13 January 2011

FemAct yataka meya Arusha ajiuzulu

Na Gladness Mboma

SERIKALI imetakiwa kuufuta uchaguzi wa Meya Arusha na kuitisha uchaguzi mwingine huru  ili wananchi wachague meya mwingine wanayemtaka, ikiwa ni pamoja na kumtaka aliyepo madarakani kwa sasa ajiuzulu ili kupisha
uchaguzi urudiwe kama alivyofanya Naibu wake Michael Kivuyo.

Pia wameitaka serikali iunde tume huru itakayowashirikisha wananchi, polisi, vyama vya siasa, wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu kushughulikia suala hili  na kuwahakikishia wananchi wa Arusha kuwa tukio kama hili halitatokea tena.

Wito huo ulitolewa Dar es Salaam jana na Mashirika yapatayo 50 yanayotetea Usawa wa Kijinsia, Haki za Binadamu, Maendeleo na Ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi (FemAct).

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Usu Mallya ambaye alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya FeMAct alisema kuwa wanalaani ukiukwaji wa haki za binadamu, demokrasia na uvunjivu wa amani uliosababisha kuumizwa na mauaji ya raia wasiokuwa na hatia mjini Arusha.

Alisema kuwa mashirika hayo yameshtushwa  na vurugu na matumizi ya nguvu za dola dhidi ya raia waliokuwa katika harakati za kudai haki zao kupitia  maandamano ya amani  na mkutano wa hadhara  ulioandaliwa na chama halali cha  siasa jijini Arusha.

" Vurugu hizo ziliendana na unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia kwa baadhi ya waandamanaji, huu ni ukiukwaji wa haki za msingi za kibinadamu na za wanawake,"alisema.

Alisema kuwa FemAct inalaani kitendo cha Halmashauri ya Jiji la Arusha  kusimamia na kuendesha uchaguzi batili  usiozingatia sheria kanuni na taratibu za uchaguzi  ambao ulimpata Meya na Naibu wake  Desemba 18 mwaka jana na kusababisha kutokea kwa vurugu hizo.

Bi. Mallya alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari na jeshi la Polisi watu wanne wamepoteza maisha na zaidi ya watu 30 kujeruhiwa vibaya wengi wao wakiwa ni watoto wadogo, wazee, walemavu na wajawazito.

Alisema kuwa  FemAct inasikitika pia kuona siku nane baada  ya Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mgambo wa jiji waliwashambulia mamia ya wananchi hao waliokuwa wakiandamana, ambapo serikali imeendelea kukaa kimya bila kuunda tume au kuwachukulia hatua zozote wale wote waliosababisha  vurugu hizo.

Pia FeMAct imedai kushtushwa na ukimya huo na maelezo yasiyojitosheleza  na uzito wa kuchukua hatua za haraka ili kutenda haki kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutaka kutafuta suluhu na kurejesha demokrasia na haki miongoni mwa wananchi wa Arusha.

"FemAct tunalaani kwa nguvu zetu zote ubabe na matumizi mabaya ya vyombo vya dola, hasa Jeshi la Polisi ambacho  ni chombo cha ulinzi na usalama wa wananchi  kugeuka na kuvunja sheria  ya kuwazuia wananchi kutoa sauti zao na kupigania haki zao za msingi,"alisema.

Alisema kuwa  wao kama sehemu ya jamii wanapinga mwenendo  unaoweza kujengeka na kuonekana kama jambo la kawaida  hapa nchini la kunyamazisha  wananchi wasitoe sauti zao.

Bi. Mallya alisema kuwa  tabia ya serikali kuzidi kuonesha ubabe  katika matukio mbalimbali  ya kudai haki  nchini na kutolea mfano wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma na UDSM.Alisema kuwa wakiwa kama wanaharakati wamelitaka jeshi la Polisi na serikali kuweka wazi muktadha na hali halisi ya tukio la Arusha, kuwataja na kuwachukulia hatua za kisheria walioshiriki kuvunja sheria na kutoa idadi kamili ya wananchi waliojeruhiwa na kupoteza maisha katika tukio hilo.

Bi. Mallya alisema kuwa kitendo cha kuendesha uchaguzi kwa ubabe ni kuikaba koo demokrasia, kukiuka haki za kibinadamu  na kuwalazimisha wananchi viongozi wasiotaka.

Hali hiyo, ambapo wamekemea kwa nguvu zote na kwamba kamwe wananchi wa Tanzania hawatakubali tena kubebeshwa mzigo wa viongozi wasio na sifa za kuongoza.Bi. Mallya ameitaka pia  serikali,vyama vya siasa na vyombo vya dola kutokuwanyamazisha wananchi, viongozi wa kijamii na dini wanaolizungumzia suala la Arusha kwani hivyo ni  kinyume na demokrasia iliyoendelea na kukomaa nchini Tanzania.

11 comments:

  1. Tatizo kubwa la Tanzania sasa hivi ni kwamba wasomi, wanaharakati, na baadhi ya viongozi wa dini ni watu ambao wanatoa matamko yanayoegemea upande wa upinzani. Nampongeza Professa Mwesiga Baregu kwa kuamua kuwa mwanachama wa chadema na kuamua kupoteza haki zake. Ningewaomba na wengine wafanye hivyo kwa maslahi ya umma kwa sababu wanatuchanganya sis wananchi wa kawaida. Kilichotokea Arusha kinaeleweka kuwa tatizo ni madiwani kususia uchaguzi shauri ya Chatanda kupiga kura. Chadema walifanya vurugu wakijua wanachodai si sahini. Hawa wanaharakati hawagusii maneno ya Slaa akiwaambia wafuasi wake kwenda polisi kuwatoa viongozi. Nyie wanaharakati, wasomi, na baadhi ya viongozi wa dini chukueni kadi za chadema ili mtakayosema tuwajuwe kuwa nyinyi ni wana chadema, la sivyo mnatuvuruga na taasisi zenu zinakosa credibility mbele ya wananchi. Mnazalilisha kazi zenu kwa kushabikia upande mmoja. Kwa hili la Arusha, Chadema wana kesi ya kujibu. Msipoteze malengo.

    ReplyDelete
  2. WEWE KAMA(ON TOP) KAMA HUNA MCHANGO C UNYAMAZE KAMA CHADEMA NDO WAMEFANYA VURUGU MBONA JANA POLISI HAWAKUWEPO NA MAMBO YAKAWA SWARI? WE ACHA KUJIFANYA MPUUZI KAMA NDUGUYO MAKAMBA NA CHITANDA NANI KAKWAAMBIA CHADEMA WALIGOMA WAKATI HAWAKUPEWA BARUA ZA MWAALIKO NA WEWE ULUVYOFANYWA MPUUZI KAMA CCM UNATAKA WAKAZI WA ARUSHA TUKUBALIANE NA MBUNGE WA TANGA KUPIGA KURA ARUSHA KWA SABABU NI KADA WENU SAHAU TUTAPAMBANA MPAKA KIELEWEKE, BORA KUFA UKITETEA HAKI KULIKO KUISHI MIAKA MINGI KAMA WEWE UKAFA KAMA MNYAMA.

    ReplyDelete
  3. Ndiyo zenu chadema kutukana mawazo ya wengine. Toa hoja usitukane watu. Hapa tumepewa uwanja kila mtu kutoa mawazo yake. Nyie chadema mnadhani mnayosema tu ndiyo sahihi tu. TUTAFIKA?

    ReplyDelete
  4. CHADEMA ACHENI UPUUZI, POLISI HAWAKUWAUA WATU KWENYE MAANDAMANO, WATU WALIUWAWA BAADA YA SLAA KUWAAMBIA WEHU WENZIE WAENDE KUWATOA KINA MBOWE KWA NGUVU, HIVYO BASI HAO WALIOUWAWA WALIKUFA MITA CHACHE KUELEKEA KITUO CHA POLISI TENA BAADA YA POLISI KUONA USALAMA WAO UPO HATARINI, JIULIZENI KWANINI SLAA HAKUKAMATWA?

    ReplyDelete
  5. wewe ni mjinga unategemea watu wote ni wajinga kama wewe maskini wa mwisho unaongea nini hivyo umefurahia watu kufa, litakupata tu hata wewe wala huna mda mrefu jambazi wewe, wewe ndo uache upuuzi mshamba wewe nenda darasani kwanza kwani huna hata chembe ya akili mbona hatukuwa na polisi jana na hakujatokea fujo yeyote ngombe wewe.tumia akili usitumie visogo vya wanaume wenzio tu. toka uonekane choka mbaya wewe.Arusha tuna wanaume na wanawake wenye elimu sio matahira mlivyo wewe na familia yako.omba msaada.

    ReplyDelete
  6. hawa wananojiita wanaharakati wanatuchanganya tu. hawana lolote. wanaacha kuangalia wapi tumejikwaa wanalaumu tulipoangukia. tuache unafiki. kama hao wanaharakati wanaushahidi kuwa sheria na taratibu za uchaguzi wa meya zilikiukwa waende mahakamani kupinga kama walivyofanya kwa malipo ya Dowans.tuache ushabiki wa kisiasa kwenye ukweli lazima tuseme hata kama unauma. mimi sijuona hata mara moja hao wanaharakati wakikemea kitendo cha kiongozi wa siasa aliyeamuru wanachama wake waende wakavamie kituo cha polisi ili kuwatoa wafuasi wao. je hili nali ni kutenda haki? au mnataka haki mtendewe nyinyi tuu. hivi kama wewe ungekuwa polisi na watu wanakuja kwa mawe kuvamia kituo cha polisi ungefanya nini? polisi nao ni binadamu nao pia wala roho na wanaogopa kufa. tauche unafiki tuseme ukweli ili tujikosoe na kujifunza kutokana na makosa kwa lengo la kujenga nchi yetu.

    ReplyDelete
  7. kwa hiyo wewe mchangiaji wa 5 hapo juu hiyo ndiyo elimu yako ilipofikia? kama elimu yako inakuwezesha kutoa maoni ya matusi kama hayo ni bora tu kutokwenda darasani. hongera sana kwa kwenda kwa hiyo elimu yako kubwa uliyonayo..

    ReplyDelete
  8. Habari wapenzi wa gazeti la majira,kwa masikitiko,majonzi na huzuni makubwa napenda kutoa pole kwa wale wote waliopata maafa na kupoteza uhai wao kwa ajili ya kupigania haki Jiji Arusha.Polisi hammkutenda haki kabisa kwani ilitakiwa mtumie mabomu tu sio risasa.

    CMM damu iliyomwagika Arusha inawalilia tambueni hilo mapema, hu sio utawala wa kiudikteta wala kimabavu bali ni wa kidemokrasio ilyo huru ya mfumo wa vyama vingi na wala sio chama kimoja. hivyo basi tunaomba meya wa Arusha ajiuzulu iwezekanavyo. uchaguzi urudiwe upya hiyo ndiyo njia pekee ya kusuluhisha mgogoro huo.

    ReplyDelete
  9. Tatizo kubwa ni siasa chafu Tanzania, polisi ni chombo cha dola ambacho hakitakiwi kutumiwa kisiasa sasa wamekitumia na kupoteza maisha ya watu wasio na hatia. Hatuangalii Chadema au CCM suala je kutumia risasi za moto katika maandamano ya raia wasio na silaha ni sahihi? wanasiasa walumbane na yao lakini jeshi la polisi litueleze ukweli juu ya utumiaji wa risasi za moto katika maandamano.

    ReplyDelete
  10. Mchangiaji wa mwisho unaonekana hulijui hili suala, iko hv.Polisi hawakuwafuata waandamanaji na silaha la hasha, walikwenda kuwakamata kina mbowe ambao ndio viongozi wa maandamano, na huko walikokamatiwa ambapo ni mitaa ya Ilboru hakukua na fujo, ila fujo zilitokea wakati slaa alipopata taarifa kua mbowe kakamatwa,ndipo alipo waamuru wafuasi wake waende kuwatoa kituoni kwa nguvu, na kuna maneno aliyasema kua sasa tz atakua km ivory cost kwani nae pia anaweza kuanzisha serikali yake. sasa kilichotokea watu wa dk slaa walikua wanaeleke kituoni kwa lengo la kufanya fujo ili hatimae wamuokoe mbowe, ndio polisi walipoamua kutumia mabomu, bbada yakuona wanazidiwa ndipo walipoamua kutumia risasi za moto, tena ilikua ni mita chache tu kabla hujafika kituoni, sasa jiulize nani kamfuata mwenzake. polisi walistahili pongezi kwa hili na slaa ashtakiwe.

    ReplyDelete
  11. Nyinyi wake za mapolisi na mabwana wa mapolisi acheni ushamba. polisi ndio chazo cha vurugu zote hizi, Wangekuwa hawajakosea kama wasingeingilia hayo maandamano. Wao polisi walikuwa wanajua ya kuwa watu hao wanaelekea wapi wangewapa ulinzi mpaka wafike kama wangekosea ndio hapo wangejibu ya kuwa mnakwenda wapi? Acheni kuzingua watu maji yako jikoni yanachemka. Mnafikiri kila mtanzania ni wakupiga kama mpira. hata mnyama anaheshimika sembuse binadamu.

    ReplyDelete