03 January 2011

Pinda atolea macho mashamba yaliyobinafsishwa

Na Sammy Kisika, Sumbawanga

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewaagiza wakuu wa mikoa nchini kuanza kufuatilia mara moja mashamba yote ya serikali yaliyouzwa au kubinafsishwa kwa wawekezaji mbalimbali kwa lengo la kutaka kufahamu iwapo yanafanya
kazi iliyokusudiwa au la.

Bw. Pinda alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa chama na serikali mkoani Rukwa katika ikulu ndogo ya mjini Sumbawanga.

Alisema kuwa yapo mashamba ambayo yalikuwa na serikali na kuuzwa kwa wawekezaji hao lakini baadhi yake yamekuwa hayatumiki kwa malengo yalikusudiwa kinyume na makusudio ya serikali kuyauza mashamba hayo.

Ipo haja sasa viongozi wa mikoa ebu fuatilieni ili kufahamu iwapo mashamba hayo ambayo mengi kati yake yalikuwa ya mifugo na wawekezaji wake waliyanunua wakiahidi kuyaendeleza, lakini kwa haraka haraka unaona kuwa wameshindwa kufanya hivyo,รข€ alisema Pinda.

Alisema lipo tatizo la viongozi wa mikoa kutofuatilia utendaji wa sekta binafsi, hivyo baadhi yao huchukulia mwanya huo kujifanyia mambo yao kama wanavyotaka pasipo
kufahamu kuwa sekta binafsi nayo ni muhimu katika kuchangia uchumi wa mikoa hiyo na maeneo husika.

Waziri Mkuu alitolea mfano mkoa wa Rukwa ambako kuna mashamba matatu ya mifugo yaliyouzwa, hivyo kutakiwa kuyafuatilia utendaji wake akiyataja mashamba ya mifugo ya Nkundi na Kalambo yaliyopo wilayani Nkasi na NAFCO iliyopo Sumbawanga mjini.

Ebu viongozi fuatilieni haya mashamba, mfano lile NAFCO ambalo mlinipeleka likiwa linamilikiwa na Nabii Mwingira, kama kweli lipo kwaa jili ya kuendeleza ufugaji au ni porojo tu, ipo haja tufahamu ili serikali ifanye tathimini ya uwekezaji wao,alisema Pinda.

Waziri Mkuu alilitaja shamba jingine kuwa ni la Nkundi ambalo lilinunuliwa na mbunge wa zamani wa Kwela, Dkt. Christant Mzindakaya ambalo alihitaji maelezo ili apate kufahamu iwapo linafanya kazi iliyokusudiwa.

1 comment:

  1. pinda ukiwa sumbawanga swal la mashamba siotatizo kwetu, wewe ongelea haki na amani nasi mashamba. wana sumbawanga tumeonewa wewe unakuaja kueleza swala la mashamba.

    ReplyDelete