19 January 2011

Neema ya ajira yazidi kuwafuata walimu

Na Benjamin Masese

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imewapa matumaini ya ajira nyingine wanafunzi waliohitimu mafunzo ya ualimu mwaka 2009/2010  na kuachwa kutokana na sababu mbalimbali mbali ya  wale 9,226 waliotangazwa na
Waziri wa wizara hiyo, Dkt. Shukuru Kawambwa.

Katika tangazo lilitolewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Hamisi Dihenga liliwataka wanafunzi wote ambao wamefaulu na majina yao hayakuonekana kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi kuandika barua kwa Katibu Mkuu na kuambatanishwa vyeti halali na taarifa ya matokeo ili zifanyiwe kazi.

Hata hivyo alitoa onyo kwa waombaji na wahitimu kwamba wizara haifanyi mabadiliko yoyote kwa wale walimu waliopangiwa vituo vya kazi.

Kutolewa kwa ajira hiyo  kumetokana na wanafunzi waliohitimu mafunzo yao kuvamia wizara hiyo juzi wakitaka kuelezwa vigezo vilivyotumiwa na serikali kutoa ajira 9,226 huku wakiachwa wanafunzi walio na sifa.

Hata hivyo wanafunzi hao jana waliendelea kufika hapo wizarani mbali ya viongozi juzi kuwaeleza kuwa suala lao linafanyiwa kazi

Kwa mujibu wa maelezo ya wanafunzi hao walisema kuwa wameahidiwa kufanya mazunguzo na viongozi wa wizara hiyo leo ili kujua hatma ya ajira yao.

Juzi Wanafunzi hao kutoka vyuo mbalimbali vikiwemo cha Mtwara, Marangu, Morogoro na vinginevyo walifika wizarani hapo na kuzua tafrani getini baada ya kuzuiwa na walinzi huku wakitaka kuonana na Waziri wa Elimu Dkt. Kawambwa kitendo kilichosabisha ulinzi kuimarishwa.

Walisema kuwa tangu wahitimu masomo yao Mei mwaka jana wamekuwa wakipewa ahadi ya kuajiriwa na serikali lakini hadi leo ajira hakuna kilichofanyika zaidi ya hali ya sasa inayoanza kuonesha ubaguzi kwenye suala hilo.

2 comments:

  1. tunawapa pole walimu wote waliokosa ajira mungu atawatangulia

    ReplyDelete
  2. Poleni walimu bila shaka Prof amewatia matumaini muandike hizo barua ingawa zinaweza zikachukua miezi sita (6)bila majibu.

    ReplyDelete