24 January 2011

Dowans kuhatarisha uhalali wa serikali

"Kama watalipa faster faster (haraka) watakuwa wameongeza upana wa hoja yangu, badala ya kuliomba bunge kumpigia kura Ngeleja ya kujiuzulu, nitaliomba bunge kadri litakavyoona inafaa, lipige kura ya kutokuwa na imani na serikali," alisema David Kafulila.

Na Tumaini Makene

SAKATA la Kampuni tata ya Dowans bado tete na
bichi sasa imeelezwa kuwa kama halitafanyiwa kazi kwa umakini litaipotezea serikali uhalali wa kisiasa wa kuongoza wananchi walioiweka madarakani.

Iwapo serikali itafikia uamuzi wa kuilipa mabilioni ya fedha kampuni hiyo bila ukweli kuwekwa bayana ili kuondoa 'mazonge mazonge' yanayolizunguka sakata hilo, utakuwa uamuzi mbaya, ukifananishwa na kujitia kitanzi.

Kwa mujibu wa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), Bw. David Kafulira, kama serikali itaendelea na mipango yake ya 'fasta fasta' kuilipa Dowans sh. bilioni 94 kama ilivyoamuriwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) kabla ya mkutano ujao wa bunge, ijiandae kupigiwa kura ya kutokuwa na imani nayo.

Akizungumza jana Dar es Salaam, katika mkutano wa wabunge wasiokuwa katika kambi rasmi ya upinzani bungeni na waandishi wa habari, Bw. Kafulila alilifananisha sakata hilo na kashfa maarufu ya Goldenberg nchini Kenya.

Alisema "inashangaza kuona serikali inakuwa na speed (kasi) ya ajabu kutaka kuilipa Dowans eti kwa sababu ni suala la kisheria, mbona hatujaona speed hiyo katika kuwalipa walimu waliokuwa wakiidai serikali kisheria pia, au kwa nini hatuoni kasi hiyo katika kuwalipa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wanaoidai kisheria.

"Serikali itambue wazi kuwa hili si suala la lelemama wala masihara...Ngeleja (William, Waziri wa Nishati na Madini) asicheze na moto wa Dowans, chimbuko lake ni kubwa liliwahi kuiangusha serikali, alipojiuzuru waziri mkuu. Asikurupuke kufanya maamuzi. Maana hata ndani ya serikali inaonekana hawana mwafaka juu ya suala hili," alisema na kuongeza;

"Serikali iwe makini kuna mazonge mazonge mengi katika hili, ukweli haujajulikana. Serikali inapoteza legitimacy (uhalali) wa kisiasa wa kutawala, suala hili litaiondoa CCM madarakani kama kashfa ya Goldenberg ilivyoitafuna na kuiondoa KANU na Moi (Rais Mstaafu wa Kenya, Daniel Arap) madarakani.

"Kashfa ile nchini Kenya ilianza miaka ya 1993 huko, hivi hivi, lakini ikaja ikaiangusha KANU na Moi. Unajua unapopoteza uhalali wa kisiasa wa kuongoza unaweza kusababisha machafuko, hasa katika wakati huu ambapo kuna tatizo kubwa la uadilifu wa viongozi. Waache hoja iende kwenye mkaa wa moto wa bunge, kisha ndiyo walipe."

Ingawa alisema mpaka sasa hajajibiwa rasmi kama hoja yake itawasilishwa katika mkutano wa pili wa Bunge la 10 uliopangwa kuanza Februari 8, Bw. Kafulila aliongeza kuwa iwapo serikali itaamua kufikia maamuzi ya kuilipa Dowans, itakuwa imepanua wigo wa hoja yake binafsi, kwani ataliomba bunge 'kadri linavyoona' lipige kura ya kuiangusha serikali.

Mpaka sasa hoja yake hiyo, ambayo aliiwasilisha ofisi za bunge Desemba 10 mwaka jana na kujibiwa Desemba 14 kuwa inafanyiwa kazi, ina sehemu mbili, mgawo wa umeme unaoendelea kuathiri uchumi na hukumu ya ICC iliyoiamuru TANESCO kuilipa Dowans sh. bilioni 94 kwa kuvunja mkataba wa kuzalisha umeme.

"Hatuwezi kuendeshwa kwa mambo ya mission town (ujanja ujanja wa mjini), kama watalipa faster faster (haraka) watakuwa wameongeza upana wa hoja yangu, badala ya kuliomba bunge kumpigia kura Ngeleja ya kujiuzulu, nitaliomba bunge kadri litakavyoona inafaa, lipige kura ya kutokuwa na imani na serikali.

"Ipunguze speed ya kulipa, mbona hatuioni speed ya namna hiyo sehemu nyingine...pia kama bunge litaona kuna haja ya taarifa ya Mwakyembe kusomwa yote pia hakuna shida," alisema Bw. Kafulira.

Akiunga mkono hoja ya Bw. Kafulira kuwa kamwe nchi na Watanzania wasitarajie kuendelea kiuchumi kwa matatizo ya umeme yaliyopo nchini,  Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Bw. Mohamed Habib Mnyaa, alisema kuwa uzalishaji na mahitaji (matumizi) ya umeme ni moja ya vigezo vinavyotofautisha mtu mmoja mmoja au nchi moja na nyingine, katika maendeleo ya kiuchumi.

"Kwa maana ya kiinjinia ukiuliza maana ya maendeleo ni nini, utaambiwa katika sentesi moja tu, kuwa mtu au nchi inayotumia umeme mwingi;

"Kafulila hapa kasema kuwa mahitaji ya umeme Tanzania ni megawati elfu moja mia tano, lakini wenzetu South Afrika (Afrika Kusini) mahitaji yao ni megawati arobaini na mbili elfu (42,000), tofauti hiyo ndiyo iliyopo pia katika pengo la namna nchi hizi kila moja kimaendeleo," alisema Bw. Mnyaa ambaye pia alikuwa mjumbe wa Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dkt. Mwakyembe. 

Machafuko Arusha na Katiba Mpya

Mapema, Mwenyekiti wa kamati ya wabunge wasiokuwa katika kambi rasmi ya upinzani bungeni, Bw. Hamad Rashid Mohamed (Wawi-CUF) alisema kuwa machafuko ya Arusha yamesababishwa na serikali kushindwa kutimiza wajibu wake, hasa wa kuwasiliana na raia wake katika namna nzuri, kuepusha madhara.

Alisema ingawa mauaji hayo si mara ya kwanza kutokea nchini, akikumbushia mauaji ya Zanzibar na Mwembechai, Bw. Hamad alionekana kushangazwa na tabia inayoota mizizi ya viongozi kutowajibika linapotokea suala la uvunjifu wa utawala bora, hali ambayo itaifanya nchi isitulie.

"Tunapenda kutoa pole kwa wafiwa. Mola awalaze marehemu mahala pema peponi. Tumejifunza mengi kutokana na hilo, ingawa si mara ya kwanza...sisi tulipoteza takribani vijana 43 ingawa matangazo yake yalikuwa kama amekufa mtu mmoja, Mwembechai pia walikufa watu wengi...kote huko hakukuwa na publicity (haijatangazwa) kama ya Arusha.

"Ninachomaanisha kusiwe na double standard katika mambo haya...suala la Arusha kuna pande mbili, serikali na raia wake...raia wana haki zao na serikali ina majukumu yake...serikali inapaswa kuboresha mawasiliano na raia wake ili kuepusha madhara...huwezi kuruhusu maandamano leo halafu asubuhi ghafla unakataa.

"Lakini pia serikali inaweza kuja na sababu nzito isiyoweza kusema hadharani hasa wakati huu ambapo dunia ina mambo ya ugaidi na vitu vingine, lakini ni jukumu la serikali kuboresha mawasiliano kwa namna ambayo hata raia wanaozuiwa waridhike kuwa kuna suala la msingi.

"Lakini la pili, kuna suala la kuwajibika...kuna matatizo ya serikali au viongozi kuwajibika, hili limekuwa tatizo la msingi sasa nchini, serikali lazima iwajibike, kutowajibika kunaifanya nchi isitulie maana kuna watu wanakuwa hawajaridhika," alisema Bw. Mohamed.

Akizungumzia suala la katiba mpya, Bw. Hamad ambaye alikuwa Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni katika bunge lililopita, alisema kuwa ni muhimu kuwa na katiba itakayotokana na wananchi, ambayo pia haitaacha kipengele muhimu cha kuwahusisha wananchi kila serikali inapotaka kufanya maamuzi makubwa nchini.

Alitolea mfano wa Tanzania Visiwani, ambako Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, haiwezi kufanya jambo lolote kubwa linalogusa maslahi ya wananchi bila kuitisha kura ya maoni ya Wazanzibar wote, kwani ndivyo marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar yaliyofanyika mwaka jana, yanavyosema.

"Pia wananchi wapewe nafasi ya kusema ili iandikwe katika katiba wanataka mfumo wa aina gani wa serikali nchini. Suala hili sioni likizungumzwa katika mijadala inayoendelea...hatuwezi kuacha suala hili katika sera za vyama vya siasa, CUF wanasema serikali tatu, CCM serikali mbili kuelekea moja, NCCR nao tatu.

"Masuala ya msingi kama haya yanapaswa kuwekwa katika katiba si ilani ya vyama, ukienda Marekani au Uingereza leo yako mambo ya msingi ambayo hata akija nani hawezi kuyabadili anavyotaka kwa sababu tayari wananchi wa Marekani au Uingereza walishaamua," alisema Bw. Hamad akiwa na matumaini makubwa kuwa katiba mpya itapatikana.

26 comments:

  1. JK HAKUSHINDA UCHAGUZI SASA ANATAKA KUIINGIZANCHI KWENYE MATATIZO KWA KUMTUMIA MAKAMBA. HIVI NI RAIS GANI HUYU ANAMTUMIA MKE NA MTOTO KUOMBA URAIS? SI NI KWA KUWA ANATUMIA NJIA ZA UOVU AMBAZO VIONGOZI WENZAKE WALIMKATALIA? WALIONA ALIVYOTOKA NJE YA DHAMANA YA UONGOZI WAKAJIONDOA SASA ANATAKA KUITUMBUKIZA NCHI SHIMONI. TULISEMA JK SI KIONGOZI; CCM HAWAWASIKII RAIA WNANG'ANG'ANIA TU; KWELI NI BALAA TZ KUWA NA RAIS HUYU; EEH MOLA TUREHEMU

    ReplyDelete
  2. KILA KITU NCHI HII NI KUCHAKACHULIWA; KILA KITU. WA TZ HATUNA CHA KUTEGEMEA KWA HII SERIKALI, SI LOLOTE SI CHOCHOTE. PSE PSE MSIMTAJE TENA 'JK' MNATUTIA KICHEFU CHEFU. NI BORA KIVULI KULIKO HILI DUDU LISILO NA UFAHAMU WALA HISIA KWA SBB YA UGANGA NA UCHAWI. MUNGU PEKEE ATATUONDOLEWA HILI GIZA.

    ReplyDelete
  3. Watoa maoni hapo juu, wote mko sawa. Tatizo la WaTZ ni kufikiri kwa tumbo badala ya akili iliyo kichwani. Wakapewa kofia, khanga, wali kwa maharage, na rusha roho iliyokuwa inapigwa wakati wa kuomba kura, wakaridhika navyo. Wakapewa ahadi lukuki zisizotekelezeka, wakahadaika. Njia ya kujinasua ipo, tujifunze kwa Tunisia. Hata polisi wa huko wamewaunga wananchi mkono, na hamkani mambo si shwari tena. TZ tunasubiri nini wakati wahanga wa Arusha walishatuonesha njia!

    ReplyDelete
  4. Jk is the best president we ever had jamani

    ReplyDelete
  5. Wadau ujue haya mambo ya kutokua na uwezo wamambo ila ukawa na ngekewa tu eti ya kupendwa ndio yamemfikisha huyu bwana mdogo Jk hapo alipo,akili yake inatosha kua baba wa familia na kuendesha vijimiradi vidogo sio nchi,what happens ni kua mambo yamezidi uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi

    ReplyDelete
  6. Huyo aliyesema Ni Rais gani akatumia mke na mtoto wake kuomba kura? anachekesha sana hivi ni yupi bora? SLAA ALITUMIA MALAYA WAKE KUOMBA KURA TENA MKE WA MTU NA BILA AIBU NA NDIVYO MTOTO WAKO WEWE ULIYEANDIKA MAONI YAKO ATAKAVYOKUJA KUFANYA, NA KIKWETE ALITUMIA FAMILA YAKE KUOMBA KURA NANI ANA AFADHALI?

    ReplyDelete
  7. Kikwete Rais halali wa nchi hii mtake msitake subirini 2015,ni wehu ndio bado wana mjadala wa urais ambao umeisha pita,huyo padri wenu aende kanisani akatubu kisha arejee ulingoni 2015 akiwa msafi na iwapo hao wachaga watampa nafasi

    ReplyDelete
  8. Nashangaa! Hivi hawa mafisadi wana uwezo gani wa kumudu kuitia serikali, watendaji na watu wote mifukoni mwao? Hivi ni mafisadi wenye uwezo ama ni viongozi wetu wazembe? Mafisadi wana pesa na akili gani ya kuwapofua macho na masikio viongozi wa serikali ya CCM hata wasione na kusikia ubaya wa kuilipa Dowans sh. 94 bil? Sh. 94 bil ni zaidi ya bajeti ya wizara, hivi pesa hizi zitalipwaje bila ya kupitishwa na wabunge? hata kama kanuni zinaruhusu mtu kuidhinisha malipo makubwa hivi basi hizi ndizo baadhi ya kanuni ambazo wananchi wanatakiwa kuzipinga kwa nguvu zao zote. Wananchi tupinge kwa nguvu zetu zote malipo haya bila ya kujali ICC.

    ReplyDelete
  9. Taifa letu limefikishwa mahali ambapo mafisadi na ufisadi unafanya Rais, mawaziri, makatibu, wakurugenzi, wanasheria, wakuu wa majeshi na watu wote hatuwezi kufurukuta. Watu wote tunaingizwa mkenge na watu wachache, bahati nzuri watu wote wanaotuchezea shere tunawajua kwa majina, mali zao na wanakoishi na kulala na mbinu wanazozitumia, na washirika wao. Tunawafahamu wauza madawa ya kulevya, ma EPA, wachakachua mafuta, wauza ndovu, magogo, madini, wanyama, Ma dowans na ma Richmond, n.k Tujipange kama walivyojipanga wenzetu Tunisia kulikomboa taifa, hakuna cha ICC, rais, waziri wala polisi kwenye hili!

    ReplyDelete
  10. Kuna haoa watoa maoni hapo juu, aliyesma Jk is the best president we ever had, na huyu aliyesema Slaa katumia malaya kuomba kura, inaonyesha dhahiri kuwa upeo wao wa kufikria hatuwezi kuulinganisha hata na mtoto wa Darasa la kwanza ambaye atleast anajua kusoma na kuandika au wale mateja wanaokaa kijeweni na kupeana story za kuzamia meli,ndugu zangu hao wawili huhitaji kuwa hata na elimu ya Darasani kuweza kutambua upuuzi na utumbo unaofanywa na selikari ya ccm! juzi hapa JK kampa ukuu wa wilaya binti aliyegraduate fresh from school, hvi anaexperence gani na mambo ya uongozi au ndo kuwapa nyazifa malaya wao! NI HAYO TU NIMEMALIZA, Ndg zangu fungukeni!

    ReplyDelete
  11. Sema kama uongo au kweli huyo bi Mshumbusi si mke wa mtu aliyemuasi mumewe kwa pesa alizonazo Slaa,kama si malaya ni nani? hakuwa anasimama majukwaani kumtukana Kikwete? jibu hoja hiyo maana aliyeandika alikuwa anamjibu huyo aliyeandika Kikwete kamtumia mkewe na mwanae kuomba kura,sasa kaulizwa yupi bora? aliyetumia malaya au aliyetumia familia yake? hayo mengine ya nini?

    ReplyDelete
  12. wajinga hao wanaomtukana jk watake wasitake ndio raisi wetu wachaga na waroma wachague raisi wao sisi wengine hatuwataki hata sikumoja na ukabila kabila wenu uliowajaa na chuki zenu angalia li mzee slaa lipolipo tu halina mbele wala nyuma muangalie nae mboe makengeza yale tutayapeleka wapi ?na hao wote wengine waliobaki ni maluki wetu hamna chenu 2015 mlijue hilo mapema

    ReplyDelete
  13. Hahahahahahahha, Msinichekeshe bure saa hizi!
    Ushabiki wa kisiasa huu unaniacha hoi! Yaani wenyewe Kina Slaa na Jk wapo kimya, wanakula kuku ninyi mnachambana humu. Wao wakikutana wanapeana mikono na chai wanakunywa pamoja ninyi mkikutana uso kwa uso tu mnapeana kosovo mpaka kutoana ngeu!

    Wenzenu kimya! Mtawaona kwenye Mabenzi tu na Mikutanoni! Haya Watz! 2015 si mbali nani atachukuwa Ikulu?!

    Carwin

    ReplyDelete
  14. KATI YA WATU WOTE WALIOTOA MAONI NI MMOJA TU ANA HOJA NZITO, KUWA WATANZANIA WANA TATIZO LA KUFIKIRI KWA TUMBO BADALA YA KUFIRI KWA AKILI ILIYO KICHWANI. NA NDIYO MAANA WWOTE WANAOSHABIKIA CCM NI WALE WALIOSHIBA TISHET, KANGA, VITENGE NA POSHO ZA VIKAO VYA USIKU HAWANA KINGINE, ILA NAWAHAKIKISHIE 2015 HAWAFIKI. PIA NAWAKUMBUSHA WATANZANIA KWA MARA NYINGINE KUWA WALE WALIOJIITA UVCCM WAKAJIFANYA WANAPAMBANA NA WAZEE WA CCM NI DANGANYA TOTO TU, NI WALE AMBAO WAMEPITWA NA MGAO WA FEDHA ZA DOWANS NDIO MAANA CHILIGATI ALISEMA ATAWAPA KITU KIDO WATAKAA KIMYA TU.

    ReplyDelete
  15. Watu wote wanaomsifikia JK, wanamsifia utadhani timu ya mpira, Kila nikisoma coments zao ni za matusi tu, hawana hoja, nikusema tu JK ndo raisi wetu mpaka 2015. Jamani hapa si Yanga na Simba. is about Nchi yetu, wenzenu wapoandika udhaifu wa Kikwete, nanyi andikeni ubora wa kikwete. Hivi Nchi alivyo jaa ufisadi, Umeme hakuna, malalamiko kibao, watu wanajitahidi kuelezea machungu yao, wewe Msomi unayeweza hata kutua internet unakaa kwenye computer na kuandika upuuzi, hivi uajifikiriaje? uwezo wako wa kufikiri tunapima kile unacho andika, najaribu kufikiri unatazo la akili kwa lugha ya matusi unayotumia, lakini nani angekuruhusu utumia computer hali akili yako si nzuri? lazima unaonekana machoni unaakili nzuri ila moyoni wajua wewe.
    Nawashukuru wote mnao ona nchi inakokwenda, lamsingi ni kuchukua hatua, si lazima Slaa awe Raisi watanzania, ila siyo JK. CCM watafute mtu mwenye uelewa, siyo huyo. katika Makosa makubwa ambaya CCM waliwahi fanya ni kumsimamisha JK kugombea Urais, hali wakijua kabisa kwa level ya elemu ya Tanzania, bado wanachagua Chama, hata angetolewa mtu yeyote toka MILEMBE akasimamishwa na ccm, watu wangechagua. Hiyo Dhambi wanaccm mnayo, Mateso haya yote watanzania tunayoyapata, ni juu yenu. Helo deni likipwa DAMU Nyingi itamwagika. Hatuwezi kutoa Kodi ananufaika Rostamu na wanae.

    ReplyDelete
  16. Hapa ni mpaka kieleweke tupo njiani kama TUNISIA hakuna kulala. Dr Slaa ni ngoma nzito kuna wa kufananishwa nae hata wabunge wa Chadema hakuna. CHADEMA kilia kushoto inamaana wapo makini. CCM mmesha pagawa hamuna sera zaidi ya kutukana na inaonyesha jinsi mlivyofilisika kimawazo na kiutendaji. Sasa ndio tunagundua ya kuwa kumbe CCM inaendesha serikali yake kwa kupendelea, kiukabila na kidini na kama sio hivyo kwa nini mnawaogopa wachaga. Kwa hiyo inamaana hakuna wachaga ambao wapo CCM? Basi watengwe kwa sababu serikali haiwathamini. CCM msijifiche kwa mwavuli wa ukabila wala udini. Hapa hakuna mpinzani aliyetoa maoni ya udini wala ukabila. Tunachoomba mungu tu siku tusikie CCM chali chali, pwaaaaaaa. Tunafikiri sasa hivi ipo wodini haijajulikana inaumwa nini madoctor wote wameshindwa kuitibu japokuwa kila mmoja anajifanya ni bingwa. Labda tuchukue mziki wa FEROOZ ule wa kamandaaa... atatupa jibu. Bado kidogo itolewa wodini ipelekwe kwa waganga ikapigwe viwembe.

    ReplyDelete
  17. Hadithi ya fisi kuvizia mkono wa binaadamu uanguke autafune. Hamna Tunisia wala babaake Tunisia hapa. KWANI UONGO RAIS KESHAAPISHWA KINGINE KIPI ? 2015

    ReplyDelete
  18. NINYI WOTE MLIOTOA MAONI HAPO JUU KUMBUKENI KUWA SEHEMU HII NI KWA USHAURI NA MAONI YA KITAALAMU. NINYI MNAONGELEA PERSONAL ISSUES KWA WATU. JARIBUNI KWENDA SHULE KIDOGO HATA KWA MASOMO YA JIONI. BUSARA ZENU WOTE NI "ZERO" KWA MAANA HAMJAONGEA JAMBO LA MAANA. SAFU HII SI KUDHALILISHA MAISHA YA MTANZANIA YEYOTE KUANZIA MKULIMA MPAKA KWA RAIS. NANI KIONGOZI DUNIANI HANA MAPUNGUFU?. NENDENI SHULE KWANZA NDIO MUWEZE KUTOA MAONI

    ReplyDelete
  19. WEWE ULIYETOA HOJA YA WALIOTOA MAONI WOTE NI ZERO MI NAHISI WEWE NDO ZERO, KWANI UMEANZA VIZURI HARAFU UKAISHIA KUMTAJA HUYO MUME WENU RAIS KWA KUMTETEA KUWA KILA BINADAMU ANA MAPUNGUFU. NGOJA WATUKANANE SANA NA MIMI NIMEKUTUSI KWANI NILITEGEMEA UNGETOA MAONI KUWA WATANZANIA TUDILI NA SERIKALI ILI ISILIPE HAYO MABILIONI KWA DOWANS, NA SI KWA MTU MMOJA MMOJA, HAPO NINGEKUSAPOTI, LAKINI ULIPOANZA KUSEMEA CHEO CHA MTU MAANA YAKE NA WEWE UMEUNGANA NA WALIOKUTANGULIA KUSEMEA INSHU ZA MTU BADALA YA TAIFA. SISI WENYE MAONI TUNASEMA, HAINA HAJA SERIKALI KUILIPA DOWANS WAKATI TAIFA TUNAKABILIWA NA HALI NGUMU KIMAISHA MIJINI NA VIJIJINI HATA KWA HILI LA UMEME LILILOTUFIKISHA KWENYE KUTUKANANA. BADILIKENI TULIKOMBOE TAIFA NA SIO KUSHADADIA FAIDA ZA WATU WACHACHE WAKATI HATA MNAOWATETEA NA HAKIKA MNA HALI MBAYA KIMAISHA JAPO SIO SANA KWA SABABU WENGINE NI NDANI YA WALE WALE MAFISADI WADOGO MNAZIDIANA VIWANGO. WOTE TOENI MAONI KWA JINSI MTAKAVYOWEZA HATA MKITUKANANA MWISHO WENYE MAPENZI YA DHATI NA NCHI HII WATAONEKANA NA MNAOJIKOMBA SIKU MOJA MTAKUJA KUGUNDUA UKWELI NA ROHO ZENU ZITAWASUTA. NAITWA DAVID NIPO MWANZA KAMA MNAJIAMINI TUANZE KUTAJA NA MAJINA YETU NA ANUANI KAMILI KAMA HAMJAUANA MCHANA KWEUPE KWA SABABU YA UJINGA WA KUTOA MAONI FEKI NA MATUSI BADALA YA MAONI YA BUSARA IT'S ENOUGH BWANA.

    ReplyDelete
  20. Hongereni wapambanaji wa Vita ya Rushwa Tz

    Hakika tutaendelea kupambana hadi tumepeleka Ikulu viongozi ambao
    KISIASA, KIUTAWALA, KIFIKRA na KI-UZALENDO ni watu safi kama vile Dr Wilbroad Slaa.
    Tanzania hatutafuti kuongozwa na MALAIKA. Wala hatuangalii mtu ametoka dini ipi. Tunayemtaka ni mwanasiasa ambaye :-
    1/ Anayo mapenzi ya kweli na nchi yake.
    2/ Anayechukia rushwa, wizi, ufisani, nk.
    3/ Na anajua nchi yetu inapaswa kuelekea wapi, kwa njia ipi na kwa manufaa ya Watanzania wote.

    Je, huko CCM ni wangapi wenye sifa kama hizi ????

    Watanzania wote wanajua kwamba Dr Slaa anazo sifa zote hizi.

    Ninachomwomba Dr Slaa ni hiki: usikatishwe tamaa na watu wenye mawazo finyu na wasioitakia mema Tanzania. Wewe pamoja na chama chako, Tafathali endelezeni mapambano, tupo nyuma yenu kwa hali na mali hadi kieleweke kitu!!!!

    by
    Abdalha Ali Juma.

    ReplyDelete
  21. Itakuja siku CCM ( Chukua Chako Mapema )watashurutishwa kuitoka Ikulu. Mifano hai wanaiona.Ivory Coast, Tunisia.Watawala wetu wanadhani kugawiana mali ya Taifa hakuna mwisho.Kuna mwisho.Wananchi wakichoka na kuonewa wataamua kuzichukua nyumba ( mali ya Taifa ) zote walizogawiana( majumba Osterbay ) Ole wao mtakaokutwa hai!!

    ReplyDelete
  22. na hao wanaokuja ni malaika? tena damu mbaya sana kuliko hawa na cha moto mtakiona,hii ya ccm ni trela tu.mmemuona Mramba alivyokuwa waziri namna gani alijaza wachaga katika kila wizara aliyoingia,ole wenu.

    ReplyDelete
  23. Tatizo kubwa ni Ngeleja kumheshimu fisadi kuliko raisi alyemuweka madarakani. lakini pia rais kuogopa fisadi kama mama mkwe (sorry baba mkwe!!).Ngeleja anatumikia bwana wake bila kujali kama anawasaliti watanzania. Ukimwangalia tu hata uso wake unaonyesha jinis alivyojaa uongo na utumwa ndani yake. Viongozi kama hawa ni hatari sana kwa nchi yetu

    ReplyDelete
  24. Wananchi tumechoka kumwona Mengi kwenye vyombo vyake vya Habari. Yeye siyo Rais wa pili wa Tanzania. Kila siku Mengi kafanya hili , Mengi katoa zawadi hii( pipi ) n.k kila siku ya Mungu Mengi tu.Kama anataka kutoa zawadi kwa Watanzania basi alipe deni hili la Dowans. Huu nao ni Ufisadi wa kimawazo!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  25. anonymous wa juu yangu kichwa chake kina moto

    ReplyDelete