Na Andrew Ignas
RAISI Mstaafu wa awamu ya tatu, Bw. Benjamini Mkapa amewataka Watanzania kumuombea aweze kusimamia upigaji kura za maoni Januari 9 mwaka huu ambazo
zitakuwa ndio zinatarajiwa kutoa mstakabali wa amani ya Sudani.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili jana ofisi kwake jijini Dar es salaam, Msemaji wake, Bw. Azizi Mlima alisema kuwa, Watanzania wanapaswa kumuombea dua Bw. Mkapa ambaye anatarajiwa kuondoka leo kuelekea nchini humo kusimamia shughuli hiyo ifanyike kwa amani na utulivu.
Alisema kuwa Mkapa ambaye aliteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon anatarajiwa kuondoka leo kwenda kusimamia shughuli ya upatanishi baina ya serikali mbili, Sudani Kusini na Sudani Kaskazini, ili kupata muafaka wa kuunda serikali moja.
"Mkapa anatarajia kuondoka kesho (leo) ili kuandaa taratibu za awali kwa ajili ya siku ya kura za maoni ambayo inatarajia kufanyika tarehe 9 ya mwezi huu nchini humo, hivyo Watanzanai wanatakiwa kuiombea nchini hiyo kuwepo amani wakati wa zoezi hilo," alisema Bw. Mlima.
Hata hivyo, alisema kuwa kiongozi huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Usimamizi wa Kura za maoni kwa nchi hiyo, anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhakisha anasimamia kwa ukamilivu shughuli hiyo ili hali ya amani iweze kupatikana.
No comments:
Post a Comment