24 January 2011

Maslahi ya taifa kwanza, siasa baadaye-Mengi

Na Omari Moyo, Arusha

SERIKALI, vyama vya kisiasa na viongozi wa kidini wametakiwa kushirikiana katika utatuzi wa migogoro inayojitokeza nchini hasa ya kisiasa kuhakikisha amani ya
nchi haichafuki kama ilivyowahi kutokea kwenye nchi za Rwanda na Burundi.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Bw. Reginald Mengi wakati akizungumza kwenye mahafali ya 19 ya kidato cha sita cha Shule ya Sekondari Ilboru, mjini Arusha.

Alisema kwamba malumbano ya kisiasa yanayoendelea nchini na matamko mbalimbali ya viongozi wa dini na wa kisiasa hayana faida kwa mustakabali wa taifa la Watanzania, kwa kuwa matamko hayo yanaashiria machafuko, siyo kuleta amani.

Bw. Mengi alishauri kuwa ni vyema dini zingekuwa zikitoa matamko yasiyokinzana na yasiyokuwa na  muelekeo wa kisiasa na kuwataka viongozi wa kisiasa badala ya kuchafua zaidi hali ya hewa, wakae chini na kukubaliana kuhusu tofauti zao, kwa mustakabali wa Tanzania.

“Hawa viongozi wa dini, wa siasa na serikali zisifanye maamuzi kwa ajili ya matakwa ya wachache, lazima waelewe wazi kwamba hakuna jambo muhimu kama la kuweka maslahi ya taifa mbele. Wakubaliane kwenye hoja za kuliondoa taifa kwenye machafuko, kwanza wazungumze ya kwao, na wajue kwamba yaliyotokea nchi za Burundi na Rwanda hata Tanzania yanaweza kutokea,” alisisitiza Bw. Mengi.

Aliongeza, “mimi mmenialika hapa Arusha shuleni kwenu, na nimekuja kwa raha kabisa na kifua mbele, je, kungekuwa hakuna amani ningekuja? Kwa hiyo ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha suala la amani ya Watanzani mbele ndipo yafuate mambo mengine,” alisema Bw. Mengi.

7 comments:

  1. Asante sana mzee mengi.
    tatizo hapa ni Serikali ya CCM isiyotaka kukosolewa wala kutubu.
    Mfano mzuri tuangalie yaliyotokea Arusha . Polisi hawakuwa na sababu ya kuzuia yale maandamano na kuuwa watu wasio na hatia. maaskofu walilaani kile kitendo na kutotambua uchaguzi wa meya wa Arusha kutokana na mchakato mzima ulivyokuwa na utata. Pia asasi za kiraia hata mabalozi wa nje walihiji yaliyojiri Arusha. Makamba aliwaambia maaskofu wavue majoho waingie ktk siasa. Last week ktk ukumbi wa Diamond Jubilee mashekhe walikutana wakatoa tamko la kumsifu Rais na serikali yake kuhu wakijidai kukemea udini. nauliza Mbona Makamba hajawaambia wavue kanzu waingie kwenye siasa wakati wote wameshiriki politics? Tatizo hapa ni Serikali yetu isitotaka kukosolewa na kukubali pale inapokosea. Udini haupo ila unachochowa na viongozi waliopo serikalini wasioitakia mema nchi yetu. watanzania wengi wameamka na wana ufahamu sana kuhusu haki zao. Wana uwezo mkubwa sana wa kujua nani mdini na ni nani anatetea maslahi ya Taifa. Tunamwomba Mungu things will be alright.
    intelijensia1@gmail.com

    ReplyDelete
  2. Hapana cha Makamba wala Serikali kutokubali kukosolewa hapa tatizo ni 'double standards za maaskofu na udini wao kwa chadema dhidi ya waislamu na viongozi waislamu walio serikalini kwa sasa " imekuwaje matamko ya maaskofu yaingilie kutomtambua meya tokea lini wao wamepata mamlaka haya wapi? ktk mchakato wa uchaguzi waliwabeba dhahir chadema nani asiejua ? hapa kuna namna nadhani hawa jamaa wameona maslahi ya kanisa katika serikali yanaanza kuondoka baada ya ule utamaduni wa kubebwa na serikali na ndio maana KIkwete amekuwa nongwa sasa .hapa lengo ni kumfanya ashindwe kuendesha nchi alafu waislamu waambiwe hawawezi kuongoza hawana elimu nauliza hivi kwa nini kila wanalofanya chadema sasa maaskofu wanalazimika kulibariki ?

    ReplyDelete
  3. ndugu naona na wewe umejaa udini tena uanatetea uislam wakati hapa hoja ya msingi siyo uislam na ukristo. kuna sheria inasema maaskofu lazima wakubaliane na kila inachofanya serikali hata kama serikali inachemsha? kama unamaanisha unachokisema nami nawezasema hapa pia kuna udini wa mashekhe kwa ccm maana maaskofu wakiikosoa ccm ni kosa ila mashekhe wakiisifu siyo kosa. tanzania hakuna udini. Ungejua maana ya udini tungeona huku mitaani tunakoishi kukiwa na migawanyiko. waislamu wanafanya kazi na wakristo,wanaishi pamoja,wanakula pamoja,wanakunywa pamoja,wanasoma pamoja,wanashirikiana vema kwenye misiba kwenye harusi etc sasa huo udini umetoka wapi fafanua. hapa wanasiasa wanatumia hoja ya udini kwa kutotaka kukosolewa. fanya utafiti hakuna kundi la maaskofu wanaochukia serikali ya ccm,wanaonya na kusisitiza haki itendeke katika jamii ya watanzania na sii vinginevyo.

    ReplyDelete
  4. TATIZO LA WATANZANIA KUWA WANAFIKIRI KWA TUMBO BADALA YA KUFIKIRI KWA AKILI ILIYI KICHWANI. MIMI NAUNGANA NA ALIYETOA MAONI HAPO JUU KWAMBA WATU WENGINE WANAFIKI WATU WOTE TUNAISHI MJINI. SUALA LA DINI NA SIASA NI HUKO MINJINI TU HUKU VIJIJINI HAKUNA DINI WALA SIASA WOTE TUNAANGALIA MBELE NAMNA YA KUPAMBANA NA MAISHA YA SASA NA VIJINA WETU BAADAYE.

    ReplyDelete
  5. Nashauri watoa maoni muwe mkizingatia na mada husika. kwangu mimi, pamoja na uzuri wa maneno ya mgeni rasmi kwenye mahafari ya kidato cha sita, sidhani kama audience ilistahili kupata hayo maneno, hawa vijana wa shule nafikiri haya hata walikuwa hawajui yanakujaje, anyway wachangia ndiyo kabisa mmekwenda nje ya mstari kuna huyu anayesema watu wanawaza kwa tumbo, amechangia kila heading ya gazeti la leo ni ni hayo hayo kuwaza kwa tumbo, jamani tuache kupoteza muda wa wenzetu

    ReplyDelete
  6. Ndugu mtoa maoni namba 2.
    Unaposema ya kuwa maaskofu wanapendelea cha Chadema sio kweli sema mnatafuta mwavuli wa kujificha. Kama wakristo wangekuwa na upendeleo wa kidini kama unavyofikiria wewe huyo meya ambae nasikia kwanza ni M/kiti wa parokia wangekuwa wa kwanza kumtetea kwa sababu ni mkristo. Wewe unafikiri upo Dar es salaam unajua zaidi ya waliopo Arusha? Sisi tumeona mazingira yalivyogubikwa na giza ule uchaguzi na ndio maana tuliomba huo uchaguzi urudiwe ili kila mmoja ajiridhishe. Halafu serikali ilipokosea ni pale ilipotumia polisi kuingilia maandamano. Kama kweli hatakama ni wewe fikiria polisi wanamfuata mtu mpaka mbele ya kanisa na kumpiga risasi na kumwacha anajigalagaza. Hata maaskofu waliopo Arusha kiliwauma na kuona yale mateso watu waliyoyapata bila sababu. Kama waliona CHADEMA walikosea wangefetulia risasi walipokuwa kwenye maandamano.

    Lingine unasema imekuwaje matamko ya maaskofu yaingilie kutomtambua meya tokea lini wao wamepata mamlaka haya wapi?
    Unajua ndugu yangu umeshaonyesha wazi kabisa ya kuwa wewe una jazba, unaubinafsi wa dini na unaubaguzi tena mkubwa sana na sidhani kama wewe ni raia wa TZ. Na mimi nikuulize Je huyu Askofu sio raia wa Tanzania, hastahili kujua juu ya serikali yake na kukemea maovu yanapotokea? Na lingine hao mashehe waliokaa na kutoa tamko wao walitoa tamko kama nani na walipata wapi mamlaka? Maoni yangu nyinyi wenyewe ndio mbadilike muende na mwenendo wa wananchi, raia wanayotaka sio kufanya kwa kumkomoa mwananchi. Humkomoi unajikomoa mwenyewe. Sasa mnalalamika maaskofu wanayumbisha serikali isitawalike, wakati mnauliza wamepata wapi mamlaka acheni kuwazushia baba wa watu waliotulia nyumbani kwao, au mnataka wapite humo majumbani mwa watu wawalazimishe. Hawa maaskofu wanauwezo kama wa serikali kweli,haiingi akilini.

    ReplyDelete
  7. 1.Sasa Askofu mwenzao kasema wanapata Uaskofu kwa rushwa

    2. Uchaguzi wa Arusha ni propaganda za kisiasa
    mbona Hai wamepiga kura wabunge wateule ambao
    hawaishi pale? hapo kuna kaujanjaujanja
    kanapikwa,sheria ziko wazi

    3. Usimuite mwenzio kuwa sio raia wa Tanzania kwa kupingana na wewe kwani wewe unamjua baba yako? pengine ni Mkenya kwani mama yako ndiye anayejua siri ya kuwa wewe ni mtoto wa nani,kwa hiyo ukome kumuita mwenzio sio raia kwa kutofautiana mawazo na wewe

    ReplyDelete