Na Rehema Maigala,Kinondoni
MNENGUAJI wa bendi ya FM Academia, Stephania Mchunguya, amelia mbele ya Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, baada ya Hakimu kumwambia kuwa, amefuta dhamana yake na anakwenda mahabusu Segerea.Mshitakiwa huyo
ambaye alikuwa na kesi ya kutumia lugha ya matusi dhidi ya mlalamikaji Sheha Abed, ambaye alikuwa amemtukana matusi ya nguoni.
"Leo nakufutia dhamana yako, itakuwa ni vizuri ukiwa unatokea huko huko Segerea kwani tutakuwa tunakupata kwa urahisi na unawahi zaidi kuliko unavyokuwa huru," amesema Hakimu Mariamu Masamalo.
Mshitakiwa huyo baada ya kusikia kauli ya Hakimu huyo, aliangua kilio na kuomba msamaha kwa hakimu ili amsamehe, kwani atakuwa anafika Mahakamani kila tarehe yake.
Ilidaiwa Mahakamani hapo, mshitakiwa huyo alikuwa hafiki Mahakamani mpaka askari wa Mahakamani walipomfuata mshitakiwa huyo nyumbani kwake kwa ajili ya kumkamata na kumfikisha Mahakamani hapo.
Kesi hiyo ipo mbele ya Hakimu Mariamu Masamalo, na Karani Dola Chambo kuwa, Oktoba mwaka jana mshitakiwa alimtukana mlalamikaji Sheyha Abed matusi ya nguoni.Mshitakiwa alikana shitaka hilo na alikuwa nje kwa dhamana ambayo aliwekewa na wanamuziki wenzake, kesi hiyo itatajwa tena Januari 20 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment