14 January 2011

Mashabiki 20,000 wamlaki Ronaldinho

SAO PAULO, Brazil

MASHABIKI wapatao 20,000 juzi walijitokeza kumlaki mshambuliaji  Ronaldinho, wakati akitambulishwa rasmi katika klabu yake mpya Flamengo ya nchini Brazil.Taarifa zilieleza jana kuwa kundi la ngoma ya Samba, ndilo lililoongoza
mapokezi hayo ya Ronaldinho, ambaye alikuwa akiwapungia mikono mashabiki huku akiwashukuru kwa mapokezi hayo akisema kuwa ataweza kurejesha shukrani zake akiwa uwanjani.

Ilielezwa kwamba, kabla ya Ronaldinho kuwasili uwanjani mashabiki walikuwa wamejipanga kwenye lango la kuingilia uwanjani kwa shauku kubwa wakimsuburi nyota huyo.

Nyota huyo wa zamani wa Brazil, alijiunga na klabu hiyo Jumatatu wiki hii akitokea katika timu ya AC Milan, hivyo kumaliza kipindi cha miaka kumi akicheza soka barani Ulaya.

Mkataba wa Ronaldinho, unaripotiwa kuwa na thamani ya dola milioni 235 pamoja na marupurupu kibao.

No comments:

Post a Comment