ya mseto haitatokea tumechoka kuwasikia mboe slaa jamani tuhurumieni nanyi wananchi kwa nini mnaendekeza ujinga umasikini wenu utawaponza mboe au slaa hawata wasaaidia kitu wanafamilia zao wakusaidie wewe?hawana jupya chadema chadema pls tumechoka kusikia kila kukicha tunamambo mengi ya kufanya siokila kukicha mboe kasema slaa kasema nini sasa hii?mnatukata tu

    ReplyDelete
  11. Mashabiki wa CCM utawajua tu. Hawana punctuation au busara kama viongozi wao.

    ReplyDelete
  12. TUNAOMBA SAID MWEMA UTOE TATHMINI YA ZOEZI ULILOLIENDESHA JANA MKOANI ARUSHA KWAMBA KWA AMRI YAKO UMEUA RAIA WANGAPI, WALIOJERUHIWA ILI WANANCHI TUELEWE KAMA ULIFANIKIWA NA HILO ZOEZI AU LAH, NA LAANA NA DAMU YA HAO WALIOKUFA NA DAMU ZAO KUMWAGIKA ZIKUSUMBUE MPAKA SIKU UTAKAPOINGIA KABURINI,UNGEWAACHA WAANDAMANE WENYEWE UNGEPUNGUKIWA NINI? AU ULITAKA KUUA RAIA NDIO UONEKANE NAWE UNA SAUTI. KUMBUKA SIKU YA MWISHO INAKUJA NA HUTASEMA KUWA ULIAGIZWA NA RAIS AU MTU YOYOTE UTASIMAMA MWENYEWE KITANZINI KUJIBU MASHTAKA YA KUUA RAIA NA KUJERUHI WATU WASIO NA HATIA

    ReplyDelete
  13. If you don't stand for something you will fall for anything.

    ReplyDelete
  14. Mh.IGP.usigeuzwe kuwa wakala wa CCM,kama ungelitaka kuzuia maandamano ungetoa kwa maandishi sio kwenye vyombo vya habari.Ninaomba utumie busara zaidi kuliko kusukumwa kama gari bovu.

    ReplyDelete
  15. Mbona matusi.Kwa mujibu wa sheria polisi wana haki ya kukataza maandamano. Hiyo ni sheria ya nchi. Basi kama tunaona haifai basi tuifute hiyo sheria. Na Raisi yeyote ana haki ya kuheshimiwa. Wana Chadema mmeanzisha mtindo mbaya. Huenda katika siku za usoni mwanachadema akachaguliwa kuwa Raisi. Je, itafaa huyo Riasi kuvunjiwa heshima ?

    ReplyDelete
  16. Polisi ni wakala wa CCM na Serikali yake na si WATUMISHI WA KULINDA WANANCHI......watu wameiba mabilioni ya EPA wakajigawia wenyewe. Mafisadi wanakula nchi hii kama nzige [wanakula huku wanakunya]....SAUTI YA WATU NI SAUTI YA MUNGU ...Chadema hawana jeshi..Lakini Mungu aliye hai mpaka leo na kesho ...atawaonyesha CCM ya kuwa YUPO na hatavumilia madhambi kwa watu wake....its just a matter of time...CCM watapata majibu toka kwa Mungu na si muda mrefu....CCM wanafikiri Mungu ameshazeeka...Lol ..kweli Nyerere alisema ukianza kula nyama ya mtu utaendelea tu.......

    ReplyDelete
  17. tena ninyi na huyo fisadi wenu et raisi matakufa kifo kiaya sana. wala hamta tawala inchi hii.

    ReplyDelete
  18. NGUVU YA UMMA INATOKA KWA MUNGU ...CCM WASUBIRI MAJIBU...KWAKUWA WANAFIKIRI MUNGU ASHAZEEKA...!!!

    ReplyDelete
  19. Chadema ....Oyeeee....CCM nikama BABO wa Ivory Coast......mtajuta - TANZANIA imeumbwa na Mungu kama CCM waliiumba Tanzania tusubiri tuone mwisho wake..hakuna haja ya kubishana ........

    ReplyDelete
  20. Mwisho wa ccm ndo huoooooo.......... kuanza kuuwa watu mpaka sasa bbc wameripoti watu 10 wamepoteza maisha. sijui IGP ATAJIBU NINI akipelekwa ICC kama mwenzake wa Kenya, yetu macho ila serikali hii haijali haki za binadamu ila madaraka HAIINGII AKILINI Mbunge wa Tanga kupiga kura Arusha ili kuisaidia tu CCM.
    Halafu nauluiza swali kwa IGP mbona Olesendeka alimvunjia heshima mkuu wa mkoa mbele ya wananchi hakagoma kutolewa nje wala hakushtakiwa na yule mgombea wa mashwa aliyempiga ocd mtama vp? Mbona wanawapiga hawa wa upinzani?

    ReplyDelete
  21. KWA KWELI WATANZANIA WENZANGU TUWE NA BUSARA NA KAULI ZA KIUTU . KILICHOTOKEA ARUSHA JANA NI AIBU KWA SERIKALI INAYOTAWALA.
    TUJIULIZE MTU AKIKAIDI AMRI YA KUTOKUFANYA MAANDAMANO HUKUMU YAKE NI KUUAWA? WAMEUAWA WATU WAWILI JANA KWA MUJIBU BBC LEO JIONI. TUJIULIZE KABLA YA POLISI KUINGILIA HAYO MAANDAMANO KUNA VURUGU ZOZOTE ZILITOKEA AMA ZILIZOFANYWA NA WAANDAMANAJI...? Hata mwizi akiiba Serikali inakataza wananchi kuchukuwa sheria mkononi... Wangeachwa waandamane na there after kama waliandamana kimakosa then viongozi wa Chadema wafunguliwe mashtaka. hii kuuwa watu wananchi leo wakihamasishwa wajibu mapigo hii nchi itakalika? IGP be so carefull. Damu zilizomwagika ,maisha ya watu yaliyosimama...mtu kufa ni kusimamisha kizazi chake...IGP UMEFANYA NINI? mtu anatoka Tanga anakuja kumchagua Meya wa Arusha leo Chadema wanahoji then Serikali inajibu kwa kuuwa? Watanzania tuache upumbavu ,,,nani katuloga? Tusiwalaumu Chadema kwa ushabiki tu wa kisiasa. Mimi sii mwanachama wa Chadema ila tuwe wakweli. its pain. Mungu wa Ibrahim,Isaka na Yakobo ulipize kisasi maana umesema kisasi ni juu yako. Wafiji familia zilizopoteza wapenwa wao.. Eee Mungu wa mbinguni usikae kimya ututeetee watanzania.

    ReplyDelete
  22. Mwenye kulaumiwa ni Slaa aliyewaambia maskini hawa vijana wasio na elimu eti waende Polisi wawatoe viongozi. Jamani huyu ndiye mtu ambaye tungempa urais. Katika nchi yoyote hairuhusiwi kupambana na polisi hata kama uko sahihi, na hakuna mtu anayepambana na polisi na kutoka salama. Nyie manoongea kama vile poisi ilikuwa inapambana na watu watulivu hamtendi haki. Hawa watu wamefanya uharibifu mkubwa. Hivi Slaa hajui hili? Chadema wanaweza kuwa na ajenda sahihi lakini njia wanazotumia hazifai. Slaa anataka maadamano nchi nzima. Akumbuke kuwa hata vyama vingine vina wafuasi hata kuzidi hao wa wachadema. Hiki kitu kinachoitwa nguvu ya umma ni umma gani? wafuasi wa chadema ndiyo wamekuwa umma? CCM ikiamua wafuasi wake waandamane ndiyo mtajua nguvu ya umma ni ipi. Jamani tanzania hatujafikia pahala ambapo tunahitaji nguvu ya umma. Kikwete ni msikilizaji. Kwa mfano amesikia kilio cha katiba mpya, na amefanya mambo mengine mengi kwa kufuata public opinion. Siyo dikteta kama chadema wanavyojaribu kumpamba. Nawaomba chadema wawe na moyo wa kujadiliana badala ya kupambana kama sare zao zinavyoonyesha. Kikwete anashaurika acheni hiyo tabia ya kumdhalilisha mheshimuni kama kiongozi wa nchi yetu.

    ReplyDelete