Na Rabia Bakari
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba ambaye alisema kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Jenerali Said Mwema ametumika kisiasa katika kuzuia maandamano hayo kwa kuwa sababu alizotoa ni
za kisanii na hazina maana yoyote.
Profesa Lipumba alilaani jeshi la polisi kwa kuwapiga na kuwaumiza viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao na pia kukamatwa na kuhojiwa, kisha kushtakiwa kwa baadhi ya wabunge na mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe.
Profesa Lipumba alitoa tamko hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho, Buguruni, Dar es Salaam, alipowaita kulaani vitendo vya polisi vilivyofanywa katika maandamano ya CHADEMA Arusha juzi.
Alisema kuwa ushahidi wa mazingira, unaonesha wazi kuwa IGP Mwema alitumika kisiasa, jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa demokrasia nchini na kinatia doa kubwa.
"Nilikuwa namuheshimu sana Bw. Mwema, ni kiongozi aliyekuwa anaheshimika na vyama vya siasa, lakini vitendo hivi vya kushambulia maandamano ya amani ya kidemokrasia, vinazidi kuharibu sifa na uaminifu juu ya Mwema. Ni muhimu sana kwa taifa letu kwa IGP kulinda heshima yake na asikubali kutumika kisiasa kukandamiza demokrasia ndani ya nchi," alisema Profesa Lipumba.
Aliongeza kuwa amri ya kusitisha maandamano iliyotolewa na IGP saa chache kabla hayajafanyika ilitokana na shinikizo la kisiasa na hoja iliyotolewa kuwa taarifa za kiintelijensia zinaonesha uvunjifu wa amani ili kuzuia maandamano ni usanii mtupu.
"Kama kweli polisi wana taarifa za kiintelijensia, kuwa kuna watu watavunja amani, basi wazitumie taarifa hizo kuwadhibiti watu hao, lakini kuyasitisha maandamano ni kuwanyima wananchi uhuru wa kisheria wa kufanya maandamano.
"Hivi sasa jeshi la polisi limekuwa mstari wa mbele kuzuia kila aina ya madai yanayotolewa na vyama ili mwisho wa siku lifanye kazi yake kuu ya kulinda CCM na utawala wao wa kijeuri na kisanii," alidai Profesa Lipumba.
Aliongeza kuwa CUF inaamini kuwa polisi na serikali ya CCM wanataka kutumia kitisho cha ugaidi kilichozikumba Kenya na Uganda kama sababu ya kupinga mikusanyiko mikubwa ya kisiasa kwa lengo la kuitetea serikali.
"Lazima tujiulize hivi magaidi wakitaka kulipua Tanzania mbona kuna sehemu nyingi sana mbazo wanaweza kufanya hivyo bila kusubiri maandamano ya CHADEMA au CUF au vyama vingine?"Hivi tujiulize kama kweli pana tishio la ugaidi, iweje mechi za mpira ziendelee bila kuzuiwa na polisi? Mikusanyiko yote inafanyika isipokuwa maandamano ya vyama vya siasa tu? Hawa magaidi walio tishio kwa jeshi la polisi wanaotaka kulipua maandamano peke yake wametoka wapi? Kwanini nchi hii iendeshwe kisanii na kiujanja ujanja namna hii? Kwa nini serikali inaogopa maandamano?" alihoji Profesa Lipumba.
Alifananisha ukatili huo uliofanywa na jeshi la polisi na ule waliofanyiwa wafuasi wa CUF Desemba 28, mwaka jana wakati wakifanya maandamano ya amani yaliyokuwa yaongozwe na Kaimu Naibu Katibu Mkuu, Bw. Julius Mtatiro ya kupeleka rasimu ya katiba kwa Wizara ya Katiba na Sheria.
Alisema kuwa maandamano hayo yalipigwa marufuku ghafla na kisha mamia ya polisi wakasheheni na silaha za kila aina wakaanza kuwapiga na kuwakamata wafuasi wa CUF na wananchi wengine walioshiriki katika maandamano hayo.
"CUF kinaamini kuwa ustawi wa demokrasia, utawala bora, usawa, maendeleo ya nchi yetu na amani ya nchi havitaletwa kwa mtutu wa bunduki wala mabomu wala kila aina ya nguvu, hata kama CCM wataendelea na mbinu zao za kuwadhibiti wapinzani, hatatokaa kimya na wala hatutoacha kutumia fursa za kikatiba kutoa maoni yetu kwa njia ya amani," alisisitiza.
Profesa Lipumba alisema wanaamini walichokuwa wakipigania CHADEMA jijini Arusha ni kitu cha msingi sana, walikuwa wakipinga kitendo cha kukiuka demokrasia katika uchaguzi wa meya, na hawakuwa na budi kutumia njia za kidemokrasia kuonesha kutokukubali na kutotambua utaratibu huo wa kinyemela ulioendeshwa na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kwa manufaa ya CCM.
Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi na serikali ndio wanaostahili kulaumiwa kwa uvunjifu wa amani uliotokea Arusha, na kudai kuwa CUF kinaamini CHADEMA kama chama cha siasa kilichosajiliwa kihalali ndani ya nchi kilikuwa na haki ya kikatiba na kisheria na kimazingira kufanya maandamano ya amani.
"CUF inalaani ukatili huu waliofanyiwa wakazi wa Arusha katika maandamano hayo na kuwa hauvumiliki na unahatarisha amani na utulivu wa kweli wa nchi yetu."CUF inawapa pole wote waliopigwa na kuumizwa na mabomu, risasi, maji ya kuwasha nakadhalika katika tukio hilo la kihistoria la kudai haki ya wanyonge, tuko pamoja nao katika kuendelea kupigania haki," alisema Profesa Lipumba.
Pia mwenyekiti huyo alimtaka Rais Jakaya Kikwete kutumia busara za hali ya juu katika kuendesha nchi katika kipindi hiki ambacho anamalizia miaka yake mitano ya mwisho.
MNAOTETEA UDHALIMU WA CCM JIBUNI HILI SWALI TANGU LINI ADHABU YA MTU ANAYEANDAMANA KUDAI HAKI IKAWA KURUSHIWA RISASI/KIFO. NI NANI ANAYEVUNJA SHERIA ZA NCHI HAPA ??.POLISI/WAUAJI AU MUANDAMANAJI??. SHERIA ZA UKATILI DHIDI YA RAIA ZINASEMAJE?? NI KOSA KUTUMIA UNNECESSARY EXCESSIVE FORCES DHIDI YA RAIA.POLISI ANAMVAMIA MKE WA SLAA ALIYENYOOSHA MIKONO JUU KUJISALIMISHA NA KUMPIGA VIRUGU KAMA MWIZI KISA KAANDAMANA. KIKWETE HATUTAKUBALI KUONA UNAIGEUZA NCHI HII YA WATU WASTAARABU ZIMBABWE ILI UTUTAWALE KWA MABAVU.
ReplyDeleteInasikitisha sana, na tena inauma hadi kwenye pembe za moyo. Kumbe waliruhusiwa mkutano,sasa walitakiwa wapitie wapi hadi wafike sehemu ya mkutano wao? kumbe kosa ni kukanyaga barabara ya nchi yao ili waelekee kiwanjani wakahudhurie mkutano wao, je wangetumia ndege kufika uwanjani? je wangetumia ungo kufika uwanjani? kumbe kuna jopo kubwala usalama uliomwagwa kuwadhibiti wasiandamane,kwanini hilo jopo lisipelekwe kuwalinda wakati wanaandamana kuelekea uwanjani? je kuntofauti gani kati ya Jambazi na raia mwema anayedaihaki kwa amani? kumbe wote ni sawa! wanastahili kuuwawa,kupigwa virungu na kushambuliwa kama jambazi. Damu iliyomwagika ipo mikononi kwa kila aliyehusika kwa namna moja au nyingie, na malipo ni hapa hapa duiani.
ReplyDeleteMIMI NI KADA WA CHAMA CHA MAPINDUZI NILIWAPA KURA ZAKO CCM NIKIAMINI KIKWETE NA WENZIE WATABADILIKA LAKINI KWA HILI.........
ReplyDeleteCCM INAJICHIMBIA KABURI YENYEWE NA LAZIMA IBADILIKE USANII HAUTOWASAIDIA NA KIKWETE AJUE HATA KAMA YEYE ANAWAKOMOA KWASABABU ANAMALIZA MUDA WAKE AKUMBUKE CCM BADO ITAPENDA KUSHIKA HATAMU NA JANJA YA NYANI HAIZAIDII.
POLENI WATANZANIA WENZANGU
The responsibility of Police force is to defend the society and their properties not to broke the demonstration,where did the article on the constituion have been written that Police have an authorities to allow and broke political meeting,I hope they need to go to school in order to know how to translates different articles.(POLICE+CCM)=DICTATORIAL REGIME.For all Arusha's dwellers and Tanzanian at large they need to know that the time for liberation is coming soon.
ReplyDeleteIGP MWEMA ANAPASWA KUJIUZULU PAMOJA NA WAZIRI NAHODHA HAWAWEZI KUSABABISHA VIFO,VILEMA KWA WANANCHI WA TANZANIA KWA KUWAPIGA RISASI ,VIRUNGU NA MABOMU YALIYONUNULIWA KWA KODI YA WANANCHI HAO,NCHI MNAIPELEKA KUBAYA.HUO USHEMEJI WA MWEMA NA KIKWETE NDIYO UNATUPONZA,POLENI WOTE WAHANGA ILA KUMBUKENI DAMU ILIYOMWAGIKA ITALIPWA TU HAPAHAPA TANZANIA,SERIKALI YA CCM INAUWA WANANCHI WAKE.
ReplyDeleteKuna haja ya Polisi kusoma na kuielewa hiyo Katiba mbovu kwani inaeleza wapi kuwa wajibu wa Polisi ni kutoa vibali vya mikutano na kuzuia maandamano? kama si kutumika kuilinda CCM na usanii wao,hebu jiulize kama hizo taarifa za kiintelijensia wangezitumia kuchunguza wezi na mafisadi wanaowaibia watanzania si ingekuwa bora au wanataka maandamano ya kinafiki ya kumpongeza Rais kwa usanii anoufanya wa kuwatumikia mafisadi? Mwema,Nahodha na Thobias Andengenye must step down no need to compromise.
ReplyDeleteUkiangalia kwa makini Mwema na Nahodha walivyokuwa wanaongea na waandishi wa habari bila shaka utabaini unafiki na usanii ndo alichonacho hata elimu zao nina mashaka nazo.Nahodha anaongea kuwa"katika nadharia ya mgogoro kuwa huwezi kusuluhisha mgogoro hadi wahusika wakubali kuwa kuna mgogoro" hapa ninaona hata hiyo elimu yake ya OUT inamzingua tu watoke watu wanAuawa,uharibifu unatokea Mtu linasimama eti "kama kuna ukweli polisi walisababisha vurugu nitjiuzulu"(SAID MWEMA).Achia ngazi nenda Interpol labda ndo wanakuhitaji sisi Tz tunakuona wewe ni shemeji wa mheshimiwa hivyo uko tayari kufa kwa ajili yake ngoja katiba mpya ije tutaanza na wewe.
ReplyDeleteWewe unayetaka kujibiwa tunakuambia haki yako ya kuandamana pia iangalie haki ya watu wengine kufanya shughuki zao kama kawaida,hatutaki maandamano ya CUF,CCM,CHADEMA wala vyama vingine kwani vinatuletea kero katika shughuli zetu za kawaida,andamaneni saa sita za usiku kwani mchana inakuwa kero kwetu. wala msijivike ndio watoaji maamuzi ya wananchi kwani mko wachache kulingana na population ya nchi hii.hivi ilihusu nini kuharibu mali za watu na wengine wakataka kuvamia nyumba za ibada? hii unaiona haki wewe? HAKI YAKO ISIKERE HAKI ZA WATU WENGINE
ReplyDeleteWell done Police force. askari utakae subiri uje uchinjwe na waandamanaji kama ilivyotokea Pemba wewe utakuwa si askari sahihi,wewe utakapo chinjwa watafunga midomo yao kwa sababu ni haki askari kuchinjwa,kama ningekuwa mimi hao watatu ni kidogo sana,wa kulaumiwa ni Slaa aliyewaambia waende ktuo cha polisi kuwatoa viongozi wao,kwa nini asiende yeye peke yake kwa dhamana inahitaji mamia ya watu.Polisi wa Tanzania fanyeni kazi yenu hao wanasiasa wanagombea hazina ya nchi kwa manufaa yao,mtu akija polisi kwa taratibu zake mpokeeni vizuri akija kwa shari mpokeeni kwa shari.NASEMA TENA WELDONE USINGOJE UKATWE KICHWA ANZA WEWE,NA HAO WANAOTAJA OCAMPO WAMESOMA HISTORIA YA KENYA AU WANAJISEMEA TU,OCAMPO INASHUGHULIKIA WALIOFADHILI NA KUCHOCHEA WANANCHI KUFANYA UNYAMA ULIOFANYIKA HUKO,NA WAFUASI WA CHADEMA WAMECHOCHEWA NA VIONGOZI WAO WAENDE POLISI KUWATOA VIONGOZI WAO NA AKATAMKA WAZI WENYEWE WATAJUA LA KUFANYA YEYE ASILAUMIWE,KWA MAANA HIYO WAKIUA,WAKICHOMA MALI ZA WATU,WAKIUMIZA WATU KWAKE NI SAWA,HIVYO JUENI KWA OCAMPO SIO MAHAKAMA ZA TANZANIA KAMA INAVYOMUANGALIA ALIVYOBEBA MKE WA MTU NA LICHA YA KUFUNGULIWA MASHTAKA BADO ANATESA NAE,OCAMPO HAMNA HILO HAKI INATIZAMWA PANDE ZOTE MCHOCHEZI NA MUUAJI.
ReplyDeletenimewaona live wao makamanda huyo nimnyakyusa najua anaasili ya ukatili mojakwa moja na anatoa maelezo kitoto mpaka dunia inamshangaa hivi hivyo vyeo wanapata kwa kusoma au kama mtu amefanikiwa kuuwa watu wengi,huyo mkuu wa opresheni ndio anaongea pumba tu jamani kazi ya polisi si kupiga watu nikulinda watu,hivi sijui kama mwema nimsomi kama aliona tatizo analo liita lakigaidi angelishughulikia hilo,mbona watu hawa hawakuonesha fujo mfano hivi kulikuwa na haja yeyote yakutumia nguvu kumpiga huyo mwanamama kiasi hicho au ndiye alikuwa gaidi jamani Tanzania tumeaibika sana hivi kweli hawa wakubwa wajeshi mbona wote wapo kama wamelewa bangi au ndio staili ya maadili yenyewe sasa wanapo toka nje kujifunza wanajifunza nini kwa wenzao wastarabu sioni kama kuna haja ya kutumia nguvu kiasi hicho kwa taifa kama la Tanzania.
ReplyDeletewana ccm wamesha gawana kilicho chao kwa miaka mitano mimi nasema kwa maoni yangu hivi kweli serikali ya daktari huyu kikwete inahuruma kweli,jana dunia inashuhudia bila aibu wazili wake akitamka bila haya wala uchungu kulipa deni la 185 b kwa watu si jui makampuni ambayo hata haiingii akilini,hizo ni pesa za vikongwe wajane zaidi walala hoyi wa nchi ya Tanzania ccm na watoto wa mabosi wanao faidi hujuma hizo wanashangilia,mwema alitakia azuie hapo ndipo kwenye ugaidi sasa mambo haya yote kama asingekuwa slaa kutufumbua macho watanzania tungejua wapi jamani walau katika hilo tumshukuru,serikali inaamua kunyonya taifa lake bila huruma watanzania umeme juu nauli juu,ada ndio sijui,kikwete mwenyewe ndio huyo tafrija ikulu na ndugu zake na mafisadi wake,hivi kweli tz hakuna washauli wa zuri hivi zile barua za wazi anazo andika ulimwengu kikwete anasoma kweli'? MHESH PInda mtoto wa mkulima watu bado wanayakumbuka machozi yako bungeni mshauri bosi wako aweke watu wenye maadili ya kazi leo hii jeshi la polisi nikama utoto fulani wanaufanya,wanaonyesha wazi ni washirika wa ccm,kama kweli mwema anaweza kukusanya askari kibao kuja arusha kwa nini asiwahimize walinde amani kwa watu hao na anapo sema askari hawatoshi wale wajana walitoka wapi walio jaa arusha,waziri ndio huyo huwezi kuamini kama kweli nimsaada kwa walala hoyi hivi jamani askari arusha wameua hakuna mashitaka mbona hatuja ona mtukukamatwa nakufikisha mahakamani hizi usiuwe ni amri kwa raia tu wakimwua polisi,haiingii akilini majambazi ya naiba kwenye mabenki yanaua watu jibu askari hawatoshi ila wanatosha kudhibiti watu wakidai haki yao tumesha sahau aibu aliyo ileta mkapa na mahita nzanzibar hongera lipumba kwa kuwa mwazi wakati katibu wako anapo kula kuku kw mrija katika serikari dhalimu jna katili.
ReplyDeleteKazi kwenu m/ mungu hamfichi mnafiki malizaneni wenye kwa wenyewe kama mlivyokuja pemba mkatuua sasa zamu yenu hata badooooooooooooooooo
ReplyDeletehaya jamani,hayo ni malipo waliosaidia kuwaibia kura kwenye uchaguzi,sasa wameshapata hawana haja tena na Raia,wameanza kupiaga na kuuwa,kwa kisingizio cha kuzuia maandamano,hii serikali si wananchi bali ni ya wafuja nchi,ona hata wazee na mababu zetu walipigwa mabomu ya machozi walipokusanyika kwa kudai mafao yao africa mashariki,jee hamkuwaona?ndi hao FFU.
ReplyDeleteNaomba muachiani mungu atawahukumu hao,watapat maradhi na kifafa na kupofua macho,iko siku mikono yao haitoweza tena kunyanyua bunduki wala kupiga mabomu ya machozi,wangapi walikuwepo na wakauwa pemba kwenye maandamano ya januari 66/27 2001,wengi wao wamekufa vifo vya mateso,Basi muachieni Mungu atawaadhibu na serikali haitakuwa na uwezo wa kuwasaidia,wanajidanganya tu eti tumewadhibiti,Yaguju.
Mtanzania.
wanaolalamika juu ya sakata hili la arusha nafikiri hawakuepo katika ukio,mimi niwaeleze hivi,hapa hakuna kosa lolote kwa serikali jinsi mnavyotoa maneno yenu,au kwa polisi mimi nilikuwepo karibu kabisa kila tukio japo sikuandamana.Hapa kwa hili wa kulaumiwa ni slaa ,nilimsikiliza maneno yake aliyoyatoa ya kuruhusu wananchi wakapambane na polisi,nilimshangaa sana nilijiuliza ni slaa ninayemfahamu au mwingine? kweli watu waliondoka wakiwa wamebeba mawe na vifaa vingine sasa polisi hapa wangesubiri wauawe ?pia hamuoni kuwa slaa ndio aliyevunja amani ya arusha kwa kitendo hicho?tusilaumu polisi maana wao pia wangesimama tu wangeuawa,hivyo watanzania tusijifanye kuwa tatizo ni serikali mkemeeni huyo mpendwa wenu slaa anayewadanganya kuwa yeye ni mkombozi wa wanyonge.mnashinikizwa kuvunja amani na mnakubali yeye si mungu lazima uhoji kabla hujaamua kutii.hapa slaa ashitakiwe kwa hili na wala si polisi.sasa amesema ataitisha maandamano nchi nzima andamaneni mjue polisi hawatakubali wapoteze uhai kamwe watawamiminia slaha tu.acheni upumbavu wa kuendeshwa hivyo kama hamnazo.mnaanzisha wenyewe lawama kikwete na serikali na polisi tafuteni haki mezani na wala sio kwa jazba.poleni waliofiwa.kwa jinsi nilivyoshuhudia nilijua haya yote yatatokea.
ReplyDeleteMimi ninadhani aliyeandika hapa juu anahitahika Muhimbli haraka sana kabla mambo hayaja mwaribikia. huyu ni kichaa, mwenda wazimu, au ni nyang'au tuinaishinalo huku mitaani. Sasa subiri maandamano hayoooo yanakuja tuone mshezi ni nani. Na huo mfano uliotoa Zanzibar uchunge sana. Kwa hiyo kisasi cha Zanzibar ndio mmekuja kukilipizia Arusha. Ndugu watanzania mambo hayo mjue kunakisasi cha kuchinjwa askari Zanzibar. Ndio maana makamba anatumia biblia kutukejeli.
ReplyDeleteSasa naona hii sehemu imekuwa kama dampo,kila mwenye uozo wake kichwani anakimbilia hapa kuumwaga.Naona kuna umuhimu wa kuwalazimisha watu waweke utamblisho wao labda hilo linaweza kupunguza huu uozo.Option ya anonymous iwekewe mipaka.
ReplyDeleteinamaana serikali pamoja na hizo taarifa zao wanazosema za kiintelijensia hawakuona hatari hiii kwamba watu wangeweza uwawa na polisi bilasababu za msingi nawenyewe wangeanza kuzitanisha pandembili ili kuepusha janga hili kutotokea?.....Ninachokiona mimi hapa hakuna uwajibikaji maana kama ni kazi WZR na IGP wanapaswa kujiuzulu kwahili.
ReplyDeleteMimi ni Mwana CCM, lakini naona CCM imeshindwa kazi. Viongozi wote waliohusika naomba mjihuzuru. Mshangazo mkubwa kwa Kikwete, kama Kiongozi wetu wa Taifa anapaswa kukemea haya mambo na kufukuza kazi Maaskari wa Police waliohuska kwenye kisa hiki especially huyo IGP. CCM nafikiri huu ndio uongozi wa mwisho tulonao kwenye madaraka ya juu. Sidhani kama tutapita tena.
ReplyDeleteGeorge,
USA
IGP M/Mungu atakuona tu.kwa haya yote
ReplyDeletenasema hivi. anayeuwa kwa upanga naye mauti yake ni kwa upanga. na hivyo hivyo risasi kwa risasi. ninawahakikishia, kikwete, nahodhda, mwema, mkurugenzi wa jiji arusha, meya feki, makamba, chatanda na kila mmoja aliye na sehemu directly au indirectly katika mauaji ya watu wa mungu yaliyotokea arusha ni lazima nao miili yao itapokea risasi ili wajue na waonje maumivu yaliyowapata binadamu wenzao. mungu lazima atasababisha ana walinzi wao, au majambazi, au hata vichaa watekeleze azma hiyo. haiwezekani mungu akubaliane binadamu aliowaumba kwa mapenzi yake mwenyewe wafanyiwe hivi na binadamu wenzao. ni tamaa tu ya madaraka na vitu vya duniani kana kwamba wataishi milele. na nakwambia baada ya maisha yao hapa duniani juu yao ni hukumu ya milele. na andiko lazima litimie juu yao na hata kwa vizazi vyao. auwae kwa upanga atakufa kwa upanga na mifano ni mingi kwa watu kama hao.
ReplyDelete