Na Jumbe Ismailly, Singida
MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki (CHADEMA), Bw. Tundu Lissu anakusudia kuwasilisha hoja binafsi katika mkutano ujao wa bunge kuomba
iundwe Kamati Maalumu ya Bunge kuchunguza matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Mbunge huyo alitangaza azma yake hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa Habari wa Mkoa wa Singida alipokuwa akifafanua sababu za kupimga wananchi wa jimbo lake kuchangia elimu wakati fedha zilizotengwa na serikali hazitumiki hazi zinarudishwa hazina.
Kwa mujibu wa Bw. Lissu, hotuba ya Bajeti ya Waziri Mkuu aliyotoa katika bunge Juni mwaka jana, katika mwaka wa fedha wa 2009/2010 serikali ilitenga sh. 2,151,000,000 kwa ajili ya Mkoa wa Singida kwa ajili ya sekta ya elimu, lakini sehemu kubwa haikutumika na kurejeshwa hazina.
Hata hivyo, Bw. Lissu ambaye pia ni mwanasheria wa CHADEMA alifafanua kuwa kati ya kiasi hicho cha fedha hadi kufikia Machi mwaka jana ni 1,187,000,000 zilizokuwa zimetumika na kwamba 905,000,000 zilirudishwa hazina baada ya kukosa kazi ya kufanya.
Bw. Lissu aliweka wazi kwa mkoa wa Singida peke yake zilizotolewa kwa sekta ya elimu, zilizotumika na kubakia sh. 465,000,000 na kwamba kwa miaka miwili mkoa huo umerudisha hazina zaidi ya sh. 1,350,000,000.
"Mwaka wa fedha 2008/2009 na takwimu hizo zipo kwenye hotuba hiyo hiyo ya Waziri Mkuu bungeni mwaka jana zinaonyesha kwamba kwa Mkoa wa Singida peke yake fedha zilizobaki kwenye elimu zilizotolewa na serikali wakatumia zikabaki, ni sh.
465,000,000.
"Haya ni mahesabu ya serikali, ni mahesabu ya Waziri mkuu bungeni, sasa wananchi wanachangishwa kwa sababu gani?" alihoji mbunge huyo huku akionesha kukerwa na hali hiyo ya changia.
Hata hivyo Lissu aliendelea kuhoji sababu za wananchi kunyang'anywa mifugo yao na mali nyingine wakati fedha za serikali hazitumiki na kurudishwa hazina.
Lakini hata hivyo mbunge huyo wa CHADEMA alifafanua kuwa wananchi wamejikuta wakiwa
na hali hiyo kutokana na michango hiyo wakati serikali yenyewe kupitia kwa Waziri Mkuu alilihakikishia bunge hilo kwamba kwa miaka miwili fedha iliyoletwa imerudishwa serikalini sh. 1,350,000,000.
mheshimiwa TUNDU LISSU unachokifanya ndio kinachotakiwa kufanywa na wabunge wote kwanini kazi za serikali tufanye sisi wananchi?? sisi kazi ni kulipa kodi na kazi ya serikali ni kuzitumia kwa niaba yetu kwenye shule na miradi mingine hivyo hakuna haja ya michango ya ajabu ajabu kila siku. kama mimi mwananchi inanibidi kuchangia kwenye kila kitu basi sasa kodi yangu inafanya kazi gani? kuhusu swali lako la kurudishwa pesa watendaji wa serikali wanafanya hivyo ili kujikomba kwa serikali ili wapate bonus kubwa lakini wakati huo huo wakiwaumiza wananchi. cha msingi hapa ni kufuta kabisa michango yote ya lazima na kubakiza ile ya hiyari tu ambayo mtu uchanga kwa sababu zake binafsi.
ReplyDelete