24 January 2011

Mtikila apongeza UV-CCM kuhusu Dowans

Na Grace Michael

MWENYEKITI wa Democratic Party, Mchungaji Christopher Mtikila amesema kuwa kitendo cha ujasiri kilichofanywa na Umoja wa Vijana wa
Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM) cha kupinga kulipwa kwa mabilioni ya fedha kwa Dowans kiwe daraja kwa Watanzania wote katika kuhakikisha fedha hizo hazilipwi.

Mbali na hilo, pia amewataka Watanzania kutoogopa kupinga suala hilo kwa kuwa hakuna sheria yoyote inayoweza kuwabana wakati wa kudai maslahi ya taifa na haki za Watanzania.

Mchungaji Mtikila aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hukumu ya fidia ya sh bilioni 94 za Watanzania kwa Dowans, kitendo ambacho alisema ni 'uporaji wa nchi kwa bastola ya Dowans'.

UVCCM wanapaswa kupongezwa kwa kile walichokifanya kwa kuwa wanawakilisha mawazo ya Watanzania wazalendo, hivyo tukitumie kitendo hicho kama daraja muhimu la kutuunganisha sisi wana wa Tanganyika katika vita ya ukombozi ili kuangamiza magenge ya uporaji wan chi yetu,รข€ alisema Mchungaji Mtikila.

Alhamisi iliyopita, UV-CCM ilitoa msimamo wake kuwa Dowans wasilipwe fedha na serikali, bali waisaidie kuipata kampuni ya Richmond iliyohamishia mkataba wake ili iwalipe fedha hizo.

Vijana hao walipendekeza suala la Dowans lirejeshwe bungeni kwa majadiliano zaidi, ili kuchukua hatua dhidi ya yeyote aliyehusika na madudu hayo.

Alisema kuwa wananchi wanapoamua kulinda maslahi ya taifa lao huwa hawafungwi na sheria kwa kuwa sheria ni chombo kinachoweza kutumiwa kwa ajili ya kudhulumu haki au kutoa haki, hivyo katika mapambano ya haki sheria hukaa pembeni.

Alisema kuwa ibara ya 27(2) inataka wazawa wa nchi kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa, hivyo akawataka wananchi kujiuliza Dowans inaiuzia bidhaa gani taifa kwa hayo mabilioni ya fedha.

Uzalendo tunaolazimishwa na katiba ni kuipuuza mahakama ya kimataifa na kuwashughulikia waliohusika na uporaji kuanzia wa IPTL, SONGAS, AGGREKO, DCP, EPA, Kagoda Agriculture Ltd, hujuma za mitandao ya simu za mikononi, alisema.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa umefika wakati kwa Watanzania 'kuhamia barabarani kama familia moja' kwa ajili ya kuondoa utawala uliopo kwa kuwa unadidimiza haki za wananchi.

Alisema kuwa Dowans italeta ukombozi katika nchi hii kwa kuwa hata Rais Jakaya Kikwete anahusika kwani alipotuhumiwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa hakuweza kukanusha tuhuma hizo.

6 comments:

  1. MIMI NAMUUNGA MKONO MTIKILA ILA AWE MACHO NA HAWA WANAOJIITA UVCCM. NAJUA HAWATACHUKUA HATUA YOYOTE ILE KWA KUWA NI MIONGONI MWA WALE AMBAO WAMENYIMWA MGAO WA FEDHA ZA DOWANS NA NDIO MAANA CHILIGATI ALISEMA ATAWAPA KITU KIDOGO WANYAMAZE

    ReplyDelete
  2. KIKWETE ACHE KUZEEKA VIBAYA KUCHAGULIWA NA SISI SIO KWAMBA UKO KAMILI KULIKO SISI,KAMA UZALENDO UMEMSHINDA ATUACHIE NCHI WENYE UCHUNGU NA HALI YA UMASKINI KWANZA PESA ZA MISAADA ANAZIFANYIA MIZAHA.HAKIKA HANA MALENGO NA TANZANIA YA KESHO

    ReplyDelete
  3. ukiona rais anakuwa mjinga ujue wananchi watakuwa na akili,viongozi wajinga tena waheshiwa nasema hivi kwa kuwa najua hawa kuzaliwa na uheshiwa bali tumewapa tu iki kivumishi,baba mjinga hapendwi na watoto,CCM Tanzania sio yenye ni ya Watanzania.Serikali sio mgodi cha kujikwamua na umaskini.Hakika mnatuuzi na huu upuuzi wenu wa kugawana kidogo chetu kwa kisingizio cha Dowans,oneni huduma za afya,kilimo,kupanda kwa bei,elimu yenu ni bure hata kama kuna maprofesa ndani ya CCM bora wakasome upya.

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli tamko la UVCCM si kosa likajadiliwa maana ina point kwani ,kama richmond ilichunguzwa na wasomi wanaoozwa na mwakyembe na timu yake na kubaini richmond ni kampuni hewa iweje sasa tuwalipe Dowans pesa ya richmond? lakini mimi nataka viongozi walihusika wafanyiwe kazi, kama Rais Jk ajihuzulu na aweze kujibu mashitaka ya kukubali kusaini mikataba mibovu na kuliingiza taifa hasara kubwa huku watanzania wakilia na kusaga meno kwa kila kitu kupanda baada ya yeye kuapishwa(je unaijua nini siri ya kupanda kwa vitu?) ni swali gumu ila ni rahisi pia ni kwamba wakati wa kampeni ccm na mwenyekiti wao jk walitumia hela nyingi kutoka hazina na hata kuanza zoezi la kupitisha bakuli kila kiwandani, ofisi mabli mbali, sheli, maduka makubwa, wakiwahidi kuwa wakipata madaraka wapandishe bei. ndio maana unakuta vitu vimepanda kuliko bajeti ilivyopangwa. Rais ana vitu vingi vya kujibu ikiwa na pamoja ya mauaji ya arusha.

    ReplyDelete
  5. mtikila upeo wako ni mkubwa songa mbele hata wakikutungia vikesi vyao TANZANIA YA KESHO ITAKUTAMBUA KAMA SHUJAA

    ReplyDelete
  6. UV-CCM wana agenda ya siri kuzidi kunyonya jasho la WaTz kama wanavofanya wazee wao. Hatukushangaa UV-CCM kuungwa mkono na akina Mtikila, Sitta na Msuya. Hawa wote wana lengo moja tu: Kufilisi mali za Tanzania na kuendelea kuwakandamiza wananchi kwa siasa potofu na mawazo mgando.

    Hili ni suala la Mikataba. Kwa hio sheria ya kibiashara itawale. Kuliingizia siasa hakuna masilaha na Tz maana riba itaanza kutuandama, bishara zetu za nje kuathirika, na uhuisiano kimataifa utaingia doa.

    Wacheni ushabiki wa kipuuzi.

    ReplyDelete