24 January 2011

Nchi inakoelekea si salama-Askofu

Na Benjamin Masese

KIONGOZI wa kundi la waumini waliojitenga na Kanisa la Anglikana la Tanzania, Askofu Ainea Kusehna amesema kuwa nchi inapoelekea sasa si salama kutokana na
baadhi ya viongozi kuchaguliwa kwa rushwa huku wakinyosheana vidole.

Askofu Kusehna alisema hayo katika ibada maalumu iliyofanyika Mbezi Beach, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wote wa kanisa hilo la Anglikana la Kiinjilisti Tanzania (KAKT) kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.

Katika ibada hiyo Askofu Kusehna alisema matatizo manne yanayoikabili nchi na watu wake ikiwa ni pamoja na rushwa, tamaa ya fedha na mali, madaraka na ukubwa pia tamaa ya starehe.

Askofu Kusehna alisema makanisa yatasarambatika na taifa kuhangamia ikiwa watu wake hawatabadilika na kuacha uchu wa madaraka ya rushwa na kufuata haki inayoinua taifa lolote la demokrasia.

Alisema kuwa asilimia kubwa ya maaskofu na viongozi wa serikali wanachaguliwa kwa rushwa na kuwa yupo tayari kuwataja viongozi wa dini pale inapohitajika katika vikao vyao vya majadiliano.

"Mkisikia maaskofu wakitajwa, tambueni si wote ni maaskofu kutokana na matendo yao maovu ya rushwa, na ndio wa kwanza kuwanyoshea vidole wengine bila kujitambua kuwa wao wameoza.

"Sisi tunatakiwa kuwa nuru kwa jamii pia kuwa mfano wa chumvi inayoleta ladha katika chakula, hebu niwaulize leo, sisi ni chumvi katika jamii?" alihoji.  .

Aliongeza kuwa kizazi hiki cha maaskofu ni cha usanii, na hakiwezi kutoa neno la Mungu linaloburudisha na kubadili mtazamo katika jamii, bali wanatoa somo linaloweza kuwalinda wao, huku wakiunga mkono kuwepo kwa ushoga na usagaji.

Akizungumzia usajili wa kanisa hilo alisema kuwa kumekuwepo na mikakati kabambe kutoka kanisa la Anglikana Tanzania ya kuchafua kundi hilo ili likose usajili, na kuwa tayari wamepata nyaraka zao zilizopelekwa Wizara ya Mambo ya Ndani zikidai kwamba kikundi hicho kinatumia vichochezi vya kikabila, jambo ambalo ni hatari linaweza kudhoofisha mtengamano na umoja wa makanisa na nchi nzima.

Askofu Kusehna alisema kuwa nyaraka hizo ziliandikwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Valentino Mokiwa kwenda kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Laurence Masha ambaye alimjibu kwa kumhakikishia kanisa hilo halitasajiliwa.

Aliongeza kuwa tuhuma zingine ni pamoja na kudaiwa kutumia nembo ya Anglikana, vitabu vyake vya ibada, nyimbo na liturgia, kinyume cha sheria, wakati likiwa halijasajiliwa.

Askofu Kusehna alihitimisha kwa kutoa tamko kwamba hakuna anayestahili kumnyoshea mwingine kidole iwe serikali, polisi, viongozi wa dini au wananchi kwa kuwa wote wana makosa, na pia wote wanatakiwa kujisafisha kuanzia kwenye chimbuko la matatizo hayo.

14 comments:

  1. mungu akubariki sana mtumishi wa mungu ww ndio umesema sio maaskofu wa romani katoliki wanaoonyesha upendeleo dhahiri kwa chadema mungu akubariki sana mtumishi wa mungu nitazidi kuwaombea mpate ushindi mungu ni mwema ubarikiwe sana AMIN

    ReplyDelete
  2. Hao wanaopinga kanisa lako lisisajiliwe ni wa kanda ya kaskazini waliozoea kumiliki makanisa na hazina yake na sasa wameona haitoshi wanataka hazina ya serikali. umesema kweli hakuna aliyemsafi kama kanisa la katoliki linavyomsafisha mgombea wamtakaye,wanashindwa hata kumkemea kwa kupora mke wa mtu na kumtangaza hadharani kuwa mchumba wake, jeuri ya fedha zake za ubunge na ufisadi wa katika chama chake ndio inampa kiburi cha kumuonea mlalahoi mwenye mke. hamasisha waumini wako wajiandae kwa katiba mpya na hilo waliweke wazi kwenye maoni yao ili kwamba kanisa lililokuwa na hatimiliki ya kutawala nchi hii likome kuamulia watu mambo

    ReplyDelete
  3. We vipi, maoni unayotoa hapa ni ya udaku na yanayoingilia maisha binafsi ya mtu. Mh. Slaa kama anaishi na mke wa mtu hayo ni matatizo yake binafsi na wala siyo "matatizo" ya Kitaifa. Na kama hiyo ni thambi basi shauri hili ni kati yake yeye na Mungu wake. Kwa nini unataka kanisa liingilie maisha binafsi ya mtu????

    KISIASA, KIUTAWALA, KIFIKRA na KI-UZALENDO Dr Slaa ni safi. Tanzania hatutafuti kuongozwa na MALAIKA. Wala hatuangalii mtu ametoka dini ipi. Tunayemtaka ni mwanasiasa ambaye :-
    1/ Anayo mapenzi ya kweli na nchi yake. 2/ Anayechukia rushwa, wizi, ufisani, nk.
    3/ Na anajua nchi yetu inapaswa kuelekea wapi, kwa njia ipi na kwa manufaa ya Watanzania wote.

    Je, huko CCM ni wangapi wenye sifa hizi za Dr Slaa ???

    Dr Slaa, usikatishwe tamaa na watu wenye mawazo finyu na wasioitakia mema Tanzania. Tafathali endeleza mapambano, tupo nyuma yako kwa hali na mali !!!!

    by
    Abdalha Ali Juma.

    ReplyDelete
  4. Kwa hiyo rais hata akiwa mla unga anafaa,sababu hayo ni maisha yake binafsi?

    ReplyDelete
  5. Nilisikia kuwa kesi ya mke ilipelekwa mahakamani, vipi mbona hatusikii hukumu au ilikuwa kuharibiana kwenye kampeni? Mmedanganywa mkadanganyika kama watoto wadogo. poleni!

    ReplyDelete
  6. Mbona haya maoni ni ya kushambulia tu viongozi? Hamna maoni ya kueleza hoja alizotoa askofu hapo juu! mbona hamuungi mkono hoja zake ama kuzipinga? Tujuwe kweli waTz wanafuatilia taifa lao kwa makini.

    kuna hoja hapo kuwa Nchi imo kwenye hatari
    Maadili kwa Maaskofu, Rushwa ya uongozi nk mbona hatujadili haya?!

    Au ndo ile kasumba yetu watanzania kutotaka kutumia akili kwenye mambo magumu hatimaye tunatoa majibu mepesi kwenye maswali magumu?

    Sasa Dr. Slaa anatuhusu nini kwenye Personal Issue zake! Mmechimba kwa undani huyo mke wa DR Slaa kamtaka mwenyewe Dr Slaa kwa sababu ya Ujasiri wake mpaka kamkimbia mumewe, na ni muda gani toka aachane na mumewe hadi akutane na Dr Slaa wawe wapenzi haya mbona hamuyafafanuwi tuelewe!

    Kusema Dr. Slaa kapora mke si sahihi na ni kumtukana Mama wa watu na wanawake wote kuwa hawana maamuzi ya kimapenzi kwa waume wao. Wao ni vyombo tu vya wanaume kutumia kama anavyotaka kuonekana Mama Mashumbushi!

    Tuwe na Adabu kwa Wanawake kama wao walivyo na adabu kwetu sisi wanaume! Hawa si vyombo vya wanaume bali ni binadamu wenye utashi wa kukubali, kumtafuta na kumpenda mtu wanayemtaka!

    Wanawake si vyombo vyetu wanaume, ni binadamu kama tulivyo sisi wanaume. Tuache kauli za matusi kuwa Mchumba wa Dr Slaa ameporwa toka kwa mwanaume mwingine! Mbona sasa asiende kuishi kwa mume wake kama kweli bado anampenda?

    Hata akili hii inatuhitaji Digrii kuielewa? Wangapi leo wameumizwa na wapenzi wao na hawataki hata kuwaona? Tuache hivyo ndugu zangu. tujadili Taifa. Waliotufikisha kwenye sakata la DOWANS tunawafanyaje? Hakuna collective efforts zitakazofanywa na watanzania kuwafikisha mahakamani kwa kututia hasara kwa tamaa zao.

    Zinahitajika gharama gani kuwafungulia kesi wahusika wote hao nk. hizi nadhani ni baadhi ya hoja tunazostahili kuzizungumza tupate majibu kwa maslahi ya Taifa letu!

    By Carwin.

    ReplyDelete
  7. TATIZO LA WATZ NI KUWA WANATABIA MOJA TU YA KUFIKIRI KWA TUMBO BADALA YA KUFIRI KWA AKILI ILIYO KICHWANI. UKIANGALIA WOTE WNAOTOA MAWAZO YA KUWASHAMBULIA VIONGOZI UTAGUNDUA KUWA NI WALE WENYE FIKRA ZA KI-TUMBO TU. NAWAHAKIKISHIA KUWA WENYE MAWAZO YA KUUNGANA NA UFISADI WA CCM HAWATAFIKA 2015.

    ReplyDelete
  8. Kwani hamjui mahakama zetu? hukumu inatolewa kwa kumtizama mtu usoni? ungekuwa wewe mlalahoi basi saa hizi unaozea ndani. kukosa pesa kwa mume wa Mshumbusi sio uhalali wa kuporwa mke.

    ReplyDelete
  9. ASKOFU GANI ALIYEJITENGA NA WENZAKE NA AMESHINDWA KUELEWANA NA WENZAKE HALAFU ANAKUJA KUTOA MAONI KWA KUEGEMEA MGONGO WA DINI ETI ANATOA MAONI HATUKUTAKI. KAMA UNATOA MAONI KAMA MTANZANIA KARIBU LAKINI SI KAMA ASKOFU MKENGEUFU

    ReplyDelete
  10. hayaa unaanza kumtukana Askofu,nyie Watz mna laana. na laana hii ndio inawatafuna sasa

    ReplyDelete
  11. Carwin upo kwenye mstari. Hata hivyo wacha kubisha ujinsia wako. Wewe ni demu tu!

    ReplyDelete
  12. I am a man! My Professional is Community Development Specialist in Gender Relation and Development! Ndiyo maana nipo sensitive na masuala yote hasa usawa wa kijinsia! Sawa bwana!

    Carwin.

    ReplyDelete
  13. Tufikie mahali pa kutoa maoni yanayoendana na hoja na si kupachika chuki binafsi. Sishangai wahenga waliposema waangavu hujadili yenye kujenga bali wenye kutafutatafuta hutaka habari nyepesi nyepesi zisizojenga. Hivi hili la Dr Slaa limekuwa la ajabu kuliko ndoa zinavunjika kila kukicha waume kuoa walioolewa na wanawake waliokuwa na ndoa kuacha na kuolewa na wawapendao? Si himizi hilo, la hasha bali nataka niweke wazi kuwa TUFUNGUKE MACHO TUONE YANAYOTENDEKA Marekani na nchi zingine jinsi ndoa zinavyo-vunjika kila leo TENA kwa MDOA MMOJA KUDAI KUWA ANATAKA UHURU WAKE hivyo kudai talaka yake. NAOMBA HILI LISIFIKE KWETU. Pia suala la mtu MMOJA MMOJA tumwachie yeye na MUNGU WAKE...la sivyo ROHO ya YULE MWOVU ITASHIKA KASI KWETU SISI TUNAOTAFUATA TAFUATA YA WATU..TUKUBALI KUTOA BORITI KWENYE MACHO YETU KABLA YA KUTAKA KUTOA LILILO KWENYE JICHO LA MWINGINE.

    ReplyDelete
  14. nyote mnazungumza kwa kujibizana mkidhani kuwa wasomaji wa safu hii wapo ajili ya malumbano! ndg Said yaonekana umeathirika kwa propaganda za UDINI ambao ulitumiwa na CCM wakati wa Kampeni za 2010 na sasa unabaki na ukoko wa mawazo hayo ambayo yalikuwa ni Vitual.

    Rejea ujumbe wa mwanasiasa mkongwe Mh. Sinde Warioba aliyeeleza wazi bila kuuma ulimi kuwa Udini upo kwa Viongozi kwa maslahi yao na wala watu wa chini hawana huo udini. Machinga wanashirikiana waislamu kwa wakristo na hakuna anayetaka kujua dini ya mwenziwe ndipo ampe ushirikiano.

    Hayo mawazo kuwa Wakatoliki wametawala kila kitu na wanataka kuitawala serikali ni UKOKO uliohama nao toka Kampeni za CCM na sasa yamekufanya uwe mfungwa na mtumwa wayo!

    Angalia Taifa linateketea! yapo maswala makubwa yakuchangia na sio kuangalia kitandani kwa Dr. Slaa amelala nani! Wewe mwenyewe tukikutafutia muda wa kukuchunguza mbona macho yatapofuka!

    Acha hizo mtanzania mwenzangu! angalia tuendako acha kuangalia hapo ulipo tu

    bye

    ReplyDelete