MADRID, Hispania
KOCHA wa timu ya Real Madrid, Jose Mourinho na kocha mwenzake wa timu ya Sporting Gijon, Manuel Preciado, wamenusurika adhabu ya kufungiwa kutokana na jazba waliyoionesha Novemba mwaka jana, baada ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Hispania (RFEF), kuona hakuna sababu ya kuwaadhibu.
Awali, shirikisho hilo lilikuwa limeagizwa na kamisheni ya michezo selikani kuwachukulia hatua madhubuti za kinidhamu makocha hao wawili, baada ya kuonekana kutaka kusababisha ghasia na kuvuruga mchezo.
Kamisheni hiyo ilieleza kuwa, hatua ya Preciado kuja juu kufuatia kauli ya Mourinho kwamba, timu yake haikufanya jitihada kubwa kuwafunga Barcelona, ilikuwa ni ya hatari na ya kujenga mazingira ya uadui wakati wa mechi baina ya timu hizo mbili.
Klabu hiyo ya Gijon ilieleza kupitia tovuti yake kuwa, kamati ya mashindano ya RFEF ilieleza juzi kuwa, taarifa iliyotolewa kuhusu taarifa za makocha hao, haikulingana na hatua ya kupewa adhabu.Hata hivyo, shirikisho hilo liliongeza kuwa, kamati hiyo imeagiza wadau wote wa soka kupitia taarifa hiyo.
Katika mvutano huo, Preciado anamshutumu Mourinho kwa kukosa heshima na alitoa matamshi ya Kireno katika mkutano wa vyombo vya habari, jambo ambalo liliifanya timu ya Real Madrid kutoa taarifa kabla ya mechi kulaani kitendo hicho.
Hatua hiyo inaungwa mkono na makocha kadhaa wa La Liga, akiwemo kocha wa timu ya Villarreal, Juan Carlos Garrido na kocha wa Espanyol, Mauricio Pochettino ambao wanamuunga mkono Preciado.
No comments:
Post a Comment